Friday, September 23, 2016

FAN INTO FLAME

*```FANNING INTO FLAME```*

*```KUCHOCHEA```*

_Na Mwl Proo_
0762879363

Bwana Yesu apewe sifa!
πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯
Mungu wetu amejitaja kama moto ulao (Ebra 12:29), Amesema atakuwa ukuta wa moto kutuzunguka (Zek 2:5), Neno lake kalifananisha na moto (Yer 23:29), Kisha akasema anatufanya sisi watumishi wake kuwa miali ya moto (Ebra 1:7). Majini katika Quran yalijieleza kuwa yalitaka kwenda mbinguni lakini yakakutana na miali ya moto (Q 72:8), Katika yote hayo napata hitimisho kuwa moto ni bidhaa adimu ktk ule ulimwengu mwingine, ingawa moto huu wa huku mwilini hauna kazi kule ktk ulimwengu wa roho. Hata kama tukichukua tunguri za uchawi tukazipiga motoπŸ”₯, hakuna jini linaungua pale, tunaondoa tu kile chombo kinacholeta muunganiko.

SASA SISI NASI, TUKIISHA OKOLEWA TUNAFANYWA MOTO, NA SHARTI HUO MOTO UCHOCHEWE. MOTO UZIPOCHOCHEWA UNAZIMA

NA NDIO MAANA BIBLIA INASEMA,
1Thesalonike 5 : 19
*_Msimzimishe Roho; (Do not quench the Spirit)_*πŸ”₯
Mioyo yetu na maisha yetu ya kiroho, ndiyo madhabahu halisi kwa sasa. Makuhani walipewa maelekezo kuwa moto wa mashabahuni πŸ”₯, haupaswi kuzimika, ni full kusongeza kuni daima" usuzimike, ikiwakilisha kuwa maisha yetu ya kiroho, hayapaswi kuwa na ubaridi/kuzimika

Walawi 6 : 13
*_Moto utatunzwa uwake juu ya madhabahu daima; usizimike._*

Paulo mtume anamwelekeza Mchungaji Timotheo, achochee πŸ”₯karama 

2 Timotheo 1 : 6
_*Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu.*_

MAISHA YA KIROHO ILI YAWE MOTO WAKATI WOTE, LAZIMA YACHOCHEWE. NAMNA NZURI YA KUJICHOCHEA KIROHO NI KWA KUFANYA MAZOEZI YA KIROHO (SPIRITUAL EXERCISE). πŸ‹πŸΎ

1 Timotheo 4 : 7
*_Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa._*

NENO JIZOEZE LINAZUNGUMZIA EXERCISE/TRAINING. MAZOEZI YA KIROHO NI DHAHIRI NDIO HAYA.  UKIJUA HUDUMA NA KARAMA ZAKO UNAZIFANYA KWA JUHUDI, MAOMBI NA KUFUNGA, KUJIZOEZA KUOMBA KWA KUNENA KWA LUGHA KWA MUDA MREFU, KUJIFUNZA NENO LA MUNGU KUTOKA KATIKA MAANDIKO, KUTUMIA MUDA WAKO KUWASHUHUDIA WENGINE HABARI ZA IMANI YAKO, KUJIHUDHURISHA KWA BWANA KWA IBADA MARA KWA MARA (DHABIHU YA MUDA NA MWILI WAKO KUUTOA SADAKA), KUHUDHURIA SEMINA ZA NENO LA MUNGU, MAKONGAMANO YA KIROHO NA MAKAMBI YA HUDUMA. MAMBO HAYA NA MENGINE, YANAPASWA KUFANYIKA REGULARLY KUEPUKA KUWA NA NGUVU ZA MWILI,  LAKINI KIROHO UKAWA FLABBY (MANYAMA UZEMBE). MUNGU ALIKUTAZAMIA UTAENDELEA KUDUMU KATIKA KAZI YA KUUCHOCHEA ULE MOTO ALIOUWASHA KATIKA MAISHA YAKO YA KIROHO. KILA MTU AKIPOA HATA YEYE MWENYEWE ANAJIJUA NA WATU WENGINE WATAJUA. HIVI UNAJUA UKIWA MOTO, UNAWEZA KUSEMA, *"HALELUYA!!"* KAMA MAPEPO HAYATALIPUKA, KILA MTU WA ROHONI ATASIKIA ILE HALELUYA ULIYOISEMA INA MGUSO WA KIMUNGU, YAANI IMEAMBATANA NA MAFUTA MABICHI (ZAB 92:10) YA ROHO MTAKATIFU. LAKINI UKIPOA UNAWEZA KUTUSUMBUA NA SALAMU YA BWANA YESU ASIFIWE MARA KUMI KUMI, NA BADO HATUHISI MGUSO. WAKRISTO WENGI WA LEO, KWA KISINGIZIO CHA UBIZE WA MAISHA, WAMERUHUSU MOTO KUZIMA KABISA KWA KUWA MTU ANAKAA MIEZI SITA HAJAFANYA MAZOEZI YA KIROHO, ILI KUCHOCHEA MOTO. DANIEL ALIKATAA KUKAA SIKU 30 BILABILA, AKAAMUA KUCHOCHEA MOTO WA MADHABAHU YA MOYO WAKE, MARA TATU KWA SIKU.
WEWE MLOKOLE MWENYE EXCUSE KATIKA KUUCHOCHEA MOTO, MOTO WA MUNGU NDANI YAKO UTAZIMA, UKIISHA ZIMA UTAKUWA NA MAISHA YA WOKOVU AMBAYO YAKO *_CUSTOMIZED_*, YAANI YAMEJAA VITU VINGI SIO VYA KIMUNGU, MAANA HUJA-UPDATE WINDOW. MOTO HUU UKIPOA MTU HATA ILE FILTER YA NAFSI INAKUWA *_DULL_* YAANI BUTI, DUNIA INAMSOMBA TUU, KUKIZUKA STYLE YA KIDUNIA HANA NGUVU ZA KUCHUJA (FILTERING), KUNA MPENDWA NILIMSIKIA ANATAMKA NENO *_KUDADADEKI_* KATIKA KUMHOJI MAANA YAKE NINI, HAJUI, ILA KALITOA HUKO DUNIANI, SASA SIHITAJI KUJUA MAANA YAKE, ILA WEPESI KUNASWA NA KILA MSEMO, MPAKA MATUSI HUWA NI KIASHIRIA CHA MOTO KUZIMA.

