Tuesday, October 11, 2016

USITAFUTE SAPOTI KWENYE MAZINGIRA

*USISUBIRI MAZINGIRA WEZESHI*

Mwl Proo
0762879363

HALELUYA!!!!
Wengi wetu kuna mambo fulani, ambayo tunatamani kuyafanya, na tunajua kuwa hali zetu zitakuwa nzuri zaidi, tukiyafanya hayo, lakini tunasubiria mazingira wezeshi (supportive environment), ili kuanza kuyafanya. Hapo nashuhudiwa na Mungu, kuwa wapo wengi mno. Tusome andiko la msingi.....

Mhubiri 11 : 4 *_Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna._*

👆🏼👆🏼👆🏼👆🏼NI MUHIMU KUKUMBUKA, TUNAENENDA KWA IMANI, SIO KWA KUONA (2KOR 5:7). MUNGU KAMWE HAKUFANYA JAMBO LOLOTE KWA KUTEGEMEA SUPPORT YA MAZINGIRA RAFIKI (FAVORABLE ENVIRONMENT), ILI ATENDE KAZI YAKE. HAKUSUBIRI MAZINGIRA MAZURI, ILI  AUMBE, KUKIWA NA GIZA, UKIWA, AKAANZA KUFANYA ANAYOKUSUDIA (MWANZO 1:2-3). HAKUSUBIRI TUTUBU, TUJITAKASE ILI ATUOKOE, BALI TUKIWA BADO WENYE DHAMBI KRISTO ALIKUFA ATUOKOE (RUMI 5:6,8). NDIO MAANA, ANDIKO LETU LINASEMA, MWENYE KUANGALIA UPEPO, HATAPANDA! NAYE ATAZAMAYE MAWINGU, HATAVUNA!.

Ndugu yangu, kuna watu humu, wamejipa-udhuru (exemptions), kutofanya majukumu ya kiroho kadhaa, wakiamini mazingira hayaruhusu. Kuna watu wanatamani kufanya huduma, lakini wanasubiri mazingira wezeshi, kuna watu wanataka kufanya maombi na kufunga, lakini wanasema unajua kaI zangu hizi, zinanikinga, nitafunga na kuomba likizo (iko moja kwa mwaka), kuna watu wanasukumwa kutoa kwa ajili ya kazi ya Mungu, nao wameji-exempt, wakisubiri mazingira wezeshi. Hiyo ni kwa mambo ya kiroho na mambo mengine pia, kwa kuendelea kusubiria mazingira wezeshi, wengi wanaacha muhula walioandikiwa upite;

Yeremia 46 : 17 *_Wakalia huko, Farao, mfalme wa Misri, ni kishindo tu; muhula alioandikiwa ameuacha upite._*

👆🏼👆🏼MUHULA ALIOANDIKIWA AMEUACHA UPITE.  VITU VIMEFUNGWA KWENYE MUDA (MAJIRA NA NYAKATI-KAIROS/CHRONOS). BILA SHAKA UNAKUMBUKA YALE MAPEPO NDANI YA MGERASI, YALIMHOJI YESU, VIPI UMEKUA KUTUTESA KABLA YA MUHULA WETU?. YAANI YANAJUA KUNA MUDA UNAFIKA, TUTATESWA MILELE, ILA MBONA MUDA TUNAHISI BADO!!👹👹👹👉🏾⏰. UNAPOSHINDWA KUFANYA MAMBO ANBAYO ROHONI MWAKO, UNAJUA KWA HAYO UTAKUWA NA HALI NZURI ZAIDI, LAKINI UNASUBIRI MAZINGIRA WEZESHI, UNAUACHA MUHULA UPITE KWA HASARA.

*MAMBO YA KUZINGATIA*

♻ *USIOGOPE MWANZO MDOGO*
Sio lazima, mambo yaanze yakiwa level ya juu tayari, unaweza anza kwa kiwango kidogo, itaongezeka, cha msingi anza!

