*WAHUDUMU WA AGANO JIPYA:*
_*Agano La Kale Sio Vitabu 39, Na Agano Jipya Sio Vitabu Na Barua 27*_
*ʍաӀ Թɾօօ*
*+255762879363*
Mbarikiwe kwa Jina la BWANA (Yesu). Kuna jambo ambalo Mungu alitia moyoni mwangu nilifundishe, maana kumekuwa na kuchanganya maelezo sana katika hili. Agano la Kale ni lipi na Agano Jipya ni lipi, Je! usomapo maelezo kama ya Waebrania sura ya 8, huyu mwandishi anaonekana kulishambulia sana Agano la Kale kwa kiasi cha kulifananisha na kitu chakavu (kama dekio 👉🏾tambara bovu) pale asemapo, kwa kuliita hili Agano Jipya, amelifanya la kwanza kuwa kuukuu (the first covenant is made obsolete) 👉🏾 (Ebrania 8:13). Je! Haya mashambulizi makali anavishambulia vitabu 39 vile vinavyoitwa Agano la Kale?. Karibu tujifunze maandiko kwa pamoja.
*🌡 Tunayo maagano mawili (which are juxtaposed in Hebrews)*
I. AGANO LA SINAI
2. AGANO LA KALVARI
(Wagalatia 4 )
------------
*24 Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri.*
*25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto.*
*26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi.*
🇮🇱 Wako watu ambao wakisoma nyaraka za Paulo pamoja na Waebrania, wakaona mistari mingi yenye kuonesha Agano Jipya ni bora kuzidi la kale (Ebr 7:22), huenda wakawa wanawaza kuweka katika contrast labda kitabu cha nabii Isaya na Injili ya Yesu kama ilivyoandikwa na Mathayo, kisha wakaanza kulinganisha ubora wa ujumbe. Kinachotajwa kuwa bora sio vitabu 39 ukivilinganisha 27 vya Agano Jipya. Mungu alipokuwa akiahidi kwa vinywa vya manabii, kwamba nitafanya agano jipya (Yer 31:31-40) hakuwa anazungumzia hizo barua za Paulo alizowaandikia wakristo wa Uyunani, Uturuki, Roma na watu binafsi. Bali agano la kwanza (la kale) ni lile la Sinai kwa mkono wa Musa, na agano jipya (la pili) ni lile la Kalvaria (Latin) yaani Kranion (Greek) ambapo kiaramu huitwa (Golgotha) kieneo kilichopo nje tu ya kuta za Yerusalemu (Mathayo 27:33, Luka 23:33). So stop kabisa kufikiri kwamba hiki ambacho kimefanywa kuwa kikuukuu na ki karibu na kutoweka labda kitabu kama cha Zaburi, Daniel, Ezekiel etc, hapana kabisa.
Tusome hapa
👇🏽
(2 Wakorintho 3 )
------------
*14 ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo _Agano la Kale_, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo;*
*15 ila hata leo, _torati ya Musa isomwapo,_ utaji huikalia mioyo yao.*
🇮🇱 Katika italics tunakutana na jina *Agano la Kale, na torati ya Musa*, Paulo alitaja Agano la Kale akiilenga torati ya Musa kwa hapa, na aliitaja akimaanisha maandishi na sio lile agano lenyewe. Ipo hivi linapofanywa agano kunakuwa na masharti ya agano (terms and conditions), hivyo torati ya Musa zilikuwa ni terms and conditons attached to the Sinaic Covenant, na vitabu vingine vyote vimewekwa kwenye mkusanyiko ulioitwa *Agano La Kale* kwa sababu wote walioandika walitumika chini ya agano hilo la Sinai. Kwa hiyo kitabu kama Zaburi kinakuwa katika Agano la Kale kwa sababu kiliandikwa na wahudumu waliohudumu chini ya agano la huduma ya mauti, huduma ya adhabu na sio huduma ya Roho (2 Korintho 3:7, 8, 9). Na pia kama kitabu cha Dr. Luka kiitwacho matendo ya mitume, au nyaraka za Paulo au Petro zikiitwa Agano Jipya, sio vitabu hivyo ndivyo agano lenyewe bali kwa kuwa wahudumu wake wameviandika chini ya agano lililo bora la Kalvari basi vinakuwa ni vya Agano Jipya kwa sababu hiyo, I mean mafundisho ya Kristo na mitume wake ndio *terms and conditions* za Agano la Kalvari (Jipya).
*🌡 Agano jipya lilianzia Kalvari*
(Waebrania 9 )
------------
*15 Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.*
*16 Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya.*
*17 Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya.*
*18 Kwa hiyo hata lile la kwanza halikuanzwa pasipo damu.*
*19 Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote,*
*20 akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu.*
Wakati wa Agano la Sinai, kila sheria (attached terms and conditions) ilipotajwa ilisindikizwa na damu. Na Yesu naye alilifanya Agano jipya kwa damu yake mwenyewe inenayo mema (Ebr 12:24)
*"kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi."*
(Mathayo 26:28 )
Hakikisha unapata somo langu lenye kichwa cha ujumbe *Maagano yanaweza fanywa upya, kufifishwa, kuondolewa kabisa*. Niwaulize swali sasa nini kinachokuja akili mwako unaposoma andiko kama (Warumi 10:4), kwamba *Kristo ni mwisho wa sheria*, Je! kama Sheria ilisema usishuhudie uongo, kwamba you're now free to lie or testify lies? La Hasha!, hapa ndipo tumepata utata na mrafaruku wa hoja. Nini hasa ambacho kinatajwa kwamba Kristo ni mwisho wa sheria, na kwamba sheria ilikuwa kiongozi tu cha kutuleta kwa Kristo (Galatia 3:23-24). Naomba kurudia hili, torati ya Musa ilikuwa (attached string) vigezo na masharti ya kulisindikiza Agano la Sinai, kama ambavyo fundisho la Kristo na mitume wake ndiyo *attached string* vigezo na masharti ya kulisindikiza Agano jipya la Kalvari
*MOYO WA SOMO*
*🌡 SISI WAAMINI KATIKA KRISTO, TULIOAMINI FIDIA YA MUNGU YA MAUTI YA KRISTO, TUMEFANYWA KUWA WAHUDUMU WA AGANO JIPYA (MINISTERS OF THE NEW COVENANT)*
*"Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa _WAHUDUMU Wa AGANO JIPYA;_ si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha."*
(2 Wakorintho 3:6)
👆🏾👆🏾👆🏾 NAOMBA KUREKEBISHA HOJA YA WATU AMBAO UKIWASOMEA ANDIKO ILI KUWAPA MAELEKEZO, WANATUMIA ANDIKO HILI KAMA DEFENSE ETI ANDIKO HUUA. MAANDIKO MATAKATIFU NI NENO LA MUNGU KATIKA MAANDISHI (WRITTEN WORD OF GOD), WALA HAYAUI, KICHOTAJWA HAPA KAMA ANDIKO KATIKA GREEK TEXT NI *γράμματος* yaani *"grammatos"* ambapo Rabbinical interpretation yake huiita *Chumrah* kiebrania yenye maana ya Letter of law(Mosaic Law) or simply Chumrah refers to *Strict adherence to Torah*, hivyo tusikimbie maonyo ya Biblia kwa kusema maandiko huua, sicho kilichokusudiwa hapo, wala usi-intertain mambo ya kusema kwamba maandiko sio neno la Mungu, eti mpaka livuviwe, haya unayoyaona kwa Bible are God-breathed words.
Tuendelee......
✝ Jamii ya waaminio, si waaminio sio wafuasi wa Agano la Sinai, baada ya Kristo kuja, kusimama na Agano lile la Sinai ni matokeo ya kutoelewa kabisa kazi ya msalaba. Agano Jipya ni Jipya, Sio marudio, sio mapitio, sio maboresho ya la kwanza (It's not the restatement of the old testament), ni jipya kwa maana ya jipya. Mjumbe wa agano la kwanza (Musa) Yohana 1:16-17, aliwaambia waisrael kuwa Mungu atawainulia nabii (Yesu) you will have to listen to Him, hivi ninawapa viwaongoze hata atakapokuja, neema na kweli vimekuja kwa njia ya Yesu.
✝ Tusomapo vitabu vya Agano la Kale, sharti tusome in the light of the New Covenant, tukijua kuwa Terms and Conditions za Agano la Sinai ni kivuli tu cha Agano lililo bora la Kalvari (Ebrania 10:1, Kolosai 2:17). Ni hatari kama waamini watashindwa kujua kuwa kitu halisi ni Kristo wakashika kivuli, wakaacha mafundisho ya Kristo na mitume wake wakang'ang'ana vigezo na masharti ya Sinai, watapotea sana kwa sababu ya kutofahamu maandiko wala uweza Mungu.
✝ Vigezo na masharti ya Agano la Sinai havina viwango kuwaongoza waamini katika Kristo (waliozaliwa upya). Agano la kwanza na masharti yake (Sheria, Amri na Hukumu zake), viliamriwa kwa watu walioenenda kimwili kabisa, maana ilikuwa haijaja bado ile ahadi. Hapo ndipo naona ndugu zetu kama wasabato wanaposhindwa kuelewa kuhusu haya maagano. Agano jipya la Kristo limepandishwa viwango maana wahusika wake ni watu ambao wamezaliwa na Mungu kwa upya kwa njia ya Roho, hivyo hawawezi kuwa na makatazo sawa na watu wa agano la kwanza. Kuna mtu nilipomwambia hatuko chini ya Sheria, akasema hivyo wewe upo huru hata kuua, na kuzini eee?? 😁 After the Beatitudes Yesu akaanza kuonesha namna jamii mpya itakayozaliwa kwa damu ya Kalvari itapaswa kuwa. Akaanza kuwahoji kwamba mmesikia imenenwa *"Usiue"* lakini mimi nawajuza kuwa standard ya Agano la Kalvari ni hii *"Ukimchukia tu ndugu yako umekwishaua"*, mmesikia imenenwa *"usizini"* mimi nawaambia Ukimwangalia mwanamke lustfully, *Umekwisha zini naye moyoni mwako* (Mathayo 5:21ff) HIZI NDIZO STANDARDS ZA WAHUDUMU WA AGANO JIPYA, kujifungia kwenye sheria, amri na hukumu za Musa za agano la sinai (la kale), ni kujipeleka mahali ambako Yesu hakutupeleka, ni kuamua kuishi chini ya viwango. Waliozalwa upya hawakatazwi wasiue maana sio tu hawawezi kuua bali hawawezi kuwaza kuua. Musa akiwa anaaddress masharti ya agano la sinai, aka-establish sheria ya malipizi (restitution), kwamba mtu akiiba ng'ombe labda mmoja atapaswa kurudisha siju watano, waamini waliozaliwa upya, na kujazwa Roho wa Kristo, hawapaswi kuwekewa sheria za watu wa mwilini kwamba ukiiba mmoja ukipatikana utalipa mara tano, sababu ni hii kwamba baada ya kuzaliwa upya na kufanywa kuwa wahudumu wa agano jipya, hata hilo wazo la kuiba huyo ng'ombe mmoja hatuwezi kuwa nalo, hata kama tutakuta kuna mbuzi 🐐kapotea, hatuna wazo la kumwiba na hiyo ndiyo tafsiri ya kusema hatupo chini ya sheria (Galatia 5:18, 22). Kwamba hatuwezi kukatazwa kuzini wakati standard yetu ya Agano lililo bora inasema uasherati usitajwe kabisa (Efes 5:3). And as the matter of fact mnapozidi kuzama sana kwenye Mosaic Law ndivyo mnavyozidi kutengwa na Kristo (Gal 5:4).
✝ Nimefanya studies juu ya kitu kiitwacho kiebrania *Korbanot* mifumo ya dhabihu na matoleo ya kiyahudi, nilipofahamu kwa mtazamo sahihi wa kiyahudi ndipo nikagundua haya mambo tumeya-copy kwenye ukristo kimakosa na kwa kukosa ufahamu sahihi, hata kama yana mvuto masikioni kiasi gani, mikazo yote ya malimbuko, zaka za fungu la kumi etc *I DARE TO SAY THEY ARE ALL IRRELEVANT TO CHRISTIAN DOCTRINE AND CONTEXT*, ila yalipokelewa kimakosa na wanaopaswa kufundisha ukweli huu hawawezi kabisa. Kuna mchungaji aliniambia Mwl Proo ukiwa mchungaji huwezi kufundisha kuwa mafundisho kama ya malimbuko na zaka sio ya kikristo, nami sishangai maana tuna wakristo wanatoa zaka million 20 lakini sadaka za hiari na matoleo mengine wanatoa elfu 2 elfu 5, hapo ni wazi hakuna namna ya kufix hilo.. Ila fundisho lilipokelewa likiwa na makosa tayari, Ukristo upo juu kuliko hizo terms na conditions za Taurat ya Musa, kuweka hako kakiwango ka 10% ni utoto na udumavu kwa viwango vya Agano la Kalvari, maana waliowekewa 10% ni kwa sababu ya ugumu wa mioyo tu, Sisi hatupaswi kuwa na mioyo migumu kamwe, tukiisha mpa Mungu mioyo yetu tunakuwa tayari kumtolea Mungu chochote sio kwa kipimo (2Cor 9:7), forget about Abraham ambaye sio tu hakuwahi kutoa zaka ya fungu la kumi, bali hakukuwepo hata mahali pa kuipeleka hiyo zaka ya fungu la kumi, incidence ya kukutana na Melkizedeki haikuwahi kujirudia tena, na wala katika mapato yake hakuwa kutoa zaka kabisa achana na zile nyara za vita ambazo hazikuwa zake. Amani unayoisikia haiwi amani ya Kristo bali na amani ya fundisho lililotangulia (pamoja na makosa yake), ni sawa tu na kumtaabisha mprotestanti kwamba kubatiza vitoto vichanga au kwa kununyiza maji ya kibakuli sio sawa, atakaza kujitetea huku akishindwa kung'amua kuwa ni fundisho ambalo kimakosa lilivushwa (halikuchujwa) toka Kanisa Katoliki, ni kwa namna hiyohiyo tu, kinakuwa kitu kigeni, lakini hiyo hainizuii kuandika ukweli wa Biblia ni upi, na kipi tunakifanya kimakosa. Haka katabia ketu ka kuwa machotara tunadonyoa na kunyofoa kasheria kamoja kati ya zile 613 za Taurati, hakafai, hakana maana kabisa. Yaani unabandua sheria kuhusu riba unaishika, halafu ya kutopanda mbegu mbili katika shamba moja unaivunja, unashika siku ya pumziko (sabato) ila unavaa nguo yenye vitambaa vya aina mbili tofauti ambayo ni dhambi kwa mujibu wa terms za Agano la Sinai. Sheria ya Musa ina dai moja kubwa ukishika uzishike zote, ukivunja moja umevunja zote, bila kubagua sijui ceremonial laws au moral laws, ukitaka kujichomoa kwa hilo kongwa la utumwa ni kwa kuamua kuwa mhudumu wa Agano Jipya, hilo tu. Nisiongelee hilo sana maana nimechambua kwa kina kwenye somo la *UKWELI KUHUSU ZAKA YA FUNGU LA 10* ukilihitaji naweza kukurushia. Hoja yangu ya msingi ni kwamba sisi ni wahudumu wa Agano Jipya lililo bora, tunatarajiwa kuishi sio kwa ufunuo mdogo wa zamani au mafundisho ya awali ya ulimwengu, bali kwa njia ya Kristo, Mungu ameifunua siri ambayo ilisitirika yangu enzi na enzi.
*TUKUTANE KWENYE SOMO LIJALO*
*Mwl Proo*
0762879363
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment