_*NIENDESHE MAHALI PANGU PALIPOINUKA*_
*(Make me walk on my high hills)*
*Mwl Proo*
_0762879363_
Haleluya kwa BWANA! Nawasalimu kwa Jina la Yesu Kristo, Mwokozi wetu. Naamini mnasonga mbele katika imani.
_WATU WA MUNGU, HUSUSANI WEWE AMBAYE UMEPATA NEEMA YA KUSOMA UJUMBE HUU; KUNA MAHALI AMBAKO MUNGU ANAKUSUDIA KUKUWEKA, KUNA MAHALI ULIANDIKIWA KWA MAJIRA YAKE UTAPASWA KUWA SEHEMU FULANI HIVI, MAHALI PA JUU SANA, IWE NI KATIKA HUDUMA, KIUCHUMI, KIJAMII (SOCIAL STATUS), NA KATIKA NYANJA ZOTE (IN ALL LIFE'S ENDEAVORS). KILA MWAMINI UNA MAHALI PAKO PALIPOINUKA, HUTAKUWA CHINI DAIMA, HUPASWI KUBAKI NA HALI ULIYO NAYO DAIMA, WEWE NI MCHUNGAJI UKO NA HUDUMA UNAISIMAMIA, NYUMBA YA IBADA HAIJAWAHI KUVUKA WATU 50, SHAUKU YAKO NI MAMIA KWA MAELFU, HAIJAWAHI KUWA KWELI HIYO NDOTO!, WEWE NI BABA WA FAMILIA UMETAMANI KWA MIAKA MIAKA MINGI UONDOKANE NA AIBU YA KUPANGA CHUMBA NA SEBULE HUKU FAMILIA YAKO NI KUBWA TAYARI, NDOTO HIYO HAIJAWAHI KUWA KWELI!, WEWE NI MAMA/MWANAMKE KATIKA NDOA, MIAKA IMEPITA NDOTO YAKO YA KUZUNGUKWA NA WATOTO WAKICHEZA KWA FURAHA HAIJAWAHI TIMIA!, WEWE NI MFANYA BIASHARA FAIDA ULIYOIOTA KUIFIKIA SIKU MOJA HAIJATOKEA, UMEBANGAIZA MPAKA UNAHISI MOYO WAKO UNAINAMA NDANI YAKO; UNA SAFARI NGUMU KATIKA ELIMU UME-RESIT UKACHOKA, CARRY OVERS/DISCONTINUE ZIMEKU-DISAPPOINT MPAKA UKASEMA HUENDA SIJAANDIKIWA MAFANIKIO KATIKA ELIMU; NA WENGINE WAMEPUNGUKIWA UTUKUFU NA FAHARI KATIKA MAISHA, WANAUGULIA NDANI YAO KUWA HALI ZAO ZA SASA NI MBAYA KULIKO ZAMANI_
*______ kwa maana hali yangu ya zamani ilikuwa njema kuliko hali yangu ya sasa."*
(Hosea 2:7 )
✍๐พ *Mungu hajawahi kuwaza kukusahau, hujasahaulika kabisa ewe mpendwa wangu (Isaya 49:15-16), kuta zako (your issues&situations) ziko mbele za BWANA daima. Lakini leo kuna jambo la kujifunza*
๐ฉ *HATMA ZILIZOCHELEWESHWA (DELAYED DESTINIES)*
๐ฏNi kweli kwamba Mungu anakuwazia mema, na ni mambo tunapenda zaidi kusikia, yaani kutiana moyo kwa ahadi za Mungu, kiasi kila mtu anaweza kunukuu (Yeremia 29:11) kwa kichwa/moyo bila kusoma. Ni kweli kwamba makusudi ya Mungu hayawezi kuzuiliwa (His plans can't be thwarted) Ayubu 42:2, lakini Je! hayo mambo yako mepesi hivyo? Jibu hapana, ziko sababu zinaweza kawilisha mafanikio, hatma njema zenye utukufu.
๐ฏ Shetani kwa kupitia idara yake ya falme na mamlaka pamoja na wakuu wa giza, wameshikilia hatma nzuri nyingi sana, zisiwafikilie wahusika...
๐๐ฝWakuu wa anga/giza hili wamejitahidi kuwapumbaza watu wa Mungu, maana bila kufanya hivyo hakuna falme za giza za kuweza kushindani na kanisa la Kristo (wala individual believers). Hivyo kwa kuwa wanajua kwamba hawa watu wakisimama sawa kwa Bwana watatoboza daima kuzielekea hatma zao njema (their brilliant futures/blossomed destinies), njia pekee ni kuwapumbaza.
๐๐ฝZiko hatma njema, tuliandikiwa, lakini kuzipokea kunategemeana na hali ya kiroho ya wakati husika, yaani unaweza kuharibikiwa kiroho kwa kiasi ambacho Mungu akimwagiza malaika aachilie ule mbaraka wako, anakukuta haujastahili, hivyo kukawa na *waiting time* kuona kama utayaweka mambo sawa, ukayafua mavazi, na kuwa tayari kuzipokea ahadi (delaying).
