Wednesday, July 24, 2019

FALME NA MAMLAKA

*FALME NA MAMLAKA*

*ʍաӀ Թɾօօ*
```+255762879363```

```Ndugu zangu katika Yesu Kristo, aliye Mwokozi na Bwana, karibuni katika kujifunza siri zilizofunuliwa (The revealed mysteries not  myths) ambazo Mungu kwa Roho wa Kweli anazifunua ili atusaidie. Waamini wanahudumiwa kwa namna nyingi na malaika (Ebrania 1:14), na walipaswa wafanye huduma zao nyingi kwa maelekezo ya waamini ambao kwa bahati mbaya hawana maarifa sahihi juu ya mambo haya, na kupelekea kufanya mengi kwa kupapasa-papasa na kupepesa-pepesa tu.```

*🏹 KAMA NDUGU MSOMAJI UNA MAONO YA KUTUMIKA KWA VIWANGO VIKUBWA VYA KUTENDA KAZI, BASI USIYAACHE MAARIFA HAYA SAHIHI. I BET YOU KAMA KUNA KITU KIMEZUIA KAZI KUBWA KUTENDWA NA WATU WA MUNGU, BASI NI MAARIFA. WATU WAMEKESHA MILIMANI, WAMEFUNGA MAOMBI YA KUTOKULA KABISA KWA MUDA MREFU (DRY FASTS), LAKINI KAZI ZINAZOONEKANA HAZILINGANI HATA NAMNA WALIVYOJIDHILI KWA MAOMBI. MUNGU HAYUKO MBALI HIVYO, KILICHOKOSEKANA ZAIDI NI MAARIFA SAHIHI. KILA MWENYE MAARIFA SAHIHI NA YA KUTOSHA KIROHO, HUKO ALIPO ATAKUWA NA TOFAUTI KATIKA KUTENDA KAZI. UKIKOSA MAARIFA HAYA SAHIHI HATA KAMA UNAJIANDAA KWA UTUMISHI UNAWEZA KUINGEZA IDADI YA WATUMISHI WA KANISA/DINI YENU LAKINI USIWE MIONGONI MWA WALE AMBAO BWANA ALIWATAJA NI WATENDA KAZI (MATH 9:37). THE TIME COMES AMBAPO WALE WALIOZOEA KUWA NA MANENO MATUPU WITH NO IMPACTS HAWATAKUWA NA CHA KUFANYA ZAIDI, UFALME HAUWI KATIKA NENO BALI NGUVU (1KOR 4:20). YESU ANATAFUTA WATENDA KAZI ATAKAOWEZA KUWATUMIA KWA KAZI KUBWA KWENYE HIKI KIZAZI CHA SIKU ZA MWISHO, ILI HATA WASIPOAMINI MANENO, AU WATUMISHI, WAZIAMINI KAZI ZITAKAZOSHUHUDIA WAZI-WAZI KWAMBA NENO LA KRISTO NI LA KWELI NA AMINI (YOHANA 10:38). WENGI WAKIKEMEA KWA JINA LA YESU, WAKIONA PEPO WAMEPAZA SAUTI VILIO BASI WANAHISI WAKO KWA GOOD POSITION, WATUMISHI SHARTI WAZINGIRWE NA ISHARA, AJABU NA MIUJIZA (2KOR 12:12), HIYO YA KUTOA PEPO NI ISHARA TU YA KAWAIDA KWA WAAMINI WOTE (MARKO 16:17), HAINA U-SPESHO WOWOTE, MAANA KAZI ALIKWISHA IMALIZA YOTE YESU, TUNAPOYATOA MAPEPO/MAJINI, TUNAYAKUMBUSHA TU NI MAMLAKA IPI ILITUELEKEZA KAZI HIYO, NAYO YANAJUA HAKIKA KAMA NI KWA MAMLAKA YA HUYO YESU BASI HAKUNA KINGINE, NI KUTII TU... MIMI BINAFSI SIKO TAYARI KABISA KUWA MTUMISHI WA MANENO MATUPU, KUWASOMEA WATU STORI ZA BIBLIA AMBAZO HAZIKO HAI KWAKO, KWA MUDA HUU MFUPI WA UTUMISHI NIMESHUHUDIA ISHARA, AJABU, NA MIUJIZA, NATAZAMIA KUMWONA MUNGU KWA KAZI KUBWA SANA NINAPOENDELEA KUSHIKAMANA NA UTIMILIFU WANGU KWA MUNGU*

*🏹 WAKRISTO (WAAMINI) KUNA MISTARI KATIKA BIBLIA HAWAJAWAHI HATA KUIELEWA KWA SABABU YA SIRI KUTOFUNULIWA. MKRISTO AMBAYE AMEKOSA HELA YA CHAKULA HATA USIKU WA JANA ALIPIGA DESHI (⛔) KWA KULALA NJAA, THEN UMSOMEE MSTARI KWAMBA SISI WAAMINI TUMEKETISHWA JUU SANA NA KRISTO, KULIKO UFALME WOTE, KULIKO NGUVU ZOTE, USULTANI WOTE, KULIKO ENZI NA VITI VYA ENZI VYOTE, AKIYAAKISI MAISHA YAKE, NA MAANDIKO HAYA ANAWEZA ASIYAELEWE KABISA, SIMAANISHI KWAMBA WATU WAKILA NA KUSHIBA WATAELEWA SIRI ZA UFALME (WARUMI 14:17, IMEZINGATIWA)*

*❶ UUMBAJI WA ULIMWENGU (CREATION OF THE UNIVERSE)*

☄ Maneno haya mawili _"Dunia na Ulimwengu"_ yamekuwa yakitumika kwa pamoja kwa kubadilishana *interchangeably* na hivyo tunakosa maana nzuri kwenye Kiswahili, lakini katika Kiingireza neno Universe halitaji hili litufe la dunia bali (space+time), hivyo kama kuna sayari zingine mbali na dunia na chochote kingine in the space ni *universe/ulimwengu*

☄ Mungu alipoumba (Mwanzo 1:1), aliumba mbingu na nchi (Ha'Shamayim & Erets), sasa  neno la kwanza halizungumzii tu mbingu ile ambayo ni ya kiroho BUT  limejumuisha all the skies ambazo zinaweza kufikiwa physically 🚀👨🏾‍🚀👩🏾‍🚀 na la pili linaitaja nchi/earth (land/ground).....

☄ Sasa alipoumba Universe/Space (ulimwengu) aliumba maumbile mengi si dunia tu 🌏, na hayo maumbile (bodies) 🌓🌞🌪 yaliwekewa wasimamizi, viumbe vya kiroho wakiwa in charge of those bodies. Hawakuwa na uhusiano wowote na sayari ya dunia ambayo kimsingi kerubi mmoja ambaye sasa ni shetani alikuwa in charge wa dunia (Ezekiel 28:14, Isaya 14:12-15)... Shetani alikuwa huru kupanda mbinguni muda wowote, mpaka alipopata wazo la kumpindua Mungu....

Shetani hakuanza makeke yake Bustani ya Edeni, alishafanya hivyo tangu akiwa msimamizi wa dunia mwanzo kabisa... Yesu anasema jambo moja very sensitive katika Yohana 8:44

*"Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo."*

Shetani haitwi baba wa uongo kwa kumdanganya Eva, alikwisha danganya viumbe vya kiroho vingine vilivyowekwa kwenye ukuu wa kusimamia maumbile mengine ya uumbaji wa Mungu, si hivyo tu, katika harakati zake za kumpiku aliyemwumba na yeye alishawishi viumbe vya kiroho (malaika) wanaotajwa kama nyota (Ufunuo 12:4), na kwa mkia wake akawakokota theluthi ya malaika waliokubaliana na uongo wake, hapo ni kabla ya Adamu huyu baba wa wanadamu wa leo.

*❷  FALME NA MAMLAKA*

_*"ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na FALME na MAMLAKA katika ulimwengu wa roho;"*_
(Waefeso 3:10)

*_"Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya FALME na MAMLAKA, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."_*
(Waefeso 6:12)

☄ Mungu aliumba wakuu (princes) wa kusimamia maeneo yote katika ulimwengu (including large bodies in skies and all starry hosts).... Ziko mamlaka ambazo zilimtii shetani kwa kuwa alizishawishi (aliumbwa na hicho kipawa cha influencing)...nimemsikia  Prophet Sadhu akifafanua kuwa hata lugha za malaika hazifanani, na shetani alitumia lugha fulani fulani kuwasiliana na watawala (angelic beings) wa sayari zingine...
(Mfano wakuu hawa hapa chini wanasimamia sayari saba wajulikanao kwa jina la *ARCHONS* these make up the powers of darkness)
1. Yaldabaoth (Saklas/Samael)
2. Iao
3. Sabaoth
4. Astaphanos
5. Adonaios
6. Elaios
7. Horaios
Majina haya yako kwa matamshi ya Kiebrania na Kiyunani, na majina ya mapepo mengi ni majina ya nyota/other heavenly bodies na ipo sababu (nitaieleza katika somo jingine). Majina kama Maimuna ﻣﻴﻤﻮﻧﺔ
lenye maana ya *lucky/blessed* i.e.; mwenye bahati/mwenye heri, haya sio majina kamili/sahihi ya hizi roho za kipepo hata kama muda unakemea pepo akajibu mimi ni Jinn Aisha.

