Wednesday, April 22, 2020

WANYAMA WANNE (DANIEL 7)

*πŸ…¦πŸ…πŸ…πŸ…¨πŸ…πŸ…œπŸ… πŸ…¦πŸ…πŸ…πŸ…πŸ…”*
*Four Beasts In Daniel 7*

*ʍՑӀ ΤΉΙΎΦ…Φ…*
+255762879363

*1⃣ UTANGULIZI*
Neema, amani, uzima  baraka, na ushindi toka Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ziwafunike. Namwomba Mungu kwamba awatunze, awahifadhi, na kuwanusuru na tauni za nyakati hizi za mwisho. Amini Mungu kuwa mtalindwa salama, kwa Jina la Yesu.
Nakukaribisha kujifunza kweli ya neno la Mungu, muhimu kwa majira yetu.
Daniel na Ufunuo wa Yohana ni vitabu vimeongea mambo yote muhimu kwa nyakati za mwisho, hizi tuko nazo.. Ni muhimu kuelewa, na usiache kufuatilia mfululizo wa masomo haya. Nashauri kama hujasoma masomo yaliyotangulia ya Daniel 2&9 basi hakikisha unayapata hayo pia.

☄ Danieli anasimulia kwa kuandika ndoto na maono aliyoyaona mwanzoni mwa kutawala kwa Belshazzar mfalme wa Babeli. Maono haya  yaliyorekodiwa katika sura ya saba aliyaona kati ya mwaka 556BC--553BC. Mpangilio wa sura katika kitabu hiki haukufuata muda, ndio maana sura ya 6 unaona Dario ni mtawala, lakini sura ya saba anatajwa Belshaza aliyekufa sura ya 5

☄ Mafunuo waliyoyaona Daniel na Yohana mtume yana accuracy ya 100% bila kuhitaji estimation. Maandiko yao yanakubaliana 100% yenyewe kwa yenyewe huku yakikubaliana na maandiko mengine ya Biblia nzima yaliyogusia habari sawa.

☄ Usifanye kosa la kutafsiri andiko la unabii pahala pamoja kwa kuwa unaona linafaa hapo, huku linakataa kufaa pengine. Ni lazima maandiko hasa ya unabii yakubaliane kote, we don't just pick a verse and fix it where we want because it sounds good to us kuweko hapo, hapana!!!!.

*NB:*
*KWA NINI MAFUMBO YA NAMBA, VITU, WANYAMA N.K VITUMIKE KUSEMA UJUMBE WA KINABII (WHY SYMBOLISMS IN PROPHETIC WRITINGS?) SABABU YA KWANZA NI KULIFANYA JAMBO LIELEWEKE ZAIDI (FAMILIARITY), KAMA ATATAJWA MNYAMA BASI ATATAJWA AMBAYE JAMII YA HADHIRA INAMWELEWA NA KUMFAHAMU SANA,NA MNYAMA HUSIKA ATAWAKILISHA TABIA ZA UFALME HUSIKA NA MFALME HUSIKA YESU ALIPOSEMA KAMWAMBIENI YULE MBWEHA LEO NA KESHO NATENDA MIUJIZA NA SIKU YA TATU NITATHIBITIKA, HAKUWA ANATUDUNDISHA KUTUKANA VIONGOZI, BALI ALIJUA UFALME ULE UNAONGOZWA NA ROHO YA MBWEHA KIROHO, BASI ZIKITAFUTWA TABIA ZA MBWEHA ZITAONEKANA ZOTE KWA MTAWALA HUSIKA.  NA PIA KUFANYA WATU WAUTAFUTE UKWELI, MFANO AKITAJWA NYOKA KUMWAKILISHA SHETANI, HUO NI UKWELI/SIRI INAYOJULIKANA NA BIBLIA YENYEWE THROUGH THE ENTIRE SCRIPTURAL TEXT. PIA MAFUMBO HUTUMIKA KUFICHA MAANA ILI KUMLINDA MWANDISHI NA MAANDIKO YENYEWE. MFANO YOHANA MTUME ALIONA JAMBO KUHUSU RUMI KUANGUKA AKAITAJA KATIKA UFUNUO KAMA BABEL (MYSTERY BABYLON) (SHIKA HII KICHWANI KUWA KINABII KUNA BABELI YA KISIASA/POLITICAL BABYLON πŸ‘‰πŸΌINAYOJUMUISHA SYRIA+LEBANON+IRAQ) NA BABELI YA KIDINI/RELIGIOUS BABYLON (RUMI/ROME). HIVYO KAMA YOHANA MTUME ANGEITAJA RUMI KWA UWAZI HIVYO, KITABU CHAKE KINGEHESABIWA KAMA DOCUMENT YA KISIASA KINYUME NA DOLA INAYOTAWALA, HUENDA ANGENYONGWA ALIPOTOKA PATIMO, NA WAKATI KAMA ULE DIOCLETIAN ALIPOTANGAZA VITABU VITUKU (SACRED BOOKS) VYOTE VITIWE MOTO, UFUNUO KINGEKUWA CHA KWANZA. HIVYO MUNGU ALIMTAJIA BABEL KWA FUMBO, KUMLINDA MWANDISHI NA MAANDIKO YENYEWE.*