AMBAO WANADUMU MUDA MREFU NA MOTO USIOCHOCHEWA, UKAZIMA, NDIPO UNAKUTA MTU ALISHAOKOKA, ILA MUDA WA MAOMBEZI NAYE ANAANGUSHWA CHINI CHALI, ATI ANA PEPOπŸ‘Ή, PEPO WACHAFU WANA TABIA YA KUJA KUTEST. YAKIKUTA MOTO WA MADHABAHU UMEZIMA YANAKUINGIA KABISA. TENA MOTO UKIZIMA NDANI YAKO, UTAJIGUNDUA KWA WEPESI SANA, TABIA AMBAYO ULIKWIAHA KUISHINDA UNAITENDA KWA UPYA KWA MWENDOKASI HATARI.

WENGI KATI YA WALIONGUKA KATIKA UZINZI/UASHERATI, HAIKUWA BAHATI MBAYA. MOTO ULIZIMA, WAKENDELEA KUJIKAZA, JARIBU (TEMPTATION) LILIPOKUJA HALIKUMKUTA NA NGUVU. NA WEWW MSOMAJI UNAJIJUA WAZI, KUNA WAKATI UNAKUWA UMEPOA, HADI UNAJIGUNDUA KUWA KWA HALI, IKITOKEA GHAFLA NIPO NA BINTI AU KIJANA WA KIUME, SINA NGUVU YA KUSHINDA KUFANYA UZINZI (HIYO MTU NAFSINI MWAKE ANAKUWA ANAJUA). SASA KUJINASUA JITENGE NA MAZINGIRA YA MAANGUKO *_UNTIL YOU REACTIVATE!_* USIJIPELEKE KWENYE MAZINGIRA HATARISHI WAKATI ULE MOTO UMEZIMA, HUTASALIMIKA

ISIPOKUWA. UKIGUNDUA MOTO UMEZIMA FANYA MPANGO WA KUCHOCHEA, KAMA KUNA SEMINA IHUDHIRIE KWA BIDII, MPAKA UNASURIWE SEHEMU ULIPOKWAMA, UWEZE KUANZA KUCHOCHEA UPYA. MOTO UNAWEZA UKAZIMA UKAKUTA UNAWEKA ALARM CLOCK⏰ ILI UAMKE KUOMBA, KUAMKA UNAAMKA NA KUOMBA HAUOMBI. WEWE MWENYEWE ULIFUNGA MPAKA SIKU 7, LAKINI SASA SIKU MOJA YA KUFUNGA UNAKUTA NI KAMA MTIHANI!?

UKIYAONA HAYO, USISUBIRI ANGUKO KAMILI, BALI FANYA FASTA UUCHOCHEE MOTO

Mwl Proo
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment