Sunday, October 16, 2022

KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO (PART 4)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
_*Rightly Dividing The Word of Truth*_ (2Timothy 2:15b) 
_mwlproo_

*SEHEMU YA NNE*

_YESU ALIMFUNUA MUNGU NA TABIA ZAKE KWA WATOTO WAKE_

Kama hujasoma sehemu ya kwanza, ya pili, na ya tatu ya mfululizo huu, usijaribu kabisa kusoma sehemu hii, haitaeleweka!.
Kama tulivyoona sehemu ya tatu, kwamba imani ya   Ukristo sio imani ya kuunga-unga, sio imani isiyo na fundisho la msingi kiasi cha kufanya kila mtu kujiongeza kwa chochote anachobahatisha kukisoma kutoka kwenye Biblia. Imani ya Ukristo (Kumfuata Kristo) inaongozwa na fundisho la Kristo na Mitume wake, na yote yaliyoandikwa kwenye Torati, Zaburi, na Manabii yaliyomweleza Kristo kwa picha (typologically), yataelezwa kwa kutokea kwa Kristo au Kristo kama kiini (Christocentrically). Kuna mahali nilihudhuria mkesha mwaka 2011, na somo la mkesha wa maombi lilikuwa, *KUKATALIWA NA BWANA*, mhubiri alitia mkazo mkubwa kwamba kama kuna jambo haukumtii Mungu, Mungu amekukataa tayari, hata kama umekuja kuomba, ila Mungu amekukataa.. huku akiongezea na andiko toka 1Samweli 16:1-2. Somo hilo linaonekana kuwa zuri, ila lina makosa mengi kwenye ujuzi wa Mungu kupitia Kristo. Lilifanya watu kuona hawastahili, wametengwa na Mungu, uhusiano wao na Mungu ni kama umeungwa kwa _Sellotape_, na kwamba makosa yao yanawafanya mara moja kuwa sio watoto wa Mungu tena. Watoto wa Mungu hawakataliwi na Mungu (Baba yao) kwa kukosea, pamoja na ukweli kwamba wanapaswa kujifunza namna ya kujenga tabia za uungu kama watoto wa Mungu wawe na mienendo isiyolaumika kabisa. Ili kuepuka makosa ya nini sio sahihi kuhusu Mungu, kipi sio sifa na tabia yake, yapi yasiyo matendo yake kwa watoto wake, ni lazima kujifunza kuhusu Mungu kwa kutokea kwa Mwanae, Yesu Kristo aliyemfunua (Yohana 1:18, Ebrania 1:1).

A. *MTAZAMO USIO SAHIHI WA KUWAJIBISHWA KWA KUKOSEA*

Watu wengi wametumia andiko kama Ufunuo 3:19, bila ku-exegete (rejea sehemu ya pili kuhusu exegesis), na kutoka na mahitimisho kuwa watu wa Mungu wanaweza kupigwa na Mungu, kupatwa na mabaya ikiwa ni sehemu ya kuonesha Mungu anawapenda, ili warudi watubu. Mtu anafanya matumizi ya mstari huo nje ya muktadha, bila kuzingatia ujumbe wote kwa kanisa la Laodikia, na kuupuza kabisa simulizi ya andiko kimuktadha (history of the text & history in the text). Dhana hii inaenda mbali zaidi ya hapo, wengi wenye dhana hii wamekuwa wakisoma vitu jumla jumla bila kuwa na msingi mzuri kwenye fundisho la Kristo na Mitume. wanachotumia ni kile kiitwacho kitaalamu *_DEUTORONOMISTIC VIEW OF HISTORY_*  yaani, "You  do good, you're rewarded. You do bad, you get punished". Hiki kimetawala sehemu kubwa ya mafundisho ya makanisani. Hakijasaidia kujenga wakristo kama namna ambavyo  kimewaletea mashaka tu, mpaka sasa watu walio ndani ya Yesu  wanaulizana ukifa sasa hivi utaenda wapi? Parapanda ikilia 🎺  utanyakuliwa kweli? Watu hata hawaelewi ni basi tu wanaendelea kujifariji kwa sala za kutubu za asubuhi, mchana, na usiku muda wa kulala. Mtazamo huo hauwasogezi watu kwa Mungu, unawaweka mbali. Upi mtazamo sahihi kwa imani ya Kikristo?? Endelea kufuatilia mfululizo huu, ukifika sehemu ya 10 utakuwa tayari na kilicho halisi kwa imani hii.

