Saturday, March 28, 2020

CORONA (English)

*I SUMMON THOSE WITH GRACE TO PRAY, LET'S PRAY!*

My name is Minister Prosper, Before I slept last night, I was meditating on a video clip showing dead bodies in Italy 'are just dumped' like rubbish (mass burial), and I asked God what is this!?. I wanted to know what really happens. At midnight I saw in the spirit a dark gang of unknown folks (evil spirits from hell) conspiring to bring "corona virus disease". Suddenly I saw an abyss,  it was deep (Rev 9:1ff, Isaiah  5:14), As I was looking at the mouth of the pit, a very big serpent came up out of the abyss (Isaiah 27:1ff), the serpent's height reached the sky (Dan 4:20). I couldn't see its head which was about 24,000 feet high. I got an idea to call my friend who's a prayer warrior so that we can intervene through prayers. The serpent was able to destruct lives of people of the city in minutes. I was shocked because this prayer warrior changed his mind and went to attend lecture session instead of offering prayers.

*Interpretation*
*The destroyer (satan) Nahum 2:1, has come to destroy (John 10:10), what's happening now in the world about COVID-19 is devil's work (I leave away the idea of God punishing the wickedness of the world), because of what  I saw. The prayer warrior I saw represents those who are able to pray  but have just ignored it, and are busy with other things. The presence of Christ's church in the world should bring relief to all humanity including the wicked. The life of these people who are dying just like fowls is entrusted to the church. We can do something and save lives. The life of people who travelled with Paul (Acts 27:9-28) was entrusted to Paul the apostle read verse 24 and see. Don't be hasty to say God is punishing  the globe because of iniquity. He is not delighted in the death of sinners (Ezekiel 18:32)*

*WE CAN STOP THE DEVIL FROM KILLING PEOPLE. THE BELIEVERS USE PSALMS 91 FOR THEIR OWN PROTECTION, THAT IS NOT ENOUGH, EVEN UNBELIEVERS CAN BE RESCUED THROUGH YOUR PRAYERS. LET'S JOIN TOGETHER AND PRAY, LET'S STAND TO INTERVENE THE SITUATION, GOD WILL SAVE THESE PEOPLE WHO ARE DYING. BY HIS GRACE THEY WILL BE SAVED ONE DAY, THEY CANNOT RECEIVE SALVATION AFTER DEATH*
+255762879363 (WhatsApp)

CORONA

*WENYE NEEMA YA KUOMBA KWA JUHUDI, TUOMBE*

*_Usiku kabla sijalala mimi Mwl Proo niliitafakari video ambayo wameonesha miili ya watu huko Italy  ikimwagwa kama takataka kwenye jaa la takataka.. Nikasema Mungu hii ni nini lakini!?, nilitamani kujua nini kinaendelea. At midnight nikaona mpango ukisukwa kuhusu corona virus disease (naamini ule mpango ulisukwa kuzimu)... Ghafla nikaona kuna shimo linaloonekana kwa wazi kuwa ni refu sana (Ufu 9:1ff, Isaya 5:14),  muda nalitazama nilitarajia kitu kitoke, na kweli lilitoka joka 🐍🐉 (Isaya 27:1ff), urefu wake unafika hata mbinguni (Dan 4:20), ni mkubwa na mrefu, pale niliposimama sikuweza kuona juu kichwa chake chafika mpaka wapi maana alienda juu kiasi cha kufika hata futi 24,000 kwenda juu. Nikapata wazo nimfuate mwanamaombi mmoja ambaye  najua yeye yuko tayari kwa maombi kila wakati hasa ya dharura, ili tushughulikie hilo swala kwa maombi, maana nilivyomwona yule joka anaweza kuudhuru hata mji mzima in minutes. Nikafika kwa huyu mwanamombi najisikia vizuri kwamba tunaenda kuomba, tukiwa njiani nikaona ghafla amebadili uelekeo akawa anaingia kwenye jengo kama  "lecture theatre" na akaniambia ana vipindi huko, nikawa shocked maana naona hatari ni kubwa na hajaonesha kujali sana._*

