Wednesday, October 16, 2024

MAISHA YA VIJANA WA KILEO

*NACHELEWA KIDOGO KUELEWA, AU KUAMINI MAISHA YA VIJANA WENGI WAKRISTO WA KILEO* πŸ€”πŸ€”πŸ€”


_Anaandika Mwl Proo_ ✍️ 

Mwaka huu nimetimiza miaka 20 tangu nilipoamini Injili na kuokoka. Miaka ya hapa usoni, nimechunguza maisha na mienendo ya maisha ya vijana wakristo, ukiacha wachache, wengi wao (majority) maisha yao huoni tena ule ushindi, ile ladha, ule uchaji/kicho, ile bidii, ule ukiroho... Najiuliza hawa wanashindaje? wanaishije maisha ya utauwa katikati ya uchafu mwingi ulioletwa na utandawazi? Mbona hawazipigi mbio zile tulipiga? πŸ€”πŸ€”πŸ€” 

Wakati ule naamini na kuwa mwongofu, hakukuwa na maendeleo makubwa ya teknolojia, Shule ya Sekondari Ya Wavulana 1,400, wenye viswaswadu tulikuwa wachache mno. Nakumbuka kule kuomba kusikokoma, nakumbuka mifungo ya lazima na hiari, iliyofanya kuwa na siku mpaka 204 za kufunga kwa mwaka, mpaka ikawa desturi ya kuwa na wastani wa siku 3 au 4 za kufunga kila wiki. Nakumbuka kuhusu gatherings & fellowships siku 6 kila wiki, ukikosa siku moja, jiandae kupokea wapendwa kibao huko kwako wakija  kujua sababu ya kukosa ibada. Nakumbuka namna tulisumbuka kuomba ruhusa ili kuhudhuria semina zote za Mwakasege, mikutano ya injili kule Biafra na Jangwani. Nakumbuka namna ambayo hakuna Joint-Mass tuliwahi kuikosa weekends zote pale DIT, IFM, UDSM na penginepo, makongamano yote ya pasaka hakuna hata moja tuliwahi kukosa kwa sababu yoyote. Nakumbuka jinsi ambavyo tulishikamana na mafundisho ya fellowship yetu kuwa hakuna mahusiano (relationship)  kwa wanafunzi wa Sekondari kidato cha kwanza mpaka cha sita.. Uhusiano halali pekee ni  'Kaka' & 'Dada' (Na watu tukaishi maisha hayo hayo) kile kinachoitwa Boyfriend &. Girlfriend kuna sisi hapa hatukuwahi jua kama kipo... Na ndio maana haikuwa ajabu, si ajabu kwa sisi wa kizazi kile na maisha yale yenye nidhamu ya kiroho kuwa tuliishi bila zinaa, haikuwahi kutajwa kwetu kamwe, tulikuwa hata hatufananii mambo hayo... (Our walk with the Lord shaped our lifestyles)... Tunao ujasiri wa kusema tulishinda tamaa za dunia na mambo yake. Yale maisha ya utauwa yalifanya hata nikiona kapicha tu kwenye gazeti au Tv kenye viashiria nudity (uchi) tachukia hapo vya kuchanwa vitachanwa, vya kufutwa vitafutwa, vya kuondolewa vitaondolewa, na nitafanyia kazi fikra zangu kuhakikisha no memories za huo uchafu zitabaki hata kwa mbali 🧠. Sasa kwa nini naandika haya.... Nimeona miaka ya usoni yale mazoezi ya kiroho yaliyotupa kuishi maisha ya wokovu yenye   ushindi, yenye usafi kimwenendo, ni kama yanakwepwa sana na vijana... Hesabu idadi ya vijana kwenye mikesha ya maombi, kwenye makusanyiko ya mifungo, na huduma nyingine...... Vijana wengi utawapata kwenye programs & events (they live too ceremonial)... Ndio najiuliza kwa lifestyle hii ya kwao, wanaweza kuishi maisha ya utauwa hawa? Na uchafu wote wa kwenye TV wanaweza kuepuka hawa kujaza vitu vichafu  kwenye nafsi zao? Nguvu zao chache watashinda kweli na ushawishi wa mitandaoni, picha za uchi kila mahali, sio Facebook, sio Instagram, sio TikTok sio WhatsApp, hata kama huja-follow kurasa mbaya utakutana tu na watoto wa Belial ambao kutwa nzima wanatengeneza contents za utupu.... Vijana wa sasa wanashindaje? Wanaepukaje uasherati? Wanaepukaje usagaji na kujichua? Mnaepukaje kuwa na mazungumzo mabaya mkiwa mnawasiliana wa jinsi mbili tofauti? Mnawezaje?  Yale ambayo yalikuwa ni sababu ya kuwapa ushindi hamyafanyi, mmeyakimbia, mnawezaje kushinda? Ni vijana wangapi wa kileo wapo serious na ratiba za kusoma na kujifunza maandiko, na wakawa strict kuhakikisha wanazifuata? Nilihitaji miezi 8 tu kwa mwaka kumaliza vitabu 66 vyote vya Biblia (tena nasoma kwa parallel-system:- English Bible juu/Swahili Bible chini)... Kijana ambaye kinachomfurahisha ni matamasha ya muziki pekee, anavukaje kwa ushindi??

_mwlproo_
Ujumbe huu ufikishwe kwa vijana. Kwamba maisha safi ya Kikristo yanahitaji nidhamu, utauwa ni wa kujizoeza, mpaka ifikie mahali mambo yote yasiyofaa unayachukia, huwezi puuzia mambo ya muhimu ya kiroho na ukabaki salama tu, ukipuuza nidhamu na bidii kwenye kujifunza maandiko, nidhamu na bidii kwenye kuomba, nidhamu na bidii kwenye kufunga, nidhamu na bidii kwenye kufanya huduma, jiandae kuwa na maisha ya hovyo, kurudi nyuma, na kutawaliwa na matendo ya mwili... Zingatia sana hayo nisemayo, inawezekana kabisa kuwa na mienendo safi, maisha yasiyo na uchafu, uadilifu kama iwapasavyo watumishi wa Kristo Yesu... Katika zama za Teknolojia hizi unaweza kuchagua kubaki kijana wa mfano, kinara kwa mambo ya kiroho, mnyoofu kabisa kiuadilifu na maadili, si tu ukiwa kwa watu, bali ukiwa sirini sana, bado uwe mnyoofu!


Asante kwa kusoma... Tuwasaidie, tuwaombee vijana!

Mwl Proo
0762879363
Bado tunatoa ofa ya vyombo vya muziki kwa makanisa kwa bei ya sadaka. Piga simu uweke oda yako

Thursday, December 22, 2022

KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO (PART 7)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
_*Rightly Dividing The Word of Truth*_ (2Timothy 2:15b)

*SEHEMU YA SABA*

*CHANZO CHA NGUVU*

Mwandishi: *Mwl Proo*

Mmebarikiwa ninyi nyote mnaoendelea kuufuatilia mfululizo huu. Leo nimepewa kuzungumzia nguvu na chanzo chake.

Nguvu zote zilizopo, zilizokuwapo, zitakazokuja zote (za zamani zijazo) ni za Mungu, chanzo cha nguvu zote ni Mungu. Hata nguvu zinazotajwa kuwa ni za shetani (Mdo 26:18) zote ni za Mungu, na chanzo cha nguvu hizo ni Mungu. Suala la shetani ku-manipulate, au kuzitumia nguvu alizopewa kwa uovu, haibadili ukweli kama chanzo cha nguvu hizo ni Mungu. Hata zile nguvu maarufu ziitwazo za asili (natural powers), chanzo chake ni Mungu, ni za Mungu... Kama kuna nguvu inaizungusha dunia bila kupungua spidi yake, kama kuna mikandamizo ya hewa kukaleta upepo, kama kuna nyota na sayari katika miendo yake kuna aliyeamuru viwe vikawepo, alipoamuru aliruhusu nguvu zake kutekeleza na kuyashikilia mambo yote kwa uratibu wa hali ya juu (Isaya 40:26, Zaburi 8:3)

Andiko la Warumi 13:1b linatumia neno _'exousia_' kutaja uweza/nguvu/mamlaka. Neno hilo limetumika mara 29 katika Agano Jipya la Kiyunani na mara nyingine limetumika kwa kubadilishana (interchangeably) na neno dΓ½namis (dunamis πŸ‘‰ specifically to perform miracles) likitaja nguvu. Andiko hilo katika versions nyingi (mfano: KJB,  ASV, DRM) linasomeka, _Hakuna nguvu ila za kutoka kwa Mungu tu_
*For there is no power but of God: the powers that be are ordained of God.*

Nguvu za Mungu zinaweza kuwekwa katika vitu kutekeleza makusudi fulani fulani. Kwenye Biblia yote Agano Jipya na la Kale, viko visa vingi ambavyo nguvu za Mungu ziliruhusiwa kuwepo (transmit) katika vitu na vitu hivyo vikatumiwa kutekeleza kazi iliyokusudiwa. Hebu fikiria kisa cha Elisha katika 2Wafalme 4:29ff... Elisha alitransmit nguvu za Mungu kwenda kwenye fimbo yake, akampa Gehazi akamgusishe mtoto aliyefariki, ili afufuke. Nguvu za Mungu ndani ya Elisha hazikukaa tu ndani ya roho na nafsi yake hai, bali hata mwili, damu, nyama, na mifupa yake (soma 2Wafalme 13:21) utagundua mifupa yake ilisalia na nguvu zilizoweza kufufua mtu yeye akiwa amekufa kwa homa siku nyingi. Tunasoma katika Matendo 19:11, leso na nguo ambazo zilimgusa Paulo zilipelekwa kwa wagonjwa wakapona, na pepo wabaya wakawatoka. Matukio kadhaa yanaonesha nguvu za Mungu ndani ya watu zilikuwa transmitted kwa vitu (kumbuka kisa cha chumvi kwenye chanzo cha mto huko Yeriko, kumbuka kisa cha unga uliotiwa sufuriani ili kuiondoa mauti, kumbuka  pindo la vazi la Yesu, tope lenye mate ya Yesu, birika la Bethzatha na mengine mengi). _mwlproo_

Kuna upotoshaji mwingi unaotokana na kukosekana kwa maarifa. Kuna makelele mengi yanaleta aibu kama sio huzuni. Leo hii tuna watu ambao hiki kitu wamekipokea kimakosa utasikia sabuni, utasikia mafuta, utasikia maji, utasikia pipi, utasikia keki, utasikia stika, utasikia chumvi, utasikia udongo, utasikia kitambaa cheupe.... Vyote hivi vitaenda kwa jina la upako... Kwa miaka mingi vimekuwa vikiitwa visaidizi (erroneously), na miaka michache iliyopita nilimsikia mhubiri mmoja wa Dar akiviita vifaa vya kiroho, jina ambalo sasa linatumiwa na wengi. NDUGU ZANGU WAKRISTO VITU NILIVYOTAJA HAPO JUU VYOTE HAVINA NGUVU. NGUVU ZIKO NDANI YA WATU, NA WATU NDIO WANAOWEZA KURUHUSU NGUVU ZILIZO NDANI YAO ZIENDE KWENYE VITU (TRANSMISSION), NA KURUHUSU NGUVU ZIENDE KWENYE VITU KIBIBLIA NI PALE TU ROHO AMEKUPA UFUNUO (NENO LA HEKIMA) KWAMBA SHIDA HII IHUDUMIE HIVI ZIRUHUSU NGUVU ZIENDE KWENYE MAJI AU CHOCHOTE KIWE NA CONTACT NA MWENYE SHIDA TATIZO LIKAONDOLEWA, AU KWA NAMNA ILIVYO KATIKA MAZINGIRA NI NGUMU KU-ADMINISTER HUDUMA ZA KUPONYA NA MATENDO YA MIUJIZA KWA NENO LA IMANI, KWA KUOMBA, KWA KUWEKA MIKONO NA NAMNA NYINGINE YA UTENDAJI. HIZI NI NAMNA MBILI KWA MUKTADHA WA UKRISTO VITU HIVI VYAWEZA HAMISHIWA NGUVU ZILIZO NDANI YA MTU KURUHUSU VIKATENDE KAZI.

Dramas zinazoendelea leo hii Afrika ni nyingi mno. Wakristo wanakimbizana na hivi vitu kiasi cha wao kupumbazika kabisa kubakia watumwa mara billion ya walivyokuwa kwanza. Nilipewa ushuhuda wa mama aliyemwaga chumvi yake ya upako bahati mbaya na akasikitika sana na kilio juu. Nilishuhudia kwa macho yangu mhubiri mmoja huko Dar, aliivua tai yake πŸ‘”  na kuirusha kwa watu kwamba ina upako (sikatai maana upako unahamishika), lakini iligombaniwa sana na washirika, na kijana mmoja alifanikiwa kutoka nayo nje,  katika vutavuta mwingine aliikata kipande... wamama wawili wakamwomba wamlipe laki 3 awaachie kipande hicho cha tai. Dramas hizi za vile vinavyoitwa visaidizi au vifaa vya kiroho ziko Afrika kuliko mahali pengine popote palipofikiwa na pentecostal & charismatic movements, kwa nini haswa?

