*π
π
π
π
π
π
π
π
€π
π
, π
π
π
π
π
‘π
€, π
π
π
’π
π
π
€ ❷,❸⓿⓿*
*_The Ram, The He-Goat, And The 2,300 Days_*
*DANIEL 8:1-27*
*ΚΥ‘Σ ΤΉΙΎΦ
Φ
*
*0762879363*
Shalom Aleichem!!
Nawakaribisha katika mwendelezo wa masomo ya awali, yanayotuandaa katika masomo ya matukio ya siku za mwisho, siku chache zijazo. Mungu ameweka moyoni mwangu kuanza na ufafanuzi wa moja ya vitabu vya ufunuo wa siku za mwisho (Apocalyptic Books For Eschatological Events).
Daniel aliona maono haya mwaka wa tatu wa kutawala kwake Belshaza, akiwa Shushani (Susa) miaka mitatu baada ya maono ya wanyama wanne. Hii desturi ya Mungu kuja kusema kuhusu jambo mara ya pili na ya tatu (Ayubu 33:14-16), ili kutia mkazo wa utimilifu wa unabii au ujumbe wake ambao unakaribia utimilifu wake, na akiurudia anaweza kuuleta kwa lugha pana ya kueleweka (with intricacy).
*1️⃣ DONDOO ZA DANIEL 8*
*❶. KONDOO-MUME/ THE RAM*
π Daniel aliona kondoo-mume mwenye pembe mbili, lakini pembe moja ndefu zaidi. Kisha anasema, *"Akisukuma upande wa magharibi, na kaskazini, na kusini"*
*❷. BEBERU/ HE-GOAT*
π Daniel alipokuwa akifikiri kuhusu yule kondoo-mume akatokea beberu toka magharibi mwenye pembe mbili pia.
ππ Huyu beberu akamwonea hasira kali yule kondoo, akamshambulia. Badala ya huyu beberu zikazuka pembe nne...
π Kutoka katika moja ya zile pembe nne ikazuka pembe ndogo, ambayo badae ilikuwa sana.
π Pembe hii ndogo imetajwa kwa sifa nyingi ambazo nitazijadili sehemu inayofuata kuhusu tafsiri. Lakini miongoni mwa mambo yalifanya na pembe hii ndogo ni kuondoa au kukomesha sadaka ya kutekezwa, patakatifu kukanyagwa na kuangushwa
*❸. SIKU 2,300 (2,300 EVENINGS & MORNINGS)*
π Swali linaulizwa mastari wa 14 kwamba hayo matukio yatachukua muda gani, yaani tangu kukomeshwa kwa dhabihu (daily sacrifice) mpaka kutakaswa kwa patakatifu (Cleansing of the sanctuary), jibu likatolewa kuwa jioni na asubuhi 2,300 (complete 24h-hours day). Mstari wa 17 (v17) Daniel anajuzwa kuwa maono hayo ni ya wakati wa mwisho,. Ndugu msomaji najaribu kurahisisha uelewa wa hiki kitu hivyo kuna mambo sijayaweka kwa summary nitayaweka na kuyawekea tafsiri yake moja kwa moja.
_mwlproo_
*2️⃣ TAFSIRI/INTERPRETATION*
π€΄πΎ Kuanzia mstari wa 16 Daniel anasema alisikia sauti ya mwanadamu ikimwagiza malaika Gabriel amfahamishe maana ya yale aliyoyaona. Mstari wa 20 inatolewa tafsiri.