Unajua mtu anajisomea zake kitabu cha Yeremia, bila ufahamu wa kutosha   wa injili, anaibuka na taswira yake kuhusu Mungu kwa namna isiyo sahihi. Kuanzia Yeremia sura ya 14,  mpaka utimilifu wa unabii wa kwenda utumwani, kila mahali anasoma Mungu atawaletea njaa, atawapiga kwa tauni na upanga kwa kuwa mmemwudhi na kumtenda dhambi... Hivyo utamaliza umemfahamu Mungu kwa ufunuo wenye muktadha huo, kuwa Mungu amekaa zake huko, anasubiri ukosee ili akuadhibu kwa majanga fulani fulani. Hii imepelekea waamini (Wakristo) kudhania magumu mbalimbali, magonjwa, ajali, kupungukiwa kokote kunapowakuta (umaskini), ni adhabu na laana toka kwa Mungu. Hata yale ambayo walipaswa wao kwa mamlaka waliyopewa wayaondoe kutoka katika maisha yao, bado wanaendelea kulia nayo, wakiamini wanapaswa kusali kwa kuomba msamaha kwa Mungu. Haya yote hayako sahihi kwa mtazamo wa mafundisho ya  msingi katika Kristo.

*B. KUTUMIA NGUVU ZA MUNGU KUDHURU WATU*

Yesu aliyemfunua Baba yake wa upendo  (God of Love), ametufundisha njia sahihi ya kuzitumia nguvu za Mungu. Yesu hakuwahi kuzitumia nguvu za Mungu kuangamiza uhai, bali kuokoa na kuponya. Kama Yesu katika huduma yake angeua mtu mmoja, au wawili watatu, asingekuwa tofauti sana na Mtume Muddy (Muhammad) ambaye katika maisha yake mbali na kuagiza wafuasi wake kuua, aliwahi kupigana na mtu (Ubayyi ibn Khalaf) na kumwua. Kama Yesu angefanya kitu cha namna hiyo,  Mimi Mwl Proo, nisingekubali kumfuata, nisingemwamini. 

Hatujifunzi tabia za Mungu, wala mwenendo wa Ukristo mbali na tabia   zilizofunuliwa na Yesu. Ukichomoa-chomoa vifungu vya Biblia na kuvifanyia kazi ukiamini tu kwa kuwa vipo kwa Biblia basi vinakuhusu kama vilivyoandikwa, unaweza kuzitenda kazi za shetani kwa kutumia nguvu za Mungu. Ukisoma Luka 9:51-56, utaona kisa cha wanafunzi wa Yesu waliotaka kujifunza tabia za Mungu toka kwa Eliya... Na Yesu akawaambia sio kwa Roho wa Mungu wanataka kufanya hilo, bali wanasukumwa na roho nyingine, kuzitumia nguvu za Mungu kudhuru wanadamu. Yesu katika huduma yake hakuwahi kudhuru uhai wa mwanadamu aliyekuja kumfia, ampe uzima wa milele uliopotezwa. Aliwahi kuudhuru mtini (fig-tree), na labda kuruhusu wale pepo kuwaingia nguruwe, ambapo nguruwe wale walifia majini 🐖🐖🐖🐖 🌊 ,tunaweza kutaja kuhusu matumizi ya kikoto cha kambaa hekaluni? hakutoa uhai wa mtu zaidi ya kuleta order (utaratibu) hekaluni.  Ukiondoa visa hivyo vya Yesu ambavyo havihusishi uhai wa mwanadamu, Yesu hakuwahi kwa sababu yoyote kuangamiza. Hii ndiyo standard ya Ukristo, kuokoa sio kuua, kuponya na sio kuangamiza!

i.) Eliya alichinja watu na kuutoa uhai wao. Eliya alitumia upako wake kuruhusu moto uunguze watu... Moto 🔥  ukashuka na kugeuza watu mishikaki... Wengi mkisoma mnafurahi, mnatamani kufanya kama yeye. Hilo kwa muktadha wa Ukristo ni matumizi mabaya ya nguvu za Mungu (Hatupaswi kuliiga hilo)

ii.) Elisha alipotaniwa na wale vijana (2Falme 2:23-24), aliwalaani kwa Jina la Bwana, wakaja dubu 🐻  🐻 . Ni Yeye Elisha aliutumia upako wa kiMungu ndani yake kufanya dubu waje kuwaua wale vijana. Mwenendo huo wa kina Elisha sio wa kiKristo, na wala waKristo hawajifunzi tabia za kuwadhuru watu wanaowaudhi.