*2⃣ NDOTO NA MAONO YA DANIEL KUHUSU WANYAMA WANNE*

☄ Daniel aliota na kuona ndoto na maono. Katika sura ya saba anajaribu kutuambia haikua zote kwa mara moja, mstari wa 2, wa 7, na wa 13. Na hivyo tunaweza pata mgawanyo wa sehemu tatu za maono yake, sehemu ya kwanza anaona wanyama watatu, sehemu ya pili anamwona mnyama wa nne, na sehemu ya tatu anaona mmoja aliye na mfano wa mwanadamu akija na mawingu ya mbingu.
_mwlproo_

☄ Daniel anaoneshwa kitu kilekile tulichojifunza  katika somo lililopita la Daniel sura ya 2. Nebukadreza alioneshwa tawala nne za dunia kwa kielelezo cha sanamu ya mtu na utawala wa mwisho wa Masihi Mkuu Yesu aliyeonekana kama jiwe lililochongwa mlimani likivunja utawala wa kibinadamu, na Danieli sasa anaoneshwa kitu kilekile, wanyama wanne wakionesha tawala za dunia mpaka wakati wa mpinga kristo na utawala wa mwisho wa Yesu Kristo duniani, kisha katika mbingu na nchi mpya.

☄ Daniel anatueleza kuhusu pepo nne za mbinguni kuvuma, na kisha kutoka katika bahari kubwa wanatoka wanyama (moja ya vyanzo vya kithiolojia vimejadili pepo nne za dunia kama _agitations of political sea_ iko hivi wanyama wanaotajwa ni wafalme/tawala kwa mujibu wa Daniel 7:17, tawala hizi zote zilipatikana kwa njia za mapinduzi ya kisiasa na uvamizi wa kivita, utawala wowote una grounds za kisiasa au za kidini ndivyo historia inavyoonesha, na hiyo ndio sababu ya wanyama katika Daniel na Ufunuo kutoka either katika bahari au katika nchi, bahari inataja mataifa, jamaa, kabila za watu na lugha (Ufunuo 17:15 pia ona Ufunuo 13:1, Luka 21:25, Yer 46:7,8). Na hivi ndivyo itakavyokuwa kwa mpinga kristo na nabii wa uongo, wakati mpinga kristo (mnyama wa I, Ufunuo 13:1) atatoka katika bahari (political sea), nabii wa uongo (mnyama wa II, Ufunuo 13:11) atatoka katika nchi (religious grounds).
_mwlproo_

*❶  SIMBA/LION* 🦁
☄ Mnyama wa kwanza kumwona alikuwa simba, huyu ni kama kile kichwa cha dhahabu katika sanamu ya Nebukadreza. Na Simba huyu mwenye mabawa ya tai, aliwakilisha utawala wa Babeli. Nebukadreza na Babeli mara kadhaa ililinganishwa na simba katika maandiko ya unabii yakitaja nguvu yake na ari yake, na hali yake ya kivita (Yer 4:7)...utawala ulioanza kutawala  dunia mwaka 606 BC mpaka 539BC, kinabii tawala hizi zina-exist maana zitakuja kuinuka tena (nitalifafanua hili mbele kidogo)

*❷  DUBU/BEAR* 🐻
☄ Dubu (the all-devouring animal) aliwakilisha Waajemi (Persians).. Tabia za Dubu maisha ya milimani, ukatili, ni sifa ya utawala wa kiajemi (Isaya 13:17, 18)... Watawala wawili wakiAjemi kama Cambyses, na Ochus walikuwa wakatili sana wakisadifu sifa za dubu 100%, unaweza ukaona namna mtu akikiuka sheria za kiajemi (Daniel 6:24) sio tu yeye atashughulikiwa, bali wanabeba na wake zako, na watoto wote mnanywea kikombe cha ghadhabu ya kiajemi. Ametajwa kuwa na meno ambayo kwayo anaweza akayashughulikia mataifa (subjugate many nations) na ana mbavu tatu mdomoni, zikiwa zinawakilisha mataifa matatu aliyoyafanyia ukatili wakati wa kuingia kwake katika kushika hatamu yaani  Egypt, Lydia, na Babeli