*❶. KONDOO MUME (RAM)*
π€΄πΎ Kondoo mume mwenye pembe mbili aliwakilisha utawala wa Umedi-Uajemi (Pembe mbili ziliwakilisha wafalme wawili, two horns ππΎ kings of Media/Persia). Pembe ya pili (Persia/Ajemi) ilikuwa kubwa kuliko ya kwanza (Umedi) na ndivyo ilivyokuwa. Ikumbukwe Daniel mtumishi wa Mungu alikwishajua kwamba Babeli inaenda kuanguka. Na yeye ni waziri katika serikali hiyo hiyo inayoenda kuanguka, maana alioneshwa mambo haya mapema sana katika utawala wa Belshaza. Belshazzar hakuingia madarakani mara baada ya Nebukadreza, ilipita miaka mingi sana hapo kati Babeli ikiwa chini ya Evil-Merodaki, bado haijajulikana sana sababu za Daniel kutoandika matukio ya wakati huo wote. Jambo jingine hapo ni kwamba watumishi wa Mungu manabii, kama hawatajihusisha na siasa kwa ushabiki na mihemko ya kibinadamu, wanatoa nafasi nzuri kwa Mungu kuwajuza kila kinachoenda kutokea. Daniel aliendelea kufanya kazi za mfalme kwa utii na kicho, huku akijua six years to come hakuna kitu kitabaki mikononi mwa Babeli
π€΄πΎ Mstari wa 4 anasema alimwoma Kondoo akisukuma pande kadhaa za dunia... Ni muhimu kufahamu kufahamu maeneo ambayo nabii ameyataja tu kusini au kaskazini..Mfano magharibi ilitaja maeneo ya kiutalawa (Mesapotamia, Syria, Minor Asia), kisha kaskazini yaani Colchis, Armenia, Iberia, Caspian Sea, na kisha kusini yaani Judea, Egypt, Ethiopia, Libya, na India pia (wakati wa Dario), Mashariki haijatajwa maana Uajemi yenyewe ndiyo mashariki (Isaya 46:11)
_mwlproo_
*❷. BEBERU (HE-GOAT)*
π€΄πΎ Daniel alimwona Beberu π tokea magharibi akiwakilisha mfalme wa Uyunani (King of Grecia), anatajwa kuwa pembe kubwa (mfalme wake wa Kwanza) tafsiri chache zikimtaja King Philip (Grecian King), na vyanzo kadhaa vimemjadili Caranus mfalme wa Macedonia, lakini kwa yanatojwa hapo yako dhahiri wakati wa utimilifu wake kuwa aliyetajwa hapo ni Alexander the Great (Iskanda Mkuu), mstari wa tano umetaja kitu cha ajabu (v5) yaani huyu Beberu anaeza akaenda bila kugusa nchi, ikiwa inazungumzia *swiftness* sifa ya Alexander katika conquests zake zote za kivita. Na utaona Beberu ana sifa zilezile za Chui/Leopard tuliyejifunza somo lililotangulia (Daniel 7:6). Haya yanathibitishwa na simulizi ya namna Alexander alivyovamia Medo-Persia mwaka 331BC na kumshinda Darius Codomanus.
_mwlproo_
*❸. PEMBE NNE/ THE FOUR HORNS*
π€΄πΎ Pembe nne zilizozuka zinawakilisha falme nne, kama tu yule Chui (Uyunani) tuliyemwona kuwa na vichwa vinne katika somo letu lililopita (jitahidi ulipate, liko mtandaoni) vichwa vinne viliwakilisha watawala-warithi (successors of Diadochi kingdoms), ambapo popular interpretation inatuambia ni Cassender, Lysimachus, Ptolemy na Seleucus. (Haya siyajadili kwa kina hapa maana yako kwa masomo yaliyotangulia).
*❹. PEMBE NDOGO/LITTLE HORN*
π€΄πΎ Daniel anaitaja pembe ndogo ambayo badae ilikuwa kubwa sana kuelekea kusini. Ni nani huyu pembe ndogo? Pembe ndogo ametajwa na sifa ambazo sifa kadha wa kadha zinaweza kumwakiliha mfalme aliyetokea kwa Seleucus ambaye ni Antiocus Epiphanes kwa popular interpretation imekubaliwa lakini bado ziko sifa na matendo ambayo yanamwondoa Antiochus na kumweka hapo mpinga kristo.
π Alternative ya kwanza ya kuzilinganisha pembe nne zilizozuka kama watawala wanne walimrithi Iskanda Mkuu, inaonekana Antiochus Epiphanes anafit kuwa mlengwa wa unabii. Lakini yako mambo kadhaa yanayotuambia si yeye. Mfano ufalme wa Mungu ulipaswa kuwa established mara baada ya pembe ndogo hapa duniani, ambapo mwaka 164 BC alipokuwa Epiphanes hayakufanyika hayo. Pembe ndogo ya Daniel 7 na Daniel 8 inaonekana kutaja kitu kimoja (Identical). Antiochus hakutimiza nabii zote za pembe ndogo, ikiwemo kupaangusha patakatifu (casting down of the sanctuary), na kuna swala jingine kuhusu warithi wanne wa Iskanda, inasadikika uwepo wa washindani karibu na nane na tawala tatu (hili tuliacha kuepusha mjadala mrefu)..Ukiachana na sababu hizi... Pembe ndogo inatajwa kuwa na uso mkali (fierce countenance), afahamuye mafumbo (understanding dark sentences), kuwaangamiza walio hodari na watakatifu. Pia pembe ndogo atashindana na aliye Mkuu wa wakuu (Jesus is the Prince of princes), then huyu pembe atavunjika bila kazi ya mikono (rejea somo letu la Ndoto ya Nebukadreza kuhusu Jiwe lililoponda miguu). Hizi sifa ambazo zimewekwa hapa zinamwondoa tena Epiphanea Antiochus katika nafasi... Alternative ya pili ni kwamba pembe nne zinapaswa kuwekwa parallel na tawala kuu nne za dunia sawa na sanamu ya Nebukadreza, pia maono ya Daniel kuhusu wanyama wa nne. Na hivyo kwa alternative hii pembe mdogo (mpinga kristo) atatokea baada ya utawala wa nne (miguu ya chuma) au mnyama wa kutisha. Ila hili sio hitimisho, tuendelee mbele kidogo.
