*MAANA HAUJATIMIA UOVU WA WAAMORI BADO*
_Ufafanuzi mfupi na Mwl Proo_
0762879363
Bwana Yesu Kristo apewe sifa! Naamini BWANA Mungu anaendelea kukutunza na kukuhifadhi (Zaburi 91:14). Tauni hii _covid-19_ itapita nawe utahifadhiwa na wema wa Mungu, iko neema ya kukunusurisha na kila janga litakalozuka katika nyakati hizi, pokea hiyo neema kwa Jina kuu la Yesu Kristo ✋🏾
Niliwekewa moyoni mwangu kuandika ufafanuzi wa mstari huu hapa chini, Mwanzo 15:16, wakati Mungu akizungumza na Abramu (badae Ibrahim) juu ya uzao wake.
_*"Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado."*_
(Mwanzo 15:16)
*_"But in the fourth generation they shall come hither again: for the iniquity of the Amorites is not yet full."_*
(Genesis 15: 16)
⚖ Katika somo langu la _Kikombe changu kinafurika_ nilitoa moja ya tafsiri za kinabii kuhusu kikombe ☕ nikikihusianisha na ghadhabu/hukumu.. 👉🏼 (Yeremia 25:15, Ufunuo 14:10, 16:19). Kabla Mungu hajaachilia hukumu yake lazima kuwe na kiwango fulani cha uovu kimeenda beyond His tolerance (before He execute His divine judgement, iniquity/wickedness should reach a certain degree beyond tolerance and beyond His dispensational time)... Inaweza kuonekana kana kama haijakaa sawa kwa namna tunavyomfahamu Mungu alivyo wa rehema na msamaha. Mungu hataadhibu bila kuleta maonyo kwa ustahimilivu mkuu. Ni kama kunakuwa na kikombe kimehifadhi uovu 👉🏼☕ watu wakitubu, zinafutwa na Mungu hawahesabii tena huo uovu/dhambi (Zaburi 32:1, Isaya 43:25), lakini kama watu hawatatubu wakaendelea tu kutenda maovu juu ya maovu, kikombe kinaweza kujaa, kikombe cha uovu kikijaa, hukumu ndicho kitu pekee kitakachofuata, maana pamoja na Mungu kujaa rehema na msamaha (Daniel 9:9) hawezi kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia (Kutoka 34:7) labda kuwe na michakato hapo kati iliyohusisha toba, au neema kwa njia ya Yesu watu wakiikubali. Kuna wanaofundisha neema to the extreme bila kujua kuwa neema iko na terms and conditions za kwake, mtu akiipungukia neema kuna namna atakuwa _dealt out_ na hasira ya Mungu na wasiolewa watashangaa. Neema ya Mungu haijambadilisha Mungu (Malaki 3:6), God's attributes zimebaki vilevile, He's always willing to save the sinners, lakini nani asiyejua kuwa mtu akifanya uovu, anamfuta katika kitabu chake alichokiandika? (Kutoka 32:32-33), na *UKWEKI HUU UWAFIKIE WAHUBIRI WANAOHUBIRI NEEMA YA MUNGU BILA KUZINGATIA MIPAKA YA MAANDIKO, KUWA KUNA SIKU HUYU MUNGU WA NEEMA YOTE ATAWATUPA KATIKA ZIWA LA MOTO BILLIONS OF HUMAN RACE INTO THE LAKE OF FIRE, IKIWA NI ETERNAL PUNISHMENT*. Neema imewabadilisha wanadamu, neema imewawezesha na imewafundisha wanadamu kuwa kama Mungu (Tito 2:11-13) 👉🏼 nayo yatufundisha kuukataa ubaya (hii ni side B ya neema ambayo wengine wamekuwa wakiiacha). Mfano kama kuna mchungaji ambaye kaipokea neema, anaijua, anaihubiri, ila anaendelea kuziishi dhambi (in the full knowledge), anazini na washirika, anafanya kila ubaya, pamoja na kuwa kwenye kipindi cha neema, wema wa Munyu utakuwa unamvuta atubu, lakini kuna muda wa Mungu kuvumilia (2Petro 3:9 👉🏼 Huvumilia kwetu, He's patient with us), kunakuwa na muda aliouweka katika mamlaka yake mwenyewe huo ni kama matazamio, kuona kama utatubu kwa kule kuvutwa na wema wake au la (Ufunuo 2:21, Rumi 2:1-4, 11:22-24). Hivyo moyo wa toba (Rumi 2:5) utapelekea dhambi/uovu kufutwa, kuendelea na uovu/dhambi kunaweza pelekea kikombe kujaa. Kikombe kikijaa hakuwi na kingine zaidi ya hukumu... Unasikia Mungu anasema kuwa dhambi za Sodoma na Gomora zimefika mpaka juu mbinguni, akiwa ana-infer kwa issue ya kikombe kujaa 👉🏼☕ _mwlproo_
