Wednesday, July 24, 2019

FALME NA MAMLAKA

*FALME NA MAMLAKA*

*ʍաӀ Թɾօօ*
```+255762879363```

```Ndugu zangu katika Yesu Kristo, aliye Mwokozi na Bwana, karibuni katika kujifunza siri zilizofunuliwa (The revealed mysteries not  myths) ambazo Mungu kwa Roho wa Kweli anazifunua ili atusaidie. Waamini wanahudumiwa kwa namna nyingi na malaika (Ebrania 1:14), na walipaswa wafanye huduma zao nyingi kwa maelekezo ya waamini ambao kwa bahati mbaya hawana maarifa sahihi juu ya mambo haya, na kupelekea kufanya mengi kwa kupapasa-papasa na kupepesa-pepesa tu.```

*🏹 KAMA NDUGU MSOMAJI UNA MAONO YA KUTUMIKA KWA VIWANGO VIKUBWA VYA KUTENDA KAZI, BASI USIYAACHE MAARIFA HAYA SAHIHI. I BET YOU KAMA KUNA KITU KIMEZUIA KAZI KUBWA KUTENDWA NA WATU WA MUNGU, BASI NI MAARIFA. WATU WAMEKESHA MILIMANI, WAMEFUNGA MAOMBI YA KUTOKULA KABISA KWA MUDA MREFU (DRY FASTS), LAKINI KAZI ZINAZOONEKANA HAZILINGANI HATA NAMNA WALIVYOJIDHILI KWA MAOMBI. MUNGU HAYUKO MBALI HIVYO, KILICHOKOSEKANA ZAIDI NI MAARIFA SAHIHI. KILA MWENYE MAARIFA SAHIHI NA YA KUTOSHA KIROHO, HUKO ALIPO ATAKUWA NA TOFAUTI KATIKA KUTENDA KAZI. UKIKOSA MAARIFA HAYA SAHIHI HATA KAMA UNAJIANDAA KWA UTUMISHI UNAWEZA KUINGEZA IDADI YA WATUMISHI WA KANISA/DINI YENU LAKINI USIWE MIONGONI MWA WALE AMBAO BWANA ALIWATAJA NI WATENDA KAZI (MATH 9:37). THE TIME COMES AMBAPO WALE WALIOZOEA KUWA NA MANENO MATUPU WITH NO IMPACTS HAWATAKUWA NA CHA KUFANYA ZAIDI, UFALME HAUWI KATIKA NENO BALI NGUVU (1KOR 4:20). YESU ANATAFUTA WATENDA KAZI ATAKAOWEZA KUWATUMIA KWA KAZI KUBWA KWENYE HIKI KIZAZI CHA SIKU ZA MWISHO, ILI HATA WASIPOAMINI MANENO, AU WATUMISHI, WAZIAMINI KAZI ZITAKAZOSHUHUDIA WAZI-WAZI KWAMBA NENO LA KRISTO NI LA KWELI NA AMINI (YOHANA 10:38). WENGI WAKIKEMEA KWA JINA LA YESU, WAKIONA PEPO WAMEPAZA SAUTI VILIO BASI WANAHISI WAKO KWA GOOD POSITION, WATUMISHI SHARTI WAZINGIRWE NA ISHARA, AJABU NA MIUJIZA (2KOR 12:12), HIYO YA KUTOA PEPO NI ISHARA TU YA KAWAIDA KWA WAAMINI WOTE (MARKO 16:17), HAINA U-SPESHO WOWOTE, MAANA KAZI ALIKWISHA IMALIZA YOTE YESU, TUNAPOYATOA MAPEPO/MAJINI, TUNAYAKUMBUSHA TU NI MAMLAKA IPI ILITUELEKEZA KAZI HIYO, NAYO YANAJUA HAKIKA KAMA NI KWA MAMLAKA YA HUYO YESU BASI HAKUNA KINGINE, NI KUTII TU... MIMI BINAFSI SIKO TAYARI KABISA KUWA MTUMISHI WA MANENO MATUPU, KUWASOMEA WATU STORI ZA BIBLIA AMBAZO HAZIKO HAI KWAKO, KWA MUDA HUU MFUPI WA UTUMISHI NIMESHUHUDIA ISHARA, AJABU, NA MIUJIZA, NATAZAMIA KUMWONA MUNGU KWA KAZI KUBWA SANA NINAPOENDELEA KUSHIKAMANA NA UTIMILIFU WANGU KWA MUNGU*