*Tafsiri fupi*
*Shetani mharibifu (Nahumu 2:1) amejiinua anaua wenzetu sana, kinachoendelea duniani ni kazi ya shetani, (sipingani na wanaosema ni Mungu anaadhibu uovu huo ni mtazamo wao), ila nasema kwa nilichoona mimi kazi hii ya uaribifu ni ya shetani na mpango huu haujaandaliwa mbinguni bali ni kambi ya uharibifu (ya shetani), yule mwanamaombi amewakilisha wote wenye uwezo wa kuomba lakini wamepuuza na kuwa bize na mambo yao. Uwepo wa kanisa duniani unapaswa ulete relief/ahueni kwa wanadamu wote hata waovu. Dhamana ya uhai wa hawa wanandamu wanaokufa kama kuku wamekumbwa na castle disease iko kwetu kanisa.. Tunaweza fanya wakanusurika na uharibifu wa shetani, (Matendo 27:9-28 soma mstari wa 24l)..Abiria wote waliosafari na Paulo, uhai wao uliwekwa mikononi mwa Paulo Mtume. Uhai wa wanadamu wote unatutegemea sisi, usikimbilie kusema Mungu anawaadhibu, Mungu hapendi kufa kwa hao watu (Ezekiel 18:32), we can stop the devil, kuwa acha hawa watu.. Wewe unayetumia Zaburi 91 kujitamkia usalama wewe peke yako haitoshi hiyo, hata ambao Biblia hawaisomi, unaweza wanasuru na huu uharibifu, swala la kukokoka watavutwa na Bwana mwenyewe huko mbele kwa mapenzi Yake, lakini kumzuia shetani na kuwakingia kifua hawa wanadamu wenye roho, nafsi, na mwili hilo kila mwokovu analiweza.*

Tuesday, March 24, 2020

MAJUMA SABINI

*πŸ…œπŸ…πŸ…™πŸ…€πŸ…œπŸ… πŸ…’πŸ…πŸ…‘πŸ…˜πŸ…πŸ…˜*
_*SEVENTY WEEKS OF DANIEL*_
*ʍՑӀ ΤΉΙΎΦ…Φ…*
_+255762879363_
~70|70|70|70|70|70|70|70|70~

Ndugu msomaji na mpendwa wangu katika Yesu aliye Kristo na Bwana, nakukaribisha katika bandiko hili, litakalokupa mwanga wa siri za Mungu zilizofunuliwa kwa neno lake lililoandikwa. Hiki ni kizazi sahihi cha kuelewa mafumbo yote ya Mungu (1Kor 2:10ff), hakuna jambo ambalo limeandikwa katika vitabu 66 vya maandiko ya Biblia ambalo hatupaswi kulielewa, kama kuna siri hatupaswi kuzijua (Kumb 29:29) basi hazijaandikwa kwenye Biblia.

*❶. KANUNI YA KUHESABU SIKU NA MIAKA*

πŸ“‰ ```KUNA MASWALA MENGI KUHUSU NYAKATI ZA KIBIBLIA (BIBLICAL CHRONOLOGY) BADO HAYAJAELEWEKA KWA WATU WENGI, MFANO NI WACHACHE WANAJUA KUWA ISRAEL HAIKUWA UTUMWANI MIAKA 400. ILE SIKU WANATOKA MISRI (EXODUS) ILI UFIKIE MIAKA 400 INABIDI URUDI MPAKA SIKU MWENYEZI MUNGU ANAZUNGUMZA NA IBRAHIMU JUU YA JAMBO HILO (MWANZO 15:13), NA ILI ITIMIE MIAKA 430 ILE YA KUTOKA 12:40 INABIDI URUDI NYUMA MPAKA WAKATI IBRAHIMU ANAITWA (KUTOKA 12:1ff). HILI NDIVYO LILIVYO NA PAULO AMELISEMA ILA KWA KIFICHO KIDOGO (GALATIA 3:17)```

πŸ“… Katika somo langu la _Ukweli kuhusu Krismasi_ nilifanya utangulizi mrefu kidogo juu ya majira/muda na yanavyohesabiwa. Kwa somo hili nitaenda upande ambao sikuugusa mwanzo

πŸ“… Kuna Kalenda nyingi duniani, lakini kwa msingi wa mafundisho haya naweza kukutajia walau nne hizi ambazo zinahusiana na mambo tunayojifunza. Kalenda ya Henoko (yenye siku 364 kwa mwaka), Kalenda ya Julia (yenye  siku 365.25), Kalenda ya Gregory (yenye siku 365 kasoro mwaka mrefu wa nne), na Kalenda ya Kiyahudi (yenye siku 360). Kuhesabu siku za mwezi ni kitu kilichotegemea mwezi, nyota, jua, na uhusiano wake na nafasi ya dunia 🌍🌟⭐πŸŒ›πŸŒ—πŸŒ’☀ .  Yako mambo yanayojadiliwa kuwa yaliifanya dunia isiwe katika nafasi yake ya asili ambayo sitayajadili hapa maana sio kusudio la somo. Lakini jua kwamba idadi ya siku katika kila Kalenda hutofautiana, ninayo maelezo mengi hapo mimi binafsi, kwa kuwa ni mwalimu wa Earth Sciences (Geography).

