*🅖🅘🅕🅣🅢 vs 🅒🅗🅐🅡🅐🅒🅣🅔🅡*
_*KARAMA NA TABIA*_
*Mwl Proo*
~0762879363~
~0718922662~
Mbarikiwe kwa Jina la BWANA aliye Mwokozi na Kristo. Wale ambao akili zao kwa kutumiwa zimezoezwa kupambanua mema na mabaya nawakaribisha kula chakula kigumu, ili tujengwe zaidi na kupokea hatua nyingine kiroho.
💎 Neno karama ambalo kwa somo hili nitatumia kama Gift, ni pana kimaana ambalo limetumika kote katika Agano la Kale (O.T) na katika Agano Jipya (N.T). Biblia ya kiEbrania (Tanakh) imetumia maneno kama _Shachad, Mattan, Nathan, Minchah_ ikitaja neno Gift, ikiwa inatofautisha kidogo kati ya kipawa, kipaji, na karama... lakini tafsiri za kingereza maneno yote hayo yalitaja tu *Gift*..... Agano Jipya ambalo liliandikwa kwa lugha ya Kiyunani (Greek) limetumia maneno mawili kutaja Gift, yaani Dorea (karama ya asili 👉🏾 Gift of nature au kipaji na wakati mwingine hata huduma.... Pia imetumia neno _Charisma_ ikitaja karama ya Roho (karama au kipawa kinachohitaji uwezesho wa kiMungu kukitumia 👉🏾 divine enablement) kimetajwa zaidi kama Charisma.
💎 Kuna karama za Mungu, kuna karama ya Kristo, kuna karama za Roho Mtakatifu
👉🏾 Za Mungu (mfano; Rumi 11:29, Mhubiri 5:19, 1Petro 4:10
👉🏾 Za Kristo (Ephesians 4:7)
👉🏾 Za Roho (1Korintho 12:7ff)
Kuna wakati fulani ambapo maneno haya vipawa, vipaji, na huduma hutumiwa tofauti... Lakini kwa kuwa vitu hivi watu hupokewa (Dorea), kwa ujumla wake (1Kor 4:7) huitwa "Gifts", pamoja na kuwa na huduma (services/offices) za Bwana, lakini kwa somo letu la leo, tutavijumuisha vyote kwa neno moja tu *Gift* (1Kor 12:28ff) katika andiko hili unaona namna fulani Paulo Mtume amechanganya huduma za Bwana na karama za Roho, zote kama Gifts tu....
Warumi/Romans 11:29
*"For the gifts and calling of God are without repentance"*
Andiko hili linasema kwa maana karama za Mungu hazina majuto wa mwito wake.. Katika Biblia za Kiswahili cha kisasa pameandikwa..... _Karama za Mungu hazifutiki_ Mimi nimepekua tafsiri nyingi na commentaries kadhaa, kilichoandikwa hapa Warumi 11:29 ni kwamba *The gifts of God are not to be withdrawn... cannot be revoked, when given, not even to be regretted* Mungu akikupa Gift...haifutiki, haiondolewi, hainyang'anywi
💎 Mungu akiishatoa gift hana desturi ya kuiondoa.
Mungu alimwumba kerubi mmoja ambaye sasa anaitwa "Mshtaki" yaani shetani, ibilisi, mwovu, akiwa amemwekea *Gifts* yaani vipawa vizuri mno
EZEKIEL 28 (Sitajadili hapa kwamba hizi sifa ni za shetani au mfalme wa Tiro na Sidon, maana nimefafanua hayo katika masomo yangu matatu tofauti)
shetani ambaye aliumbwa kwa daraja la kerubi (sio malaika) aliumbwa na gifts hizi hapa
👉🏾 Karama ya hekima (Gift of wisdom) mstari 3-4, 11
👉🏾 Karama ya uzuri (Gift of beauty) mstari 11-13
👉🏾 Karama ya maongozi (Gift of administration ) mstari wa 14 (ulikuwa kerubi afunikaye...a cherub that covereth...kiEbrania pameandikwa _Sakak_ ikiwa inataja eneo la kiutawala lenye mipaka... (see also Isaiah 14:16)
👉🏾 Karama ya Muziki (Gift of Music).. mstari wa 13 (see also 14:16ff)
👉🏾 Karama ya ushawishi (Gift of influence/convincing) (mstari wa 9)..