Ayubu 8 : 7
*_Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana._*

Unaamka kuomba, hauhisi hata kauwepo kidogo. Usisitishe anza na huo ukame hivyo hivyo, nguvu itakuja tuu, hata kama utaona nusu saa ya kwanza ni kama haizai matunda, just press on!

♻ *USIYAOGOPE MAUMIVU MADOGO YA MUDA MFUPI, YANAYOTOKANA NA  MAZINGIRA YASIYO WEZESHI*
Wewe ni mfanyakazi, ukiangalia number of tasks kutwa nzima, kazi zinazohitaji energy kubwa,unaamua kupitisha maamuzi, kuwa sitafunga, hadi likizo. Sasa kuisubiria likizo (mazingira wezeshi) unapoteza sana ndugu yangu. Yavumilie hayo maumivu madogo kwa muda, utagundua kuna nguvu itakuwezesha, anza kwa nguvu uliyonayo

Waamuzi 6 : 14  *_Bwana akamtazama, akasema, Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma?._*

👆🏼👆🏼KAMA GIDEON ANGEENDELEA, KUSUBIRIA MAZINGIRA MAZURI, HAKUNGEFANYIKA KITU, LAKINI ALIPOINUKA NA KUANZA KUTENDA, NDIPO AKAJIGUNDUA NI MTU HODARI HASWA! KWA HIYO NENO LA BWANA KWAKO UNAYE-POSTPONE MAMBO YA KIROHO, KWA KUHISI LABDA SHIDA NI MAZINGIRA, LA HASHA. NILIPOTIA MOYO WANGU UFAHAMU WIKI ILIYOPITA, KUWA NAPASWA KUFUNGA, NIKAANZA NA LEO NI SIKU YA NANE MFULULIZO NIPO KATIKA KUFUNGA, SIPO LIKIZO, NI MTUMISHI WA SERIKALI, NAENDELEA NA MAJUKUMU YANGU YOTE KAMA KAWAIDA TOKA ASUBUHI MPAKA JIONI. LAKINI NINGESUBIRI MAZINGIRA RAFIKI, NINGESUBIRI WAKATI MWINGINE, MAANA UNAWEZA KUTA MAJUKUMU MENGINE UNAPASWA KUYAFANYA, UKIWA UMECHOKA SANA MWILI. ILA UNAPOENDELEA, NDIPO UNAGUNDUA KUNA NGUVU KUBWA YA KUKUWEZESHA KWA UWEZO WOTE (KOL 1:11).

♻ *MUDA WA SASA NI BORA ZAIDI, KULIKO ULE UNAOSUBIRI*
Wewe ni kijana, nguvu ulizo nazo leo za mwili, hutakuwa nazo ukifika miaka 45 na kuendelea. Mungu anajua umuhimu wa muda wa ujana, na akatoa ushauri kwamba kama unataka kuitwaa nira yake Mungu, ufanye katika ujana maana unazo nguvu (Maombolezo 3:27, 1Yohana 2:14). Shetani naye anajua siri nyingi sana za kimungu,anajitahidi kuwapotezea muda vijana, kwa mambo mengine. Wale wanaosubiri wastaafu 👴🏾👵🏿, ili waanze rasmi kujitoa kwa BWANA, wanakuja kugundua kuwa muhula walioandikiwa, waliuacha upite. Mzee wa miaka 60, akikazana kuamka kusoma Biblia saa nane usiku, usingizi unamshinda kabisa kabisa, akikazana kufunga muda huo,anaishia kupata ULCERS (vidonda vya tumbo) tuu. Kumbe kulikuwa na wakati, alipaswa kuyabana yote, hata kama mazingira hayakuruhusu kabisa.

♻ *KWA SISI WATU WA IMANI, SIO LAZIMA VIGEZO VYOTE VIZINGATIWE, ILI MAMBO YATENDEKE, BALI KWETU NENO LA MUNGU NDIO HATMA YETU*
Waswahili wanasema dalili ya mvua ni mawingu 🌧☁🌦🌨. Na kuna msemo mashuhuri unaosema, vigezo n masharti kuzingatiwa (terms&conditions applied). Sasa hiyo sio lazima iwe kwetu, Sisi tunao mfumo wetu, ambao tuki-adopt huu wa dunia, ni kumwekea Mungu mpaka (Zab 78:41). Kwa hiyo hata hiyo ya kusema, dalili ya mvua ni mawingu, sio lazima iwe applied kwetu, maana Mungu alinyesha mvua ingawa kulikuwa na kawingu☁ kadogo kama mkono wa mtu✋🏾 (1Falme 18:44-45). Kwetu alichosema kwenye Neno lake, ndicho kilicho halisi, kuliko tunachoona huku nje. Akisema Nimeamuru kunguru wakulishe 🕊🕊🕊 (1Falme 17:4ff), haihitaji *Reasoning*, kwamba sasa itakuwaje?🤔

♻ *SHETANI ATALETA VIKWAZO FEKI, ILI USIANZE LILE UNALOKUSUDIA*

❌Atakuinuliwa watu wa kukukatisha tamaa, ukiwa katika mchakato. Kumbuka walichokifanya Sanbalati na Tobia. Muda Nehemia na wengine wanatia juhudi kujenga ukuta wa mji, wao wanawapumbaza eti, haka kaukuta hata akipanda mbweha🐱 katadondoka haka.

Nehemiah 4 : 3
*_Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe._*

>Unaweza ukawa unawaza kufungua biashara, mtu akakuwahi, sikuizi fremu ni shida kupata...huyu anakuwa ni Tobia mjumbe wa Shetani kwenye kusudio lako.

>Unaweza kupanga maombi na kufunga, kanainuka kaugonjwa hukaelewi elewi 💊💉. Ukiona hivyo kuwa mjanja, kupanda nao kwa kuukemea kabla ya kuwahi madawa, maana unakuwa ni ugonjwa feki tu, sio halisi.

♻ *KATIKATI YA HALI MBAYA, KWAKO WEWE KUTAJAA NEEMA*

Usiogope kuanza chochote, eti kwa sababu watu wanalalamikia inflation (mfumuko wa bei), au kodi za TRA zimekuwa nyingi. Kumbuka Biblia inasema, Mungu ametujalia sisi neema iliyozidi. Katikati ya hizo kodi nyingi, bila hata kukwepa au kuiibia serikali, Wewe utazidishiwa neema ya kupata faida tu. Kumbuka wakati wa njaa ile wakati wa Isaka, akakimbilia na mkewe huko Gerari, kwa Abimeleki. Ardhi na utaratibu wa kilimo haukuruhusu, lakini yeye alipopanda mbegu, alipata kipimo kimoja kwa mia (Mwanzo 26:12) yaani kama alipaswa kupata magunia 10 yazidishe (10x100)= 10,000. Na Mungu yuleyule aliyefanya mazidisho yale habadiliki, hajabadilika (Mal 3:6, Ebr 13:8, Yak 1:17), anaweza kutenda kwako leo.

*_MUNGU AKUBARIKI ULIYESOMA, USISITISHE CHOCHOTE CHENYE MANUFAA YA KIROHO, KIUCHUMI AU KIJAMII, KWA KUYAONA MAZINGIRA HAYARUHUSU, HAYAKUPI SUPPORT, WEWE ANZA, UTAUONA MKONO WA MUNGU UKIKUSHIKA NA KUKUWEZESHA._*

Mwl Proo
0762879363( All Truth Whatsapp Group)

alltruth5ministries@gmail.com

Thursday, October 6, 2016

YAANGALIE HAYA MWENYEWE!

*YAANGALIE HAYA WEWE MWENYEWE!*

Na Mwl Proo
0762879363
Mjumbe wa Matengenezo

Haleluya watu wa Mungu!!

Baada ya kutafiti na tafakari ya muda mrefu, juu ya maisha ya wanadamu! Nimeliona hili tu;
*_"KUWA NA MUNGU, NDILO JAMBO LA PEKEE TUNALIHITAJI KABLA/KULIKO CHOCHOTE"_*

Wanadamu hawana neno jema na wewe, ila Mungu. Wanaokushabikia utende dhambi, wanaokupamba kwa uovu, wanaokushawishi kwa mazuri ya dunia, wanaokutaka u-compromize na ulimwengu, kwamba fanya tu jambo hili utatubu, kwani mwenye dhambi ni peke yako?, wanaotaka kutumia shida zako utoke kwa Mungu; _*HAO NDIO WATAKUWA WA KWANZA KUKUSUTA, NA WALA HUTAWAONA WALIPOTELEA WAPI,  UTAKAPOACHWA NA MUNGU*_.

Ujumbe wetu, una kichwa chenye sentensi ya kusuta  *_(MSUTO๐Ÿ‘Œ๐Ÿฝ๐Ÿ‘Œ๐Ÿฝ)_*, Wale wale, waliomtia ushawishi Yuda Iskariote, awafanyie dili la kumsaliti Yesu, yaani mtu ambaye alikuwa na standards za kuwa mtume akaharibiwa future yake kwa vipande 30 vya fedha (Shilingi 90 za kitanzania, haitoshi hata Andazi moja). Wakiwa wamemharibia, naye huenda alihisi Yesu angetumia uwezo wake kutoroka. Sasa alipogundua hadi hukumu imesomwa wala Yesu hajatoroka kimuujiza. Akawafuata wale waliomharibia future ya kitume. Akawarudishia pesa, na kulialia mbele zao, kuwa mlinishawishi vibaya ๐Ÿ˜ซ๐Ÿ˜ซ. Walichomjibu ni msuto wa hatari

Mathayo 27 : 4 *_Wakasema, Basi, haya yatupasani sisi (YAANI INATUHUSU NINI SISI)? Yaangalie haya wewe mwenyewe(MAANA YAKE UTAJIJU NA TAMAA YAKO MWENYEWE๐Ÿ‘Œ๐Ÿฝ๐Ÿ‘Œ๐Ÿฝ)._*

Hivyo ndivyo wale mashoga zako mnaoenda kusukana, huku wanakushawishi, huwezi kukaa na mwanaume mmoja tuu, lazima nje uwe naye mwingine wa kukuhudumia matumizi nawe unamlipa tendo la ngono. Siku ndoa ikiharibika, watakuletea misuto classics๐Ÿ˜›๐Ÿ˜›๐Ÿ‘Œ๐Ÿฝ๐Ÿ‘Œ๐Ÿฝ๐Ÿ‘Œ๐Ÿฝ. Hapo ndipo utakapojua kupambanua kati ya yaliyo matakatifu na ya siku zote (Lawi 10:10).

*MUNGU ALITUTOA KATIKA HALI MBAYA, TULIPOOKOKA (TUSISAHAU HILO)*

EZEKIEL 16:4-14
๐Ÿ”ดAlitukuta wachafu, hatuna msaada, wala hakuna aliyetuhurumia.

_*4 Na katika habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa.*_
_*5 Hapana jicho lililokuhurumia, ili kukutendea lo lote la mambo hayo kwa kukuhurumia; lakini ulitupwa nje uwandani, kwa kuwa nafsi yako ilichukiwa, katika siku ile uliyozaliwa.*_

๐Ÿ”ดKatika hiyo hali mbaya, ni Mungu pekee alitupenda, akatuhurumia. Akaiondoa hali ya ufu, iliotokana na dhambi, akatuhuisha, akatuongeza katika kila nyanja. Zaidi sana alitufichia ile aibu ya dhambi zetu za kwanza

_*6 Nami nilipopita karibu nawe, nikakuona ukigaagaa katika damu yako, nalikuambia, Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai; naam, nalikuambia, Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai.*_
_*7 Nalikufanya kuwa maelfu-elfu, kama mimea ya mashamba, ukaongezeka, na kuzidi kuwa mkubwa, ukapata kuwa na uzuri mno; matiti yako yakaumbwa, nywele zako zikawa zimeota; lakini ulikuwa uchi, huna nguo*_
_*8 Basi, nilipopita karibu nawe, nikakutazama; tazama, wakati wako ulikuwa wakati wa upendo; nikatandika upindo wa vazi langu juu yako, nikakufunika uchi wako; naam, nalikuapia, nikafanya agano nawe, asema Bwana MUNGU, ukawa wangu.*_

๐Ÿ”ดNa baadaye akatutakasa, akatufunika kwa utukufu wake, mataifa wote wanatutamania, ameyapamba maisha yetu kwa kila uzuri, ndivyo tulivyo leo.

*_9 Kisha nikakuosha kwa maji; naam, nalikuosha kabisa damu yako, nikakupaka mafuta;_*
*_10 nikakuvika nguo ya taraza, nikakupa viatu vya ngozi ya pomboo, nikakufunga nguo ya kitani safi kiunoni mwako, nikakufunika kwa hariri._*
*_11 Nikakupamba kwa mapambo pia, nikatia vikuku mikononi mwako, na mkufu shingoni mwako._*
*_12 Nikatia hazama puani mwako, na pete masikioni mwako, na taji nzuri juu ya kichwa chako._*
*_13 Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; na mavazi yako yalikuwa ya kitani safi, na hariri, na kazi ya taraza; ulikula unga mzuri, na asali, na mafuta; nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata kufikilia hali ya kifalme._*

SASA NENO ALILONIPA BWANA KWAKO NI HILI; USIYAHARIBU MAISHA YAKO, MAANA AMEKUTENGENEZA KWA GHARAMA (1KOR 6:20). USIJIANGALIE MWILINI, KATIKA ULIMWENGU WA ROHO, UNAPENDEZA SANA, PAMOJA NA KWAMBA HUKU NJE UMEZOEA KUDUNGUA MITUMBA YA MANZESE ๐Ÿ‘—๐Ÿ‘•๐Ÿ‘š๐Ÿ‘˜, KATIKA ULIMWENGU WA ROHO UMEVIKWA VITU VYA UKWELI AMBAVYO HATA FIRST LADY WA MAREKANI HAWEZI MUDU KUVINUNUA, ULIVIKWA NA MUNGU ULIPOOKOKA.

Kuna watu wanataka kujisahaulisha walipotoka. Wewe mdada ambaye leo unashika maikrofoni๐ŸŽค kutuabudisha kwa nyimbo, umesahau kuwa ni wewe ulikuwa unapanga foleni, pembeni mwa barabara ya Sinza, ukijiuza kwa ukahaba? Tena hata kingereza hamkukijua, ila mlitumia cha kuungaunga *_"take me, me good"_*. Yesu ameifuta historia yako ya ukahaba leo ni *PRAISE LEADER*. Wewe mwanaume ambaye ulikuwa unatoka Bar ukiwa chakari (full tungi ) ๐Ÿบ๐Ÿป๐Ÿ˜ž, unaokotwa mtaroni. Leo Yesu kakufanya eti ndio mzee kiongozi wa kanisa lake takatifu. Kumbuka kule ulipotoka, na alipokuweka Yesu sasa. Umeyapata yote huku kwa Yesu pamoja na heshima kubwa.

Usithubutu kuyaharibu maisha, ambayo kwa gharama kubwa ulitengenezwa. Ukiyaonja haya mazuri ya Mungu, ukajiangusha tena, kulipiwa tena ile gharama ya kwanza mmmh sijui (IT IS NOT GUARANTEED; Ebrania 6:4-6, 10:26).
USIFANYE MAMBO  YANAYO HARIBU MAISHA AMBAYO MUNGU AMEYAFANYA YAPENDEZE *_COLOURFUL_*
1.USITHUBUTU KUFANYA TENDO LA NDOA, NAWE HAUPO KWENYE NDOA, PENALTY ITAKUKUTA TU
2.USITHUBUTU KUTOA MIMBA, KAMA ULIANGUKA TUBU,VUMILIA UZAE TU ULEE KA-BABY๐Ÿ‘ถ๐Ÿพ
3.USITHUBUTU KUTEMBEA NA MUME WA MTU UKAIHARIBU NDOA YA MTU (UKIHARIBU LAZIMA UHARIBIWE isaya 33:1) USISEME MME WAKE NDIYE ALINISHAWISHI.
4.USIKUBALI USHAWISHI, WA WATU KUIIBIA KAMPUNI (Mith 1:10)
5.USIKUBALI KUOLEWA NA MTU AMBAYE SI IMANI MOJA NAWE (KWA  MAANA YA efeso 4:4-5), SIZUNGUMZII DHEHEBU, MBAYA ZAIDI IMANI ISIYO YA YESU (ETI UNAONA KUKAWIA UKAPATA TAJIRI WA KIISLAMU, UKAJILIPUA ๐Ÿ’ฃKWA KUOLEWA HUKO
6.USIVUNJE UAMINIFU WA NDOA, HATA KAMA MUME AU MKE YUPO MASOMONI ULAYA MUDA MREFU.
7.USIKUBALI KUWA NA MARAFIKI WA NAMNA YA YONADABU, ALIPOKWISHA MSHAWISHI AMNONI AMBAKE DADA YAKE KWA NGUVU, HATUJUI HATA ALITOROKEA WAPI MUDA MAMBO YAMEHARIBIKA.

NA MENGINE YOTE YANAYOHARIBU MAISHA _*YOU, NAME THEM!!*_ ILA KUMBUKA UKIWAJULISHA WALE WALIOKUSHAWISHI, WATAKUJIBU KWA MSUTO KAMA KICHWA CHA UJUMBE HUU. PIA KUMBUKA HALI YAKO YA MWISHO ITAKUWA MBAYA, KULIKO ILE AMBAYO MUNGU ALIKUKUTA NAYO, UTUKUFU UTAGEUZWA TENA KUWA AIBU. (Math 12:43ff, Hosea 4:7)

Nimemaliza alichoniwekea Bwana, moyoni.

Mwl Proo
0762879363
0718922662

alltruth5ministries@gmail.com

Friday, September 23, 2016

FAN INTO FLAME

*```FANNING INTO FLAME```*

*```KUCHOCHEA```*

_Na Mwl Proo_
0762879363

Bwana Yesu apewe sifa!
๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ
Mungu wetu amejitaja kama moto ulao (Ebra 12:29), Amesema atakuwa ukuta wa moto kutuzunguka (Zek 2:5), Neno lake kalifananisha na moto (Yer 23:29), Kisha akasema anatufanya sisi watumishi wake kuwa miali ya moto (Ebra 1:7). Majini katika Quran yalijieleza kuwa yalitaka kwenda mbinguni lakini yakakutana na miali ya moto (Q 72:8), Katika yote hayo napata hitimisho kuwa moto ni bidhaa adimu ktk ule ulimwengu mwingine, ingawa moto huu wa huku mwilini hauna kazi kule ktk ulimwengu wa roho. Hata kama tukichukua tunguri za uchawi tukazipiga moto๐Ÿ”ฅ, hakuna jini linaungua pale, tunaondoa tu kile chombo kinacholeta muunganiko.