πŸ“… Katika maswala ya unabii wa Biblia, tunalazimika kutumia Kalenda ya Kiyahudi (ambayo naweza kuiita ya kinabii) maana hesabu za wazi zilizotajwa kwenye Biblia zinaBalance kwa Kalenda yao tu. Kalenda yetu ya siku 365 inafanya tofauti ya mwezi mzima kila ndani ya miaka 6, ikilinganishwa na lunar calendar. Mfano mgawanyo wa miaka saba ya Ufunuo 11:3 & 13:5 (siku 1260 kwa miezi 42) zinaleta hesabu kamili kama tu tutatumia mwaka mmoja wenye siku 360 (i.e., 42x30=1260, na kinyume chake 1260÷30=42). Itakapobidi kutumia hizo zingine zitatumiwa pia ili kutoleta hesabu nyingi kuliko fundisho la msingi.

*❷. SIKU MOJA NI MWAKA MMOJA KINABII*

πŸ“… Kuna muda, na kuna wakati (Kairos&Chronos), maswala ya nyakati Israel kama taifa na matukio yao ni   pahala pa kurejelea _point of reference_. Taifa la Israel ni taifa la kinabii, na hivyo Mungu alianza kuwazoesha mapema sana wayajue mafumbo ya kinabii hata katika maisha yao ya kawaida. Mfano alitaka wapate ujuzi wa kinabii kuwa siku 1 ni mwaka 1, angalia Hesabu 14:34

*",....... yaani, siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka, ........."*

Na katika zama za manabii jambo hili likawa dhahiri zaidi kwao.. Hebu tazama hapa Ezekiel 4:6

*"Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu wako wa kuume, nawe utauchukua uovu wa nyumba ya Yuda; siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagizia."*

HIVYO KWA HATUA YA KWANZA NAOMBA TUONDOKE NA TAFSIRI HII YA KINABII, MAANA TUNAENDA KUSHUGHULIKA NA UNABII WENYE NAMBA (CIPHERS).

*❸. MAJUMA 70 YANAANZA LINI, YANAISHA LINI?*
_mwlproo_
Daniel aliposoma vitabu akakutana na unabii wa Yeremia (Yer 25:11) kuwa utumwani wataitumikia Babeli miaka 70, na wakati huo walikuwa wamekwishakaa miaka 68. Aliingia kwenye maombi ili kuona ahadi ya Bwana kuwajilia tena inatimia. Ndipo Gabriel anakuja na issue muhimu sana... Daniel 9

Mstari wa 24.... anasema _"Muda wa majuma 70 umeamriwa juu ya watu wako..."_

⌚ Malaika Gabriel, alikuwa akimjuza Daniel kuwa swala la ninyi kutoka huku after 2 years liko guaranteed, ila sasa kuna muda wa majuma 70 ulio mbele yao, kuhusu watu wake (Israel) na kuhusu (Jerusalem)... Huo muda umeamriwa na baraza ya Mungu, ndio umebeba kila kitu kuhusu taifa la Israel kuanzia hapo utakapoanza kuhesabiwa mpaka mwisho wake, ndipo itakuwa mwisho wa vipindi kwa taifa hilo la Israel....Usisahau juu ya watu wako, na juu ya mji wako (Jerusalem).

*HESABU 1*
Neno la Kiebrania _Shabuwa_ ni majuma (specifically likitaja miaka/years)

Majuma 70 (70 Weeks)
Ni sawa na miaka 490, Kwa namna gani? Kila siku moja ni mwaka mmoja. Hivyo
Juma 1= Siku 7
Majuma 70= Siku 490
Then, Siku 490=Miaka 490

Majuma haya 70 (miaka 490) kama siku 173,880 (kwa lunar calendar) Malaika aliyagawa mafungu matatu, ambapo mimi nitaweka vipindi vinne kuufikia mwisho wa juma la sabini (seventieth week). Yaani Majuma 7 (miaka 49), kisha majuma 62 (miaka 434) kuna gepu hapo kati ambalo linaitwa _Majira ya Mataifa_ ambacho pia ni kipindi cha kanisa (Church Age), kisha kuna juma la sabini (miaka 7) ya mwisho ili kutimiza majuma 70 juu ya watu wa Daniel (Israel).  Sasa majuma 7+ majuma 62 tunapata majuma 69 ambayo ni sawa na miaka 483