iii.) Kuna mahali nilisema Petro ndiye aliyewaua Anania na mkewe Safira, na watu wakakataa, sikuwalazimisha maana nilijua nipo na watu ambao hawajafahamu kweli na neno la haki kwa  kiwango hicho. Lakini hebu nikuulize mtu mwenye upako wa Mungu ndani yake, ambaye akitembea kivuli chake kinaondoa maradhi yote kwa wagonjwa, mtu ambaye akimwinamia mfu  anafufuka mara moja. Je! kwa upako huo akiwa na shauku ndani kuona mtu ameadhibiwa mara moja kwa makosa yake, unadhani huo upako hauwezi kufanya mtu apoteze maisha?. Usianze kufikiria Petro ambaye ni mkamilifu sana, chukua picha ya Petro ambaye naye pia bado anakua katika neema, lakini upako unatenda kazi kwa kiasi kile. Soma maneno ya Petro kwa mke wa Anania, utagundua moyoni mwake alikuwa aki-execute hukumu ya kosa la wanandoa wale, upako ulio ndani yake ungeweza kuwaponya au kuwaua. Na ni wazi kwamba Petro alikuwa katika neema na kulifahamu pendo la Mungu, hakuna visa tena vya yeye kuruhusu upako wa kiMungu kuua watu. Hapo unachagua kujifunza kwa Yesu, aliyeonesha namna njema ya kutumia nguvu za Mungu ndani yako. Pia jiulize mambo mangapi huko kanisani kwenu mmevunja makubaliano yawe ni masuala ya fedha, mali, n.k, Je! mlipokosa uaminifu mmekufa? Mbona hatusikii vifo vya wakosaji huko kanisani kwenu??

iv.) Tunao waKristo wengi siku hizi, wanapita mbele kutoa shuhuda jinsi walivyoomba mpaka waganga, wachawi walivyokufa baada ya maombi yao. This is 'abuse of power' (matumizi mabaya ya nguvu). Kwenye Agano Jipya, wachawi, waganga, na washirikina wote ni wenye dhambi kama wenye dhambi wengine tu, hawana lolote la ziada. Makosa yale-yale niliyoyaeleza sehemu zilizopita yanafanya waKristo wasio na ufahamu wanukuu KUTOKA 22:18, na kuanza kuua wachawi. Mungu haui hao wachawi, ila ni ninyi wakristo mnaziruhusu nguvu za Mungu (zinazoweza kuokoa) ziwaue. Ni aibu kwa mwamini kupita mbele kushuhudia kuwa kuna mganga mtaani kwetu nilifunga siku tatu, na sasa kuna mazishi yake. 

*KUNA WATU UTASIKIA WAKISEMA, "UKRISTO SIO UJINGA". NI KWELI KABISA UKRISTO SIO UJINGA, ILA KUOMBA MAOMBI KUUA WAGANGA NA WACHAWI NI UJINGA. MNAO UWEZO WA KUHARIBU KAZI ZOTE ZA UCHAWI, NA UTENDAJI WOTE WA KIPEPO NA MASHETANI, ILA SIO KUUA WANADAMU WANAOTUMIKISHWA NA  ROHO HIZO ZA KICHAWI.*

*KAMA KUNA NGUVU ZA KICHAWI, ZA KIGANGA, ZA KIPEPO ZILIFANYA KAZI NA KUKUDHURU MWAMINI, HIYO NI MATOKEO YA WEWE MWAMINI KUKOSA MAARIFA TU. MAANA UKWELI NI KWAMBA, HAKUNA LEVEL YOYOTE KWENYE FALME ZA GIZA NA MAMLAKA ZOTE, ZINAZOWEZA KUMDHURU MTOTO WA MUNGU (MWAMINI), MWENYE MAARIFA SAHIHI YA KAZI ALIYOIFANYA YESU, NA NAFASI YA MWAMINI HUKO ROHONI. SO BADALA YA KUHANGAIKA KUUA WACHAWI, TAFUTA MAARIFA SAHIHI, WAFUNDISHE NA WENGINE*


C. *MATUMIZI MABAYA YA MAANDIKO YASIYO NA MUKTADHA WA KIKRISTO KWENYE MAHUBIRI NA NYIMBO ZA KIDINI*

Mtu yuko huru kuhubiri au kuimba ujumbe wa Biblia toka katika kitabu chochote tu, ila kiwango (standard) cha kupimwa kwa ujumbe huo ni fundisho la Kristo na Mitume wake. Huwezi kunyofoa andiko la Ayubu sura ya kwanza, kwamba Ayubu alinyoa kichwa chake baada ya kufiwa, nawe ukalitumia tu yaani, tukakuta msibani wafiwa waKristo mmenyoa vichwa vyenu. Nimesikia mahubiri, nyimbo zikitungwa kwa kutumia zaburi na kutumika kwenye muktadha wa Ukristo, haya mambo hayaendi hivyo ndugu zangu. Mfano Daudi akisema  wokovu (soter) hakumaanisha huu wokovu tulioupata kwa kufa na kufufuka kwa Yesu. Kwake wokovu ilikuwa ni yeye kufanikiwa kuua maadui zake, kuwapiga mishale 🏹  askari wa nchi jirani, akarudi jioni hajafa. Kumbuka aliwaua kabisa iwe kwa upanga, iwe mkuki au mawe ya teo, aliua wakubwa kwa wadogo, wanaume kwa wanawake.... (kwake mauaji hayo ndiyo anayaita wokovu una Bwana). Sasa ghafula anatokeza mwimbaji anafungua ZABURI 109:6-20, Naye anatunga wimbo akiwaombea wanaomwudhi na maadui zake (wanadamu) wakutwe na hayo aliyoyata Daudi yatimizwe kwa washtaki wake na maadui zake. Ukristo haufundishi hivi, tabia za Wakristo wanajifunza kwa Yesu, tabia za Mungu, na matumizi ya nguvu za Mungu ndani yao wanajifunza kwa Yesu Kristo. Hivyo utunzi wa nyimbo za kiKristo au mahubiri, lazima yawe sambamba na fundisho la msingi ndani ya Ukristo (The teachings, preachings, songs should be in-line with the truth of the gospel)

NAKUPA SHAURI, USIKOSE SEHEMU YA TANO (5) YA MFULULIZO HUU. TUTAJIFUNZA KITU CHA MUHIMU SANA CHA KUYAFAA MAKANISA YA MUNGU POPOTE YATAKAPOFIKA MAARIFA HAYO.

Mwl Proo
0762879363

alltruth5ministries@gmail com

Monday, October 10, 2022

KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO (PART 3)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
_*Rightly Dividing The Word of Truth*_ 2Timothy 2:15b

*SEHEMU YA TATU*

*_KIPI KINAPASWA KUWA FUNDISHO KWA WAAMINI?_*

Sikushauri uanze kusoma sehemu ya tatu (3) kama hujasoma kwa kuelewa, sehemu ya kwanza na ya pili, huu hapa ni mwendelezo tu. Sehemu ya pili ya somo nieleza namna mbili za kutafsiri maandiko yaani (Eisegesis na Exegesis). Leo nakuonesha kipi kinapaswa kuwa fundisho kwa waamini (Wakristo). Ukristo (imani ya kumfuata Yesu) sio imani ya mchongo, wala sio imani ya dini ya Kiyahudi (Judaism). Ukristo sio imani iliyokosa vyanzo vya kufundishia (sources & materials), au kwamba kuna mambo hayana mwongozo, na mtu yeyote anaweza akatengeneza kitu chake tu chochote (coined teachings); Hasha!

Natambua kuhusu magawanyo ya Roho (Ebrania 2:4), natambua kuhusu tofauti ya kutenda kazi (1Kor 12:6), natambua kuhusu neema mbalimbali za Mungu (1Petro 4:10). Lakini pamoja na hayo yote kusanyiko la waamini, hawafundishwi tu chochote atakachokinyofoa mtu kwenye Biblia. Mfano kama Torati ni kivuli, wala si sura halisi.... Kila utakapotaka kusoma kivuli utapaswa kukisoma kutokea kwa sura halisi (Kristo). La sivyo utaangukia katika upotovu mkubwa. Kwa kusema hivi simaanishi kamwe Torati au kitabu chochote cha Agano la Kale kisisomwe au hakiwahusu waamini katika Kristo (Warumi 15:4), hapa ni suala la matumizi yake ni yapi?? Ndio maana somo letu linaitwa *KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*

Kwa sababu ya kukosa msingi, nini haswa kinapaswa kuwa fundisho kwenye kanisa, Watu wameingiza chachu za kifarisayo nyingi sana, huku ikidhaniwa ni mafunuo. 

*MIFANO HAI YA MATUMIZI YASIYO SAHIHI YA MAANDIKO*

1. Huwezi kuja kwenye kusanyiko la Wakristo, ukawasomea Kumbukumbu La Torati 22:8, na kuwaelezea wapendwa Mungu anatuagiza kujenga ukuta mdogo wa fensi (parapets/battlements). Hili sio agizo la Mungu kwa waamini katika Kristo.. Taratibu za ujenzi kwa waamini zitazingatia tu uwezo wao kifedha, vibali vya ujenzi toka manispaa, utamaduni wa majengo ya mahali walipo... Wala usiwaongoze kwa desturi hizo za kiyahudi.

2. Huwezi kwenda kwenye kusanyiko la waamini huko Uarabuni, ukawasomea andiko la Walawi 11:4 (Na kuwaambia jamani ndugu zangu Wakristo msile kabisa ngamia 🐪  🐪  Mungu kakataza. Waamini hawajakatazwa kula ngamia.. Ni wewe hujatumia kwa halali neno la kweli. Suala la vyakula halali vya kuwafaa kwa afya vitategemea desturi za huko walipo, kanuni za afya kisayansi kama wanyama hao hawana madhara na sio kutafuta mwongozo wa Torati ya Musa kuwajuza wanyama wa kuliwa... (Torati ya Musa na Isaya imetaja kuwa panya 🐀🐁hawapaswi kuliwa, niwaambie tu kama kuna Wamakonde na Wayao wanaokula panya na ni Wakristo, hayo makatazo hayana uhusiano na imani yao.

3. Huwezi kwenda kwenye kusanyiko la waamini (waKristo),  ukawasomea Walawi 19:27, na kuwaambia ni chukizo kunyoa denge (cutting hair by sides). Umetumia neno isivyo halali, ulipaswa ujifunze kwanza maana ya maagizo hayo kabla ya kuwaambia Wakristo, labda msichonge ndevu zenu mkienda Saluni (Barber Shop). Kama Mkristo atakatazwa kunyoa au kuchonga ndevu, au nywele zake iwe ni katazo kwa sababu jamii yenu kitamaduni, hawalikubali hilo.... wala sio utii kwa makatazo ya Torati (maana kila katazo linalo muktadha wake).

4. Huwezi kwenda kwenye kusanyiko la waamini ukawaambia jamani Kumbukumbu la Torati 22:11, Biblia imekataza kuvaa nguo yenye aina tofauti ya vitambaa (two different linens) yaani nguo isiwe na satini, na pamba, au hariri, au sufu au kitani, au kitenge etc). Kwamba ukifanya hivyo ni machukizo.. Hicho ulichosoma ni kizuri ila sio maagizo ya Mungu kwa waamini. Kama kuna kitambaa utaacha kukivaa ewe Mkristo ni labda kama kwenye jamii yenu kinakataliwa kijamii, isiwe na correspondence yoyote kwa makatazo ya Torati.

Kuna watu wanasema Mwl Proo, unazuia watu kutumia vitabu vya Agano la Kale... La Hasha!.  Ninchofanya ni kuwaondolea utaji (veil) na kuwafanya waamini wapate kumwona Kristo hata kwenye Torati.