*❸  FALME NA TAWALA ZA DUNIA NI UVULI WA TAWALA ZA FALME/MAMLAKA ZILIZOKO ROHONI*

☄ Katika historia ya kale 3000BC ---- 476AD, kulikuwa na tawala za dunia zilikuwa zinapata nguvu na kuzishinda zingine  (ANCIENT DYNASTIES AND GREAT POWERS OF THE ANCIENT WORLD). Shetani ni mmoja, naye ni roho, alipotaka kutekeleza mambo fulani fulani juu ya dunia, aliweza kusababisha utawala mmoja uanguke na mwingine ushike nguvu...
Hivyo kuna wakati ASHURU (ANCIENT ASSYRIAN EMPIRE) Ilikuwa na nguvu, kwa sababu fulani-fulani Shetani akafanya Babeli ya kale (Ancient Babylonian Empire 1894BC kushika nguvu ya dunia), na baada ya hapo nguvu ilishikwa na Misri, baada ya hapo Uyunani baadaye Rumi

*NB:-*
```OUR SUPREME GOD IS THE SOVEREIGN LORD, HAKUNA CHA KUMZUIA KWA LOLOTE MAANA YEYE NDIYE AMEVIUMBA VYOTE. HIVYO KUNA WAKATI SHETANI ANAWEZA WEKA MIPANGO YAKE, MUNGU AKAPACHIKA LA KWAKE HUMO-HUMO, AND THE DEVIL GETS CONFUSED..... ILI NAYE AKUMBUKE KUWA ALIUMBWA (EZEKIEL 28:13-14)```

🧨 Shetani alitaka kuvuruga mpango wa Mungu wa kumleta Yesu, aliouahidi pale Mwanzo 3:15 (Woman's seed/offspring), na hivyo alikusudia kuichafua human race ili Kristo asiwe sadaka ya kufaa kwa ukombozi... Na alifanikiwa kuharibu human race (degeneration) pale Mwanzo 6:2-12... Nuhu aliingia kwenye safina na Shetani kwenye genes za wakweze.... Ham, Shem na Yaphet na wake zao hawakuwa salama kwa ule uchafuzi... HISTORIA INAONESHA HAM NA YAPHET WOTE WALIKUJA KUZAA MAJITU (GIANTS) KWENYE VIZAZI VYAO, LAKINI MUNGU ALIMHIFADHI SHEM NA HISTORIA INAONESHA VIZAZI VYAKE HAVIKUWA NA MAJITU, ILI KRISTO APITIE HAPO (Najua ni wachache wameelewa hapa, nitayafafanua katika masomo yajayo)
(mwl proo)

🧨 Kesi zote za Yusufu, Musa, Yesu Shetani akikuwa anaweka mpango wa kuangamiza, Mungu akautumia mpango huohuo kuokoa.

☄ Falme na Mamlaka zina uwezo wa kuweka mtu awe mtawala juu ya eneo (dominion and territory), kwa makusudi fulani ya Shetani.

*_"Yeye hubadili majira na nyakati; huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa;"_*
(Danieli 2:21)

Ni ukweli usiopingika, Mungu ndiye anayeweka tawala na falme za kutawala wanadamu wengine (Warumi 13:1ff), Lakini ni ukweli wa Biblia pia falme na mamlaka za giza, zinaweza kuweka viongozi/watawala juu ya eneo fulani la dunia kwa makusudi ya Shetani.

*NDIO MAANA WATU WA ROHONI, HAWAPASWI KUWA WASHABIKI WA KISIASA MAANA USHABIKI UTAWAONDOLEA KUYAJUA MAKUSUDIO YA MILELE YA MUNGU JUU YA WATAWALA WANAOPASWA KUWEPO. TUNAPOLEKEA KWENYE UCHAGUZI WATU WA ROHONI WANAPASWA KUOMBA MAANA, SHETANI ANAWEZA KUWEKA MTU WAKE (BWANA MGUMU) ILI AWEZE KU-TORTURE KANISA NA WATU WENGINE KWA MKONO MZITO, MKIKAA KISHABIKI HAMWEZI GUNDUA HILO, NA MTAACHA KUOMBA MKIHISI KILA ANAYEPITA AMEWEKWA NA MUNGU.

(Danieli 10 )
------------
*20 Ndipo akasema, Je! Unajua sababu hata nikakujia? Na sasa nitarudi ili nipigane na mkuu wa Uajemi; nami nitakapotoka huku, tazama, mkuu wa Uyunani atakuja.*
*21 Lakini nitakuambia yaliyoandikwa katika maandiko ya kweli; wala hapana anisaidiaye juu ya hao ila huyo Mikaeli, mkuu wenu.*

☄ Falme na Mamlaka za giza, zinaamua eneo husika la chini ya Dunia, liweje kiroho, kiuchumi, kisiasa, kidini n.k... Zilifunika eneo kwa giza la umaskini, hata kama hilo eneo litapokea misaada toka Benki ya Dunia, litabaki na umaskini wake mpaka watu wa nuru waliondoe lile giza kwanza. Kuna maeneo yana machafuko ya kisiasa miaka nenda rudi, zitatajwa sababu nyingi na wanaharakati ila sababu moja watakayoiacha ndioya kweli, kwamba falme na mamlaka za eneo hilo zimeachilia spirit of political instability... UN itapoteza resources zake mpaka siku ya unyakuo, shida iko rohoni... Mambo yanayoendelea EUROPE kwa sasa ni kazi za falme na mamlaka, nimeona picha za makanisa yanauzwa (Church Buildings For Sale) 💒⛪🏛

☄ Watu wenye vifungo vigumu zaidi ni wale ambao wako *initiated* kwenye hizi falme na mamlaka. Bila shaka umewahi sikia wanawake/mabinti kadhaa wakisema nilienda kuzimu 👩🏾👩🏾‍🦰👱🏾‍♀ nikafanywa kuwa malkia 👸🏾👸🏾... Sasa swali linaweza kuwa malkia wanakuwa wangapi huko kuzimu? Hawa watu hata kama walikutana na mkuu aliyejitaja kama Lusifa, kiukweli wanakuwa wapo tu kwenye moja ya falme na mamlaka (Kingdoms and Principalities), vifungo vya ambaye yuko initiated kwenye ngazi hii ya pili toka kwa shetani, inaweza kuhitaji nguvu kubwa zaidi katika kumfungua kuliko ambaye yuko possessed na mapepo. Mtu akiwa initiated kwa falme na mamlaka anakuwa ni wakala wa hizo nguvu ni tofauti na mtu aliyepagawa pepo kwa kawaida.

☄ Falme na Mamlaka kwa kuwa ni ngazi ya juu sana, inatawala eneo kubwa la uso wa nchi. Chini yao kuna wakuu wa giza hili (au wakuu wa anga). Rejea chati iliyo katika somo langu la *VITA VYA ROHONI* hizi ngazi za chini zinawezeshwa na kupokea maagizo toka nguvu ya juu zaidi... Vyote vinatimiza makusudi ya moyo wa Shetani... Waamini ambao wana maarifa kamili ya ulimwengu wa roho ndio jamii pekee ya wanadamu yenye uwezo wa kushughulikia hizi ngome zote.  Kuna wakati nilisikia Mwl Christopher Mwakasege akisema, *"Kuna maeneo ukienda usianze kusema nakemea mapepo yote  yahame hapa, kwamba kuna sehemu yapo kihalali kabisa"*, hiki kitu ni cha ufahamu wa juu ambacho wasiozingatia maarifa hawawezi kuelewa.

KUNA MAENEO MNAWEZA MKAENDA KIHUDUMA, MKAONA MAMBO MAGUMU TU, MNASHAMBULIWA NINYI NA VITU VYENU. KUMBE MKUU WA ANGA WA ENEO HILO AMEFANYA VITA NANYI HAMSTUKI (MATHAYO 12:29), USIDHANI KWAMBA HIZI FALME NA MAMLAKA HAZINA NGUVU KABISA. MUNGU YUKO SYSTEMATIC, ALIWAUMBA NA NGUVU NA UWEZO, NA WALIPOASI HAKUWANYANG'ANYA NGUVU WALA ULE UWEZO (i.e, THE FALLEN ANGELS POSSESS GOD'S POWER BUT THEY USE IT FOR EVIL PURPOSES, AND THUS MAKES POWER OF LIGHT TO BE POWERS OF DARKNESS). MKISHAMBULIWA KIROHO MNAWEZA KUDHURIKA KIROHO, MKADHURIKA MIILI YENU, AU PHYSICAL ASSETS, MAGARI, VYOMBO VYA MUZIKI, MAJENGO, HATA MIFUGO INAWEZA KUPATA SHIDA IKIWA NI KIASHIRIA KUWA MKUU WA ANGA AMEFANYA VITA NANYI NA KUNA MAHALI AMEWASHINDA. KAMA MTAFANYA VITA VYA ROHONI NA KUMSHINDA KABISA MKUU WA GIZA NA MAJESHI YA PEPO, BASI ANAWEZA KUTUMIA HUMAN-AGENCIES KUJA KULETA HATA VURUGU ZA KAWAIDA TU AMBAZO SIO ZA KUKEMEWA BALI KUSHUGHULIKIWA KWA HATUA STAHIKI BAADA YA KUOMBA. HAPA WAZOEVU WA MAMBO YA KIROHO WATASAIDIA ZAIDI, MAANA  MNAWEZA TUPIWA ROHO YA CONFUSION, MKAANZA KUSHINDANA KWENYE MAMBO YA KIJINGA TU, MKAKATU MMEBADILISHIWA FOCUS NA TARGET (mwl proo).

*❹ YESU KRISTO AMEKITI KUUMENI MWA KITI CHA UKUU MBINGUNI, PAMOJA NA WOTE WALIOMWAMINI*

Ufunuo 5:9-10
1Kor 15:24-28
Kolosai 2:10, 15, 1:16
Efeso 1:21, 2:6
Somo hili limekupa kutambua kuwa kuna falme na mamlaka za giza rohoni.... Kuba Ufalme, mamlaka, nguvu, usultani. kuna majina yenye nguvu, kuna vitu vya enzi.... LAKINI YUPO YESU KRISTO ALIYEINULIWA JUU YA KILA NGUVU, KILA JINA, KILA UFALME, KILA USULTANI.... ALIPOKETISHWA YEYE AMEKETI NA KILA MWAMINI KWA JINSI YA ROHO

☄ Mtu anapomwamini Yesu kabisa kabisa na kuokolewa, ananyofolewa kule kwenye ufalme wa giza (Kolosai 1:13), wanakofungiwa wasioamini wote. Tukio la Yeye kuketishwa mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha ukuu pamoja na Kristo linafanyika mara moja. Mtu akiamini na uchanga wake huo, anakuwa ameketishwa juu sana....(Far above ) kuliko hizo falme kuliko mamlaka za giza, kuliko wakuu wa giza, kuliko majeshi ya pepo...

Mwaka 2004, nilihudhuria ibada moja ya saa ya maajabu kwa Askofu Kakobe... Aliita mbele watu ambao kwa mara ya kwanza wanataka kumwamini Yesu awe Mwokozi na Bwana... Kisha baada ya hapo, akafanya maombezi ambayo pepo wachafu walidhihirika kwa wengi... Alipata ufunuo kwamba pepo hao wanapswa kutolewa na waamini wapya waliokata shauri muda huo huo...Na kila mwomgofu mpya alitoa pepo siku yake ya kwanza, hata hawakuwa wamejua namna nzuri ya kuomba. Nakumbuka pepo mmoja alikuwa akinguruma kama simba 🦁 akijisema kuwa yeye ni pepo-simba, hawezi kutolewa na mwongofu mpya,akamwambia Kakobe "mimi unitoe wewe mwenyewe, na si hawa".... Lakini ili kuthibitisha neno la kweli katika ufunuo, akaitwa mwamini wa siku hiyo, ambaye bado hajajua hata mambo ya ufalme huu, lakini ameamua kumwamini Yesu, na jina la Yesu likafanya kazi yake sawa-sawa.

*☄ NIWEKE SAWA JAMBO MOJA HAPO. KUKETISHWA NA KRISTO JUU SANA KULIKO FALME NA MAMLAKA, KULIKO USULTANI NA NGUVU NA MAJINA YOTE YATAJWAYO, NI TOFAUTI NA KU-OPERATE AU KUTENDA KAZI KWA MAMLAKA NA MADARAKA MAKAMILIFU YA KRISTO. MTU ANAWEZA KETISHWA NA KRISTO NA AKABABAISHWA VIPEPO VIDOGO TU. MTU AKISHAAMINI, LAZIMA AKAE KATIKA UTAKASO (1THES 4:7), LAZIMA AUKULIE HUO WOKOVU (1PETRO 2:2) KWA MAZIWA YASIYOGHOSHIWA, LAZIMA APATE NENO LA KWELI NA MAARIFA YA ROHONI ILI KUMFANYA IMARA AWEZE KU-OPARATE KAMA *MFALME NA KUHANI* MWENYE KUTAWALA PAMOJA NA KRISTO.