 Hapa Afrika vimekuwa maarufu kwa sababu ya imani za asili au za kienyeji kwa jamii ya watu wa Afrika. Maishani mwangu nilipata neema ya kusomea dini za asili za Afrika (African Traditional Religion πŸ‘‰  ATR). Kwenye dini zetu za asili na tamaduni vitu vya kuonekana, vya kushikika, manuizo, matambiko, ulozi, na mengine mengi yaliyohitaji vitu vya kuonekana yalihitajika sana. Fikiria jamii ambayo ilizoea wakitoka kwa mganga wa kienyeji,  wamechanjwa miili, wamepewa vitu vya kutia kwenye maji ya kuoga, wamepewa vitu vya kufunga mikononi, viunoni, shingoni, wamepewa vitu vya kulalia chini ya kitanda, cha kupaka ukutani, cha kumwaga na kunuiza kwenye kuta za nyumba, cha kuweka darini na kadhalika.... Haya yamekuwa mambo ya kawaida kwa karne nyingi Afrika, yamerithishwa vizazi vingi kiasi cha kuwa ni kama kitu cha kuzaliwa nacho. Kila atakayekuja Afrika akawa na vitu tangible vya kugawa kwamba vina nguvu za kusaidia atake au asitake lazima atafanikiwa kupata ufuasi mkubwa maana imegusa asili ya Afrika. Hapa sasa ndio sababu haswa ya kila mhubiri kwa sasa anakomaa na vitu hivi.. Hata mahali ambako angeweza kumgusa mgonjwa kwa mkono wake, atamwagiza ashike kitu, hata mahali ambako angetamka tu 'kansa kauka'... atatafuta kwenye briefcase πŸ’Ό  chupa cha mafuta aliyoyabeba toka Israel bila hata maelekezo ya Roho wa Yesu (mtu akiongozwa na anaweza kuthibitisha hilo hakuna tatizo) Lakini 95% ya watumiaji wa hivi vitu, hawana maelekezo yoyote ya Yesu... wanaunga-unga na kujaribu-jaribu tu, mambo yakitokea kweli wanaendeleza bila kujua nguvu zipo ndani yao.. Na matokeo yanatokea si kwa sababu wapo sahihi... Ni kama tu mtu kunywa sumu akiamini ni juisi tu, haitazuilia sumu kufanya kazi yake ya kumwua, au mtu anywe maziwa akiamini ni maji tu, haitaizuia maziwa yasimpe nutrients zinazopatikana kwenye maziwa. Lakini tatizo limekuwa kwenye kufanya waamini wasijue kuwa nguvu ziko ndani ya watu si ndani ya hivyo vitu.. Niliongea na rafiki yangu mmoja ambaye dada yake ni mhudumu (usher) kwenye huduma moja ya maombezi. Alisema waliuza maji ya uhai (katoni za kutosha) ambayo yaliombewa na mtumishi wiki nzima, yakaisha na watu bado walikuwa wengi, hivyo ikabidi maji yakanunuliwe direct toka dukani na kuuzwa kwa watu kama maji ya upako... bila hayo maombi ya siku saba. Guess what! Kwa sababu ya imani ya miujiza ndani ya hawa watu haya maji yaliyotoka dukani directly yakipelekwa kwa wenye shida yanawezaleta shuhuda pia. Lakini ufahamu wa juu kabisa kwa waamini ni kufahamu nguvu zote hizo ni za Mungu, na jamaa ya waamini (WOTE) walipobatizwa katika Roho wa Kweli nguvu hizo bila kipimo zilikuwa superimposed ndani yao. Waamini wote wanazo hizo nguvu, utendaji utatofautiana tu kulingana kiwango cha maarifa, na unafanya nini katika ufalme, na Roho Mtakatifu amekupea karama zipi, au wewe mwenyewe unatembeaje katika kutumia vilivyowekwa ndani yako tayari. KWA KUSEMA HIVYO WAAMINI HAWANA HAJA WAO WENYEWE KUKIMBIZANA NA CHOCHOTE, MAANA NGUVU ZENYEWE ZIKO NDANI YAO. KAMA KUNA NGUVU ZIPO KWENYE UDONGO WA ISRAEL, AU MAJI YA YORDAN, AU SABUNI, AU CHUMVI AU KITAMBAA KILICHOOMBEWA, NGUVU HIZO SI KWA AJILI YA MKRISTO YEYOTE MKOMAVU, MAANA YEYE MWENYEWE NDIYE MZALISHAJI WA HIZO NGUVU KUTOKEA NDANI YAKE ZIKASAIDIE WALIOFUNGWA NA ADUI HUKO NJE (YOH 7:38). MWAMINI ANAYEHISI KUWA KWA POSTI HII NINAWAPINGA WAO AU MHUBIRI YEYOTE HONGERA YAKE KWA KUCHAGUA KUWA MTUMWA WA DAIMA.. ENJOY YOUR SLAVERY, REMAIN CAPTIVE TO IGNORANCE. MIMI BINAFSI NGUVU ZIPO NDANI YANGU, NIKISTULIWA SAA NANE USIKU KUTOA HUDUMA YOYOTE YA KIROHO, NITATOKA NIKIWA NA NGUVU ZOTE BILA KUHITAJI KUTAFUTA KICHUPA FULANI ETI NIMEKIFICHA  KWA KABATI, HATA BAADA YA KUTRANSMIT NGUVU KWENDA KWENYE VITU, NIMEPEWA UWEZO KUJI-RECHARGE πŸ”Œ  πŸ”‹  MIMI MWENYEWE SI MIMI KUTEGEMEA VINGUVU NILIVYOVIHAMISHIA KWENYE KITU.


Tukutane sehemu 8, kuna mambo mazuri utayafahamu


alltruth5ministries@gmail.com

Tuesday, November 15, 2022

SWALI NA JIBU (KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*

_*Majibu ya swali nililoulizwa na mchungaji mmoja kwa inbox, kufuatia sehemu ya tano ya somo letu*_

Kufuatia sehemu ya tano ya mfululizo wa somo letu la *Kulitumia Kwa Halali Neno La Kweli*, sehemu iliyojikita kuzungumzia *UTOAJI/MATOLEO* nimeulizwa na mchungaji mmoja kuwa Je! kwa namna hiyo niliyofundisha mapato hayatapungua na kurudisha kazi ya Mungu nyuma?

Niseme hivi, watu wanachofanya sasa hivi ni matokeo ya mafundisho, utoaji uliopo sasa hivi (wa kichoyo) ni matokeo ya mafundisho (tena yenye makosa). Kwa fundisho sahihi la Ukristo juu ya utoaji lililojikita juu ya ukarimu (generosity), kanisa wala wahudumu wa injili hawakupaswa kubakia na mahitaji (Mdo 4:34, 2Kor 11:9,  Mdo 20:34-35, Filipi 4:16). Tatizo tulichagua mafundisho yaliyoumodoa Ukristo na watu wakaamini katika Ukristo, utoaji kiwango chake ni kuweka ka-kakapu (kitunga ) na kupokea masilesile πŸͺ™πŸͺ™πŸ’°πŸ’°, au Ukristo kiwango chake ni kutoa million 10 kila upatapo million 100. Ukristo kiwango chake cha utoaji ni kuhudumia mahitaji kwa ukarimu hata pasiwepo uhitaji. Ukipata million 100 kama kuna uhitaji wa million 85, unapambana kuondoa huo uhitaji kwa kadri cha kiasi cha ukarimu wako. Tutawatambua wakristo waliokomaa katika fundisho la Kristo kwa namna yao wanavyohudumia mahitaji ya kazi za injili, na namna wanavyosapoti wahudumu wa injili, ili kusiwe na mikwamo yoyote. Kama waamini wakifundishwa usahihi wa utoaji kiKristo wataacha uchoyo wa kutoa kidogo kwa asilimia wakati uhitaji ni mkubwa. Wakristo wakifundishwa fundisho sahihi la utoaji, mtaona ghafula tu mabadiliko, watu wataanza kutoa magari, hati za nyumba zitamiminika, viwanja vitamiminika, wafanyabiashara wakubwa na watu wenye tenda za mabilioni ya pesa wataacha uchoyo wa percents na badala yake vyombo vya matoleo vitajaa cheques (cheki) za benki zenye figures tu kubwa, mtu hataona kazi kuandika cheki yenye million 700 kuituma kanisani. Ila kwa sasa kwa kuwa mnafundishana uchoyo, mtu anaishi chini ya viwango vya ukristo huku akiamini amefika. Kwa wahudumu wa neno (mafundisho) wafundisheni waKristo mwenendo unaopatana na tabia mpya za asili yao mpya waliyoipata kwa kuzaliwa kwa njia ya Roho wa Yesu. Mapato ya kanisa hayatapungua, badala yake hakutakuwa na mahitaji tena, na itawapunguzia wahubiri kuwa na mahubiri ya mchongo ya *naona watu 50 wenye elfu 50 kwenye wallets πŸ‘›  zao, wazitoe na watapata upenyo ndani ya siku 50* πŸ˜€ Na wengine wametumia 1Samwel 9:7-9, kuweka gharama za kumwona mtumishi (consultation charges), mara ambatanisha sijui what. All sorts of kuambatanisha, kujiambatanisha kwa sadaka, kuifanya kama catalyst ichochee mchakato wa wewe kupokea ahadi au wema wa Mungu, katika Ukristo vyote hivyo ni vya mchongo. Usiulize swali juu ya haya majibu kama hujasoma sehemu ya 1, 2, 3, 4, 5 ya mfululizo huu. Ukiyakataa haya yakatae tu. Endelea kuufurahia uongo kwamba ikitokea sijui kama hujafanya jambo fulani la kimatoleo utalaaniwa, kwamba utakufa kama Anania na Safira, kwamba hutauona ufalme wa Mungu, kwamba sijui what you name them..... Hayo mmeyachagua kuyaamini kinyume na fundisho la Kristo, mitume wake na matendo yao.......