*☝🏾☝🏾☝🏾☝🏾 Hiyo mistari ni ya Ezekiel 28*
💎 Tabia "character" ya shetani ilibadilika (Eze 28:17). Mungu hamkunyang'anya shetani zile *Gifts*, alimwumba kama kerubi akampa nguvu, hakunyang'anya nguvu zake kwa kule kuasi, alimwumba akampa dunia awe a cherub in charge wa 🌎.... Hakunyang'anywa hiyo kwa ile *Rebellion* aliyoiwaza juu ya Mungu
👉🏾 Yesu anasemaje? anamwita shetani *The Prince of this earth* yaani mkuu wa ulimwengu huu (Yohana 12:31, 14:30, 16:11)...... Paulo mtume anamwita shetani ni _mungu wa dunia hii_ (2Kor 4:4)
💎 Malaika waasi (malaika za shetani 👉🏾 hawa sio mapepo wachafu/majini) hawakunyang'anywa *GIFT* kwa kukubali kumtii kerubi mwasi "shetani".
La sivyo yule prince wa uajemi (medes&persia)..asingekuwa na namna ya kuweka resistance kieneo hata kumchelewesha malaika Gabriel siku 21 kampiga pini asivuke (Daniel 10), so to say nguvu za shetani ni za Mungu, ila baada ya kuasi anazitumia kwa uovu (power of darkness)
*HITIMISHO LA UTANGULIZI*
*_Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya Gifts/Karama na Tabia/Character_*
*❷. Juxtaposition of Gifts & Character*
(Kuzilinganisha karama na tabia)
👉🏾 Karama haimvuti Mungu, ila tabia (Mdo 13:22)
👉🏾 Mungu hawi surprized na gifts lakini tabia hufanya hivyo (Ayub 1:6-9)
👉🏾 Shetani hashambulii karama ya mtu bali tabia (he doesn't fight against the gift but character )
👉🏾 Anointing/upako wa kugusa maisha ya watu haupo kwenye gift bali kwenye tabia
👉🏾 Lazima ujue kuwa tabia _good character_ inaweza haribiwa (can be corrupted) 1Kor 15:33
❸. SEXUAL SINS (DHAMBI ZA KIZINAA/KINGONO)
👉🏾 Nimetumia lugha hiyo hapo juu ili kujumuisha sex of all types (tendo la ngono na matendo yote ya kingono 👉🏾 sexual activities and sexual plays)..Watu wanaweza fanya zinaa hata mawasiliano (sexchats).. Ndio maana lile andiko la mazungumzo mabaya huharibu tabia........limeandikwa _evil communication _ kiYunani *Homilia au Kakos Homilia* hapo ndani mpaka Sex imehusishwa na zile njia ovu za kikahaba za mawasiliano (evil communication ways) MITHALI 6:12-13..Zinaa kama kosa kuu (Ayub 31:9-10)..... ni miongoni mwa vitu vikubwa vinavyoCorrupt (haribu) TABIA (character) kwa haraka sana... Mimi ni mwalimu wa sekondari kwa miaka mingi tu sasa...Wanafunzi waliokwisha jihusisha na ngono...reaction kwenye tabia huwa ya mara moja tu... anaweza ghafla tu kuona walimu wote mko sawa naye..
👉🏾 Sex (Ngono) ni silaha ya mwisho ya shetani ambayo imempa mafanikio makubwa mno...