Ni aljebra rahisi sana hii hapa: Torati, Zaburi, na Manabii vilizungumza habari za Kristo kwa picha (Typologies)....  Ujumbe wa kuhubiriwa ni Kristo. Hivyo tu (Kolosai 1:28, 1Korintho 1:23). Yaani, ili watu wawe waamini (watoto wa Mungu) hawahitajiki kunakili (kuCopy) chochote kwenye desturi ya dini ya kiYahudi. Wanapaswa kuhubiriwa kuhusu Kristo (kazi aliyoifanya na kuikamilisha) wakiziamini hizi habari njema (Injili), wanapokea wokovu (kufanywa watoto wa Mungu). Na baada ya hapo watendelea kufundishwa kuhusu Yesu (Kuzaliwa kwake, kufa, kuzikwa, na kufufuka kwake), kumewafanyia nini wao (kumfunua Yesu), huku  pia wakifundishwa wao wamekuwaje kwa kupitia Kristo (kilichotendwa ndani yao, na nafasi zao wakiwa ndani ya Yesu)... Haya yanatosha kumfanya mwamini kuwa mtu mkamilifu, mwenye kuweza kutembea kwenye madaraka makamilifu, kama mtoto wa Mungu. Waamini wataendelea kujifunza kuhusu mwenendo ndani ya imani kwa Yesu (asili yao mpya baada ya kuzaliwa upya), na watakaa kwenye fundisho la Yesu na mitume wake. HABARI HIZI NI NYINGI ZINATOSHA KUZIHUBIRI NA KUZIFUNDISHA HATA KAMA ULE MWISHO UTAKAWIA KWA MIAKA MILIONI 10 BAADA YA SASA _(mwlproo)._ MKIPIGA CHENGA FUNDISHO LA KRISTO NA MITUME WAKE MNAJIINGIZA KWENYE MAFUNDISHO YA MCHONGO. MTAPEANA UTUMWA, HOFU, NA MAFUNDISHO MENGINE YA KUFANYA MSALABA UBATILIKE.
SIKU YA JANA KUNA MKRISTO AMENISHIRIKISHA KUWA JUMAPILI ILIYOPITA WAMESOMEWA EZEKIEL 16:1-5, NA KUFUNDISHWA NGUVU ILIYOSHIKILIA HATIMA, ILI WAWEZE KUOMBEA VITOVU VYAO VILIVYOKATWA MIAKA MINGI. 😀 NI KAMA MAFUNUO MAZURI VILE, SI NDIO!!! HAYA SIO MAFUNDISHO YA KUWAFUNDISHA WAAMINI. WAAMINI WANGEAMBIWA ALICHOFANYA YESU, NA WAO WAMEKUWAJE KWA KUZALIWA, KUFA, KUZIKWA, NA KUFUFUKA KWA YESU. HAKUNA LEVEL YOYOTE KATIKA UFALME NA MAMLAKA ZA GIZA INAYOWEZA KUWASHIKA WAO WALA HATMA ZAO.  MKIKATAA HAYA MNAWEZA KUCHAGUA KUENDELEA KUJIFUNZA UTUMWA AMBAO HAUPO, ILA UNAUMBWA KWA KUWA MMECHAGUA KUUSIKILIZA NA KUUAMINI. YOYOTE MTAKAYOYABUNI KWA KUNYOFOA VIMISTARI KWENYE BIBLIA NJE NA UJUMBE WA MSINGI (FUNDISHO LA KRISTO NA MITUME) MTAKUWA MMECHAGUA KUJIFANYISHA KAZI AMBAYO BWANA MKUBWA YESU KRISTO ALIIKAMILISHA. LEO HII UKIAMUA KUFINDISHA WATU LAANA ZA ARDHI ZINAVYOLETA UMASKINI, SIJUI SADAKA YA KUTANGUA MADHABAHU ZA MAGONJWA, MARA NAMNA DAMU ZA KAFARA ZINAVYOLETA MATESO KWA MKRISTO, NA TAKATAKA ZINAZOFANANA NA HIZI, NI UCHAGUZI WENU TU KUURUDISHA UTUMWA AMBAO HAUPO. NA ANAYEJARIBU KUSEMA YEYE NDIYE ANAWEZA KUWASAIDIA WAAMINI KUTOKA KWA HAYA ANAJARIBU KUJIPA KAZI YA KUWA MWOKOZI MSAIDIZI. WAAMINI WANACHO CHA KUFUNDISHWA SIO HAYO!

*CHRIST IS OUR MESSAGE (COLOSSIANS 1:28 TPT)*


NIKUOMBE SANA,USIKOSE SEHEMU YA NNE (4), UTAPATA MAMBO YA KUKUSAIDIA SANA KUIELEWA IMANI HII NA KUIFURAHIA

alltruth5ministries@gmail.com.