*π ’π π π π π € π ¨π π π π π €π π π π ‘π π ©π *
_*Nebuchadnezzar's Statue*_
*ΚΥ‘Σ ΤΉΙΎΦ
Φ
*
*+255762879363*
Shalom Aleichem!!
Nambariki Bwana, aliye Kristo (Yesu) kwa neema amenipa kukuandikia ndugu mpendwa, namwamini Mungu kwa bandiko hili, litakuwa msaada na nuru gizani. Zaidi sana litakupa msingi wa kujifunza matukio ya siku za mwisho (end-time events).
*_❶. KUHUSU UNABII NA UTIMILIFU WAKE_*
π Unabii wa kiMungu haufungwi na chochote. Mungu anaujua mwisho tangu mwanzo (Isaya 42:9, 46:10) na hivyo akisema, hata ikipita miaka elfu 4,000 lazima kila kitu kije kitukie kwa namna ile ambayo alisema... (ona Maombolezo 2:17b)
*" The LORD hath done that which he had devised; he hath fulfilled his word that he had commanded in the days of old....."*
(Lamentations 2: 17b SUV)
π Muda wa kutimizwa kwa unabii ukifika, kila kitu kitajisogeza chenyewe kwenye nafasi ya kuruhusu unabii utimie. Hata kama inadhaniwa kuwa ni ngumu sana kulingana na mazingira, muda wa unabii ukifika unakuja na njia ya kuufanya utimie. Haikuingia kichwani mwa Belshaza, wala Nebukadreza baba yake, wala Nebopolasa babu yake kwamba kufumba na kufumbua Babeli (mji) ungevamiwa kwa usiku mmoja tu bila vita kubwa wala nini. Muda wa unabii ulipofika Koreshi wa Uajemi usiku mmoja wa tarehe 2 mwezi Oktoba mwaka 539 aliuvamia na kuipindua Babeli. Hakukuwa na mazingira wezeshi kwa jeshi la kiajemi, ila majira ya unabii yalikuja na namna, kulikuwa na mto mkubwa Euphrates (Frati) ambao walioufanyia *diversion* (badilishia uelekeo) ⚡ wakapata njia ya kuingia.
π Isaya alitoa unabii mwaka 742BCE kwamba kuna wakati mfalme Koreshi ataamuru Hekalu lijengwe, na mji wa Yerusalemu pia... Haya aliyaongea kinabii yakatokea kama alivyosema miaka 200 badae, kama nilivyoeleza katika somo lililopita kuhusu majuma 70 ya Daniel.
*_❷. SANAMU ALIYOIONA NEBUKADREZA_*
*(Danieli 2 )*
------------
*32 Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba;*
*33 miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo.*
Nebukadreza hakuoneshwa ndoto hii kwa sababu ya hali yake nzuri ya kiroho wala mahusiano yake na Bwana, bali madhabahu ya nafasi aliyokuwa nayo. Katika ule mzunguko wa mataifa yenye nguvu (superpower nations) wakati huo (606BCE mpaka 539BCE) Babeli ndiyo ilishika hatamu. Hivyo Mungu akamwonesha huyu mtu yajayo kwa sababu ya madhabahu ya nafasi aliyokuwa nayo. Na alimsahaulisha ili kumtengenezea njia ya ukuu Daniel mtumishi wake. Unaweza kutembelea familia fulani, mji, nchi fulani, kama kiroho kiko safi, ni rahisi sana kuoneshwa issues za familia, mji, au nchi hiyo.
Nebukadreza alioneshwa sanamu (statue made of different metals/minerals).. Sanamu ilikuwa ni ya mwanadamu, ikionesha utawala wa kibinadamu duniani tangu wakati huo mpaka mwisho wa zamani zijazo. Katika mstari wa 32&33 tunasoma
1⃣ Kichwa (Head) ππΌ Dhahabu (Gold)
2⃣ Kifua/Mikono ππΌ Fedha (Silver)
3⃣ Tumbo/Viuno ππΌ Shaba (Copper/Brass)
4⃣ Miguu ππΌ Chuma (Iron)
5⃣ Nyayo π£ ππΌ ½ Iron (chuma) na ½ Clay (Udongo)
*❸. TAFSIRI YA KILA KIUNGO CHA MWILI KATIKA SANAMU*
Sanamu ilionesha tawala za kibinadamu juu ya uso wa nchi kuanzia wakati wa ndoto hiyo hiyo 599BC mpaka mwisho wa nyakati zote.