⌚ Tunahesabu kuanzia lini?
_mwlproo_

Mstari 25
*"Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba;*

⌚ Kuna jambo ambalo ni huru kwa lumbano (open to debate) kuhusu tamko lilitoka lini haswa, kuna makadirio fulani tangu mwaka 460 BC mpaka mwaka 445 BC, Watawala hawa wa Umedi&Uajemi (Medes& Persia) walitawala zama hizo. Koresh/Cyrus [538-529]BC, na Dario [wa I, 521-485]BC, na Artaxerxes (Artashasta) [wa kwanza, 464-423] mfalme wa Ajemi, yuko Artashasta wa II, ambaye hana la kumhusu kwa case hii. Sababu hasa ya tofauti hizo ni kwa kuwa kuna matamko (decrees) kadhaa katika Ezra na Nehemia tangu kwa Koreshi (Cyrus), Dario mpaka Artashasta (Artaxerxe) yanayotoa order ya kujengwa kwa hekalu hiyo kuanzia Ezra 1-6, utakutana nayo. Lakini katika sura ya 7 agizo lilikuwa likisema Yerusalem ujengwe, hii ndio inaweza kuhusishwa moja kwa moja na tamko la Gabriel katika Daniel 9:25. Documents kadhaa zimetumia amri ya Artashasta (Ezra 7:21-26) kuwa ni mwaka 457BC, kwa kuwa alitoa tamko lake mwaka wa saba wa kutawala kwake ambapo alianza kutawala  464BC. Wako wengine wametumia decree ingine, ya kile kilicho kwenye Nehemia kwamba mwaka wa 20 wa kutawala kwake............ (inayokadiriwa kuwa 445/444 BC).. Tofauti hapo ni kwamba, Mwaka 457BC iliwekwa amri Yerusalem ujengwe, ila ujenzi haukuanza instantly, na wakati huu sasa kwenye Nehemia 1&2 unaona Nehemia anapewa tena orders baada ya yeye kuweka request kwa mfalme, akiwa ni mnyweshaji huko ikulu. So mwaka 445BC ni mwaka wa kuanza kwa ujenzi na sio kuwekwa amri ya kujengwa kwa Yerusalem. Jambo hili liko  open to debate,  kwa kutumia lunar year 360 days  mwaka huu 445BC unaangukia "close to" wakati wa masihi kukatiliwa mbali (Crucifixion) yaani 483 ukitoa 445 utapata miaka 38 ya baada ya Kristo, ambao hiyo miaka karibu nane inayozidi hapo inaelezwa kwamba kama itahesabiwa zile siku 173,880 kwa kwenda mbele kwa siku za Lunar Calendar hilo gepu linatoweka.. Mimi sijasimama kwa hayo makadirio, badala yake napendekeza kuhesabu majuma 70 kuanzia ilipitolewa amri na Artashasta Longimanus mwaka 458BC mwishoni au 457BC mwanzoni.Na tukianza kuhesabu haya majuma tangu siku Mfalme Artashasta (Artaxerxe) alipotoa agizo/amri ya kuutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu, Majuma 69 yatakamilika karibu sana na kipindi cha kutokea kwa masihi aliye mkuu (Kristo). Wale wanaoanza kuhesabu toka 457 inabalance kama watatumia kalenda ya Julian Caesar. Lakini waandishi wa awali wa Seventh-Day Adventist kama bwana Smith, Larkin, na waandishi wa miaka ya 90 kama bwana Shea, wameanzia 457 BC na kuyamaliza majuma yote 70 (490) inayokuja kuangukia kama mwaka 34 AD, kwa kuwa unabii wa Daniel 8:13-14  yaani 2300 yrs, wameufanya uumeze muda wote wa majuma 70 bila gepu.  Wahubiri kama William Branham na wengine (walioshika msimamo wa kutumia 360 calendar) walihesabu kuanzia mwaka 445 BC mpaka kukatiliwa mbali kwa masihi aliye Mkuu inaleta jumla ya miaka 475 badala ya 483 yani majuma 69, na inagharimu kutumia Kalenda ya mwezi (360) ili hesabu ije kamili (msomaji upo huru kujifunza zaidi kuhusu hilo, nimekupa mwanga tu (soma tena Ezra 7:21-26)..
Jambo moja linalothibitishwa na historia ni kwamba ujenzi ulitumia miaka 49 kamili, yaani majuma saba kama alivyosema malaika Gabriel. Pia miaka hii miaka 483  inaishia muda ambao Yesu alisulibiwa (mijadala ya lini haswa alisulibiwa mwaka 29AD, 30AD, 33 AD au 34AD) haitatosha kwa mjadala huu. Ila Malaika Gabriel was accurate, hizi distortions zimetokea njiani kwa binadamu kujivuruga katika maswla ya tarehe.

*❹. MAMBO YANAYOTIMIZWA KATIKA MAJUMA 69 (MIAKA 483)*
_mwlproo_

1. Kukomesha makosa,
2. Kuishiliza dhambi,
3. Kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu,
4. Kuleta haki ya milele,
5. Kutia muhuri maono na unabii,
6. Kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu."
(Danieli 9:25 )

"Na baada ya yale majuma sitini na mawili (483 years), masihi atakatiliwa mbali (Kusulubiwa kwa Kristo, possibly from  30-33 AD), naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu (Commander Titus of Rome) atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu (70 AD); na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa."
(Danieli 9:26 )

HIVYO, KUFIKIA MWAKA 70 AD, YOTE YALIYONENWA KUHUSU MAJUMA 69 YANAKUWA YAMETIMIA YOTE, YALITIMIA YOTE BILA KUPUNGUA. HIVYO TUMEBAKIWA NA JUMA MOJA TU, JUMA LA SABINI (7 YEARS) ILI KUIMALIZA MIAKA 490 ILIYOAMRIWA JUU YA WANA WA ISRAEL.

*❺. MAJIRA YA MATAIFA*
⌚ Watu wote waliojaribu kufanya makadirio ya kuja kwa Yesu walijikuta katika kukosea kwa sababu kuna kipindi cha majira ya mataifa au pia twaweza ita kipindi cha kanisa ambacho ni _unknown_ na hivyo kufanya ujio wa Yesu kwa ajili ya kanisa uwe haujulikani, MPAKA SASA KUNA MIAKA 1986 IMEPITA TANGU HIKI KIPINDI KIANZE. Unabii wa Daniel ni mwepesi kueleweka maana kuna numericals (ciphers) zinazorahisisha kazi, lakini unabii wa Yesu kuhusu mwisho wa zama za majira ya mataifa (utimilifu wa nataifa) hayana hesabu badala yake yana dalili/ishara tu.. waliotumia unabii wa Daniel 8 (2300yrs), na kutaka kuamini kwamba 1884 kuna tukio kubwa lazima litokee, au kosa kama lilifonywa na Branham katika mahesabu na kutaka kuamini mwaka 1977 kitu fulani kitokee, yalikuwa ni majaribio ya kutafuta kuDeal na _the unknown/concealed_ yaani *The Times Of the Gentiles*

Hebu tusome......

_*"Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia."*_
(Luka 21:24)

⌚Yako mafafanuzi mengi yaliyohusisha mstari huu na UN, WWII, tukio la 1948, na lile la 1967... Ukweli uliofichika ni kwamba, Malaika Gabriel kwa kuwa alikuwa akiongea na Danny haswa juu ya watu wake, na juu ya mji wake mtakaitifu..Utaona ghafla mastari wa 27 anazungumza habari ya Mpinga Kristo (Ufunuo 11&13), ambapo kuna kipindi kilirukwa intentionally, na ndicho kinatenganisha Majuma 69 na Juma la 70 (miaka 7 ya mwisho). Hayo yanayotajwa katika verse 27 ni yale yatakayofanywa na Antichrist katika miaka saba ya juma la 70. Juma la 70 litaanza mara majira ya mataifa au (utumilifu wa mataifa) yatakapitimia... Wakati wowote ambao kanisa la Kristo litakuwa  duniani kabla ya Mungu kuanza kushughulika na taifa la Israel kwa upya, kipindi hicho chote kinatajwa kama *Majira ya Mataifa*. Najua tayari tumeingia kwenye mjadala mwingine wa Unyakuo (Pre-Tribulation, Mid-Tribulation, na Post-Tribulation).. Well, hatutaingia huko sasa, lakini katika mfululizo huu wa sasa hatutaepuka mjadala huo kwa masomo yanayofuata siku za usoni.
Hivyo kusema ni kwamba, miaka saba ya kipindi chote cha mpinga Kristo, ndilo juma la sabini litakalotimiza miaka 490 iliyoamriwa juu ya Israel.   Kilele cha miaka hiyo ni pamoja na Harmagedoni (Somo hili la vita vya Armageddon lipo tayari mtandaoni, nililiandika miaka mitatu iliyopita)...

*Mwl Proo*
+255762879363

alltruth5ministries@gmail.com