SASA SISI NASI, TUKIISHA OKOLEWA TUNAFANYWA MOTO, NA SHARTI HUO MOTO UCHOCHEWE. MOTO UZIPOCHOCHEWA UNAZIMA

NA NDIO MAANA BIBLIA INASEMA,
1Thesalonike 5 : 19
*_Msimzimishe Roho; (Do not quench the Spirit)_*๐Ÿ”ฅ
Mioyo yetu na maisha yetu ya kiroho, ndiyo madhabahu halisi kwa sasa. Makuhani walipewa maelekezo kuwa moto wa mashabahuni ๐Ÿ”ฅ, haupaswi kuzimika, ni full kusongeza kuni daima" usuzimike, ikiwakilisha kuwa maisha yetu ya kiroho, hayapaswi kuwa na ubaridi/kuzimika

Walawi 6 : 13
*_Moto utatunzwa uwake juu ya madhabahu daima; usizimike._*

Paulo mtume anamwelekeza Mchungaji Timotheo, achochee ๐Ÿ”ฅkarama 

2 Timotheo 1 : 6
_*Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu.*_

MAISHA YA KIROHO ILI YAWE MOTO WAKATI WOTE, LAZIMA YACHOCHEWE. NAMNA NZURI YA KUJICHOCHEA KIROHO NI KWA KUFANYA MAZOEZI YA KIROHO (SPIRITUAL EXERCISE). ๐Ÿ‹๐Ÿพ

1 Timotheo 4 : 7
*_Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa._*

NENO JIZOEZE LINAZUNGUMZIA EXERCISE/TRAINING. MAZOEZI YA KIROHO NI DHAHIRI NDIO HAYA.  UKIJUA HUDUMA NA KARAMA ZAKO UNAZIFANYA KWA JUHUDI, MAOMBI NA KUFUNGA, KUJIZOEZA KUOMBA KWA KUNENA KWA LUGHA KWA MUDA MREFU, KUJIFUNZA NENO LA MUNGU KUTOKA KATIKA MAANDIKO, KUTUMIA MUDA WAKO KUWASHUHUDIA WENGINE HABARI ZA IMANI YAKO, KUJIHUDHURISHA KWA BWANA KWA IBADA MARA KWA MARA (DHABIHU YA MUDA NA MWILI WAKO KUUTOA SADAKA), KUHUDHURIA SEMINA ZA NENO LA MUNGU, MAKONGAMANO YA KIROHO NA MAKAMBI YA HUDUMA. MAMBO HAYA NA MENGINE, YANAPASWA KUFANYIKA REGULARLY KUEPUKA KUWA NA NGUVU ZA MWILI,  LAKINI KIROHO UKAWA FLABBY (MANYAMA UZEMBE). MUNGU ALIKUTAZAMIA UTAENDELEA KUDUMU KATIKA KAZI YA KUUCHOCHEA ULE MOTO ALIOUWASHA KATIKA MAISHA YAKO YA KIROHO. KILA MTU AKIPOA HATA YEYE MWENYEWE ANAJIJUA NA WATU WENGINE WATAJUA. HIVI UNAJUA UKIWA MOTO, UNAWEZA KUSEMA, *"HALELUYA!!"* KAMA MAPEPO HAYATALIPUKA, KILA MTU WA ROHONI ATASIKIA ILE HALELUYA ULIYOISEMA INA MGUSO WA KIMUNGU, YAANI IMEAMBATANA NA MAFUTA MABICHI (ZAB 92:10) YA ROHO MTAKATIFU. LAKINI UKIPOA UNAWEZA KUTUSUMBUA NA SALAMU YA BWANA YESU ASIFIWE MARA KUMI KUMI, NA BADO HATUHISI MGUSO. WAKRISTO WENGI WA LEO, KWA KISINGIZIO CHA UBIZE WA MAISHA, WAMERUHUSU MOTO KUZIMA KABISA KWA KUWA MTU ANAKAA MIEZI SITA HAJAFANYA MAZOEZI YA KIROHO, ILI KUCHOCHEA MOTO. DANIEL ALIKATAA KUKAA SIKU 30 BILABILA, AKAAMUA KUCHOCHEA MOTO WA MADHABAHU YA MOYO WAKE, MARA TATU KWA SIKU.
WEWE MLOKOLE MWENYE EXCUSE KATIKA KUUCHOCHEA MOTO, MOTO WA MUNGU NDANI YAKO UTAZIMA, UKIISHA ZIMA UTAKUWA NA MAISHA YA WOKOVU AMBAYO YAKO *_CUSTOMIZED_*, YAANI YAMEJAA VITU VINGI SIO VYA KIMUNGU, MAANA HUJA-UPDATE WINDOW. MOTO HUU UKIPOA MTU HATA ILE FILTER YA NAFSI INAKUWA *_DULL_* YAANI BUTI, DUNIA INAMSOMBA TUU, KUKIZUKA STYLE YA KIDUNIA HANA NGUVU ZA KUCHUJA (FILTERING), KUNA MPENDWA NILIMSIKIA ANATAMKA NENO *_KUDADADEKI_* KATIKA KUMHOJI MAANA YAKE NINI, HAJUI, ILA KALITOA HUKO DUNIANI, SASA SIHITAJI KUJUA MAANA YAKE, ILA WEPESI KUNASWA NA KILA MSEMO, MPAKA MATUSI HUWA NI KIASHIRIA CHA MOTO KUZIMA.

AMBAO WANADUMU MUDA MREFU NA MOTO USIOCHOCHEWA, UKAZIMA, NDIPO UNAKUTA MTU ALISHAOKOKA, ILA MUDA WA MAOMBEZI NAYE ANAANGUSHWA CHINI CHALI, ATI ANA PEPO๐Ÿ‘น, PEPO WACHAFU WANA TABIA YA KUJA KUTEST. YAKIKUTA MOTO WA MADHABAHU UMEZIMA YANAKUINGIA KABISA. TENA MOTO UKIZIMA NDANI YAKO, UTAJIGUNDUA KWA WEPESI SANA, TABIA AMBAYO ULIKWIAHA KUISHINDA UNAITENDA KWA UPYA KWA MWENDOKASI HATARI.

WENGI KATI YA WALIONGUKA KATIKA UZINZI/UASHERATI, HAIKUWA BAHATI MBAYA. MOTO ULIZIMA, WAKENDELEA KUJIKAZA, JARIBU (TEMPTATION) LILIPOKUJA HALIKUMKUTA NA NGUVU. NA WEWW MSOMAJI UNAJIJUA WAZI, KUNA WAKATI UNAKUWA UMEPOA, HADI UNAJIGUNDUA KUWA KWA HALI, IKITOKEA GHAFLA NIPO NA BINTI AU KIJANA WA KIUME, SINA NGUVU YA KUSHINDA KUFANYA UZINZI (HIYO MTU NAFSINI MWAKE ANAKUWA ANAJUA). SASA KUJINASUA JITENGE NA MAZINGIRA YA MAANGUKO *_UNTIL YOU REACTIVATE!_* USIJIPELEKE KWENYE MAZINGIRA HATARISHI WAKATI ULE MOTO UMEZIMA, HUTASALIMIKA

ISIPOKUWA. UKIGUNDUA MOTO UMEZIMA FANYA MPANGO WA KUCHOCHEA, KAMA KUNA SEMINA IHUDHIRIE KWA BIDII, MPAKA UNASURIWE SEHEMU ULIPOKWAMA, UWEZE KUANZA KUCHOCHEA UPYA. MOTO UNAWEZA UKAZIMA UKAKUTA UNAWEKA ALARM CLOCK⏰ ILI UAMKE KUOMBA, KUAMKA UNAAMKA NA KUOMBA HAUOMBI. WEWE MWENYEWE ULIFUNGA MPAKA SIKU 7, LAKINI SASA SIKU MOJA YA KUFUNGA UNAKUTA NI KAMA MTIHANI!?

UKIYAONA HAYO, USISUBIRI ANGUKO KAMILI, BALI FANYA FASTA UUCHOCHEE MOTO

Mwl Proo
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com