⚖ Wakati Mungu anaongea na Ibrahim, ambaye alikaa kati ya mataifa ya Kanaani (Canaanite nations), uovu tayari ulikuwepo mwingi mno (Mwanzo 13:13, 18). Lakini Mungu aliona bado kikombe cha ghadhabu yake hakijaa, akatoa muda zaidi (dispensation). Anasema hivi *_Maana haujatimia uovu wa Waamori_* kwenye KJV iko hivi *_For the iniquity of the Amorites is not yet full_*, kama watu watatubu kikombe kinakuwa _emptied_, lakini wakiendelea muda ukifika kitajaa, na hukumu itakuja. Mungu anamwambia Ibrahim kuwa uzao wako nitawapa hii nchi, wakazi wa Kanaani, mataifa yote yale (Maana Kanaani mtoto wa Ham alizaa makabila yote ya kule Canaan 👉🏼 Mwanzo 10:15ff). Sasa walikuwa wanakaa kule kwa halali kabisa, na walipewa nchi ile kwa halali kabisa... Nimesikia mjadala katika kundi huko Facebook wakisema Mungu wa WaKristo ni KATILI, anaua mataifa mengine bila sababu ili awaweke wazayuni (wayahudi). Sasa Je! Mungu ni mkatili? God is just (Righteous Judge).... Tusome maandiko hapa chini
_*"Si kwa haki yako, wala kwa unyofu wa moyo wako, hivi uingiavyo kuimiliki nchi yao; lakini ni kwa uovu wa mataifa haya Bwana, Mungu wako, awafukuza nje mbele yako; tena apate kuliweka imara hilo neno Bwana alilowaapia baba zako Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo."*_
(Kumbukumbu la Sheria 9:5)
Mungu hakuja kuyaangamiza yale mataifa for fun, alifanya accurate calculations, kuwa kwa muda wa miaka ambayo uzao wa Ibrahim utakuwa Misri, basi kikombe cha haya mataifa kitakuwa kimejaa tayari kwa hukumu, na akikusudia alitumie taifa dhaifu la Israel kuyapiga mataifa ambayo hayakuwa na human races za kawaida.
⚖ Iko hivi, Mungu anasena haujatimia bado uovu wa Waamori, uovu gani, kwa nini Waamori? Waamori imetajwa kuwakilisha mataifa yote ya Kanaani kwa kuwa lilikuwa kabila kubwa, lenye nguvu zaidi, lililojieneza magharibu yote ya Mesapotamia. Mataifa yote haya yalifanya machukizo, Mungu aliamua ku-buytime kungoja kikombe kijae (utimie uovu wa waamori)... Wale majitu (Nephilims ambapo wana wa Anaq majitu yalitokea kwa Wanafeli, Gibborim (Nimrod naye alikuwa ni jitu kutoka kwa jamii hii), kuna mfalme aitwaye Ogu wa Bashani alitokea kwa Warefai (Rephaim). Nchi ya Kanaani ilijaa majitu (Giants), and God always wished to wipe away hii jamii ya watu. Alifanya jambo la kwanza kuwaondoa kupitia Noah's flood (gharika), mafanikio hayakuwa ya 100%, maana kwenye safina shetani alikuwa amekwisha penyeza uzao wa kijitu kupitia wakweze Nuhu, na hivyo katika hawa watoto wa Nuhu yaani Ham na Yafeti wote walikuja kuzaa majitu kwa mujibu wa Historia, kasoro Shemu tu (babu wa Yesu)... Ukweli huu unatupia nje dhana zote kuhusu *Double Incursions* kwamba wale Wanefili tunaowaona katika Hesabu 13, ni uvamizi mwingine wa majitu katika dunia... Wale wote ni products za kizazi cha Nuhu fuatilia vizuri vizazi katika *Mwanzo 10*, ... Haya majitu (giants) hawajawahi kuwa wema wala kuwa na tabia za maadili, kila unapotaja Majitu una *Moral Depravity* kila ubaya ulibuniwa na hii jamii ya watu. Na vyanzo vinaonesha miongoni mwa mambo yalimfanya Mungu aandae mpango wa kuitoesha kabisa hii jamii (it was His dream that one day giant-races are all extirpated)... Miongoni mwa mambo yalichochea sana urafiki wa Mungu na Daudi, ni pamoja na Daudi kwa kutumia watu wake wenye nguvu kushambulia masalia ya majitu.
⚖ Kuhusu kizazi cha nne, ambapo tafsiri nyingi za kingereza zimesema *In the fourth generation*, kuna dhana kazaa hapo kati... Kwanza neno la kiEbrania kwenye kizazi limetumika *dowr/dor* katika kiYunani wameweka neno *genea* ikiwa inafanana kabisa na maana ya kiRumi ya neno *Soeculum/Seculum* lenye maana ya Century hivyo ikitujuza kuwa kizazi kimoja kiko denoted na miaka 100 (kuna mjadala mpana kwamba hilo neno huashiria miaka 30/40, that discussion is purposely excluded in this topic ili niwe focused na jambo moja...). Hivyo kuna uwezekano wa kwanza kuwa vizazi vinne ni vya Ibrahim, ambapo vyanzo vingi vimekubaliana kuwa ni kuanzia kwa Lawi, Kohath, Amram, hadi Musa/Haruni.. (alternatively tukianzia kwa Yuda kizazi cha nne ni Kaleb)... Hili limehusianishwa na miaka 400 aliyoisema Mungu hapo nyuma kidogo yaani (Mwanzo 15:13)
Lakini pia inaweza kuwa vizazi vinne vya waamori (more probable) kwa sababu ya mfuatano wa hoja katika sentensi, kama tusomavyo hapa Mwanzo 15:16
_*"Lakini nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini naliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini."*_
(Amosi 2:9)
*MUNGU WA HAKI, ALISUBIRI KIKOMBE KIJAE, AKA-ANNIHILATE JAMII YA WAOVU, NA ARDHI YAO AKAWAPA TAIFA LA ISRAEL AKIWAONYA MBELE KUWA WASHIKE SHERIA ZAKE, ISIJE NCHI YA KANAANI IKAWATAPIKA KAMA ILIVYOTAPIKA MAJITU. AMBAO UOVU WAO ULIJAZA KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU. WALE WAPELELEZI KUMI WALIOLETA TAARIFA MBAYA, HAWAKUDANGANYA, NI KWAMBA TU HAWAKUMPENDEZA MUNGU KWA KUWA NA WOGA, ILA WALIONA MAJITU KWELI, KWAMBA WALIONA NCHI ILE IKILA WATU, NI TABIA ZA MAJITU KULA WATU WA KAWAIDA, TABIA HIYO WALIIFANYA ZAMA ZA YAREDI MPAKA NUHU, NA KIPINDI HIKI TENA WALIIRUDIA HIYO TABIA, NA MUNGU AKAWAWEKA AKIBA KAMA VYOMBO VYA GHADHABU, AKASUBIRI UOVU WA WAAMORI UTIMIE, AKASHUSHA HUKUMU*
Mungu akubariki msomaji wangu unapoendelea kufuatilia masomo haya kuongeza maarifa ya Neno la Mungu ndani yako..
Pokea ufahamu wa Neno la Mungu (Katalambano ✋🏾)
Mwl Proo
*0762879363*
alltruth5ministries@gmail.com
Asante Sana Sasa mtumishi wa MUNGU, Ila nisaide hapa, najiuliza kulikuwa na umuhimu gani? Wa MUNGU kuwapeleka utumwani? ili huo uovu utimie..?
ReplyDeleteI guess Mungu ni WA REHEMA ni sawa na jinsi alivyoenda sodoma na gomora ili aangalie uovu wao na kitendo cha kwenda yy ni kuona kama watamsikia na kutubu ndio kwanza wakaanza kutaka kuzini hata na malaika.. kadhalika kitendo cha kubuy time ni sawa na kusema niwape muda kama watabadilika basi angeandaa ajenda nyingine Mungu lakin mwanadam hatuko tayari kuacha ouvu pale dhambi inapokuwa imeingia mwilini wakt mwingine mpka kwenye damu. Basi huo ukawa utimilofu wa Mungu kuondoa hicho kizazi.
DeleteNaomba nipoze swali apa...mwalim umeongelea juu ya wanefili...mwanzo 6 inaelezea hao watu kuwa Wana wa Mungu waliwapenda Wake wa binadam lakin inasema nao wanefili walikuweko siku zile..je apo mwanzo hao walitokea wap?.. maana badae umeonyesha hiyo MBEGU ni kutokea wakwe wa Nuhu..je kbla walitokea wap