๐๐ฝKuna tabia za asili (matendo ya mwili) ambazo haziendani na hatma ya mafanikio uliyoandikiwa. Na hapa ni shida zaidi, wengi katika waamini baada ya muda wanajikuta wanapambana na utu wa kale tena. Wakuu wa giza wana desturi ya kujengea ngome (making strongholds/pinning) baadhi ya tabia za mwenendo wa kale, wakipata nafasi, kisha hata wao wakikaa pembeni, unabaki unashindana na ile tabia hali ukikawilishwa kuiingia hatma yako njema (2Korintho 10:4-5)
๐๐ฝUnaweza kujikuta mwaka mzima umeisha, hujawahi kuwa sawa kiroho, hatia, makosa, kushindana kumekuzinga kote, kila unapoponyoka toka katika vifungo vya zile ngome za wakuu wa giza (vya tabia za utu wa kale ambazo unakuta umechomekewa tu), unajiona ni mtu usiyestahili kuomba mahitaji, huna uhuru wa kuamuru mapambazuko yako, na badala yake unakuwa bize na maombi ya kutengeneza, kurekebisha njia, kujijenga upya, kutafuta tena connection ya kwanza, unatubu tena na tena na unahisi kama bado hivi, unarudia kuyatubia yaleyale, huu muda wa kutengeneza kiroho chako ukiwa prolonged (refushwa sana), unaweza kuta umekutana na wakati mwingine wa ukame kiroho. Hivyo kabla hujashughulikia kunasua hatma yako iliyoshikiliwa, unaanza upya ratiba ya matengenezo (circular repetitions).
๐๐ฝUhuru wa kuomba mahitaji, kupeleka hoja zenye nguvu, hata kiwango cha kumwagiza Mungu (giving orders to God), kinaanzia na moyo usiohukumiwa, moyo ukiwa na ujasiri utaomba mahitaji na utakuwa huru kuamuru maadui walioshikilia jibu lako lolote njiani waachie, malaika waliokwama njiani kwa sababu ya makosa yako, kwa sababu ya wewe kutosimamisha madhabahu yako katika msingi wake, wataweza sasa kukufikishia waliyopewa kwa ajili yako. (Isaya 45:11, 41:21, 1Yohana 3:21).
๐ฏ Kwa sababu hizo hapo juu, kuna watu hatma zao zimecheleweshwa. Hajazuiwa Mungu, ila imezuiwa kwa kucheleweshwa hatma yako njema (mbaraka uliopaswa kukujia na kukupata). Hivyo muda wako kamili wa kukutanishwa na mume sahihi ulifika, huenda miaka mitatu imepita, ila hatma imekawilishwa, maana ukikaguliwa moyoni mwako, umejaa mashaka (doubts), umechoka kumngoja Bwana, binti umeona miaka 35 hii hapa na hakuna mwanaume anayekuja akiwa serious na ndoa, kila anayekuja anataka tu mvuane nguo kwanza.
*NB๐จ*
_*THIS GOES TO ALL WOMEN OUTSIDE THERE, HUWEZI KUMTHIBITISHIA MWANAUME UNAMPENDA KWA KUMCHOJOLEA ๐๐ฝ๐, AND AS THE MATTER OF FACT FROM PSYCHOLOGICAL POINT OF VIEW, WANAUME WENGI WAKIISHAFANIKIWA KUKUDINYA, KWENYE VILINDI VYA MIOYO YAO WANAKUWA WAMEFUTA SWALA LA KUKUOA. UKIOLEWA NA MWANAUME AMBAYE AMEKWISHA KUKUDUNGUNYUA UMEPATA BAHATI TU. MAANA KILE AMBACHO ILIBIDI AKIPATE KWA GHARAMA NYINGI ZA KIROHO NA KIJAMII NA HITIFAKI NYINGI ZA KIROHO NA KIJAMII, AMEKIPATA TU BURE KWA KUKUTUMIA TEXT MOJA, "naomba uje ghetto mara moja"*_
Hivyo dada miaka kufika 35 ukiwa bachelorett (single), sio sababu ya kuamua kugawa mwili, sio sababu ya kufanya maamuzi kama vile sio mwana wa Mungu, eti ngoja nizae zangu, niwe na mwanangu, tena kanuni haikosei, ukigusa ngono siku moja tu na mimba juu, mimba hazitoki kwa Mungu bali kwa kanuni ya asili ya uzazi tangu uumbaji, kwamba yai likirutubishwa na mbegu na hakuna matatizo yoyote (biological/reproductive dysfunctions) basi conception inatokea (Kinachotoka kw Mungu ni roho ya mwanadamu muda wa conception). Lakini nje ya kanuni za Mungu, na kwa kuwa umefanya kusudi kabisa (Ebrania 10:26), basi kurudi kwa ile nafasi yako ya kuaminiwa na Mungu kwa mambo makubwa, itachukua muda na gharama kubwa.
๐ฉ *HATUA YA KWANZA YA KUSHUGHULIKA NA HATMA ZILIZOKAWILISHWA NI KUTENGENEZA MAMBO YAKO KIROHO*
๐ฏJitahidi sana, usome kwa utulivu somo langu lisemalo, "Mambo ya kiroho yakiharibika; tengeneza". Humo ndani utapata vitu vingi sana.
๐ฏMambo ya kiroho yakiwa sawa๐๐ฝ, wewe utajua na maadui zako wa kiroho watajua.
๐๐ฝUtakuwa huru kuomba mahitaji kwa ahadi za Mungu wala hutazuiliwa neno tena...
๐๐ฝMambo ya kiroho yakiwa sawa, kuna vitu utapewa kama ofa, kama zawadi tu, maana mtoto haombi kila kitu kwa baba yake, mengine baba anajiongeza tu, kuwa mmmh mwanangu hana viatu, mmmh uniforms za shule zimepauka sana, ndivyo Mungu atafanya kwako maana njia zako zampendeza, (Isaya 65:24, Math 6:8).
๐ฉ *HATUA INAYOFUATA NI KUFANYA VITA DHIDI YA WAKUU WA GIZA NA MAJESHI YA PEPO WABAYA, WALIOHUSIKA KUSHIKILIA HATMA NJEMA, KWA KUWA WALIKUWA NA SABABU HALALI MWANZO*
๐ฏ Hapa unapaswa kuwa na maarifa kamili kuhusu kushindana kiroho. Jitahidi kusoma masomo yangu haya mawili
1⃣ VITA VYA ROHONI
2⃣USHINDANI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO
๐ฏHii ni muhimu, maana sio mara zote roho za kipepo zitaachilia nyara zako, kisa umetengeneza mambo yako na Mungu. Kuna wakati (so often times) unalazimika kuwafurumsha kule rohoni wakimbie waache nyara zote walizoteka wakati ukiwa katika usingizi/ukame/kuchoka kiroho.
๐๐ฝThis is so real, kuna watu wamewahi tengeneza mambo yao kiroho. Walipofanya vita kwa usahihi, ndipo mafaili yakafunuliwa upya, wakakuta wanitwa kufanya interviews ya kazi walizoapply miaka mitatu iliyopita, wengine wakaanza kutafutwa na wachumba na waume zao waliowa-dump miaka ya nyuma, kuwataka warudiane/ waoane seriously, kilichotokea hapo ni kwamba roho za kuzimu zilizoshikilia hatma sasa zimeachilia.
*M̸͟͞O̸͟͞Y̸͟͞O̸͟͞ W̸͟͞A̸͟͞ S̸͟͞O̸͟͞M̸͟͞O̸͟͞*
_M̸͟͞w̸͟͞l̸͟͞ P̸͟͞r̸͟͞o̸͟͞o̸͟͞_
๐ฉ *MWAMBIE BWANA AKUENDESHE MAHALI PAKO PALIPOINUKA*
*_"YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka."_*
(Habakuki 3: 19)
๐ฏ *THIS IS GOD'S PROMISE, FANYA KUMBUKUMBUSHA TU, KWAMBA BWANA ULISEMA KWA KINYWA CHAKO, TENDA KWA MKONO WAKO SASA. HII NI AHADI YAKE, SPEAK HIS WORD BACK TO HIMSELF, YEYENI MWAMINIFU ANALIANGALIA NENO LA AHADI YAKE, AMBALO AMELITUKUZA KUILIKO HATA JINA LAKE (YER 1:12, ZAB 138:2)*
๐ฏ *AIFANYE MIGUU YAKO KUWA KAMA KULUNGU, KULUNGU NI DEER๐๐ฝ๐ฆ*
*HILI NI OMBI LAKO KWAKE, HAPA ANAZUNGUMZIA SPEED&FINALITY, ATALITEKELEZA NENO LAKE AKILIMALIZA NA KULIKATA*
*_"Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya nchi, akilimaliza na kulikata."_*
(Waruma 9:28)
*AHADI YA MUNGU KWAKO, UNAYOPASWA KUISHIKA MPAKA UIINGIE HATMA YAKO NJEMA, NI HII KWAMBA BWANA ULIAHIDI UTATOA NENO NALO LITATIMIA, HALITAKAWILISHWA, HAYATAKAWILISHWA*
Ezekiel 12:21-28
_*PRAY UNTIL SOMETHING HAPPEN, USIKUBALI KUKONDEANA NA KUSINYAA WAKATI UNAPO MAHALI PAKO PALIPOINUKA, UTAKAPONG'AA NA KUWA MTU WA KUTAMANIWA NA MATAIFA YOTE. MWAMBIE BWANA SASA, AKUENDESHE MAHAI PAKO PALIPOINUKA. NAFSI WANGU KWA NINI KUINAMA NDANI YANGU? MTUMAINI MUNGU ALIYE AFYA YA USO WAKO*_
Mwl Proo
0762879363
alltruth5ministries@gmail.com