Asante! Tukutane sehemu ya 6 ambayo iko njiani

Mwl Proo- +255762879363

KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO (PART 6)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
*_Rightly Dividing The Word Of Truth_* (2Timothy 2:15b)

*SEHEMU YA SITA*

_MwlProo-0762879363_

*KUHUBIRI NA KUFUNDISHA (Mathayo 11:1)*
 
Karibu katika mfululizo huu wa kuifahamu kweli, jitahidi usome sehemu tano zilizotangulia utaelewa zaidi hapa. Leo napiga hatua kuingia ndani zaidi. Kuna kipindi fulani hivi katika kanisa, mafundisho mengi yalijengwa juu ya shuhuda za watu waliodai kuchukuliwa mbinguni na kuzimu ma kurudishwa. Wengi wa waliotoa madai hayo hawachukuliwa na shetani, wengi katika wale encounters zao zilikuwa za kweli. Kukatokea tatizo kwa kutojua msingi kamili wa fundisho la Kristo, na hawakuwa na namna sahihi ya kuyafikisha waliyoyaona. Kwa ufinyu wa maarifa ya imani ya Ukristo waliyatafsiri mambo kinyume na kweli, ikapelekea kuwa na vitu vingi kwenye mafundisho vyenye kuwakosesha target waamini. Nyakati hizo mtu angezuka kusema nimemwona mchungaji fulani kuzimu (aliyefariki kitambo) anateseka katika moto, kosa lake alizini kwa siri. Nimemwona bibi yangu kuzimu, kosa lake alikuwa mchawi. Yesu amenionesha kwenye maono wote wanaovaa hereni, mawigi na mikufu wapo motoni wanachomwa, Yesu amenionesha wasiotoa zaka kamili hawana nyumba zao mbinguni, na wanaotoa sadaka chache nyumba zao hazijafungwa lenta au hazina canopy. Kwa hiyo waamini wakawa wakirushwa huku na huko na kila upepo wa fundisho toka katika chanzo kisicho sahihi cha mafundisho na mahubiri. Sipo kinyume na shuhuda zao, nipo kinyume na uwasilisho na tafsiri zinazokinzana na kweli ya injili, pamoja na kutumia maono na ndoto za mbinguni na kuzimu kama chanzo cha mafundisho ya msingi ya kanisa. 

Kwa nini kumetokea makosa (errors) mengi kwenye mafundisho na mahubiri mengi kwenye mwili wa Kristo? Andiko nililoliweka hapo juu (Mathayo 11:1) tunaona wanafunzi wakitumwa kufundisha na kuhubiri. Kuna watu wamepewa karama ya kufundisha, na kuna watu kuhubiri, na inawezekana vyote vikawepo. Mtu ambaye hajapewa kufundisha anapolazimisha kufundisha ni rahisi sana kuwaingiza watu katika makosa. Kuna watu walijaliwa neema ya karama za Roho za matendo ya miujiza, karama za kuponya, na karama zingine zenye mvuto tu, wakaaminika kwamba kama wanaweza kutumika kwa karama za nguvu kiasi hicho wanaweza kufundisha, kwa bahati mbaya ikawa kinyume chake. Miongoni mwa ambao waliingiza chachu nyingi za kimafundisho ni watu waliowahi kutembea katika karama za nguvu _(Rejea somo langu la Karama za Roho)_ na wakaamini pia wanaweza kufundisha, kumbe hawakupewa kufanya hilo (Unaweza ukaelewa fundisho la mtu aliyetoka kufufua mfu, linavyoweza kuwa na nguvu, hata kama lina makosa. Watu waliondaliwa na kupewa huduma ya kufundisha wanayo neema ya kufanya uchambuzi wa maandiko (exposition of  scriptures) na kuleta *BALANCE* ya mambo yote yahusuyo imani. Nimesoma kisa fulani ambapo Kenneth Hagin alimwandikia mwalimu mmoja wa neno la Mungu kwa jina Gordon Lindsay (ambaye aliwahi kuwa manager wa mhubiri wa miujiza na uponyaji aitwaye William Branham), katika ujumbe wake alimwambia nimeona maono kadhaa moja wapo ilikuwa Bwana anamwondoa Branham kwa sababu ya damage anayoileta kwenye mwili wa Kristo kimafundisho. Baada ya miezi kadhaa kupita na mhubiri huyo kupatikana katika ajali ya gari na kuwa katika comma na badae kufariki, Lindsay alimjibu Hagin kuwa mtu uliyetoa unabii juu yake amefariki. Lindsay alisisitiza kusema, nilimwambia brother Branham wewe si mwalimu, unachanganya waamini, hubiri neno kisha tumia karama za miujiza na kuponya. Majibu ya Branham kwa Lindsay yalikuwa, "najua mimi si mwalimu, lakini nataka kufundisha, na nitafundisha". Unaweza kuwa na karama kuu za kiroho zenye mvuto mwingi, ila kama hukupewa kufundisha kila ufanyapo hivyo unaweza kuwaelekeza watu katika makosa. Kabla ya Lindsay kuondoka kwenye utumishi wa Branham alisaidia kuleta balance ya mambo mengi kimafundisho (NB:- SIPO KINYUME NA HAWA WOTE NILIOWATAJA AKIWEMO HUYO BRANHAM W.M, NIMETUMIA KISA CHAO KUFUNDISHA TU).

Siku moja nikiwa naandika ufafanuzi wa sura 12 za Daniel (April 2020), nilipofika sura ya 7, 8, 9, & 12 nikajigundua nimekaa nikiwa natumia nyenzo kadhaa mpaka scientific calculator (Niliandika masomo hayo baada ya Mungu kwa Roho Mtakatifu kuniahidi katika ndoto kuwa wiki hiyo atanipa kuelewa hicho kitabu). Nikasema Mungu kama imenibidi nipitie haya ili kukielewa kitabu hiki  Je! itakuwaje kwa wengine ambao labda hawana kipawa cha hivyo, ilikusudiwa wote waelewe? hapo hapo jibu la Mungu kwangu likawa, kila mahali kuna watu waliopewa vipawa vya kufanya uchambuzi wa maandiko (Labda kama hawatatumiwa, au kunyamazishwa). Na hapa niandike ushauri tu kwa viongozi wa makanisa, wasizime vipawa vya waliopewa kufundisha, kwa kuwa unaweza kuwa senior pastor lakini labda una neema ya kuhubiri tu si kufundisha, ukawa na watu dhaifu kwa upande wa fundisho la Kristo, wakasombwa na ukengeufu wowote utakaojitokeza, kumbe hawakupata nafasi ya kufundishwa. Nimesoma andiko la mtu mmoja kasema walimu wanaofundisha masomo ya neema wanapenda sana kutumia maneno ya kiyunani na kiebrania na wanatumia ufahamu wao zaidi kuliko ufunuo wa Roho. Walimu wanaweza kuwa na neema tofauti ya kufanya uchambuzi (exposition of scriptural text), ukiwaona huko kwako *WATUMIE*, USIWAPINGE, USISIMAME NAO KINYUME. Kama unakerwa na ufafanuzi wa kutumia Kiyunani na Kiebrania ni wazi tu, hukupewa eneo hilo kutumika na approach hiyo, shughulika na mzingo na mlinganyo uliopewa utumike kwa uaminifu, lakini waliopewa kipawa cha kufundisha wapewe nafasi hiyo ili kuleta balance ya kweli yote ya injili. Ilitolewa kazi kwa wanafunzi *Wafundishe na kuhubiri*,  watu hawawezi kujengwa kwa ukamilifu kwa kuhubiriwa peke yake, kuna mahali fulani hawatafika kimaarifa ya kiroho. Waamini waliojengwa katika kuhubiriwa pekee bila kufundishwa hawawi imara kiasi cha kusimama sana wao wenyewe. Hawa ndio ambao wakipata uhamisho wa kikazi mbali na mahubiri aliyozoeaga kumpiga *handel*, hasongi mbele, hawa ndio ambao mtumishi anayewaongoza kiroho akifariki na wao hawaendelei tena mbio zao za imani, hawa ndio kukitokeza kauvumi ka roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani yanawabeba alfajiri na mapema.

Kama nilivyotangulia kusema, imani ya Ukristo sio ya mchongo. Mafundisho yasiyojengwa au kutokana na kweli ya injili  lazima yawe *terminated*, mafundisho ambayo msingi wake ulikuwa ndoto na maono binafsi ya mtu huku yakikinzana na fundisho la Kristo, na mitume wake na matendo yao sharti liondolewe lisiweke kwazo wala kongwa la utumwa kwa waamini. Waliopewa kuhubiri wahubiri tu, wasijaribiwe kufundisha waka-infuse errors kwa mafundisho yenye makosa (false indoctrination). Waliopewa kufundisha, wafundishe kwa bidii, kwa ustahimilivu, wala wasichoke. Mwili wa Kristo (kanisa) ujazwe kwa maarifa sahihi ya neno la Mungu, na kuwasaidia waamini kuweza kusimama nyakati zote, na kuwa wazoevu wa maneno ya imani. Hawa wataweza kushinda purukushani zote za masuala ya kiimani katika dunia hii mbovu.


Mungu awabariki tukutane sehemu ya 7

alltruth5ministries@gmail.com

Wednesday, November 2, 2022

KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO (PART 5)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
_*Rightly Dividing The Word of Truth*_ (2Timothy 2:15b)
*_Na Mwl Proo_*