Tukutane katika somo lijalo

*Mwl Proo*
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

Saturday, July 20, 2019

SUPERNATURAL LIFE

*LIVE A NATURAL LIFE SUPERNATURALLY*
_Ishi maisha ya asili kwa namna isiyo ya asili_

*ʍաӀ Թɾօօ*
*0762879363*

Shalom Aleichem!
Karibu katika kujifunza kweli ya neno la Mungu, ili nguvu iliyo katika neno hai la Mungu ibadilishe maisha yetu kwa Jina la Yesu Kristo aliye Mwokozi na Bwana.

*🌈 MALENGO YA SOMO*

*❶ Kuwawezesha watu wa Mungu (waamini) waishi maisha ya kiwango kama watu wa rohoni.*

🧬 Tumechoka kuwa na wanaoshindwa kila eneo la maisha, elimu, biashara, huduma etc
🧬 Waamini ambao bado wana vifungo vya kipepo
🧬 Waamini ambao wanakaliwa na maradhi/magonjwa na kuishi kwa mfumo wa kitabibu badala ya kuishi kwa imani yao
🧬 Waamini ambao wana-Compromize wokovu wa Yesu wenye gharama kubwa, kwa sababu ya ugumu wa maisha. (Wapo ambao walijitahidi kulinda enzi zao kwa muda, mambo yalipokuwa magumu zaidi wakakubali kufanya mambo ambayo walijua kabisa hapa naachana na Mungu, ila compromize ililetwa na ugumu wa maisha..
🧬 Tumechoka kuwa waamini wanaorushwa na upepo wa kila elimu, mpaka wanajikuta wamejiingiza kwa manabii tapeli na feki, wakaharibikiwa ndoa zao, wakaharibikiwa maisha yao ya kiroho.

🧬 Tumechoka kuwa na wakristo tegemezi, waliofikia viwango vya kuwalipa watu pesa wawaombee, akitaka kulala anafoadi meseji kwa mtume wa mitandaoni kwanza, ndipo aamini anaweza lala salama, kila anachoota ni mpaka afoadi kwa social media kuomba msaada, utoto huu mpaka lini??

*❷ Hizi zama za mwisho, waamini wasio na ujuzi, waliolishwa dini, hawaishi wala kuenenda kwa Roho (Galatia 5:25), hawatakuwa na impact yoyote. Hivyo kwa masomo haya ya sasa, nipo kumwandalia BWANA watenda kazi (1Korintho 12:6, Math 9:37).*
_mwlproo_

*🌈 KWA NINI MAISHA YA ASILI UYAISHI KWA NAMNA ISIYO YA ASILI*
Zaburi 115:16, Yohana 15:19, Filip 3:20,  Ebrania 6:5

🧨Maandiko hayo juu yanatuundia *equation* muhimu sana. Mbingu ni mbingu za Bwana bali nchi, amewapa wanadamu, tena anasema ninyi si ulimwengu, kisha anasema wenyeji wetu (our citizenship) uko mbinguni, kisha anasema katika Ebrania 6 kuwa mtu anaweza kuishi katika dunia hii, lakini akaonja nguvu za zamani zijazo (eternity is cousin to supernaturality)... Na sisi waamini tumeitwa kuanza kuyaonja hayo yote tukiwa bado kwa hii planet earth 🌍. Hivyo maisha haya tuyaishiyo sasa duniani ingawa yako natural, but we are supposed to live supernaturally, kama tunataka kufikia kwenye standard ya kutembea na Mungu.

🧨 Mwanadamu, yuko na Mwili, Nafsi, na Roho (Mwili uliwekwa na Mungu for Naturals (bound to nature), Nafsi ni driving force (eneo la reflection), lakini roho za wanadamu ni za kiroho, sio za asili ya dunia asili ya roho zetu ni rohoni i.e., mbinguni (Enoch 15:8-9), So to say, our spirits are bound to Supernaturality (Supernaturals/Spirituality)... Hakuna namna mwanadamu  mwenye roho ndani yake atafikia kiwango cha maisha ya kiroho cha kutembea na Mungu kama hataishi na kuenenda kama mtu wa rohoni (1Korintho 2:14-15, Galatia 5:25).

🧨 Unalazimika kuishi kwa jinsi isiyo ya asili maisha haya ya asili kwa sababu, vitu halisi vyote viko rohoni, huku nje (in the physical) ni vivuli tu, ukishugulika na vivuli mwishoni utajikuta umechoka na haukufanya kitu chochote cha maana. Mambo yote yanaanzia rohoni, ili kufanya chochote cha kuathiri huku mwilini (affecting changes in the physical) sharti hayo mabadiliko uyasababishe rohoni, then huku nje yatatokea tu hata kama utakuwa umelala fofofo. Unataka kuifuta ajali iliyoko mbele, ifute rohoni haitatokea mwilini. Unataka kufuta kifo alichoandikiwa mtu na adui, kifute rohoni, hatakufa huku nje. Unataka kumbadilisha mume mlevi 🍻🍺? kwa maombi, mbadilishe rohoni, huku nje ataacha, ndivyo ilivyo kwa mambo yote, ukiweza kuli-adjust jambo rohoni, litatokea huku nje likiwa na hizo adjustments, maana dunia inazunguka huku nje (rotation/revolution) huku iki-comfrim na ku-comform mambo ambayo yalikwisha tokea rohoni. Yesu Kristo kama Mwanakondoo wa Mungu 🐑, alikwisha chinjwa kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu, kwa ajili ya dhambi zetu, lakini huku nje kulikuwa kunasubiri majira (Galatia 4:4), muda ulipofika likatukia jambo ambalo lilikwisha fanyika rohoni milenia nyingi za tangu zamani tangu milele.
_mwlproo_

*🌈 NI KWA NAMNA GANI MTU ANAWEZA KUYAISHI MAISHA UA ASILI KWA NAMNA ISIYO YA ASILI*

*🧨 Ubatizo wa Roho Mtakatifu, na kuutunza moto usizime (Baptism of the Holy Spirit, and keeping the fire unquenched)*
🕊🕊🕊🕊🔥🔥🔥🔥
Joel 2:28, 1Thes 5:19, Walawi 6:13, Yohana 14:17

💥 Holy Spirit should be very alive inside you... Mimi mwalimu wa Jiografia kitaaluma, nafundisha kuhusu *Volcanoes* zinaweza kuwa katika hali tatu za kimsingi 1. Active state (Alive/Hai),  2. Dormant state (Sleeping/Inakuwa katika usingizi) na 3. Extinct state katika kufa, Volcano yenye hali ya 1 iko hai, inalipuka muda wowote tu, hiyo ya 2 imelala hailipuki, ila imewahi lipuka muda si mrefu, na hiyo ya tatu imekufa, ina historia ya kulipuka, ila haitazamiwi kulipuka tena. Mwamini anayeweza kuyaishi maisha ya asili kwa jinsi isiyo ya asili, ```SHARTI AWE NA ROHO WA KRISTO NDANI YAKE AMBAYE NI ACTIVE & ALIVE```

*🧨 Orientation to the spiritual realms (spirituality)*
Kutambulishwa/kujuzwa mambo ya rohoni (Getting exposed to spirituals)

🧬 Mtu anaweza kuwa-oriented rohoni na
👉🏾 Ufalme wa nuru (Kingdom of light/Holy Spirit)

👉🏾 Ufalme wa giza (Kingdom of darkness )
#Shetani
#Falme na Mamlaka
#Pepo wabaya (Demons)

*SWALI*

Who introduced/oriented you to spirituals????????

🧬 Roho Mtakatifu yuko *commissioned* kututambulisha *_orienting us_* rohoni, kufanya tuyajue ya rohoni, tujulikane rohoni na kutufanye tu-operate rohoni. Usishangae rohoni tuko na badge au IDs ambazo viumbe vya kiroho vinatuona navyo na kusalimu amri. Waulize wana wa Skewa (Mdo 19), walipokemea pepo wabaya, wale pepo walisema *YESU TUNAMJUA, NA PAULO TUNAMFAHAMU*, NINYI NI AKINA NANI? WE DON'T SEE YOUR IDs KABISA, YOU KNOW THE STORY BILA SHAKA.
Yohana 16:13, 1Kor 2:10-13, Isaya 48:6.

🔥 Mtu akiishabatizwa kwa Roho Mtakatifu, na kujifunza utendaji wake, ghafla anaanza kuona mambo ya rohoni, anaona mambo yake, ya wengine, ya nchi na kadhalika Atayaona ya kiMungu hata ya Shetani atayaona, maana amekuwa oriented to spirituality mahali ambako Mungu (the spirit-God) yuko, na mahali ambako shetani (the spirit-devil) yuko, usisahau hili, Ibilisi naye ni roho, hivyo usijistress sana na vitu vya nje when dealing with him, ukawa bize kumwagia chumvi ya upako kwenye nyumba yako kumkinga shetani, wakati yeye kama roho ameyatawala maisha yako kwa dhambi (tabia ambazo yeye ni baba kwazo), unamfukuza shetani kwenye biashara kwa stika ya upako wa nabii, ila yeye amejaa moyoni mwako.

🧬 Lakini mtu anaweza kuwa spiritual-oriented kwa kutambulishwa rohoni/kiroho na roho zingine

*🌈 TOFAUTI YA MTU ALIYETAMBULISHWA ROHONI NA ROHO WA MUNGU AU ROHO ZINGINE ZA KIGENI*

🧨 Kwa aliyetambulishwa na Roho wa Mungu, darasa litaanza baada ya Ubatizo wa Roho Mtakatifu (In some few & rare cases, mtu anaweza kutambulishwa rohoni akiwa bado hajabatizwa kwa Roho, then ubatizo ukija, unakuja kumweka sawa. Unajua hata Sauli aliyeitwa Paulo alikuwa oriented to spirituals akiwa hajabatizwa na Roho bado. Kitendo cha yeye kumsikia Yesu, katika ile nuru ambayo rafikize hawakusikia (Mdo 9:1-20) ni tendo la orientation to spirituality. Ubatizo katika roho ulikuja baadae kumweka sawa katika mambo ya kiroho. Lakini masikio yale yaliyofunguliwa rohoni pale njiani kuelekea Dameski 👂🏽👂🏽 angeweza kuendelea kusikia vitu vya rohoni iwe vya Mungu au vya Shetani, maana tayari yuko spiritually-oriented to spirituals.

*NB*
```Mtu anaweza kuwa alikuwa nabii wa kweli wa Mungu, kisha akaharibu njia zake, akakataliwa na BWANA, na bado vipawa vya kiroho vikaendelea kufanya kazi, sio kwa sababu ya his/her uprightness kwa Mungu, No! alikwisha kuwa spiritually-oriented to spirituals na hivyo macho yale-yale, masikio  yale-yale, ngozi ile-ile, ufahamu ule-ule bado unaweza ku-sense na kuopereti kule rohoni. Na wengine wakiharibu systems zinaBlock, anatambulishwa upya rohoni na nguvu za kinyume na Mungu ili kupoteza na kukengeusha wengi```

🧨 Kama ni Roho Mtakatifu amekutambulisha (orient) rohoni, Woga+Kushanga na hali ya Sintofahamu (state of uncertainty) itakuwa ni ya muda mfupi sana (will be temporary)... ATAKUSAIDIA NA KUKUKOMAZA

*NA ISHARA/KIASHIRIA KIKUBWA CHA KUONESHA ALIYEKUTAMBULISHA ROHONI NI ROHO MTAKATIFU, NI UHURU (LIBERTY/AUTONOMOUS FREEDOM) MAANA PALIPO NA ROHO WA BWANA PANA UHURU (2KOR 3:17), NA MWANA AKIWAWEKA HURU MTAKUWA HURU KWELI-KWELI (YOHANA 8:36, 32).*

🧨 Kiashiria kibubwa kwamba kuna roho za kigeni *strange spirits* zimeku-orient rohoni, ni Woga, Wasiwasi, Utisho, Kukosa amani, Sintofahamu *endless dilemma and confusion* yaani kuchanganyikiwa kunakuwa permanent. Labda kama umejitoa kwa moyo kuwa wakala au machawi etc haya hayataonekana maana utakuwa umevikwa roho ya ibilisi, itakayokufanya yote uone ya kawaida tu, hata ukiambiwa utafune nyama za watu.

*KIASHIRIA KIKUU CHA KWAMBA ROHO ZA KIGENI NDIZO ZIMEKUPA ORIENTATION KATIKA ROHO, HUTAKUWA HURU!*

``` Bila shaka mmekwisha wahi ona mtu sio mwamini (hajaokoka), lakini anaona vitu vya rohoni, na akisema vinatokea kweli. Bila shaka mmekwisha wahi ona kuna watu hawajisumbui hata na maombi na kukaa katika utakaso, ila wanaona katika roho, na wamejawa na vitu vya kiroho. Huenda ni dhaifu mno kiroho na mazoezi ya kiroho, wala havipigi vita vizuri vile vya imani, lakini mkikutana kwa sala yeye ndiye anatoa unabii wa kweli. LAKINI MKIMCHUNGUZA HUYU MTU KWA MAISHA YAKE, HAYUKO HURU, ANAWATABIRIA VITU VYA KWELI KWA FELLOWSHIP LAKINI MKIANGALIA MAISHA YAKE HAYANA MUNGU, ANAHITAJI KUSAIDIWA SANA KWA NJIA YA BWANA. HUYU MTU AMETAMBULISHWA ROHONI NA ROHO ZA KIGENI.```

_*🔥 Kama unaona upo kwa hali hii, taarifa utakazokuwa unazipata rohoni ni za kweli, lakini wewe mtoa taarifa hauna uhuru utokoa kwa Mwana wa Mungu*_

⚔ LORD'S WINNOWING FORK WILL BE SENT (PEPETO LA BWANA LITATUMWA, UKIFUNGUA MOYO WAKO, MUNGU ATAKUSAIDIA, TAFUTA MSAADA KWA WATUMISHI WA MUNGU).

⚔ SOME PEOPLE ARE TO BE DISCONNECTED FROM THESE STRANGE SPIRITS, YOU CANNOT PERFORM WELL WITH GUESTS INSIDE YOU.

⚔ HIZI ROHO ZITAFANYA UJIONE UPO NA MUNGU, THEN BAADA YA MUDA ZINAKUPANDIKIZIA VIFUNGO VIBAYA SANA, ILI USIJE UKA-EXCEL KWA LOLOTE, MAANA MWIVI HAJI ILA...........(Yohana 10:10).
_mwlproo_

*🌈 FAIDA ZA KUWA SPIRITUAL-CONSCIOUS PERSON (SUPERNATURAL LIVING)*
🧨 Roho yako itafufuliwa (rectified, rejuvenated)
Isaya 57:15, roho za wanadamu hazifi (mathayo 10:28 imezingatiwa, kuwa kuua mwili na roho ni maana tofauti), lakini roho zinawezwa kupigwa usingizi wa milele, zisiwe *SENSITIVE TO SPIRITUALS* 
Hivyo, mtu akiwa oriented to spirituals na Roho wa Kweli, ataweza kuishi maximized life to full capacity...Hatukuitwa kuishi maisha kikawaida tu.. Mtu wa rohoni kwa kuwa anamfuata Yesu aliye *master of  the nature* anaweza pindua chochote cha asili hata yale ambayo yako inherent au genetically-transferred toka kwa vizazi vya kwenu au systems za serikali. Mfano huenda kwenu wote wanajifungua operations na unaambiwa hiyo iko hivyo mpaka kwa shangazi zako, hiyo issue sio mara zote inakuwa ni uchawi but it has to do with nature tu, kwamba genetically, cervical paths za uzao wenu ziko namna hiyo... mtu wa rohoni anao uwezo kubadili lolote ambalo ni la nature akitaka na akiwa spiritual-oriented.

HAPA KUNA SHUHUDA NYINGI MNO ZA NAMNA WATU AMBAO SPIRITUALLY WAKO SENSITIVE, wameweza kuvuka maeneo mengi ambapo nature imesema NO! mimi hapa mwandishi ni shuhuda wa kwanza kwa hili.

🧨 Utakuwa chombo kinachofaa kutumiwa na Bwana kwa kazi yoyote mahali popote (You'll be fit for Kingdom's ministry)

🧨 Bwana atakuamini. Ni mambo mawili tofauti kumwamini Mungu na kuaminiwa na Mungu. Ukiisha kumwamini Mungu, panda viwango ufikie pa kuaminiwa na Mungu, ili kwamba Mungu akijua mahali wewe upo basi anaamini mambo hayataharibika... atajisemea moyoni, *_" Proo yuko pale"_* kwa namna ile-ile ya kujigamba kwa shetani, umemwona huyo Ayubu? 🤓... Sasa mtu hayuko spiritual-oriented anakuwa hajasimika mizizi yake mbali sana, dakika yoyote kufumba na kufumbua mara ashaanguka kwenye zinaa, yupo juu-juu tu kama mbegu zilizoanguka kwenye mwamba.. Mungu akusaidie unapoanza kuchukua hatua mpya ya kiroho, kwa Jina Kuu la Kristo Yesu... Amen,  nimeomba kwa ajili yako...

Mྂwྂlྂ Pྂrྂoྂoྂ
*+255762879363*

alltruth5ministries@gmail.com

Tuesday, June 18, 2019

JUMBE MUHIMU KWA WENYE APP YA MWL PROO

BWANA Yesu asifiwe sana

Mungu awabariki kwa kuchagua kuwa sehemu ya maono haya, hata kuipakua app iitwayo Mwl Proo, kule palystore. Bahati mbaya App hiyo haifanyi Synchronization vyema, hivyo kati ya masomo 160 niliyoyaweka, watu wanapata 25 tu.. Hivyo niwaombe kwa sasa fuatilia masomo yangu kwa njia ya Mwl Proo Tv 📺  ya Youtube, All Truth Blog, Whatsapp Groups, Facebook etc Kwa maswali zaidi wasiliana nami kwa +255762879363

Wednesday, April 24, 2019

UNDIVIDED ATTENTION

*KUITULIZA MIOYO MBELE ZA BWANA*
_(Undivided Attention Before The LORD)_

*M͟͟w͟͟l͟͟ P͟͟r͟͟o͟͟o͟͟*
_0762879363_

Salamu nyingi kwa Jina la Bwana na Mwokozi Yesu. Ndugu msomaji imempendeza Mungu kwa majira haya ya siku za mwisho kukuandikia haya. *_Kwa kuwa Bwana hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira;_*
(1 Nyakati 28:9 ). Mapema sana mwaka jana (2018), nikiwa natoka kanisani kwenye maombi ya jioni, moyoni mwangu kukawa na namna fulani ya kusemeshwa, kuwa watu wengi huwa hawaombi. Nikaanza kuwanza huwa hawaombi kwa namna gani?. Hapo ndipo Mungu akanikumbusha andiko la msingi nilikuwa nalijua tayari kitambo ila sio kwa ufunuo huu.

*_"Katika hili tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, nasi tutaituliza mioyo yetu mbele zake,"_*
(1 Yohana 3:19 SUV)

*This is how we know that we belong to the truth and how we set our hearts at rest in his presence (Our hearts will be still in His presence)* 1 John 3:19 NIV

Mjadala huu haukuisha ndani yangu mpaka nikapata somo. Na nikaelewa kuwa tuna Wakristo wengi nyakati hizi za mwisho, hawaombi wala hawaabudu maana mioyo yao haijatulizwa mbele za BWANA (set hearts at rest in His presence/undivided attention when worshipping/praying). Mwanadamu sio roho peke yake, bali ni roho, nafsi na mwili. Mtu anaweza kuomba  kwa akili zilizomo ndani ya nafsi au akaomba kwa mwili (kinywa 👄👅) kwa sababu the spirit-man aliunganishwa na mwili wa nje ili kumwezesha mtu kuomba hasa wakati wa kunena kwa lugha zingine, lakini haya yanaweza yakaendelea wakati moyo (nafsi) haiko kwa ushirika na maombi au maabudu hayo.

Ni muhimu kukumbuka Mungu anautaka moyo/nafsi (mawazo na fikra zake), anasema katika Mithali 23:26, *'Mwanangu nipe moyo wako'*. Jambo la ajabu sana mtu anaweza akaomba saa moja au zaidi akiwa hajautuliza moyo wake mbele za Mungu (divided attention), hii inapelekea watu kutofika vilindini, wanachodhani wamepokea kwa Bwana ni *0.0001%* ya kilichokusudiwa na Mungu. Ugonjwa huu unaweza kumkuta mkristo yeyote (clergy/layman). Siku najifunza jambo hili nikagundua mtu anaweza kuanza maombi lakini mawazo ya moyo wake yamerudi ofisini anapanga mikakati ya kazi mwanzo wa maombi mpaka mwisho, mwanamke anaweza kuanza maombi lakini akili na mawazo ya moyo wake yapo saluni, anashiriki kikao na mjadala wa saluni mwanzo mpaka mwisho kwa mawazo ya moyo tu, mtu ni dereva anaomba au anaabudu huku akipanga apite njia ipi atumie spidi ipi. akwepe vipi traffic polices, hivyo mtaona mdomoni anafuliza kuomba (spontaneously) kumbe hayuko hata. Kuna watumishi wachache kwa sababu ya ratiba nyingi za kuhudumu kwa kuhubiri na kufundisha basi wamefanikiwa kidogo, muda anaomba akilini mwake anahubiri/anapanga points za kufundisha/anafanya huduma kwa fikra za nafsini. Hata wao hawajafanikiwa kuituliza mioyo mbele za Mungu. Kuomba kwa roho na kuomba kwa akili vyote vinapaswa kuwa sambamba ingawa ratios ndizo zitakuwa tofauti, kuomba kwa roho kuwe na nafasi kubwa zaidi ya 90% ya maombi yote.

✍🏾Si vibaya kuomba kwa kutembea-tembea, haswa ukigundua kuna dalili ya kuwindwa na usingizi nawe una targets zako za kutumia saa kadhaa kwa kuomba. Lakini asilimia kubwa ya wanaoomba kwa njia hii pekee ukabiliwa na ugonjwa sugu wa kuomba kwa mwili (👅👄) au kwa lugha za roho lakini mawazo ya nafsi yakiwa kwingine, yaani anakuwa na *divided attention*, anaomba anatembea akiwa amefungua macho ili kukwepa kujigongeza mahali (kumbuka hakuna andiko linaloelekeza ufunike macho muda unaomba, ila ni katika kutafuta moyo usihame, sasa hakuna maana ya kufnika macho kama moyo haupo), huku muda huo itampasa aone mambo mageni, ataona yanayoendelea nje na kutwaa usikivu/umakini (attention ya kiroho), atake asitake ataanza kujadili mambo kwa moyo wake huku kinywa kikiendelea kuomba, lakini mawazo ya moyo, ambayo ndio uhitaji mkubwa wa Mungu, yatahamishwa katika mambo mengine, anaweza kuanza kujadili juu mahudhurio hafifu kanisani, mapambo ambayo hayako sawa kanisani n.k n.k. Ndugu msomaji, Mungu atusaidie sana kwa sababu hii case iko serious, ndio maana watu wanatoka mbele za Mungu baada ya kuabudu au kuomba wakiwa hawana kitu kipya, hawana ufunuo mpya, wako tu na vitu vya kawaida maana hawakufika vilindini. Wengi wanaofundisha kwenye nyumba za ibada au hata mitandaoni, wanayoyafundisha mengi ni Basic Christian Doctrines, sio mambo yaliyotokana na ufunuo mkubwa baada ya kutuliza moyo kwa Bwana. Ni wachache sana wanaCapture hiyo frequency  na kutoka na ufunuo mkubwa wa kiMungu, hata akifundisha common topics kama za maombi, utakatifu, uaminifu, siku za mwisho, utoaji, imani n.k haitakuwa kama basic doctrine bali itabeba ufunuo mkubwa wa kiMungu wa kuwavusha watu kulingana majira waliyo nayo. Nyakati hizi si ajabu mtu karespond meseji ya WhatsApp 👩🏽‍💻 📱📲👨🏽‍💻 akiwa hajanyamaza kuomba mdomoni 👄👅. Si ajabu mtu akaendelea kuhudumu madhabhuni akiwa ame-Go Live na anataka comments za fans zote azichungulie........ Masumbufu ya maisha yamejaza mambo mengi kwenye mioyo na kuifanya mioyo kutoweza kuwa attentive au kutulia katika uwepo wa Mungu. (Nitayaongea hayo kwa kina katika somo lijalo liitwalo *"MAPITO YA ZAMANI"*). Kuna watu wanatumika kwa karama za ufunuo, wanaweza kutuliza mioyo kwa sehemu kidogo sana kwa sababu ya nature ya hizi karama, hivyo anayaona mambo ya rohoni kwa haraka sana, ila kukosekana kwa *undivided attention* wanayoyaona hawayaelewi kwa wakati ili kusaidia, sababu kubwa ni hii ya kutoweza kuituliza mioyo mbele zake, na kukosa ufahamu wa kutosha (roho ya ufahamu ina-operate kwa kiwango cha chini sana), yote ni matokeo ya kutoituliza mioyo mbele za BWANA ambaye ni Mungu wa maarifa.

(Isaya 42 )
------------
*19 Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? Au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani? Naam, kipofu kama mtumishi wa Bwana?*
*20 Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake ya wazi, lakini hasikii.*

👆🏽👆🏽👆🏽
Nilikuwa mahali fulani muda wa maombezi mhubiri akaoneshwa mwezi 🌘 kwa macho ya kiroho.... alitumia muda mwingi sana kuelewa kuwa Roho Mtakatifu anamwelekeza ahudumia wadada wenye disorders za Menstrual Periods, kumbuka lugha za roho huja zikiwa *encoded* mara nyingi zaidi, ili kung'amua kwa wepesi alama iliyotumika ina maana gani ni mpaka kuwe na undivided attention na ufahamu wa rohoni wa kutosha.

Mungu hayuko mbali, wala uwepo haujaadimika kama watu wanavyofikiri, ila watu wanakosa mguso kwa kukosa ujuzi wa kuutuliza moyo mbele za Bwana. Ni watu wachache sana wamejizoeza kukamata connection kwa kutuliza mioyo (full attention). Muda unaimba nyimbo za kuabudu kanisani, muda unaomba ukijizoeza kuwa *nia isiyogawanyika/undivided attention* you're likely to get connected na kufanya maombi na maabudu yako kuwa valid.

Usimsogelee Mungu kwa ibada na maombi ukiwa na haraka zako, utapata shida kushindana na mawazo ya moyo na ule utulivu wa kutuliza moyo kwa Mungu (Mhuburi 8:3a). Neno linasema usifanye haraka kuondoka mbele ya mfalme (Yesu ni mfalme wetu, don't  be hasty, don't be in a hurry to leave His presence, but set yourself at rest in His presence). Kuna siku tulikuwa mahali tukifanya ibada ya nyumbani, wakasema jamani tufanye haraka haraka ili tuiwahi *tamthilia* fulani kwenye Televisheni, niliwaambia bora hata tusifanye ibada hiyo...... Mungu anautaka moyo, uliotulizwa mbele zake, ila kama unawaza kuiharakisha ibada ili uwahi vipindi vya Tv, kuwahi mchuano wa mpira timu yako pendwa sana inacheza, utampunja Mungu sana kwa kumweka kwenye foleni ya mambo ya kuyatekeleza.... Mungu anapaswa kuwa Mungu tu, na mioyoni mwetu kumtakasa Kristo (setting Him apart), kumpa special attention muda umeamua kusogea mbele zake.

*HATUA ZA MUHIMU KUCHUKUA ILI KUJIZOEZA KUTULIZA MOYO KWA BWANA*

1. Ni kufanya maombi mfululizo kumwomba BWANA kwa habari ya neno hili, kwamba Mungu nisaidie na unifundishe.

2. Anza kufanya mazoezi, ukiwa kwenye maombi kila unapogundua mawazo yanahamia kwingine unayarudisha na kuConcentrate kwenye maombi yako tu.... usiruhusu dakika nzima ya kuomba moyo unajadili kikao chake. Unaweza kuwa kuna jambo limekukamata moyo, mfano una tishio la kufukuzwa kazi, au nasomo, au kufukuzwa kwenye nyumba uliyopanga, mambo haya yakajirudisha kwenye maombi au muda wa maabudu, badala ya kushiriki vikao vya usuluhishi na mijadala kwa fikra/mawazo ya moyo, unaweza kuamua kujifunza kutupa chini kila fikra ijiinuayo, ili kupata utulivu usioingiliwa kabisa *uninterrupted mind for worship*, magumu yapo tu, ila amua kumpa attention Yeye aliye mkubwa kuliko hali mbaya zote na matatizo yote..... Ukifanikiwa hapo, ni rahisi sana kila unapotoka kwenye maombi au ibada za namna nyingine ukawa na majibu ya mambo yako mengi mno. Anza sasa kufanya hili zoezi ingia kwenye maombi ya saa nzima ukijitahidi kuibakiza attention yote kwenye kuomba tu...

3. Badilisha styles za maombi na ibada zisizo-support utulivu wa mawazo ya moyo... Kama ukigundua maombi mengi unayofanya ya jumla-jumla kanisani hayakupi kuutuliza moyo, basi hakikisha pamoja na hayo, uwe na ratiba zako binafsi za mahali pasipo na watu (solitary place), na ujizoeze kuomba au kumwabudu Mungu kwa moyo wote bila kugawanyika kimawazo (HILI LINAWEZEKANA). Kuna makanisa mengine hayatoi muda wa watu kuconcentrate mbele za BWANA, dakika za watu kuimimina mioyo kwa Mungu ni kidogo sana (1Sam 1:15), muda wote wa ibada ni matukio-tukio tu, wengi wanaondoka hawaja-enjoi ule utamu wa kumsogelea Mungu, vitu vinakimbizwa kimbizwa tu, mara Ooooh Praise Team imbeni kwa ufupi sana leo tuna mambo mengi mno, na ukute ni swala la mnada tu kanisani, lina-rob nafasi ya watu kumsogelea Mungu na kujipatia nafasi kwenye vilindi vya moyo wa Mungu.

Mimi ili kupata utulivu ninaoutaka kuna muda natafuta mazingira mazuri zaidi... Niko chuoni kwa sasa, hakuna mahali pa kuomba kwa kutulia sana kiasi cha moyo kutulizwa mbele za Mungu, nikisema niombee hostel dakika yoyote Room-mate atabisha hodi na kunitoa kwenye concentration yangu..... Sijayaruhusu mazingira yaniibie nafasi yangu, na hivyo nilitafuta cha kufanya, nikagundua kwenye viwanja vya michezo, usiku kuna kuwa na mazingira mazuri, yasiyoingiliwa na chochote, hakuna anayepita wala chochote kile cha kuweza kuniondoa mawazo...Hivyo nilipopata waza hilo basi najitahidi saa nane usiku niwe kwenye viwanja vya michezo, naomba kwa sauti ninayoitaka, muda wa kutosha, utulivu mkubwa wa kimwili na kiroho and so my heart remains still before God.

HILI NDILO NENO LA BWANA KWAKO.

Mwl Proo
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

Tuesday, February 19, 2019

WAHUDUMU WA AGANO JIPYA

*WAHUDUMU WA AGANO JIPYA:*

_*Agano La Kale Sio Vitabu 39, Na Agano Jipya Sio Vitabu Na Barua 27*_

*ʍաӀ Թɾօօ*
*+255762879363*

Mbarikiwe kwa Jina la BWANA (Yesu). Kuna jambo ambalo Mungu alitia moyoni mwangu nilifundishe, maana kumekuwa na kuchanganya maelezo sana katika hili. Agano la Kale ni lipi na Agano Jipya ni lipi, Je! usomapo maelezo kama ya Waebrania sura ya 8, huyu mwandishi anaonekana kulishambulia sana Agano la Kale kwa kiasi cha kulifananisha na kitu chakavu (kama dekio 👉🏾tambara bovu) pale asemapo, kwa kuliita hili Agano Jipya, amelifanya la kwanza kuwa kuukuu (the first covenant is made obsolete) 👉🏾 (Ebrania 8:13). Je! Haya mashambulizi makali anavishambulia vitabu 39 vile vinavyoitwa Agano la Kale?. Karibu tujifunze maandiko kwa pamoja.

*🌡 Tunayo maagano mawili (which are juxtaposed in Hebrews)*
I. AGANO LA SINAI
2. AGANO LA KALVARI

(Wagalatia 4 )
------------
*24 Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri.*
*25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto.*
*26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi.*

🇮🇱 Wako watu ambao wakisoma nyaraka za Paulo pamoja na Waebrania, wakaona mistari mingi yenye kuonesha Agano Jipya ni bora kuzidi la kale (Ebr 7:22), huenda wakawa wanawaza kuweka katika contrast labda kitabu cha nabii Isaya na Injili ya Yesu kama ilivyoandikwa na Mathayo, kisha wakaanza kulinganisha ubora wa ujumbe. Kinachotajwa kuwa bora sio vitabu 39 ukivilinganisha 27 vya Agano Jipya. Mungu alipokuwa akiahidi kwa vinywa vya manabii, kwamba nitafanya agano jipya (Yer 31:31-40) hakuwa anazungumzia hizo barua za Paulo alizowaandikia wakristo wa Uyunani, Uturuki, Roma na watu binafsi. Bali agano la kwanza (la kale) ni lile la Sinai kwa mkono wa Musa, na agano jipya (la pili) ni lile la Kalvaria (Latin) yaani Kranion (Greek) ambapo kiaramu huitwa (Golgotha) kieneo kilichopo nje tu ya kuta za Yerusalemu (Mathayo 27:33, Luka 23:33). So stop kabisa kufikiri kwamba hiki ambacho kimefanywa kuwa kikuukuu na ki karibu na kutoweka labda kitabu kama cha Zaburi, Daniel, Ezekiel etc, hapana kabisa.

Tusome hapa
👇🏽

(2 Wakorintho 3 )
------------
*14 ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo _Agano la Kale_, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo;*
*15 ila hata leo, _torati ya Musa isomwapo,_ utaji huikalia mioyo yao.*

🇮🇱 Katika italics tunakutana na jina *Agano la Kale, na torati ya Musa*, Paulo alitaja Agano la Kale akiilenga torati ya Musa kwa hapa, na aliitaja akimaanisha maandishi na sio lile agano lenyewe. Ipo hivi linapofanywa agano kunakuwa na masharti ya agano (terms and conditions), hivyo torati ya Musa zilikuwa ni terms and conditons attached to the Sinaic Covenant, na vitabu vingine vyote vimewekwa kwenye mkusanyiko ulioitwa *Agano La Kale* kwa sababu wote walioandika walitumika chini ya agano  hilo la Sinai. Kwa hiyo kitabu kama Zaburi kinakuwa katika Agano la Kale kwa sababu kiliandikwa na wahudumu waliohudumu chini ya agano la huduma ya mauti, huduma ya adhabu  na sio huduma ya Roho (2 Korintho 3:7, 8, 9).  Na pia kama kitabu cha Dr. Luka kiitwacho matendo ya mitume, au nyaraka za Paulo au Petro zikiitwa Agano Jipya, sio vitabu hivyo ndivyo agano lenyewe bali kwa kuwa wahudumu wake wameviandika chini ya agano lililo bora la Kalvari basi vinakuwa  ni vya Agano Jipya kwa sababu hiyo, I mean mafundisho ya Kristo na mitume wake ndio *terms and conditions* za Agano la Kalvari (Jipya).

*🌡  Agano jipya lilianzia Kalvari*

(Waebrania 9 )
------------
*15 Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.*
*16 Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya.*
*17 Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya.*
*18 Kwa hiyo hata lile la kwanza halikuanzwa pasipo damu.*
*19 Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote,*
*20 akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu.*

Wakati wa Agano la Sinai, kila sheria (attached terms and conditions) ilipotajwa ilisindikizwa na damu. Na Yesu naye alilifanya Agano jipya kwa damu yake mwenyewe inenayo mema (Ebr 12:24)

*"kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi."*
(Mathayo 26:28 )

Hakikisha unapata somo langu lenye kichwa cha ujumbe *Maagano yanaweza fanywa upya, kufifishwa, kuondolewa kabisa*. Niwaulize swali sasa nini kinachokuja akili mwako unaposoma andiko kama (Warumi 10:4), kwamba *Kristo ni mwisho wa sheria*, Je! kama Sheria ilisema usishuhudie uongo, kwamba you're now free to lie or testify lies? La Hasha!, hapa ndipo tumepata utata na mrafaruku wa hoja. Nini hasa ambacho kinatajwa kwamba Kristo ni mwisho wa sheria, na kwamba sheria ilikuwa kiongozi tu cha kutuleta kwa Kristo (Galatia 3:23-24). Naomba kurudia hili, torati ya Musa ilikuwa (attached string) vigezo na masharti ya kulisindikiza Agano la Sinai, kama ambavyo fundisho la Kristo na mitume wake ndiyo *attached string* vigezo na masharti ya kulisindikiza Agano jipya la Kalvari

*MOYO WA SOMO*

*🌡 SISI WAAMINI KATIKA KRISTO, TULIOAMINI FIDIA YA MUNGU YA MAUTI YA KRISTO, TUMEFANYWA KUWA WAHUDUMU WA AGANO JIPYA (MINISTERS OF THE NEW COVENANT)*

*"Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa _WAHUDUMU Wa AGANO JIPYA;_ si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha."*
(2 Wakorintho 3:6)

