Wednesday, September 21, 2022

KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO (PART 2)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
*_Rightly Dividing The Word Of Truth_* (2Timothy 2:15b)

*SEHEMU YA PILI*

_Mwl Proo_ #0762979363

Sikushauri kuisoma sehemu ya 2, iwapo hujasoma sehemu 1. Sehemu ya kwanza tuliona namna maandiko ya Biblia yanaweza kutafsiriwa (Literally /kama yalivyoandikwa, Allegorically /lugha ya picha, Contextually/Kimuktadha ) ambazo nilizitolea mifano. Leo tusogee mbele zaidi!

Roho Mtakatifu anafanya kazi vile vile, kazi ile ile aliyoifanya ndani ya Mitume wa Yesu na wale wanafunzi waliopokea _Ahadi ya Baba_ pale ghorofani. Hakuna kilichopungua wala kubadilika. Pamoja na ukweli kwamba sehemu kubwa ya wanafunzi wa Yesu hawakuwa na elimu kubwa ya kidunia (Mdo 4:13, 1Kor 1:26), haikuwa kazi kwa wanafunzi wa Yesu kuelewa maelekezo waliyopewa na Yesu, wala kuelewa ufunuo wowote wa Roho juu ya imani na mwenendo katika Kristo.

Sasa yale waliyoyaandikwa wao, na kuja kusomwa na sisi miaka 2000 badae lazima kuwe na kanuni za kuzingatia katika kuyatafsiri, au sivyo, tutaangukia katika mtego wa kuwa na ufafanuzi wa mchongo (false manipulations). Kile kilichoandikwa na mitume pamoja na kuvuviwa, na kuongozwa na Roho bado ni kazi ya fasihi (It's a literature work). Hapo sasa usiseme ninaye Roho Mtakatifu atanitia katika kweli yote, ukipuuza kanuni you're prone to errors.

Kuna namna mbili ambazo watu huzitumia kufafanusha maandiko.. Kitaalamu hutajwa kwa *EISEGESIS* na *EXEGESIS*. Hiyo ya kwanza (eisegesis) ni namna ambavyo mtu anajaribu kueleza kile ambacho yeye amekielewa kutoka kwenye maandiko (scriptural text), na hiyo ya pili (exegesis) mtu anajaribu kuzingatia kanuni za kutafsiri maandiko ili aelewe mwandishi (author) alimaanisha nini?.

Mambo mengi yanayofundishwa kimakosa na yaliyoingiza ufafanuzi wa mchongo (false manipulations), ni matokeo ya kila mtu kujaribu kufundisha anachoelewa yeye (eisegesis), badala ya kujifunza kuelewa alichomaanisha mwandishi (exegesis)..... 

ANDIKO LETU LA MSINGI  KATIKA 2TIMOTHEO 2:15b RIGHTLY DIVIDING THE WORD OF TRUTH (kulitumia kwa halali neno la kweli;) Ndipo kunatupa mwanga wa kutafsiri maandiko kwa namna ya kuelewa alichomaanisha mwandishi *(Biblical Exegesis)*

Waliojikita kwenye EISEGESIS wanapenda kutumia mtindo wa kunyofoa-nyofoa vifungu (Proof-Text Method) bila kuzingatia kabisa kanuni. Ili tu anachotamani yeye Biblia iwe imekisema kionekane ni cha kweli. Wanajitahidi kuyasoma mawazo na mitazamo yao ndani ya Biblia.

SASA ILI KUEPUKA UFAFANUZI WENYE MAKOSA (FALSE MANIPULATIONS) KWENYE MAANDIKO, UNAPASWA KUZINGATIA KANUNI ZIFUATAZO.

1. Zingatia maandiko yaliyo nyuma ya mstari uliousoma (Pretext passages)

2. Zingatia mistari iliyo mbele/inayofuata (The post-text passages)

3. Zingatia muktadha (The context principle)... mind you 👉  a text without the context is only a pretext, ndio maana kuna wakati utafiti huu unaweza kuhusisha kutafuta maana za maneno ya lugha za asili. 

4. Tafuta kujua kwa uchache tu historia ya kuandikwa ujumbe huo. Ukiweza tafuta kujua hadhira ilikuwaje? Utamaduni wao ulikuwaje? (Historical& Cultural Facts)

 5. Na kama itatokea passage moja inaonekana kukinzana na nyingine, angalia na passage ya tatu na zingine zinalizungumziaje suala hilo hilo.

NB:- *NI HATARI KUUNDA FUNDISHO LOLOTE LA MSINGI KWA KANISA HUKU LIKIWA LIMEJENGWA JUU YA TAFSIRI ISIYO SAHIHI YA MAANDIKO*

HAPA CHINI, NINACHAGUA SURA MOJA YA BIBLIA. NA KUKUONESHA NAMNA *_EXEGETICAL BIBLE INTERPRETATION_* INAVYOFANYWA. ... _mwlproo_

Mfano; Nimewahi kusikia mtu akijitetea kwa mwenendo wake mbaya, akisema hata mtume Paulo alisema, "Analolipenda halitendi ila asilolipenda ndilo analolitenda" (Warumi 7:15). Kwa haraka haraka unaweza kudhani andiko hilo limenukuliwa mahali sahihi. Lakini ukweli ni kwamba  hapa neno la kweli halijatumiwa kwa halali. Hivyo nakuonesha namna ya kufanya exegesis ya Warumi 7.

Kosa la huyo ndugu, kurukia mstari wa 15 (prooftext method), 
akiwa ameacha mstari 1-14

 wala hajahangaika kusoma kwa kina  mstari 16-25 (_mwlproo_)

Exegetically, tunapaswa kuanza mstari wa kwanza

nao na unasema,

*“Ndugu zangu, hamjui (maana nasema na hao waijuao sheria) ya kuwa torati humtawala mtu wakati anapokuwa yu hai?”*
  — rom 7:1 (SUV)

1. Mstari wa kwanza, Paulo kwa mkono wa Tertio anataja jamii ya waamini anaozungumza nao, kuwa wanaijua Torati!

2. Akatoa mfano wa Ndoa (namna mke anafungwa mume akiwa hai)

3. Mstari wa 4&5 anazungumzia hali ya waamini baada ya kuifia dhambi, na anazungumzia hali yao ya kwanza wakiwa katika mwili.

4. Mstari wa 15 ambao wasomaji wengi wa Biblia wameshindwa kuuelewa, Paulo hazungumzii hali yake baada ya kuzaliwa kwa Roho wa milele, badala yake anazungumzia hali yake ya kimwili inavyokuwa na ugumu kuitekeleza Torati (ambayo ameitaja mstari  wa 14, kuwa asili yake ni ya rohoni...) Kwa Torati yenye asili ya rohoni ikimkuta yeye katika umwili wake inakuwa ngumu kuitekeleza _read between lines_ verse 13-15 upate muunganiko.

5. Mastari wa 16 Paulo mtume anasema *Nikitenda nisilolipenda, naikiri sheria kuwa ni njema*

i.e., Kama sheria imesema asiibe, na yeye ikitokea ameiba.. Basi hapo hana budi kuwa na confession kuwa ile sheria iliyomwamuru asiibe ni njema.

NB:- Sheria ndiyo inafanya kosa kuwa dhahiri... pasipo sheria hakuna kosa.

Kama mtu atajitahidi kusoma na kufika mstari wa 24, lakini kwa bahati  mbaya akaacha mstari wa 25 anakuwa amepoteza ujumbe wote unaojibu maelezo ya juu.

“Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.”
  — rom 7:25 (SUV)

*UFAHAMU WA ZIADA*
Unaposoma maandiko, kabla hujajikita kushikilia mstari, unapaswa kujua waandishi wa hivyo vitabu vyote vya Biblia hawakuweka mistari.

Mistari ya Agano la Kale (Tanakh) iliwekwa na Emperor wa Kiyunani miaka 250BCE, na Agano Jipya halikuandikwa na sura wala mistari, mpaka mwaka 1225 ambapo  Kadinali Stephen Langton  (1225) na Timu yake (For the Purpose of Readability) wakaigawanya kwa sura, na bado mistari unayotaka kukomaa nayo sana iliwekwa na Robert Estienne mwaka 1551. Hapa nakupa sababu ya kuisoma kama gazeti kuliko kukomaa na verses, inayokupelekea kuchanganya maana.

KWA NINI NIMEKUPA UFAHAMU HUO HAPO JUU KUHUSU SURA NA MISTARI?

Unachosoma kwenye Warumi 8:1-2 sio jambo jipya, anatoa majibu kusuppliment alichoongea kuhusu Torati/Sheria 👉  Uhusiano wake na utu mpya Katika Kristo

Hebu soma,

rom 8 (SUV)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
² Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
³ Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;
⁴ ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.

Soma mstari wa 3 hapa, unganisha na yale aliyoyaongea Paulo kwenye sura ya saba, ujue kwamba alipoandika hakuweka hizo namba. So usifungwe na namba 7 bila kujua kuwa namba 8 ametaja alichoelezea hapo nyuma.

KAMA WAKATI WOWOTE ULIWAHI FIKIRI KWA MANENO YA (WARUMI 7:15-17) LABDA PAULO ALIKUWA AKISTRAGOOOOOOO NA MWILI

NEVER NEVER NEVER 

KILIO CHA PAULO (Warumi 7:24) WAS NOT A CRY OF DERELICTION, BUT OF TRIUMPHANT VICTORY KWAMBA KWA NJIA YA YESU, HAKI YOTE INAYOTOKANA NA MAAGIZO YA TORATI NA MATENDO MEMA, AMEIPATA KWA KUWA NDANI YA YESU.

Umeona raha ya kutafuta kujua alichomaanisha mwandishi (EXEGESIS) dhidi ya kile unachojaribu kuelewa mwenyewe (EISEGESIS)???

USIKOSE SEHEMU YA TATU YA MFULULIZO HUU. UTANUFAIKA SANA SANA

alltruth5ministries@gmail.com

Monday, September 19, 2022

KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO PART 1

*KULITUMIA KWA HALALI, NENO LA KWELI*
*_Rightly Dividing The Word Of Truth_* (2Timothy 2:15b)

*SEHEMU YA KWANZA*
_Mwl Proo_
0762879363

Ili kuepusha ufafanuzi wa mchongo wa torati ya Musa... Wayahudi wana Talmud (yenye Mishnah na Gemara) ambayo ni fasihi andishi iliyotokana na simulizi za mdomo za desturi za utekelezwaji wa Torah.
Leo katika mafundisho ya kanisa, kuna ufafanuzi mwingi wa mchongo (falsely manipulated teachings) uliosababishwa na kuepuka kanuni za kutafsiri maandiko.

Maandiko katika Biblia (ni mkusanyiko wa taarifa nyingi zikiwemo nabii mbalimbali, hadithi, maagizo ya Mungu, simulizi za desturi za kiyahudi, na taarifa zingine nyingi zilizokusanywa pamoja, zikawa 'documented'.

Humo ndani kuna mambo ambayo yanaweza kutafsiriwa kwa namna tatu kimsingi;

1. Literally (kwa kawaida tu kama yanavyosomeka

mfano (a):- Ukisoma labda mtume Paulo anaandika Salamu.. kwamba watu wa nyumbani mwa Akila na Priska wanawasalimu, au Wasalimieni watu wa nyumbani mwa Arkipo (Hii ni salutation/maamkizi tu ya kawaida).. Utaitafsiri literally bila ku-Manipulate kuepusha upotoshwaji usio na sababu.

mfano (b):- Umesoma zako Isaya 6:1, Mwaka ule aliokufa Uzia nalimwona Bwana. Katika zama za uandishi wa Biblia hususani Biblia ya Kiyahudi (Tanakh) ilikuwa ni kawaida kuandika rejea ya muda kwa kutaja tukio gani lingine kubwa (notable) lilitokea. Mfano  Amosi 1:1 anasema miaka miwili kabla ya tetemeko la nchi/ardhi (Earthquake) ikiwa ni namna nyepesi ya kukumbushia majira gani hilo lilitokea. Ni namna hiyo hiyo Isaya anataja mwaka aliokufa Uzia kama muda rejea wa maono yake. MANIPULATIONS (ufafanuzi wa mchongo) utadai, Uzia alimzuia Isaya kumwona Mungu. Kwenye maisha yako kuna Uzia ambaye inabidi afe.. Asipokufa Uzia huwezi kumwona Mungu.. Uzia anaweza kuwa ndoa au kazi yako au simu yako... It sounds vizuri  midomoni mwa wahubiri.. na mwingine atadai ni ufunuo.. Hapana, ufunuo uliopo humo kwa Biblia ni mwingi mno tu bila hata ku-Manipulate kwa sababu ya kukiuka kanuni za kutafsiri....