*πΎ KICHWA CHA DHAHABU*
Kichwa cha dhahabu kiliwakilisha utawala/ufalme wa Babeli uliodumu kwa miaka 66 na kidogo (i.e., 606BC mpaka 539BC)
*πΎ KIFUA NA MIKONO YA FEDHA*
Kifua na mikono ya fedha iliwakilisha utawala ambao ulikuja baada ya Babeli, ambao ni Medo-Ajemi (Medes&Persia) chini ya Persian King Cyrus (Koreshi) mwaka 539BC walimpindua Belshaza mwanae Nebukadreza na kushika hatamu, utawala uliodumu ukitawala dunia kwa miaka 208 (i.e., 539BC mpaka 331BC)
*πΎ TUMBO NA VIUNO VYA SHABA*
Hii iliwakilisha utawala uliofuata yaani Uyunani (Greece), kama alivyotabiri malaika Gabriel (Daniel 10:20) kwamba nikiondoka huku mkuu wa Uyunani atakuja... Miaka 200 tangu Malaika aseme hivyo, Iskanda Mkuu (Alexander the Great) alivamia na kuushinda utawala wa Medo-Ajemi mwaka 331BC, na utawala huu ulidumu miaka 163 yaani kuanzia (331BC mpaka 168BC).. Utawala wa Alexander Mkuu ulijikita maeneo ya Egypt, Asia, Anatolia, Macedonia.. na huyu alikufa kwa kuwekewa sumu mwaka 323BC (watu wake waliotawala na maeneo yake manne makubwa ni Cassender, Lysimachus, Seleucus, Ptolemy )
*πΎ MIGUU YA CHUMA*
Miguu ya chuma iliwakilisha utawala uliofuata ukaitweza nguvu Uyunani, nao ni utawala wa Rumi (Roman Empire) mwaka 168BC. Huu ni utawala uliokaa muda mrefu zaidi kwa zaidi ya karne tano i.e., 168BC Mpkaa 476 AD
NB:
*Kila utawala uliowakilisha na aina fulani ya madini (metals/minerals) uliwakilisha sifa husika za huo utawala kwa wenye ujuzi wa maswala ya rocks au extraction of metals wanajua vyema kuwa hizi shaba, dhahabu, chuma, etc zina sifa tofauti....sifa za kila utawala zilikuwa sawa na sifa za madini yaliyofananishwa nao.
*πΎ NYAYO ZA CHUMA NA UDONGO*
Rumi ilivunjika, mtawala mmoja wa kijerumani (Germanic leader) alimshinda mtawala Romulus the Roman Emperor... Lakini hapo nyuma mwaka 395AD Roman Empire iligawanyika mara mbili magharibi na mashariki, tawala ya magharibi ilianguka, ya mashariki kama Constantinople/Byzantine mpaka 1453AD
*πΎ CHUMA NA UDONGO*
Ndoto hii ilionesha nyayo na vidole vya miguu vikiwa na mchanganyiko wa chuma na udongo, ambapo hizi materials mbili haziwezi-shikamana, ikizungumza kuwa baada ya utawala wa miguu ya chuma Yaani Rumi, hakutakuja tena kuwa utawala mmoja superpower wa kutawala dunia, kwamba hata hizo tawala ndogo zikijaribu kuungana hazitafanikiwa, maana kuufanya udongo uungane na chuma ni ngumu... Huku pia sifa za udongo na chuma zikiashiria tawala zingine zitakuwa dhaifu na zingine zenye nguvu.
*πΎ VIDOLE KUMI*
Kuvunjika kwa dola ya Rumi, kulizaa dola kumi za Ulaya... ambazo ni vidole kumi miguuni mwa sanamu
ππΌ Saxon (Uingereza)
ππΌ Franks (Ufaransa)
ππΌ Alaman (Ujerumani)
ππΌ Visigoths (Hispania)
ππΌ Suevovs (Ureno)
ππΌ Lombardi (Italia)
ππΌ Burgundi (Uswis)
ππΌ Herulous (Huu ulipotea/Vanished)
ππΌVandals (Vanished away too)
ππΌ Ostrogoths (Ulivanish pia)
*❹. JIWE LILICHONGWA MLIMANI*
Historia inaonesha watawala wakubwa wa Ulaya waliojaribu kutaka kuunganisha hizi falme, bila mafanikio. Udongo na chuma haviwezi kuungana. Lakini Daniel anamweleza Nebukadreza kitu ambacho kitatokea mwisho wa siku, kwamba aliona jiwe lilichongwa mlimani, bila kazi za mikono, hilo jiwe linawakilisha utawala mmoja wa Mungu, utakaosimamishwa hata milele. Jiwe na kazi zake, na sifa zake zinamwakilisha Yesu Kristo. Maandiko mengi ya unabii yanaonesha Yesu atakuja kuusimamisha ufalme juu ya falme zote za dunia (kwanza katika dunia ya sasa ππΌ millenial kingdom, kisha wa milele yote baada ya hapo).. Kuna mataifa 10 yenye nguvu yatampa mkono wa shirika mpinga kristo, na mpinga kristo kwa kutumia nguvu ya tawala hizo atataka kutekeleza mpango mmoja juu ya Israel ambapo Bwana Mkubwa Yesu Kristo ataingilia kati, na kuyashinda yote (Harmagedoni), hiyo itampa nafasi ya kusimamisha utawala wake kwa namna ile alioneshwa Nebukadreza. Siri za hayo mataifa na mambo yaliyosalia hapa, yako katika somo lijalo.
MUNGU AKUBARIKI UNAPOENDELEA KUFUATILIA
Mwl Proo
0762879363
alltruth5ministries@gmail.com
Halleluya,Asante kwa mafundisho. Baraka za MUNGU ziambatane nawe!!
ReplyDelete