👆🏾👆🏾👆🏾 NAOMBA KUREKEBISHA HOJA YA WATU AMBAO UKIWASOMEA ANDIKO ILI KUWAPA MAELEKEZO, WANATUMIA ANDIKO HILI KAMA DEFENSE ETI ANDIKO HUUA. MAANDIKO MATAKATIFU NI NENO LA MUNGU KATIKA MAANDISHI (WRITTEN WORD OF GOD), WALA HAYAUI, KICHOTAJWA HAPA KAMA ANDIKO KATIKA GREEK TEXT NI *γράμματος* yaani  *"grammatos"* ambapo Rabbinical interpretation yake huiita *Chumrah* kiebrania yenye maana ya Letter of law(Mosaic Law) or simply Chumrah refers to *Strict adherence to Torah*, hivyo tusikimbie maonyo ya Biblia kwa kusema maandiko huua, sicho kilichokusudiwa hapo, wala usi-intertain mambo ya kusema kwamba maandiko sio neno la Mungu, eti mpaka livuviwe, haya unayoyaona kwa Bible are God-breathed words.

Tuendelee......

✝ Jamii ya waaminio, si waaminio sio wafuasi wa Agano la Sinai, baada ya Kristo kuja, kusimama na Agano lile la Sinai ni matokeo ya kutoelewa kabisa kazi ya msalaba. Agano Jipya ni Jipya, Sio marudio, sio mapitio, sio maboresho ya la kwanza (It's not the restatement of the old testament), ni jipya kwa maana ya jipya. Mjumbe wa agano la kwanza (Musa) Yohana 1:16-17, aliwaambia waisrael kuwa Mungu atawainulia nabii (Yesu) you will have to listen to Him, hivi ninawapa viwaongoze hata atakapokuja, neema na kweli  vimekuja kwa njia ya Yesu.

✝ Tusomapo vitabu vya Agano la Kale, sharti tusome in the light of the New Covenant, tukijua kuwa Terms and Conditions za Agano la Sinai ni kivuli tu cha Agano lililo bora la Kalvari (Ebrania 10:1, Kolosai 2:17). Ni hatari kama waamini watashindwa kujua kuwa kitu halisi ni Kristo wakashika kivuli, wakaacha mafundisho ya Kristo na mitume wake wakang'ang'ana vigezo na masharti ya Sinai, watapotea sana kwa sababu ya kutofahamu maandiko wala uweza Mungu.

✝ Vigezo na masharti ya Agano la Sinai havina viwango kuwaongoza waamini katika Kristo (waliozaliwa upya). Agano la kwanza na masharti yake (Sheria, Amri na Hukumu zake), viliamriwa kwa watu walioenenda kimwili kabisa, maana ilikuwa haijaja bado ile ahadi. Hapo ndipo naona ndugu zetu kama wasabato wanaposhindwa kuelewa kuhusu haya maagano. Agano jipya la Kristo limepandishwa viwango maana wahusika wake ni watu ambao wamezaliwa na Mungu kwa upya kwa njia ya Roho, hivyo hawawezi kuwa na makatazo sawa na watu wa agano la kwanza. Kuna mtu nilipomwambia hatuko chini ya Sheria, akasema hivyo wewe upo huru hata kuua, na kuzini eee?? 😁 After the Beatitudes Yesu akaanza kuonesha namna jamii mpya itakayozaliwa kwa damu ya Kalvari itapaswa kuwa. Akaanza kuwahoji kwamba mmesikia imenenwa *"Usiue"* lakini mimi nawajuza kuwa standard ya Agano la Kalvari ni hii *"Ukimchukia tu ndugu yako umekwishaua"*, mmesikia imenenwa *"usizini"* mimi nawaambia Ukimwangalia mwanamke lustfully, *Umekwisha zini naye moyoni mwako* (Mathayo 5:21ff) HIZI NDIZO STANDARDS  ZA WAHUDUMU WA AGANO JIPYA, kujifungia kwenye sheria, amri na hukumu za Musa za agano la sinai (la kale), ni kujipeleka mahali ambako Yesu hakutupeleka, ni kuamua kuishi chini ya viwango. Waliozalwa upya hawakatazwi wasiue maana sio tu hawawezi kuua bali hawawezi kuwaza kuua. Musa akiwa anaaddress masharti ya agano la sinai, aka-establish sheria ya malipizi (restitution), kwamba mtu akiiba ng'ombe labda mmoja atapaswa kurudisha siju watano, waamini waliozaliwa upya, na kujazwa Roho wa Kristo, hawapaswi kuwekewa sheria za watu wa mwilini kwamba ukiiba mmoja ukipatikana utalipa mara tano, sababu ni hii kwamba baada ya kuzaliwa upya na kufanywa kuwa wahudumu wa agano jipya, hata hilo wazo la kuiba huyo ng'ombe mmoja hatuwezi kuwa nalo, hata kama tutakuta kuna mbuzi 🐐kapotea, hatuna wazo la kumwiba na hiyo ndiyo tafsiri ya kusema hatupo chini ya sheria (Galatia 5:18, 22). Kwamba hatuwezi kukatazwa kuzini wakati standard yetu ya Agano lililo bora inasema uasherati usitajwe kabisa (Efes 5:3). And as the matter of fact mnapozidi kuzama sana kwenye Mosaic Law ndivyo mnavyozidi kutengwa na Kristo (Gal 5:4).

✝ Nimefanya studies juu ya kitu kiitwacho kiebrania *Korbanot* mifumo ya dhabihu na matoleo ya kiyahudi, nilipofahamu kwa mtazamo sahihi wa kiyahudi ndipo nikagundua haya mambo tumeya-copy kwenye ukristo kimakosa na kwa kukosa ufahamu sahihi, hata kama yana mvuto masikioni kiasi gani, mikazo yote ya malimbuko, zaka za fungu la kumi etc *I DARE TO SAY THEY ARE ALL IRRELEVANT TO CHRISTIAN DOCTRINE AND CONTEXT*, ila yalipokelewa kimakosa na wanaopaswa kufundisha ukweli huu hawawezi kabisa. Kuna mchungaji aliniambia Mwl Proo ukiwa mchungaji huwezi kufundisha kuwa mafundisho kama ya malimbuko na zaka sio ya kikristo, nami sishangai maana tuna wakristo wanatoa zaka million 20 lakini sadaka za hiari na matoleo mengine wanatoa elfu 2 elfu 5, hapo ni wazi hakuna namna ya kufix hilo.. Ila fundisho lilipokelewa likiwa na makosa tayari, Ukristo upo juu kuliko hizo terms na conditions za Taurat ya Musa, kuweka hako kakiwango ka 10% ni utoto na udumavu kwa viwango vya Agano la Kalvari, maana waliowekewa 10% ni kwa sababu ya ugumu wa mioyo tu, Sisi hatupaswi kuwa na mioyo  migumu kamwe, tukiisha mpa Mungu mioyo yetu tunakuwa tayari kumtolea Mungu chochote sio kwa kipimo (2Cor 9:7), forget about Abraham ambaye sio tu hakuwahi kutoa zaka ya fungu la kumi, bali hakukuwepo hata mahali pa kuipeleka hiyo zaka ya fungu la kumi, incidence ya kukutana na Melkizedeki haikuwahi kujirudia tena, na wala katika mapato  yake hakuwa kutoa zaka kabisa achana na zile nyara za vita ambazo hazikuwa zake. Amani unayoisikia haiwi amani ya Kristo bali na amani ya fundisho lililotangulia (pamoja na makosa yake), ni sawa tu na kumtaabisha mprotestanti kwamba kubatiza vitoto vichanga au kwa kununyiza maji ya kibakuli sio sawa, atakaza kujitetea huku akishindwa kung'amua kuwa ni fundisho ambalo kimakosa lilivushwa (halikuchujwa) toka Kanisa Katoliki,  ni kwa namna hiyohiyo tu, kinakuwa kitu kigeni, lakini hiyo hainizuii kuandika ukweli wa Biblia ni upi, na kipi tunakifanya kimakosa. Haka katabia ketu ka kuwa machotara tunadonyoa na kunyofoa kasheria kamoja kati ya zile 613 za Taurati, hakafai, hakana maana kabisa. Yaani unabandua sheria kuhusu riba unaishika, halafu ya kutopanda mbegu mbili katika shamba moja unaivunja, unashika siku ya pumziko  (sabato) ila unavaa nguo yenye vitambaa vya aina mbili tofauti ambayo ni dhambi kwa mujibu wa terms za Agano la Sinai. Sheria ya Musa ina dai moja kubwa ukishika uzishike zote, ukivunja moja umevunja zote, bila kubagua sijui ceremonial laws au moral laws, ukitaka kujichomoa kwa hilo kongwa la utumwa ni kwa kuamua kuwa mhudumu wa Agano Jipya, hilo tu. Nisiongelee hilo sana maana nimechambua kwa kina kwenye somo la *UKWELI KUHUSU ZAKA YA FUNGU LA 10* ukilihitaji naweza kukurushia. Hoja yangu ya msingi ni kwamba sisi ni wahudumu wa Agano Jipya lililo bora, tunatarajiwa kuishi sio kwa ufunuo mdogo wa zamani au mafundisho ya awali ya ulimwengu, bali kwa njia ya Kristo, Mungu ameifunua siri ambayo ilisitirika yangu enzi na enzi.

*TUKUTANE KWENYE SOMO LIJALO*

*Mwl Proo*
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com