*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
_*Rightly Dividing The Word of Truth*_ (2Timothy 2:15b)
*SEHEMU YA SABA*
*CHANZO CHA NGUVU*
Mwandishi: *Mwl Proo*
Mmebarikiwa ninyi nyote mnaoendelea kuufuatilia mfululizo huu. Leo nimepewa kuzungumzia nguvu na chanzo chake.
Nguvu zote zilizopo, zilizokuwapo, zitakazokuja zote (za zamani zijazo) ni za Mungu, chanzo cha nguvu zote ni Mungu. Hata nguvu zinazotajwa kuwa ni za shetani (Mdo 26:18) zote ni za Mungu, na chanzo cha nguvu hizo ni Mungu. Suala la shetani ku-manipulate, au kuzitumia nguvu alizopewa kwa uovu, haibadili ukweli kama chanzo cha nguvu hizo ni Mungu. Hata zile nguvu maarufu ziitwazo za asili (natural powers), chanzo chake ni Mungu, ni za Mungu... Kama kuna nguvu inaizungusha dunia bila kupungua spidi yake, kama kuna mikandamizo ya hewa kukaleta upepo, kama kuna nyota na sayari katika miendo yake kuna aliyeamuru viwe vikawepo, alipoamuru aliruhusu nguvu zake kutekeleza na kuyashikilia mambo yote kwa uratibu wa hali ya juu (Isaya 40:26, Zaburi 8:3)
Andiko la Warumi 13:1b linatumia neno _'exousia_' kutaja uweza/nguvu/mamlaka. Neno hilo limetumika mara 29 katika Agano Jipya la Kiyunani na mara nyingine limetumika kwa kubadilishana (interchangeably) na neno dΓ½namis (dunamis π specifically to perform miracles) likitaja nguvu. Andiko hilo katika versions nyingi (mfano: KJB, ASV, DRM) linasomeka, _Hakuna nguvu ila za kutoka kwa Mungu tu_
*For there is no power but of God: the powers that be are ordained of God.*
Nguvu za Mungu zinaweza kuwekwa katika vitu kutekeleza makusudi fulani fulani. Kwenye Biblia yote Agano Jipya na la Kale, viko visa vingi ambavyo nguvu za Mungu ziliruhusiwa kuwepo (transmit) katika vitu na vitu hivyo vikatumiwa kutekeleza kazi iliyokusudiwa. Hebu fikiria kisa cha Elisha katika 2Wafalme 4:29ff... Elisha alitransmit nguvu za Mungu kwenda kwenye fimbo yake, akampa Gehazi akamgusishe mtoto aliyefariki, ili afufuke. Nguvu za Mungu ndani ya Elisha hazikukaa tu ndani ya roho na nafsi yake hai, bali hata mwili, damu, nyama, na mifupa yake (soma 2Wafalme 13:21) utagundua mifupa yake ilisalia na nguvu zilizoweza kufufua mtu yeye akiwa amekufa kwa homa siku nyingi. Tunasoma katika Matendo 19:11, leso na nguo ambazo zilimgusa Paulo zilipelekwa kwa wagonjwa wakapona, na pepo wabaya wakawatoka. Matukio kadhaa yanaonesha nguvu za Mungu ndani ya watu zilikuwa transmitted kwa vitu (kumbuka kisa cha chumvi kwenye chanzo cha mto huko Yeriko, kumbuka kisa cha unga uliotiwa sufuriani ili kuiondoa mauti, kumbuka pindo la vazi la Yesu, tope lenye mate ya Yesu, birika la Bethzatha na mengine mengi). _mwlproo_
Kuna upotoshaji mwingi unaotokana na kukosekana kwa maarifa. Kuna makelele mengi yanaleta aibu kama sio huzuni. Leo hii tuna watu ambao hiki kitu wamekipokea kimakosa utasikia sabuni, utasikia mafuta, utasikia maji, utasikia pipi, utasikia keki, utasikia stika, utasikia chumvi, utasikia udongo, utasikia kitambaa cheupe.... Vyote hivi vitaenda kwa jina la upako... Kwa miaka mingi vimekuwa vikiitwa visaidizi (erroneously), na miaka michache iliyopita nilimsikia mhubiri mmoja wa Dar akiviita vifaa vya kiroho, jina ambalo sasa linatumiwa na wengi. NDUGU ZANGU WAKRISTO VITU NILIVYOTAJA HAPO JUU VYOTE HAVINA NGUVU. NGUVU ZIKO NDANI YA WATU, NA WATU NDIO WANAOWEZA KURUHUSU NGUVU ZILIZO NDANI YAO ZIENDE KWENYE VITU (TRANSMISSION), NA KURUHUSU NGUVU ZIENDE KWENYE VITU KIBIBLIA NI PALE TU ROHO AMEKUPA UFUNUO (NENO LA HEKIMA) KWAMBA SHIDA HII IHUDUMIE HIVI ZIRUHUSU NGUVU ZIENDE KWENYE MAJI AU CHOCHOTE KIWE NA CONTACT NA MWENYE SHIDA TATIZO LIKAONDOLEWA, AU KWA NAMNA ILIVYO KATIKA MAZINGIRA NI NGUMU KU-ADMINISTER HUDUMA ZA KUPONYA NA MATENDO YA MIUJIZA KWA NENO LA IMANI, KWA KUOMBA, KWA KUWEKA MIKONO NA NAMNA NYINGINE YA UTENDAJI. HIZI NI NAMNA MBILI KWA MUKTADHA WA UKRISTO VITU HIVI VYAWEZA HAMISHIWA NGUVU ZILIZO NDANI YA MTU KURUHUSU VIKATENDE KAZI.
Dramas zinazoendelea leo hii Afrika ni nyingi mno. Wakristo wanakimbizana na hivi vitu kiasi cha wao kupumbazika kabisa kubakia watumwa mara billion ya walivyokuwa kwanza. Nilipewa ushuhuda wa mama aliyemwaga chumvi yake ya upako bahati mbaya na akasikitika sana na kilio juu. Nilishuhudia kwa macho yangu mhubiri mmoja huko Dar, aliivua tai yake π na kuirusha kwa watu kwamba ina upako (sikatai maana upako unahamishika), lakini iligombaniwa sana na washirika, na kijana mmoja alifanikiwa kutoka nayo nje, katika vutavuta mwingine aliikata kipande... wamama wawili wakamwomba wamlipe laki 3 awaachie kipande hicho cha tai. Dramas hizi za vile vinavyoitwa visaidizi au vifaa vya kiroho ziko Afrika kuliko mahali pengine popote palipofikiwa na pentecostal & charismatic movements, kwa nini haswa?
Hapa Afrika vimekuwa maarufu kwa sababu ya imani za asili au za kienyeji kwa jamii ya watu wa Afrika. Maishani mwangu nilipata neema ya kusomea dini za asili za Afrika (African Traditional Religion π ATR). Kwenye dini zetu za asili na tamaduni vitu vya kuonekana, vya kushikika, manuizo, matambiko, ulozi, na mengine mengi yaliyohitaji vitu vya kuonekana yalihitajika sana. Fikiria jamii ambayo ilizoea wakitoka kwa mganga wa kienyeji, wamechanjwa miili, wamepewa vitu vya kutia kwenye maji ya kuoga, wamepewa vitu vya kufunga mikononi, viunoni, shingoni, wamepewa vitu vya kulalia chini ya kitanda, cha kupaka ukutani, cha kumwaga na kunuiza kwenye kuta za nyumba, cha kuweka darini na kadhalika.... Haya yamekuwa mambo ya kawaida kwa karne nyingi Afrika, yamerithishwa vizazi vingi kiasi cha kuwa ni kama kitu cha kuzaliwa nacho. Kila atakayekuja Afrika akawa na vitu tangible vya kugawa kwamba vina nguvu za kusaidia atake au asitake lazima atafanikiwa kupata ufuasi mkubwa maana imegusa asili ya Afrika. Hapa sasa ndio sababu haswa ya kila mhubiri kwa sasa anakomaa na vitu hivi.. Hata mahali ambako angeweza kumgusa mgonjwa kwa mkono wake, atamwagiza ashike kitu, hata mahali ambako angetamka tu 'kansa kauka'... atatafuta kwenye briefcase πΌ chupa cha mafuta aliyoyabeba toka Israel bila hata maelekezo ya Roho wa Yesu (mtu akiongozwa na anaweza kuthibitisha hilo hakuna tatizo) Lakini 95% ya watumiaji wa hivi vitu, hawana maelekezo yoyote ya Yesu... wanaunga-unga na kujaribu-jaribu tu, mambo yakitokea kweli wanaendeleza bila kujua nguvu zipo ndani yao.. Na matokeo yanatokea si kwa sababu wapo sahihi... Ni kama tu mtu kunywa sumu akiamini ni juisi tu, haitazuilia sumu kufanya kazi yake ya kumwua, au mtu anywe maziwa akiamini ni maji tu, haitaizuia maziwa yasimpe nutrients zinazopatikana kwenye maziwa. Lakini tatizo limekuwa kwenye kufanya waamini wasijue kuwa nguvu ziko ndani ya watu si ndani ya hivyo vitu.. Niliongea na rafiki yangu mmoja ambaye dada yake ni mhudumu (usher) kwenye huduma moja ya maombezi. Alisema waliuza maji ya uhai (katoni za kutosha) ambayo yaliombewa na mtumishi wiki nzima, yakaisha na watu bado walikuwa wengi, hivyo ikabidi maji yakanunuliwe direct toka dukani na kuuzwa kwa watu kama maji ya upako... bila hayo maombi ya siku saba. Guess what! Kwa sababu ya imani ya miujiza ndani ya hawa watu haya maji yaliyotoka dukani directly yakipelekwa kwa wenye shida yanawezaleta shuhuda pia. Lakini ufahamu wa juu kabisa kwa waamini ni kufahamu nguvu zote hizo ni za Mungu, na jamaa ya waamini (WOTE) walipobatizwa katika Roho wa Kweli nguvu hizo bila kipimo zilikuwa superimposed ndani yao. Waamini wote wanazo hizo nguvu, utendaji utatofautiana tu kulingana kiwango cha maarifa, na unafanya nini katika ufalme, na Roho Mtakatifu amekupea karama zipi, au wewe mwenyewe unatembeaje katika kutumia vilivyowekwa ndani yako tayari. KWA KUSEMA HIVYO WAAMINI HAWANA HAJA WAO WENYEWE KUKIMBIZANA NA CHOCHOTE, MAANA NGUVU ZENYEWE ZIKO NDANI YAO. KAMA KUNA NGUVU ZIPO KWENYE UDONGO WA ISRAEL, AU MAJI YA YORDAN, AU SABUNI, AU CHUMVI AU KITAMBAA KILICHOOMBEWA, NGUVU HIZO SI KWA AJILI YA MKRISTO YEYOTE MKOMAVU, MAANA YEYE MWENYEWE NDIYE MZALISHAJI WA HIZO NGUVU KUTOKEA NDANI YAKE ZIKASAIDIE WALIOFUNGWA NA ADUI HUKO NJE (YOH 7:38). MWAMINI ANAYEHISI KUWA KWA POSTI HII NINAWAPINGA WAO AU MHUBIRI YEYOTE HONGERA YAKE KWA KUCHAGUA KUWA MTUMWA WA DAIMA.. ENJOY YOUR SLAVERY, REMAIN CAPTIVE TO IGNORANCE. MIMI BINAFSI NGUVU ZIPO NDANI YANGU, NIKISTULIWA SAA NANE USIKU KUTOA HUDUMA YOYOTE YA KIROHO, NITATOKA NIKIWA NA NGUVU ZOTE BILA KUHITAJI KUTAFUTA KICHUPA FULANI ETI NIMEKIFICHA KWA KABATI, HATA BAADA YA KUTRANSMIT NGUVU KWENDA KWENYE VITU, NIMEPEWA UWEZO KUJI-RECHARGE π π MIMI MWENYEWE SI MIMI KUTEGEMEA VINGUVU NILIVYOVIHAMISHIA KWENYE KITU.
Tukutane sehemu 8, kuna mambo mazuri utayafahamu
alltruth5ministries@gmail.com