_mwlproo_
*❺. SIKU 2,300 (2,300 EVENINGS & MORNINGS)*
π Miongoni mwa mambo yamefanya unabii wa Daniel 8 kuwa mgumu ni pamoja na hii *cipher* ya siku 2,300. Nikiri wazi kuwa hapa ndipo mahali ambapo waandishi wengi wameparuka na kutoandikia chochote (No comments).
Naomba niliweke tena andiko hili Daniel 8:13-14
(Danieli 8 )
------------
*13 Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi?*
*14 Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.*
HUU MUDA WA KUONDOLEWA KWA SADAKA YA KUTEKETEZWA NA YALE MACHUKIZO MENGINE YA PATAKATIFU MPAKA WAKATI WA KUTAKASWA KWA PATAKATIFU, IMEBAKI MJADALA MREFU, LAKINI LEO NITAWEKA NURU KIDOGO ITAKAYOKUPA KUJIFUNZA KWA JICHO JINGINE SWALA HILI.
_mwlproo_
*❻. UCHAMBUZI WA KINA KUHUSU SIKU 2,300*
π Moja ya tatizo kubwa la kithiolojia katika uchambuzi wa maandiko ni pale ambapo ufafanuzi unajiegemeza kwenye dhana au shule ya mawazo ya kidhehebu na imani ya kikanisa. Tatizo hili liko mpaka sasa kila panapotokea ufafanuzi wa maandiko hasa kwa haya ya matukio ya siku za mwisho.
π Katika kujifunza jambo hili nilitamani kujua commentators wakuu katika historia waliojitia kuzungumzia swala hili ambapo mafafanuzi ya wengine wote yamejiegemeza kwa moja ya watu hao. Hatuwezi kumwacha mtu aitwaye Dr C.I Scofield (msomi mkubwa wa kimaandiko wa kiProtestant) na ndugu William Miller (mchungaji wa kiBaptist) ambaye mafundisho yake na mafafanuzi yake ya mafunuo ndiyo yanaweka msingi mkubwa wa mafundisho ya Seventh Day Adventist baada ya kufanyiwa refinement kidogo na ndugu Hiram Edson na Bi Ellen G. White hasa baada ya baadhi ya mabashiri yake kukosea (predictions proved fault).
π Tatizo la kimahesabu la kwanza kutoka kwa hawa watu wawili (Scofield) na (Miller) ni kwamba, kanuni ipi itumike kuhesabu siku 2,300? Je! hesabu hiyo ianzie lini? Ikumbukwe kila kinachofundishwa na Protestant Churches kwa asilimia kubwa ni cementations za Scofield juu ya mafundisho ambayo naye aliyafanyia tu refinement toka kwa Catholic preacher (Jesuit Scholar) aitwaye Francisco Ribera (1537-1591)... Ambapo Scofield alichukua mawazo yake akaboresha machache kwa kuongeza wazo la *Pre-Second Coming Rapture* na mawazo hayo yalikuja kuingizwa rasmi kwenye *British Albury Park Conferences (1826-30)* nayasema haya ili ujue muda waProtestant na waPentekoste wanafundisha kanisa kuondolewa kabla ya mpinga kristo ni mawazo ya karne ya 16 (ya Catholic Jesuit scholar) na kufanyiwa maboresho karne ya 19 ).. Ikumbukwe pia ni wazo hili ndilo ambalo lilifanya juma moja la sabini katika majuma 70 liwekwe wakati wa mpinga kristo likiwa limetangwa na yale majuma 69 na gepu hapo kati lijulikanalo kama *Dispensation of the Christian Church*.
Na upande wa pili wa mafafanuzi ya siku 2,300 ni yale yaliyotoka kwa William Miller (Baptist Priest)... Ambapo mafafanuzi ya mafunuo ya Daniel yanavyoelezwa na SDA church asilimia kubwa ni yale yaliyowekwa kwanza na Miller.
*❼. MAWAZO YA SCOFIELD JUU YA SIKU 2,300 NA PEMBE NDOGO*
ππ€΄πΎ Mawazo makuu ya Scofield ni kwamba pembe ndogo ni Epiphanes Antiochus IV na siku 2,300 zote zinatimia katika kipindi chake. Kanuni ya kinabii ya *Day-Year Theory* ile ya kila siku moja ni mwaka mmoja, haikutumiwa na Scofield katika swala la siku 2,300 ingawa naye ameitumia kanuni hiyo kwenye majuma 70 ya Daniel 9, ambapo nimefafanua katika somo langu la Majuma Sabini. Ni kweli kwa mujibu wa historia na vitabu vya apocryphal (apocryphal writings) vimethibitisha mambo yaliyofanywa na Epiphany kwa sehemu yanatoshea kile kinaelezwa kuhusu pembe ndogo. Aliwaudhi Wayahudi, alilinajisi hekalu kiasi cha kuchinja nguruwe patakatifu... Makabayo 1:20-50 (Inaeleza juu ya kukomeshwa kwa dhabihu). Hivyo hesabu iko hivi December 6, 167BC (Desecration of the temple ) ndipo mahali Scofield alibenchmark mwanzo wa siku 2,300 na kuishia March 27, 160BC wakati ambapo Komando Nicanor aliuawa, maana hata baada ya Antiochus kufa hakukuwa na shwari mpaka alipouawa Nicanor. Kuanzia 167 mpaka 160 kuna siku 2,300 kwa kutumia lunar year (360) according to Scofield
yaani 360+360+360+360+360+360 +110=2,270
maanake kuna miaka 6 na siku 110
Ili zitimia siku siku 2,300 waliongeza siku 30 kufidia siku wa kalenda (Adjustment of 7 year calendar) haya mambo ya kufix tarehe za kalenda yako katika masomo yangu mengine. Hivyo kwa mujibu wa Scofield siku 2,300 ni siku 2,300 wala sio fumbo la miaka.
*❽. MAWAZO YA MILLER KUHUSU SIKU 2,300 NA PEMBE NDOGO*
ππ€΄πΎ William Miller, katika hesabu zake ali-maintain matumizi ya kinabii ya Hesabu 14:34 & Ezekiel 4:6 yaani *Day-Year Theory* hivyo siku 2,300 zinakuwa miaka 2,300. Na hivyo kuweka madai kuwa huu ndio unabii mrefu kuliko zote katika Biblia kuhusu wakati wa mwisho. Lini zihesabiwe siku hizi. Miller alifafanua kuwa unabii wa Daniel 8 unapaswa kuanza parallel na majuma 70 ya Daniel 9, hivyo mwaka ule ule 457BC wa Barua ya Artashasta Longimanus ndio umetumika pia kuhesabu miaka hii pia.
HESABU YA MILLER:
2,300-490= 1,810, Kisha miaka 1,810 inajumlishwa kwa 34 (34AD mwaka wa masihi mkuu kukatiliwa mbali). Hivyo 1,810+34=1844
Na ndipo akaset dhana za Kurudi kwa Kristo mara ya pili kwa mwaka huo (kusafisha patakatifu)... Wazo ambao badae akina Hiram Edson na Ellen White walilibadilisha kwa maana halikutimia, ndipo ikaingizwa concept ya *Hukumu ya upelelezi/investigative judgement* mambo ambayo yatajadiliwa katika masomo yetu yanayofuata. Ufafanuzi mwingi wa kuhusu pembe ndogo na mpinga kristo ambaye alichomekwa Papa wa kikatoliki, hayatajumuishwa katika somo hili.
*❾. π
π
π
£π
π
π
π
’π
π
*
Commentaries za Biblia zilizopo zimelalia kwenye moja ya dhana either za Scofield au Miller kwa sehemu kubwa. Lakini kuna kitu kinaonekana katika sifa za pembe ndogo, zilimzungumzia Antiochus IV (Epiphanes), kama picha ya mpinga kristo atakayekuja, na ndio maana kuna sifa Antiochus hana na kuna nabii hajazitimiza. Nimependa wazo la moja ya commentary iitwayo John Gill's Exposition ambapo hesabu za miaka 6 na siku 110 (2,300 days) wamesema ni lugha ya kinabii kumaanisha miaka mingi itakayoishia kwenye milenia ya sita (sixth millennium or thereabout) kwamba pembe ndogo itazuka na kutimiliza yote yaliyo katika unabii. Antiochus ni uvuli wa mpinga kristo kwa agano la kale, lakini anatazamiwa mpinga kristo atakayeyatimiza hayo yote, maana unabii uliotiwa muhuri unajulikana sana muda wa utimilifu wake.
Sura zilizobaki katika Daniel yaani 10&11&12 zitajadiliwa katika masomo ya kitabu cha ufunuo kuhusu matukio ya siku za mwisho.
Ubarikiwe na Bwana, naamini umepata mwanga wa kuanza kujifunza kitabu cha Daniel kwa mtazamo mwingine.
*Mwl Proo*
0762879363
alltruth5ministries@gmail.com