NB:- *MAANDIKO YA KWENYE BIBLIA HAYAWEZI LEO KUMAANISHA KITU AMBACHO MWANDISHI HAKUKIKUSUDIA WALA KUKIMAANISHA*

 Hiyo ya kudhani watu wanafunuliwa cha kuelezea ndicho kimetufikisha kwenye vituko vingi kwenye kanisa la leo.. na wengine wakiona wanalalamika tu kumbe ilisababishwa kwanza na ufafanuzi wa mchongo wa maandiko ya Biblia, na kutojua nini hasa kinapaswa kuwa fundisho katika kanisa.


2. Allegorically (Hii ni namna ya ujumbe kuwasilishwa lugha ya picha, fumbo,  mfano uliofichwa kwenye kitu kinachojulikana, na lugha za alama 👉  figures of speech (figurative language), symbolisms... 
Ni muhimu kama unataka kuepuka makosa, kabla ya kutumia kitu kilicho katika maandiko kama kilivyoandikwa (literally), ujiulize je! sio lugha ya picha (allegory...)  NB:- parables (mifano) ni allegories fupi.. ingawa zina tofauti, ila hayo yako kwa somo jingine.

Mfano:- Unasoma zako kitabu cha Ufunuo... Unakutana na maandiko yakimtaja Yesu kama Mwana-Kondoo (Lamb), mara Yesu ni Mwana-Kondoo aliyechinjwa.... Je! ni kweli kwamba Yesu alichinjwa au alifia kwenye kinyongeo cha askari wa Rumi? Hizi ni lugha za picha kutokana na kujulikana kwake kwa hadhira (familiarity). Hata kusema huyo mwanakondoo alichinjwa kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu akiwa anataka aoneshe maongeo ya mpango wa Mungu wa ukombozi tangu zamani, tangu milele. Hatari ya ufafanuzi wa mchogo ni kuleta mafundisho yenye makosa, yenye kuwakosesha sana waamini. Kila ambapo maandiko yenye lugha picha (figures of speech/allegories) yakifafanuliwa kawaida (literally) yanakosesha shabaha lengwa...nk


3. Contextually (kimuktadha)... Ingawa jambo hili nitalizungumzia sehemu ya pili ya fundisho hili, ila kwa uchache.. Kuna maandiko mengi yanapaswa kufafanushwa baada ya kufahamu muktadha husika (history of the text & history in the text). Kubeba kitu kinyume na muktadha kinaweza pelekea kuzalisha fundisho lenye makosa.

Mfano:- Mtu akisoma 1Korintho 11:13-14, kisha akawasomea wanawake wabongo kuwa mkija kanisani, mnapaswa kufunika vichwa.. Ameamua kupuuzia maandiko yenye muktadha husika na kuyaapply kama yalivyoandikwa kwa kawaida _literally_. Ulipaswa kufahamu mambo kadhaa ikiwemo ukweli kuwa kitabu/barua ya Paulo kwa waamini wa Peloponnese (Corinth) ilikuwa ni majibu ya maswali waliyomwuliza yeye kabla, kwa issues  zilizoinua disputes za hapa na pale. Kwa wanawake wa huko Uyunani hususani (elderly women, na wengine baada ya kuolewa) hawaoneshi nywele zao kwa hadhara... Kwa kufanya hivyo wanakuwa wametii desturi *_Traditional Notions of Propriety_*.. Maana mwanamke akiacha nywele ni labda kahaba au ana cheo kisiasa... Huo ndio muktadha kwa ufupi. Hivyo ni makosa, kuchukua andiko hilo la wanawake kufunika vichwa wakati wa sala, kuwasomea wandengereko, wamakua, wabena, na wamasai ukiwataka nao wafunike nywele zao wakija kanisani... Haliwahusu, halina maana hiyo, halipaswi kutumika kwa muktadha tofauti na ule wa kwenye mji wa Uyunani alikoipeleka ile barua, hata mtume Paulo hakutoa maagizo au maelekezo hayo kwa makanisa mengine kwa sababu kwao hawana tafsiri sawa na mji wa Korintho nchini Greece 🇬🇷 . Maandiko yanayohitaji kutafsiriwa kimuktadha ili kutumika.. lazima ufuate kanuni.. or else ufafanuzi wa mchongo utahusika.


USIKOSE SEHEMU YA PILI NA YA TATU YA FUNDISHO HILI, YATAKUSAIDIA SANA TU KUTOENDELEZA MAKOSA, NA UTAJIPATIA NJIA NZURI YA KUTUMIA KWA HALALI, NENO LA KWELI

alltruth5ministries@gmail.com