*❸ CHUI/LEOPARD*
Chui ni mdogo kuliko simba, ila mwenye kasi zaidi (Swiftness) Habakuki 1:8, pia ana ukali (cruelty) Isaya 11:6... Huyu chui alimwakilisha mtawala wa Uyunani Iskanda Mkuu (Alexander the Great) na utawala wake... alikuwa na mabawa manne huyu chui, pia alikuwa na vichwa vinne 🐯🐯🐯🐯 ... Vichwa vinne (Daniel 8:8, 22) tunaita Kingdoms of Diadochi (successors)... Himaya ya Iskanda mkuu iligawanyika maeneo manne ya utawala baada ya kifo chake, chini ya majemadari wake wanne ndivyo hivyo vichwa vinne. Himaya nne ni hizi (Macedon+Greece) zikisimamiwa na Cassender, pia (Thrace na Bithynia) zikiwa chini ya Lysimachus, na kisha Egyptikiwa chini ya Ptolemy, na kisha Syria chini ya Seleucus. Alexander Mkuu wa Macedon alikuwa na sifa chui katika mapambano kama chui awapo katika mawindo, na ndiye alimshambulia Dario mwajemi, na aliyatia mataifa haya katika kitanzi chake kwa miaka 12, yaani Europe, Asia, Illyricum, Adriatic, Ganges. Rejea somo langu liitwalo *Falme na Mamlaka* Alexander hakupata utawala huu kwa nguvu zake bali Mungu wa nyakati aliruhusu, maana haingewezekana jeshi lake la askari 3,000 kushinda yale majeshi yenye malaki ya askari.  Mwanahistoria Josephus (katika kitabu chake cha Antiquities) anasema Alexander aliwahi msimulia kuhani wa Yerusalemu kuwa akiwa kwake aliwahiona maono Mungu akimruhusu kwenda Asia na hayo maeneo mengine kuwa atashinda.

*❹ MNYAMA WA NNE*
Wakati ndoto ya Nebukadreza ilionesha utawala wa Rumi kama miguu ya chuma, Maono ya Daniel yalikosa mnyama halisi wa kumfananishia na utawala wa Rumi. Hivyo akasema aliona mnyama mwenye kutisha, mwenye nguvu, ana meno ya chuma (teeth of iron) ikifanana kidogo na material ya miguu ya sanamu ya Nebukadreza. Kisha mnyama huyu alionekana kuwa na pembe kumi, na kisha pembe ndogo itakayoinuka na kujing'oa pembe tatu katika hizo. Mnyama huyu wa nne yuko tofauti kabisa na wale watatu. Na hivyo fuatana nami sehemu ya tatu, ambayo nitachambua kwa kina kuhusu mnyama wa nne anayewakilisha utawala wa nne

*3⃣ UFALME WA NNE NA PEMBE KUMI*
☄ Ndoto ya Nebukadreza na maono ya Daniel vinakubaliana kuwa utawala wa tano utakuwa ni wa Mwana wa Mungu kuja kuuvunja utawala wa kibinadamu. Nebukadreza hakuona mwendelezo kamili wa utawala wa nne kuwa mwishoni kuna mpinga kristo. Daniel katika nafasi yake kama nabii akaona kitu cha ziada kikubwa. Wakati Nebukadreza aliona jiwe (Yesu) litakuja wakati wa utawala wa dola kumi (10 toes), Daniel anamwona mnyama wa nne akiwa na pembe kumi, zikiwalilosja watawala 10 (Daniel 7:24) horns=powers.. ambayo kwa hatua ya kwanza twaweza yatambua kama Roman Kingdom with Germanic & Slavonic tribes (wakati wa Reformation), ikumbukwe kuwa Empire ya magharibi mwa Rumi iliendelea mpaka 731AD, na ya mashariki mpaka 1453AD,

☄ Vidole kumi vinawakilisha falme kumi (Daniel 2:41, Ufunuo 13:1, 17:12). Daniel na Yohana Mtume katika Ufunuo, wanakubaliana pia kuwa utawala wa mpinga kristo utaingia katika wakati wa utawala wa hizo dola kumi. Lazima kutakuwa na mataifa makubwa 10 (makubwa kinabii kisha kisiasa, kiuchumi, kinguvu  etc) ambazo zitaHand over nguvu zao kwa mpinga kristo. Unapoendelea kujifunza maswala haya ya kinabii kuna kila sababu ya kuyafahamu baadhi ya mataifa yanayoambatana na unabii wa siku za mwisho. Mataifa hayo ni Iraq, Syria, Lebanon, Iran, Ethiopia, Egypt, Greece, Turkey, Israel, Russia (Haijalishi taifa litaonekana dhaifu sasa, muda wa unabii kutimia unapokuja kila kitu kitajiweka kwa nafasi. Kuna mataifa yanaweza kuwa na vurugu sasa na nguvu kubwa ila hayako katika unabii wa maandiko, na huenda muda huo ukifika yakawa yamepoteza nguvu na umashuhuri wake kabisa. Lakini pia hifadhi akilini mwako mataifa haya saba au serikali saba zinazowakilisha vichwa saba vya joka au vya yule mnyama (Ufunuo 12:3, 13:1) the seven world empires (7 heads) yaani Egyptian , Assyrian, Roman, Mid-Persia, Greece, Babylon, Anglo-America.
_mwlproo_

*❶  PEMBE NDOGO/LITTLE HORN*
☄ Daniel na Ufunuo wa Yohana vinawezwa kuangaliwa kwa pamoja kwa maswala haya, maana vimetaja kila kitu sawa, swala pembe kumi, vichwa saba. Linakuwa dhahiri sana kuhusu utawala wa mpinga kristo duniani na serikali za dunia zitakazomuunga mkono. Pembe ndogo inaonekana wazi katika maandiko kuwa ni mpinga kristo, ambayo imetajwa katika Daniel na katika Ufunuo kuwa muda wa operation yake ni miaka mitatu na nusu  (1260 days) (soma Ufunuo 12:6, 13:1, 17:11, 1214, 16, 13, 14, 16, 2Thes 2:3). Pembe ndogo inaonekana kuziondoa pembe tatu katika 10, na hivyo kufanya serikali saba za mataifa pamoja na ya nane ambayo ni hiyo pembe ndogo (Ufunuo 17:11), lakini ikumbukwe katika Daniel mnyama wa nne aliondoa wale watatu wa mwanzo ila uhai wao (verse 12) ulihifadhiwa.  Pembe ndogo inatajwa kuwa na kinywa, inatajwa kuwa na macho ya mwanadamu ikiwa inaashiria intelligence (Ezekiel 1:18, Mwanzo 3:5), na atakuja akiwa na mfano wa Kristo (Caricature of Christ). Pembe ndogo ataitawala dunia kwa hekima kubwa ya kidunia na kufanya civilization kubwa kuwahi kutokea katika historia ya mwanadamu na ataileta dunia yote chini ya utawala wake (verse 23). Ndicho kipindi ambacho utawala utajiweka kinyume na Mungu sana (Atheism, Antitheisism, and Autotheisism). Pembe ndogo atanena makufuru kinyume na Mungu kama alivyoona Daniel na kama alivyoona Yohana katika Ufunuo. Mungu ndiye mwenye kubadili nyakati (Daniel 2:21) lakini mpinga kristo atajionesha kuwa yeye ndiye afanyaye hayo naye ataazimu kubadili majira na nyakati.

*❷  VITA NA WATAKATIFU*

*☄ Daniel anasema pembe ndogo (mpinga kristo ) atafanya vita na watakatifu na kuwashinda (verse 21). Hili limathibitishwa tena katika Ufunuo 11:7, 13:7). Jambo hili kama linaweza fananishwa na adha ya kanisa katika kipindi cha mpinga kristo. Mtazamo wa unyakuo wa kanisa  kabla ya kuinuka kwa mnyama (pre-tribulation) unaweka madai kuwa hawa watakatifu ni waisrael na kwa sehemu nyingine ni wakristo waliachwa katika unyakuo. Lakini bado pia yako maandiko mengi yanayoonesha uwepo kanisa katika kipindi cha utendaji wa mnyama (mpinga kristo), yanayozaa mtazamo uitwao mid-tribulation rapture. Haya yote hayatajadiliwa kwenye somo hili kwa kuwa yatachambuliwa kwa kina sana, kwa masomo yajayo siku za usoni. Somo hili lilikuwa linaleta ufahamu tu juu ya wanyama katika Daniel 7.

*❸ UJIO WA KRISTO*
_Christ's advent during the persecution of saints_

☄ Daniel anatuambia wazi kwamba wakati pembe ndogo ikitesa watakatifu (Daniel 7:22, 26-27) ndipo hukumu itawekwa kukomesha utawala wa pembe ndogo, jambo hili linataja kuja kwa Kristo kuuvunja utawala wa mnyama na kuusimamisha utawala wake milele (Ufunuo 16:13-16), Daniel hajatenganisha utawala wa Yesu wa miaka elfu 1 duniani (Ufunuo 20) na ule katika mbingu mpya na nchi mpya (Ufunuo 21). Swala kufunuliwa kitabu na hukumu ambalo Daniel aliliona kama Yohana, litajadiliwa katika masomo yajayo siku uchache za usoni, nikipata neema na muda kuandika.

Ndugu msomaji. Usisite kupekua zaidi katika vyanzo. kwa chochote unachohitaji kujifunza zaidi... Mimi nimekuwekea tu njia. Bila kusahau kumwomba Roho wa Kweli akusaidie.

Mwl Prosper Kadewele
0762879363
alltruth5mimistries@gmail.com

No comments:

Post a Comment