*SEHEMU YA TANO* 

```MATOLEO/UTOAJI```

Ili kuepuka kuuliza maswali ambayo yamekwishajibiwa na mfululizo huu, tafadhali soma sehemu nne zilizotangulia. 
Mpaka hapa tulipofika tumeanza kuelewa kuhusu imani yetu ya kumfuata Kristo (Ukristo), tumejua kwa sehemu kubwa kuhusu mwenendo wa waamini, tumeanza pia kufahamu matumizi halali ya neno la kweli. Katika sehemu zilizotangulia tuliona kuwa imani ya kumfuata Kristo (Ukristo) sio imani ya kuunga-unga, haijakosa fundisho la msingi, haihitajiki kujiongeza (mafundisho ya mchongo) kana kwamba kweli haipo. Leo nitazungumzia suala moja tu la muhimu sana yaani UTOAJI (MATOLEO) kwa sura ya Ukristo. 

Nianze kwa kusema, *_"KAMA KUNA FUNDISHO LOLOTE LITAKALOKUELEKEZA WEWE MWAMINI UACHE KUWA MTOAJI, NI LA KULIKATAA, KWA SABABU UKARIMU NI TABIA YAKO KIASILI KWA ASILI MPYA ULIYOIPATA KWA KUWA NDANI YA KRISTO, KIUMBE KIPYA_* 

Pamoja na ukweli huo, bado unahitajika kujifunza usahihi wa utoaji. Hapa inahitajika uvue miwani πŸ‘“ ya kidini na kidhehebu, uweze kuufahamu usahihi wa maandiko na mafundisho kwenye imani hii. Haya ninayofundisha sasa si lazima sana yapatane na kile ulichowahi kufundishwa... Haya yanapatana na ile kweli ya injili, hicho ndicho nina hakika nacho 100%.

Mimi Mwl Proo ni mthiolojia kitaaluma, nilipata kujifunza _Jewish Korbanot Systems_ yaani mifumo ya matoleo ya kiyahudi. Matoleo ya sadaka ya dhambi, ya amani, za kuteketeza, za vyakula zote kwa aina zake na mitindo yake... mafuta, unga, ndege, wanyama na chochote vilikuwa ni mifano (typology) ya sadaka moja ya badae ambayo ilitolewa toka mwanzo. Bila ku-panic soma kwa utulivu tena (Waebrania 10:1-10). 

Jamii ya waamini, baada ya kufa na kufufuka kwa Kristo haiwi tena na mwenendo ule wa kivuli (Kol 2:17, Ebr 10:1), haiongozwi na kiongozi (Gal 3:24, Rumi 10:4) ambacho kiliwekwa kutuleta kwa Kristo tu.

Kutoka katika ufahamu huu, huwezi nyofoa kamstari katika Walawi, bila hata ufahamu wa kutosha wa matoleo ya kiyahudi, ukawaambia waamini jamani neno limesema sadaka ya kuinuliwa, sijui ya kutikiswa, hapana!. 

Leo hii kuna mafundisho mengi ya ovyo-ovyo kama sio ya kujichanganya na ya kinafiki (rough, hypocritic & confusing teachings) kuhusu utoaji, ni kwa vile kulikosekana nafasi ya fundisho la msingi la kanisa pahala pengi, hiyo ikapelekea matumizi yasiyo halali ya neno la kweli. Mafundisho mengi yana mzani wa hadaa (Double-Standard), yaani mtu anataka kwa wakati mmoja atumike na huduma ya mauti, wakati mchache badae atumike na huduma ya roho na ya haki (2Kor 3:7-11).

Leo ninawashangaza kidogo, kuwa mfumo wote wa utoaji, aina zote za matoleo, ikiwa ni pamoja na nia ya kutoa kama ilivyoelezwa kama picha kwenye Torah (Sheria ya Musa) hazihusiki kabisa kwenye imani ya Ukristo (THEY ARE ALL IRRELEVANT IN CHRISTIANITY). Sijachanganyikiwa, wala sijakopi fundisho la watu wala taasisi yoyote. Hiki ndicho kilichopo kwenye imani ya Ukristo, na nitakuonesheni.

 Ndugu zangu waKristo, katika utekelezaji wa sheria 613 (Decalogue inclusive) za Musa kama ulivyofafanuliwa vyema katika Talmud ya wayahudi, ni kosa kubwa kutimiza sheria 599 kwa ukamilifu ukaiacha moja ya 600 (Yakobo 2:10). Ni mchezo wa kuigiza (hypocrisy) katika ulimwengu wa torati kusema unatoa malimbuko (Walawi 23:10), halafu hautoi kodi ya Bwana (Hesabu 31:37, 38, 39). Kwa wasiojua Torati ya Musa, mbali na zaka ambayo kimsingi ni 23%, wayahudi waliamriwa pia kulipa *Kodi ya Bwana* ambayo ni 0.2%, ukitoa zaka ya fungu la kumi (Kumb 22:14), halafu ukaacha kulipa kodi ya Bwana ambayo ni 0.2% wewe ni mnafiki, mwigizaji, mvunja sheria yote, ustahiliye kupata hukumu (Jiulizeni huko kwenu, lini mlitoa kodi ya Bwana? jibu liwajuze kuwa mnaenenda kwa unafiki au kwa ujinga).

Kanisa la mitume (early church) waliweza kutofautisha utoaji kwa waamini, na utoaji waliouzoea mwanzoni wa kiyahudi (kama ilivyoamuru torati). Hawakuendelea na desturi zozote za utoaji za kiyahudi kwenye Ukristo. Kwa nini hawakuendelea nazo, hazikuwa relevant. Fanya study yoyote utakayoiweza ya kanisa lile la mwanzo, hutakutana na utoaji wowote kutoka katika _jewish korbanot system_. Ni wanafunzi wasio makini (careless learners) wa maandiko ndio wanaruka-ruka na mistari nje ya muktadha, utasikia Mathayo 23:23 na Luka 11:42, Yesu amesema wala msiache yale mengine πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚. The Bible Is The Book Of Context (Biblia ni kitabu cha muktadha), hao Mafarisayo (wa chini ya sheria) na Yesu mwenyewe amezaliwa chini ya sheria, walipaswa kuzingatia yote yaliyowahusu chini ya sheria.. iwe tohara, iwe sadaka za kuteketeza na vyakula n.k. Huwezi kurupuka na huo mstari uwasomee waamini kanisani, huku ukiwahimiza jamani Yesu alisema msiache yale mengine.. Huo ni udanganyifu, na matumizi yasiyo halali ya neno la kweli. Kaa chini ujifunze, Je! mitume wa Yesu, kanisa la awali, waliendelea na desturi za matoleo ya kiyahudi? Je! wakristo wa mwanzo huko Uyunani, Uturuki etc walipokutana kwenye makusanyiko yao (kwenye nyumba za watu) hata kabla hawajajenga majengo ya kuabudia, Je! walitoa matoleo ya kiyahudi yoyote? JIBU KUTOKA KATIKA HIYO STUDY YAKO NI *HAPANA*

Ni hivi, wale wa tohara, wale waliopewa sheria walipojaribu kuifuata sana sheria ili kuitenda, walionekana kumpendeza Mungu. Ila waKristo kila wajaribupo kuyafuata maelekezo ya sheria ya Musa kama namna na ya kumcha Mungu, wanamhuzunisha kwa huo ujinga. Najua kiu yenu kubwa sasa, ni Je! tutoeje sasa..!!!! Unasoma kitu sahihi sasa. Katika Ukristo kuna  aina mbili tu za matoleo, ambazo naweza kuzifundisha kwa Biblia, naweza andika vitabu vingi, naweza kueleza na kuthibitisha kwa ushahidi mwingi. Aina hizo za matoleo (utoaji), ni 

1. Sadaka za hiari. Watu kuamua wao wenyewe kwa ukarimu wao watoe nini kwa kiasi gani. Hapa hawapangiwi watoe ngapi, hawatishiwi wasipotoa kupatikana na mabaya yoyote...  (2Korintho 9:7)

2. Changizo (michango) πŸ‘‰ 1Korintho 16:1, Waroma 15:26

Sadaka za hiari (kutokana na ukarimu na tabia ya upendo), na changizo ndiyo matoleo yanayohusiana na imani ya Ukristo... mnaweza kuzipa majina mengi lakini kunabakia makundi hayo mawili. Wakristo hawapaswi kutoa kichoyo kama wale wa jangwani wenye mioyo migumu waliopewa torati. Wakristo wanatoa kwa kadri ya uhitaji, hata pasiwepo upungufu. Kama una million 200 na uhitaji ni million 180, utatoa million 180 kuondoa uhitaji uliopo na sio million 20, kuacha watu wapambane na uhitaji wa million 160. Katika ukristo kama kunahitajika ada za watoto wa mchungaji na jumla ya ada ni million 7, badala ya kuweka kaubunifu ka kitapeli (fraudulence)... kwamba nitagawa bahasha za kinabii (prophetic envelopes) ✉️✉️✉️✉️✉️ weka sadaka inayouma, uuguse moyo wa Mungu.... wekeni tu changizo kupata hizo million 7 basi. Matoleo katika Ukristo ni sadaka ambazo watu watatoa wenyewe kwa kuamua wao viwango, na nje hapo ni changizo (michango)..... *CHOCHOTE NJE YA HAPA NI CHA MCHONGO, SADAKA YOYOTE ILIYOAMRIWA NA MUSA IKILETWA KANISANI NI YA MCHONGO, HAINA UHUSIANO NA UKRISTO.* Usikasirike huu ni ukweli, hata kama baada ya hapa tutaendelea na desturi  za dini na madhehebu yetu, tuendelee na mazoea yetu tukiwa tumeshaufahamu ukweli na usahihi.
_mwlproo_
Kuna watu kadhaa wamejirudi wenyewe siku za usoni, huku wakisema katika Agano Jipya (ambalo nalo hawalijui wanahisi ni hivi vitabu/barua 27) kwamba tunatoa malimbuko na zaka kwa upendo sio kwa mujibu wa sheria. Kwa wakati huo huo bado wananukuu Malaki 3:8-11. Ili Malaki 3:8-11 iwe katika kutumika (in effect) ni lazima Malaki 4:4 iwe katika kutumika... Sheria na amri haziwekwi bila hukumu zake.... Yaani ukimriwa usizini, basi kuna hukumu yake ukiivunja upigwe mawe. Double Standards nilizozitaja mwanzo ni kuchagua kaupande kamoja, na kukatupa nje kaupande kengine (unafiki/ujinga πŸ‘‰ one of the two is correct).
Mara kadhaa nasikia watu wakiombea sadaka wananukuu Kutoka 34:20b, kwamba Mungu ulisema tusije mbele zako mikono mitupu. Nyie watu!!!!!!!  mnadhani kila agizo la torati mliambiwa ninyi? Kwa taarifa yenu Wakristo hawatoi matoleo kwamba wameagizwa, HAPANA! Tabia ya ukarimu (generosity) ya Baba yao (Mungu) ipo ndani yao tayari kwa kuzaliwa kwa pili... Kutoka katika huo ukarimu ndio wanatoa.. Kama hawatoi haina maana hawajazaliwa na Mungu, wafundishwe tu mafundisho sahihi ya injili, watambue asili yao mpya ina tabia zipi, watatoa mpaka hakutakuwa na uhitaji. Kuamini kwamba Mungu amewaagiza msiende mbele zake bila kitu mkononi ni kujifunga kwenye kongwa la utumwa.... PIA KILA ITAKAPOTOKEA UMEHUDHURIA IBADA UKIWA HUNA SADAKA, ITAHESABIWA KUWA NI DHAMBI. Wakristo wakomavu hawawezi kuwa kwenye makusanyiko ya ibada bila fedha na mali za kusapoti kazi ya Mungu, na kusapoti maisha ya wanaoitenda kazi ya Mungu. Lakini si kwa agizo la KUTOKA 34:20b, na hivyo kama hawana wasiache kuhudhuria, na wasipotoa hawakuhumiwi wala kulaaniwa. Yale mengine ya mchongo mfano:-kuhimizana kuwa ukiweka nadhiri (vowed offerings) inamhamasisha Mungu atende kwa haraka, ni maudambudambu tu ya kidini nje ya muktadha wa Kikristo. Baba yake Yesu ambaye ni Baba yetu hahitaji kupigwa _Handel_ ili kumhamasisha awe mwema au mkarimu. Hasubiri ahadi za 'ee Mungu nikipata ile kazi, nitanunua viti vya kanisani....' Yeye kwa njia Yesu, pamoja na Yesu amekupa vyote, unaweza kupata chochote (Waroma 8:32). Ila kama mnapenda kuwa na vitu vya mchongo endeleeni kuweka nadhiri mkiamini Yesu na mitume wake walipitiwa kuwafundisha tabia za Baba yenu wa Mbinguni!

*KUHUSU LAANA* 
Wakristo wapuuziaji (Careless Christians) ndio  pekee wanasoma Malaki 3:9 na kuamua kulibinafsisha hili andiko.... Kuwa nimelaaniwa kwa laana, na taifa hili lote.... kisa nini?????? Eti nilipewa elfu 2 ya nauli na sikuitolea 10% yaani  shilingi 200. So unahisi Yesu na Baba Yake (Mungu) wanashirikiana kukulaani kila wakigundua kuna msimbazi ulipewa 10,000/= na hukutoa buku (1000/=) bali uliitumia yote kulipa deni fulani pale  Mangi Shop????😝😝😝😝
_mwlproo_
Ndugu zangu katika Kristo, hakuna laana inayokuja kwa mtoto wa Mungu toka kwa Baba yake kisa amekosea au kutofanya jambo fulani bila ukamilifu. Si tabia ya Mungu, na wala shetani hawezi. Na huo ndio mvuto wa kuiamini injili. Hakuna mtu anayeweza kukulaani wewe mwamini, mwenye maarifa sahihi ya Yesu. Tena kama kuna kiongozi wa kiroho aliwahi kukulaani na ukalaanika, hii inawezekana tu kwa kuwa wewe umejiweka (submit)  chini yake kifundisho na maongozi ya kiroho.. Ambako hapo napo bado itategemea una-operate kwa kiwango kipi katika maarifa ya kiroho (ya kumfahamu sana Mwana wa Mungu, Yesu Kristo)... Otherwise mikwamo yote unayokutana nayo, sio matokeo ya kulaaniwa...USIIBIWE, unaweza kutoka tu kuyatumia mamlaka yako uliyoyapewa na Kristo na kufanya bidii ya kazi na matendo mema... 

*UKIRI*
Mimi ni mwamini, nimebarikiwa. Nitafanya kazi kwa bidii, nipate fedha na mali za kusaidia uhitaji na wahitaji. Nitatoa daima maana ndio tabia yangu katika Kristo. Bwana wangu Yesu amenionesha njia njema, kuwa ni bora kutoa kuliko kupokea (Matendo 20:35). Hivyo nitatoa, kama Bwana wangu alivyo mkarimu, mimi pia nitaonesha ukarimu kwa kutoa sana sana sana.


USIKOSE SEHEMU YA SITA (6) YA SOMO HILI TUTAPIGA HATUA KUINGIA NDANI ZAIDI

0762879363 (WhatsApp)

alltruth5ministries@gmail.com

Sunday, October 16, 2022

KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO (PART 4)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
_*Rightly Dividing The Word of Truth*_ (2Timothy 2:15b) 
_mwlproo_

*SEHEMU YA NNE*

_YESU ALIMFUNUA MUNGU NA TABIA ZAKE KWA WATOTO WAKE_

Kama hujasoma sehemu ya kwanza, ya pili, na ya tatu ya mfululizo huu, usijaribu kabisa kusoma sehemu hii, haitaeleweka!.
Kama tulivyoona sehemu ya tatu, kwamba imani ya   Ukristo sio imani ya kuunga-unga, sio imani isiyo na fundisho la msingi kiasi cha kufanya kila mtu kujiongeza kwa chochote anachobahatisha kukisoma kutoka kwenye Biblia. Imani ya Ukristo (Kumfuata Kristo) inaongozwa na fundisho la Kristo na Mitume wake, na yote yaliyoandikwa kwenye Torati, Zaburi, na Manabii yaliyomweleza Kristo kwa picha (typologically), yataelezwa kwa kutokea kwa Kristo au Kristo kama kiini (Christocentrically). Kuna mahali nilihudhuria mkesha mwaka 2011, na somo la mkesha wa maombi lilikuwa, *KUKATALIWA NA BWANA*, mhubiri alitia mkazo mkubwa kwamba kama kuna jambo haukumtii Mungu, Mungu amekukataa tayari, hata kama umekuja kuomba, ila Mungu amekukataa.. huku akiongezea na andiko toka 1Samweli 16:1-2. Somo hilo linaonekana kuwa zuri, ila lina makosa mengi kwenye ujuzi wa Mungu kupitia Kristo. Lilifanya watu kuona hawastahili, wametengwa na Mungu, uhusiano wao na Mungu ni kama umeungwa kwa _Sellotape_, na kwamba makosa yao yanawafanya mara moja kuwa sio watoto wa Mungu tena. Watoto wa Mungu hawakataliwi na Mungu (Baba yao) kwa kukosea, pamoja na ukweli kwamba wanapaswa kujifunza namna ya kujenga tabia za uungu kama watoto wa Mungu wawe na mienendo isiyolaumika kabisa. Ili kuepuka makosa ya nini sio sahihi kuhusu Mungu, kipi sio sifa na tabia yake, yapi yasiyo matendo yake kwa watoto wake, ni lazima kujifunza kuhusu Mungu kwa kutokea kwa Mwanae, Yesu Kristo aliyemfunua (Yohana 1:18, Ebrania 1:1).

A. *MTAZAMO USIO SAHIHI WA KUWAJIBISHWA KWA KUKOSEA*

Watu wengi wametumia andiko kama Ufunuo 3:19, bila ku-exegete (rejea sehemu ya pili kuhusu exegesis), na kutoka na mahitimisho kuwa watu wa Mungu wanaweza kupigwa na Mungu, kupatwa na mabaya ikiwa ni sehemu ya kuonesha Mungu anawapenda, ili warudi watubu. Mtu anafanya matumizi ya mstari huo nje ya muktadha, bila kuzingatia ujumbe wote kwa kanisa la Laodikia, na kuupuza kabisa simulizi ya andiko kimuktadha (history of the text & history in the text). Dhana hii inaenda mbali zaidi ya hapo, wengi wenye dhana hii wamekuwa wakisoma vitu jumla jumla bila kuwa na msingi mzuri kwenye fundisho la Kristo na Mitume. wanachotumia ni kile kiitwacho kitaalamu *_DEUTORONOMISTIC VIEW OF HISTORY_*  yaani, "You  do good, you're rewarded. You do bad, you get punished". Hiki kimetawala sehemu kubwa ya mafundisho ya makanisani. Hakijasaidia kujenga wakristo kama namna ambavyo  kimewaletea mashaka tu, mpaka sasa watu walio ndani ya Yesu  wanaulizana ukifa sasa hivi utaenda wapi? Parapanda ikilia 🎺  utanyakuliwa kweli? Watu hata hawaelewi ni basi tu wanaendelea kujifariji kwa sala za kutubu za asubuhi, mchana, na usiku muda wa kulala. Mtazamo huo hauwasogezi watu kwa Mungu, unawaweka mbali. Upi mtazamo sahihi kwa imani ya Kikristo?? Endelea kufuatilia mfululizo huu, ukifika sehemu ya 10 utakuwa tayari na kilicho halisi kwa imani hii.

