Saturday, March 28, 2020

CORONA

*WENYE NEEMA YA KUOMBA KWA JUHUDI, TUOMBE*

*_Usiku kabla sijalala mimi Mwl Proo niliitafakari video ambayo wameonesha miili ya watu huko Italy  ikimwagwa kama takataka kwenye jaa la takataka.. Nikasema Mungu hii ni nini lakini!?, nilitamani kujua nini kinaendelea. At midnight nikaona mpango ukisukwa kuhusu corona virus disease (naamini ule mpango ulisukwa kuzimu)... Ghafla nikaona kuna shimo linaloonekana kwa wazi kuwa ni refu sana (Ufu 9:1ff, Isaya 5:14),  muda nalitazama nilitarajia kitu kitoke, na kweli lilitoka joka 🐍🐉 (Isaya 27:1ff), urefu wake unafika hata mbinguni (Dan 4:20), ni mkubwa na mrefu, pale niliposimama sikuweza kuona juu kichwa chake chafika mpaka wapi maana alienda juu kiasi cha kufika hata futi 24,000 kwenda juu. Nikapata wazo nimfuate mwanamaombi mmoja ambaye  najua yeye yuko tayari kwa maombi kila wakati hasa ya dharura, ili tushughulikie hilo swala kwa maombi, maana nilivyomwona yule joka anaweza kuudhuru hata mji mzima in minutes. Nikafika kwa huyu mwanamombi najisikia vizuri kwamba tunaenda kuomba, tukiwa njiani nikaona ghafla amebadili uelekeo akawa anaingia kwenye jengo kama  "lecture theatre" na akaniambia ana vipindi huko, nikawa shocked maana naona hatari ni kubwa na hajaonesha kujali sana._*

*Tafsiri fupi*
*Shetani mharibifu (Nahumu 2:1) amejiinua anaua wenzetu sana, kinachoendelea duniani ni kazi ya shetani, (sipingani na wanaosema ni Mungu anaadhibu uovu huo ni mtazamo wao), ila nasema kwa nilichoona mimi kazi hii ya uaribifu ni ya shetani na mpango huu haujaandaliwa mbinguni bali ni kambi ya uharibifu (ya shetani), yule mwanamaombi amewakilisha wote wenye uwezo wa kuomba lakini wamepuuza na kuwa bize na mambo yao. Uwepo wa kanisa duniani unapaswa ulete relief/ahueni kwa wanadamu wote hata waovu. Dhamana ya uhai wa hawa wanandamu wanaokufa kama kuku wamekumbwa na castle disease iko kwetu kanisa.. Tunaweza fanya wakanusurika na uharibifu wa shetani, (Matendo 27:9-28 soma mstari wa 24l)..Abiria wote waliosafari na Paulo, uhai wao uliwekwa mikononi mwa Paulo Mtume. Uhai wa wanadamu wote unatutegemea sisi, usikimbilie kusema Mungu anawaadhibu, Mungu hapendi kufa kwa hao watu (Ezekiel 18:32), we can stop the devil, kuwa acha hawa watu.. Wewe unayetumia Zaburi 91 kujitamkia usalama wewe peke yako haitoshi hiyo, hata ambao Biblia hawaisomi, unaweza wanasuru na huu uharibifu, swala la kukokoka watavutwa na Bwana mwenyewe huko mbele kwa mapenzi Yake, lakini kumzuia shetani na kuwakingia kifua hawa wanadamu wenye roho, nafsi, na mwili hilo kila mwokovu analiweza.*

No comments:

Post a Comment