Kwa kutumia silaha hii, shetani amefanikiwa kutengeneza makundi mawili ya watumishi katika kanisa
I. 🚫 Watumishi wakubwa wa Mungu waliopoa.. Kuna watu ambao walipakwa mafuta kwa huduma kubwa na karama nyingi za Roho, wakawa moto sana katika mwili wa Kristo... Baada ya maanguko ya zinaa.....wakapoa...wamefyata mkia...hata kama GIFTS zinafanya kazi..ila wamejikunyata na kujificha...wanamkwepa Bwana, wanakwepa huduma...wametulia chini ya miretemu 🌳🌳🌳🌳
II. 🚫 Watumishi wakubwa wasanii... Kwa kutumia silaha ya zinaa/ngono... shetani amefanikiwa kutengeneza watumishi wakubwa tu katika mwili wa Kristo, ila ni wasanii... wameshindwa kabisa kuacha zinaa...ila kwa kuwa karama zinafanya kazi...zinavutia...zinawafanya wa-earn their living... basi wameona waendelee tu huduma (USANII)... unaweza kuwanasa hawa watu hata kwa sermons zao tu... full of compromizes.... naiweka tu hivyo, Roho atakujuza mwenyewe hapa kwa kina
NB:-
*MTU YEYOTE TU ANAWEZA ANGUKA KWENYE ZINAA AKITENGENEZA/RUHUSU MAZINGIRA, WATAFUTE WAINJILISTI AMBAO WALIKUWA FIRE 🔥🔥 THEN WAKAANGUKA KWENYE ZINAA, USIDHANI ILIKUWA KAZI KUBWA SANAAAAA, ILIKUWA TU KAMA KUMSUKUMA MLEVI CHAKARI AANGUKE CHINI, HII INATOKEA UKIRUHUSU TU MAZINGIRA*
👉🏾 Mtu akishaanguka, Yesu atasimama pembeni akuangalie, unaifanya iwe tabia au unajutia kwa toba nzito ukiangalia kuwa huanguki tena (Yeremia 13:23)... Na kuna muda wa matazamio kuangaliwa kama utafanya toba (Ufunuo 2:21), Yesu akiona huna mpango wa kugeuka anaweza kukuacha ( hakikisha unasoma somo langu _Mwl Proo_ liitwalo "kukuondolewa kinara")
👉🏾 Matendo ya ibada yanaweza kuzoeleka, huku mhusika akiwa na _corrupted character_
🌪 Mtu hapaswi kukosa kushiriki maombi, kufunga, huduma zote zinazokamilisha ibada. Lakimi hizi zote sio kipimo cha good character,mtu anaweza kuzoea hata kufunga na kuomba (fasting & prayer ) akiwa bado ana matabia ya kizinzi-zinzi tu
👉🏾 Mtu akiangalia sana kipawa na kujipa ujasiri kwacho, atapotea, atakufa..... Biblia inasema kipawa (gift) ni kito cha thamani 💎 kwake aliye nacho (Mithali 17:8)..... *BUT I bet you.... KARAMA ZITAPELEKA WATU WENGI JEHANAMU*
🌀 Mkumbuke Samsoni (Amuzi 16:1-3)..Alipewa gifts.... ila mauzinzi yake na mauasherati yake yalibaki kama yalivyo kwenye CHARACTER... Samson aliishi kukiwa tayari na Torati ya Musa, pamoja na kushukiwa na Roho ya Bwana mara kwa mara, hakuonaga tabu kulala kwa kahaba all night long akisherati.. Hivi ina maana gani Samson kukwepa divai 🍷🍇 lakini anasherati ovyo.. ALIKUFA
🌀 Nimepewa ushuhuda wa mwinjilist fulani, aliyekuwa anaaminika kwa kutoa pepo wachafu ndani ya watu... Tena watu wakipagawa pepo...yeye ndiye alikuwa anaachiwa hiyo kazi washirika wengine wakirudi makwao.. Alifikia kiasi cha kutoa pepo akiwa amekaa zake juu ya meza akinywa soda na mapepo yakawa yanapiga kelele na kutoka kwa watu.. Lakini tabia zake za uasherati hazikujulikana...mpaka binti ambaye alikuwa akisherati naye sana kanisani kwenda kujisema kwa mchungaji... na mwinjilist hakuweza kukana, ila akamwomba mchungaji asitangaze...Sasa kumbe hata ule uzinzi wake haukuzuia gifts zake kufanya kazi... Uwe makini sana...Usikae unaamini-amini watu (Mika 7:5, Mathayo 10:17)
👉🏾 Kazi nzuri na matokeo mazuri ya gifts hayamthibitishi mtumishi, bali Yesu anathibitisha neno lake tu (Marko 16;20)
*❹. KUMNYANG'ANYA YESU MAISHA YAKO*
💎 Watu wengi wanatamka vitu bila kuvizingatia sana.. Ukweli ni kwamba mtu akiokoka anakuwa amempa Yssu maisha yake...
💎 Lakini watu humnyang'anya tena Yesu maisha yao (Galatia 2:20, Kolosai 3:3, Galatia 5:13)
👉🏾 Maisha ya mtu yakiwa mikononi mwa Yesu, anakuwa huru, anakuwa salama
👉🏾 Pepo wabaya (wachafu) hawawezi kumtesa ambaye ameshibana na Yesu
🌪 Anaweza tu kusumbuliwa na pepo katika hali ya uchanga kiroho
🌪 Kama mtu alikwisha tembea katika ujuzi wa ile kweli na akaenjoi ule uhuru (ukasikia tena amekuwa demon-possessed, anakuwa alifanikiwa kumnyang'anya Yesu maisha yake... YESU AKISHIKILIA MAISHA YAKO, AKAONA UNA BIDII YA KUMNYANG'ANYA ILI UYAISHI MWENYEWE UTAKAVYO, ANAKUACHIA MAISHA YAKO (LUKA 13:34-35).... kwamba hakuna cha kututenga na upendo wa Mungu (Waroma 8:35ff) haina maana wewe huwezi kujitoa kwenye wema wa Mungu (Waroma 11:22) au kwamba huwezi ipungukia neema (Ebr 12:15ff)...
*KUNA MAKUNDI MATATU (3) YESU ANAYAONA, NA ANA NENO JUU YAO*
_mwlproo_
🌀 1. Waliompa Yesu maisha yao, ila kuna muda wanahisi kuchoka, kuna majira kunakuwa na kaukimya fulani, mpaka unasema hivi mbona wengine wanaendelea tu na uhuru wa kuyatumia maisha yao... wanajaribiwa kama nao kidogo waonje dunia.. Nimepigiwa simu na binti fulani... nikamhoji unaendeleaje kiroho? Haujaanguka? akasema sijaanguka... Ila kuna muda nahisi yani kama na mimi nifanye tu........ haya yalikuwa majibu yake...She's despairing....anakata tamaa na anachoka...amesubiri ndoa...kwa kujitunza haoni dalili....Nikamtia nguvu kuwa bakia umesimama hivyo hivyo..
🌀 2. Kundi la pili ambalo tuko nalo kanisani, ni watu ambao currently kule rohoni wanayavuta, na kukwapua maisha yao mikononi mwa Yesu
*Neno la Yesu kwao*
_Usininyang'anye maisha yako, huwezi peke yako bila mimi, mambo yanayokuvutia nje yangu, yamejaa uchungu kama pakanga (wormwood/artemisia absinthium)_ 🤮
🌀 3. Wako ambao walifanikiwa kumnyang'anya Yesu maisha yao.
👉🏾 Hawa wanakuja kanisani, maana hawana pa kwenda jumapili (it's liturgical), amekulia mazingira ambayo Jumapili wanaenda kanisani.
👉🏾 Hana haja ya kumtafuta Mungu...maana nafsini yake yajua sana kuwa hatamwona
👉🏾 Analazimika kuzitumainia njia za asili katika kutatua matatizo yake yote.
*Neno la Yesu Kwao*
Yesu ambaye sifa yake kubwa ni UPOLE, wala hakemei (Mathayo 21:5, Yakobo 1:5)....Yupo tayari kuyapokea upya maisha yako...Wema wa Mungu unakuvuta upate kutubu (Warumi 2:4)
Mwl Proo
alltruth5ministries@gmail.com
+255762879363