Unajua mtu anajisomea zake kitabu cha Yeremia, bila ufahamu wa kutosha   wa injili, anaibuka na taswira yake kuhusu Mungu kwa namna isiyo sahihi. Kuanzia Yeremia sura ya 14,  mpaka utimilifu wa unabii wa kwenda utumwani, kila mahali anasoma Mungu atawaletea njaa, atawapiga kwa tauni na upanga kwa kuwa mmemwudhi na kumtenda dhambi... Hivyo utamaliza umemfahamu Mungu kwa ufunuo wenye muktadha huo, kuwa Mungu amekaa zake huko, anasubiri ukosee ili akuadhibu kwa majanga fulani fulani. Hii imepelekea waamini (Wakristo) kudhania magumu mbalimbali, magonjwa, ajali, kupungukiwa kokote kunapowakuta (umaskini), ni adhabu na laana toka kwa Mungu. Hata yale ambayo walipaswa wao kwa mamlaka waliyopewa wayaondoe kutoka katika maisha yao, bado wanaendelea kulia nayo, wakiamini wanapaswa kusali kwa kuomba msamaha kwa Mungu. Haya yote hayako sahihi kwa mtazamo wa mafundisho ya  msingi katika Kristo.

*B. KUTUMIA NGUVU ZA MUNGU KUDHURU WATU*

Yesu aliyemfunua Baba yake wa upendo  (God of Love), ametufundisha njia sahihi ya kuzitumia nguvu za Mungu. Yesu hakuwahi kuzitumia nguvu za Mungu kuangamiza uhai, bali kuokoa na kuponya. Kama Yesu katika huduma yake angeua mtu mmoja, au wawili watatu, asingekuwa tofauti sana na Mtume Muddy (Muhammad) ambaye katika maisha yake mbali na kuagiza wafuasi wake kuua, aliwahi kupigana na mtu (Ubayyi ibn Khalaf) na kumwua. Kama Yesu angefanya kitu cha namna hiyo,  Mimi Mwl Proo, nisingekubali kumfuata, nisingemwamini. 

Hatujifunzi tabia za Mungu, wala mwenendo wa Ukristo mbali na tabia   zilizofunuliwa na Yesu. Ukichomoa-chomoa vifungu vya Biblia na kuvifanyia kazi ukiamini tu kwa kuwa vipo kwa Biblia basi vinakuhusu kama vilivyoandikwa, unaweza kuzitenda kazi za shetani kwa kutumia nguvu za Mungu. Ukisoma Luka 9:51-56, utaona kisa cha wanafunzi wa Yesu waliotaka kujifunza tabia za Mungu toka kwa Eliya... Na Yesu akawaambia sio kwa Roho wa Mungu wanataka kufanya hilo, bali wanasukumwa na roho nyingine, kuzitumia nguvu za Mungu kudhuru wanadamu. Yesu katika huduma yake hakuwahi kudhuru uhai wa mwanadamu aliyekuja kumfia, ampe uzima wa milele uliopotezwa. Aliwahi kuudhuru mtini (fig-tree), na labda kuruhusu wale pepo kuwaingia nguruwe, ambapo nguruwe wale walifia majini πŸ–πŸ–πŸ–πŸ– 🌊 ,tunaweza kutaja kuhusu matumizi ya kikoto cha kambaa hekaluni? hakutoa uhai wa mtu zaidi ya kuleta order (utaratibu) hekaluni.  Ukiondoa visa hivyo vya Yesu ambavyo havihusishi uhai wa mwanadamu, Yesu hakuwahi kwa sababu yoyote kuangamiza. Hii ndiyo standard ya Ukristo, kuokoa sio kuua, kuponya na sio kuangamiza!

i.) Eliya alichinja watu na kuutoa uhai wao. Eliya alitumia upako wake kuruhusu moto uunguze watu... Moto πŸ”₯  ukashuka na kugeuza watu mishikaki... Wengi mkisoma mnafurahi, mnatamani kufanya kama yeye. Hilo kwa muktadha wa Ukristo ni matumizi mabaya ya nguvu za Mungu (Hatupaswi kuliiga hilo)

ii.) Elisha alipotaniwa na wale vijana (2Falme 2:23-24), aliwalaani kwa Jina la Bwana, wakaja dubu 🐻  🐻 . Ni Yeye Elisha aliutumia upako wa kiMungu ndani yake kufanya dubu waje kuwaua wale vijana. Mwenendo huo wa kina Elisha sio wa kiKristo, na wala waKristo hawajifunzi tabia za kuwadhuru watu wanaowaudhi.

iii.) Kuna mahali nilisema Petro ndiye aliyewaua Anania na mkewe Safira, na watu wakakataa, sikuwalazimisha maana nilijua nipo na watu ambao hawajafahamu kweli na neno la haki kwa  kiwango hicho. Lakini hebu nikuulize mtu mwenye upako wa Mungu ndani yake, ambaye akitembea kivuli chake kinaondoa maradhi yote kwa wagonjwa, mtu ambaye akimwinamia mfu  anafufuka mara moja. Je! kwa upako huo akiwa na shauku ndani kuona mtu ameadhibiwa mara moja kwa makosa yake, unadhani huo upako hauwezi kufanya mtu apoteze maisha?. Usianze kufikiria Petro ambaye ni mkamilifu sana, chukua picha ya Petro ambaye naye pia bado anakua katika neema, lakini upako unatenda kazi kwa kiasi kile. Soma maneno ya Petro kwa mke wa Anania, utagundua moyoni mwake alikuwa aki-execute hukumu ya kosa la wanandoa wale, upako ulio ndani yake ungeweza kuwaponya au kuwaua. Na ni wazi kwamba Petro alikuwa katika neema na kulifahamu pendo la Mungu, hakuna visa tena vya yeye kuruhusu upako wa kiMungu kuua watu. Hapo unachagua kujifunza kwa Yesu, aliyeonesha namna njema ya kutumia nguvu za Mungu ndani yako. Pia jiulize mambo mangapi huko kanisani kwenu mmevunja makubaliano yawe ni masuala ya fedha, mali, n.k, Je! mlipokosa uaminifu mmekufa? Mbona hatusikii vifo vya wakosaji huko kanisani kwenu??

iv.) Tunao waKristo wengi siku hizi, wanapita mbele kutoa shuhuda jinsi walivyoomba mpaka waganga, wachawi walivyokufa baada ya maombi yao. This is 'abuse of power' (matumizi mabaya ya nguvu). Kwenye Agano Jipya, wachawi, waganga, na washirikina wote ni wenye dhambi kama wenye dhambi wengine tu, hawana lolote la ziada. Makosa yale-yale niliyoyaeleza sehemu zilizopita yanafanya waKristo wasio na ufahamu wanukuu KUTOKA 22:18, na kuanza kuua wachawi. Mungu haui hao wachawi, ila ni ninyi wakristo mnaziruhusu nguvu za Mungu (zinazoweza kuokoa) ziwaue. Ni aibu kwa mwamini kupita mbele kushuhudia kuwa kuna mganga mtaani kwetu nilifunga siku tatu, na sasa kuna mazishi yake. 

*KUNA WATU UTASIKIA WAKISEMA, "UKRISTO SIO UJINGA". NI KWELI KABISA UKRISTO SIO UJINGA, ILA KUOMBA MAOMBI KUUA WAGANGA NA WACHAWI NI UJINGA. MNAO UWEZO WA KUHARIBU KAZI ZOTE ZA UCHAWI, NA UTENDAJI WOTE WA KIPEPO NA MASHETANI, ILA SIO KUUA WANADAMU WANAOTUMIKISHWA NA  ROHO HIZO ZA KICHAWI.*

*KAMA KUNA NGUVU ZA KICHAWI, ZA KIGANGA, ZA KIPEPO ZILIFANYA KAZI NA KUKUDHURU MWAMINI, HIYO NI MATOKEO YA WEWE MWAMINI KUKOSA MAARIFA TU. MAANA UKWELI NI KWAMBA, HAKUNA LEVEL YOYOTE KWENYE FALME ZA GIZA NA MAMLAKA ZOTE, ZINAZOWEZA KUMDHURU MTOTO WA MUNGU (MWAMINI), MWENYE MAARIFA SAHIHI YA KAZI ALIYOIFANYA YESU, NA NAFASI YA MWAMINI HUKO ROHONI. SO BADALA YA KUHANGAIKA KUUA WACHAWI, TAFUTA MAARIFA SAHIHI, WAFUNDISHE NA WENGINE*


C. *MATUMIZI MABAYA YA MAANDIKO YASIYO NA MUKTADHA WA KIKRISTO KWENYE MAHUBIRI NA NYIMBO ZA KIDINI*

Mtu yuko huru kuhubiri au kuimba ujumbe wa Biblia toka katika kitabu chochote tu, ila kiwango (standard) cha kupimwa kwa ujumbe huo ni fundisho la Kristo na Mitume wake. Huwezi kunyofoa andiko la Ayubu sura ya kwanza, kwamba Ayubu alinyoa kichwa chake baada ya kufiwa, nawe ukalitumia tu yaani, tukakuta msibani wafiwa waKristo mmenyoa vichwa vyenu. Nimesikia mahubiri, nyimbo zikitungwa kwa kutumia zaburi na kutumika kwenye muktadha wa Ukristo, haya mambo hayaendi hivyo ndugu zangu. Mfano Daudi akisema  wokovu (soter) hakumaanisha huu wokovu tulioupata kwa kufa na kufufuka kwa Yesu. Kwake wokovu ilikuwa ni yeye kufanikiwa kuua maadui zake, kuwapiga mishale 🏹  askari wa nchi jirani, akarudi jioni hajafa. Kumbuka aliwaua kabisa iwe kwa upanga, iwe mkuki au mawe ya teo, aliua wakubwa kwa wadogo, wanaume kwa wanawake.... (kwake mauaji hayo ndiyo anayaita wokovu una Bwana). Sasa ghafula anatokeza mwimbaji anafungua ZABURI 109:6-20, Naye anatunga wimbo akiwaombea wanaomwudhi na maadui zake (wanadamu) wakutwe na hayo aliyoyata Daudi yatimizwe kwa washtaki wake na maadui zake. Ukristo haufundishi hivi, tabia za Wakristo wanajifunza kwa Yesu, tabia za Mungu, na matumizi ya nguvu za Mungu ndani yao wanajifunza kwa Yesu Kristo. Hivyo utunzi wa nyimbo za kiKristo au mahubiri, lazima yawe sambamba na fundisho la msingi ndani ya Ukristo (The teachings, preachings, songs should be in-line with the truth of the gospel)

NAKUPA SHAURI, USIKOSE SEHEMU YA TANO (5) YA MFULULIZO HUU. TUTAJIFUNZA KITU CHA MUHIMU SANA CHA KUYAFAA MAKANISA YA MUNGU POPOTE YATAKAPOFIKA MAARIFA HAYO.

Mwl Proo
0762879363

alltruth5ministries@gmail com