*🏹 WAKRISTO (WAAMINI) KUNA MISTARI KATIKA BIBLIA HAWAJAWAHI HATA KUIELEWA KWA SABABU YA SIRI KUTOFUNULIWA. MKRISTO AMBAYE AMEKOSA HELA YA CHAKULA HATA USIKU WA JANA ALIPIGA DESHI (⛔) KWA KULALA NJAA, THEN UMSOMEE MSTARI KWAMBA SISI WAAMINI TUMEKETISHWA JUU SANA NA KRISTO, KULIKO UFALME WOTE, KULIKO NGUVU ZOTE, USULTANI WOTE, KULIKO ENZI NA VITI VYA ENZI VYOTE, AKIYAAKISI MAISHA YAKE, NA MAANDIKO HAYA ANAWEZA ASIYAELEWE KABISA, SIMAANISHI KWAMBA WATU WAKILA NA KUSHIBA WATAELEWA SIRI ZA UFALME (WARUMI 14:17, IMEZINGATIWA)*

*❶ UUMBAJI WA ULIMWENGU (CREATION OF THE UNIVERSE)*

☄ Maneno haya mawili _"Dunia na Ulimwengu"_ yamekuwa yakitumika kwa pamoja kwa kubadilishana *interchangeably* na hivyo tunakosa maana nzuri kwenye Kiswahili, lakini katika Kiingireza neno Universe halitaji hili litufe la dunia bali (space+time), hivyo kama kuna sayari zingine mbali na dunia na chochote kingine in the space ni *universe/ulimwengu*

☄ Mungu alipoumba (Mwanzo 1:1), aliumba mbingu na nchi (Ha'Shamayim & Erets), sasa  neno la kwanza halizungumzii tu mbingu ile ambayo ni ya kiroho BUT  limejumuisha all the skies ambazo zinaweza kufikiwa physically 🚀👨🏾‍🚀👩🏾‍🚀 na la pili linaitaja nchi/earth (land/ground).....

☄ Sasa alipoumba Universe/Space (ulimwengu) aliumba maumbile mengi si dunia tu 🌏, na hayo maumbile (bodies) 🌓🌞🌪 yaliwekewa wasimamizi, viumbe vya kiroho wakiwa in charge of those bodies. Hawakuwa na uhusiano wowote na sayari ya dunia ambayo kimsingi kerubi mmoja ambaye sasa ni shetani alikuwa in charge wa dunia (Ezekiel 28:14, Isaya 14:12-15)... Shetani alikuwa huru kupanda mbinguni muda wowote, mpaka alipopata wazo la kumpindua Mungu....

Shetani hakuanza makeke yake Bustani ya Edeni, alishafanya hivyo tangu akiwa msimamizi wa dunia mwanzo kabisa... Yesu anasema jambo moja very sensitive katika Yohana 8:44

*"Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo."*

Shetani haitwi baba wa uongo kwa kumdanganya Eva, alikwisha danganya viumbe vya kiroho vingine vilivyowekwa kwenye ukuu wa kusimamia maumbile mengine ya uumbaji wa Mungu, si hivyo tu, katika harakati zake za kumpiku aliyemwumba na yeye alishawishi viumbe vya kiroho (malaika) wanaotajwa kama nyota (Ufunuo 12:4), na kwa mkia wake akawakokota theluthi ya malaika waliokubaliana na uongo wake, hapo ni kabla ya Adamu huyu baba wa wanadamu wa leo.

*❷  FALME NA MAMLAKA*

_*"ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na FALME na MAMLAKA katika ulimwengu wa roho;"*_
(Waefeso 3:10)

*_"Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya FALME na MAMLAKA, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."_*
(Waefeso 6:12)

☄ Mungu aliumba wakuu (princes) wa kusimamia maeneo yote katika ulimwengu (including large bodies in skies and all starry hosts).... Ziko mamlaka ambazo zilimtii shetani kwa kuwa alizishawishi (aliumbwa na hicho kipawa cha influencing)...nimemsikia  Prophet Sadhu akifafanua kuwa hata lugha za malaika hazifanani, na shetani alitumia lugha fulani fulani kuwasiliana na watawala (angelic beings) wa sayari zingine...
(Mfano wakuu hawa hapa chini wanasimamia sayari saba wajulikanao kwa jina la *ARCHONS* these make up the powers of darkness)
1. Yaldabaoth (Saklas/Samael)
2. Iao
3. Sabaoth
4. Astaphanos
5. Adonaios
6. Elaios
7. Horaios
Majina haya yako kwa matamshi ya Kiebrania na Kiyunani, na majina ya mapepo mengi ni majina ya nyota/other heavenly bodies na ipo sababu (nitaieleza katika somo jingine). Majina kama Maimuna ﻣﻴﻤﻮﻧﺔ
lenye maana ya *lucky/blessed* i.e.; mwenye bahati/mwenye heri, haya sio majina kamili/sahihi ya hizi roho za kipepo hata kama muda unakemea pepo akajibu mimi ni Jinn Aisha.

*❸  FALME NA TAWALA ZA DUNIA NI UVULI WA TAWALA ZA FALME/MAMLAKA ZILIZOKO ROHONI*

☄ Katika historia ya kale 3000BC ---- 476AD, kulikuwa na tawala za dunia zilikuwa zinapata nguvu na kuzishinda zingine  (ANCIENT DYNASTIES AND GREAT POWERS OF THE ANCIENT WORLD). Shetani ni mmoja, naye ni roho, alipotaka kutekeleza mambo fulani fulani juu ya dunia, aliweza kusababisha utawala mmoja uanguke na mwingine ushike nguvu...
Hivyo kuna wakati ASHURU (ANCIENT ASSYRIAN EMPIRE) Ilikuwa na nguvu, kwa sababu fulani-fulani Shetani akafanya Babeli ya kale (Ancient Babylonian Empire 1894BC kushika nguvu ya dunia), na baada ya hapo nguvu ilishikwa na Misri, baada ya hapo Uyunani baadaye Rumi

*NB:-*
```OUR SUPREME GOD IS THE SOVEREIGN LORD, HAKUNA CHA KUMZUIA KWA LOLOTE MAANA YEYE NDIYE AMEVIUMBA VYOTE. HIVYO KUNA WAKATI SHETANI ANAWEZA WEKA MIPANGO YAKE, MUNGU AKAPACHIKA LA KWAKE HUMO-HUMO, AND THE DEVIL GETS CONFUSED..... ILI NAYE AKUMBUKE KUWA ALIUMBWA (EZEKIEL 28:13-14)```

🧨 Shetani alitaka kuvuruga mpango wa Mungu wa kumleta Yesu, aliouahidi pale Mwanzo 3:15 (Woman's seed/offspring), na hivyo alikusudia kuichafua human race ili Kristo asiwe sadaka ya kufaa kwa ukombozi... Na alifanikiwa kuharibu human race (degeneration) pale Mwanzo 6:2-12... Nuhu aliingia kwenye safina na Shetani kwenye genes za wakweze.... Ham, Shem na Yaphet na wake zao hawakuwa salama kwa ule uchafuzi... HISTORIA INAONESHA HAM NA YAPHET WOTE WALIKUJA KUZAA MAJITU (GIANTS) KWENYE VIZAZI VYAO, LAKINI MUNGU ALIMHIFADHI SHEM NA HISTORIA INAONESHA VIZAZI VYAKE HAVIKUWA NA MAJITU, ILI KRISTO APITIE HAPO (Najua ni wachache wameelewa hapa, nitayafafanua katika masomo yajayo)
(mwl proo)

🧨 Kesi zote za Yusufu, Musa, Yesu Shetani akikuwa anaweka mpango wa kuangamiza, Mungu akautumia mpango huohuo kuokoa.

☄ Falme na Mamlaka zina uwezo wa kuweka mtu awe mtawala juu ya eneo (dominion and territory), kwa makusudi fulani ya Shetani.

*_"Yeye hubadili majira na nyakati; huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa;"_*
(Danieli 2:21)

Ni ukweli usiopingika, Mungu ndiye anayeweka tawala na falme za kutawala wanadamu wengine (Warumi 13:1ff), Lakini ni ukweli wa Biblia pia falme na mamlaka za giza, zinaweza kuweka viongozi/watawala juu ya eneo fulani la dunia kwa makusudi ya Shetani.

*NDIO MAANA WATU WA ROHONI, HAWAPASWI KUWA WASHABIKI WA KISIASA MAANA USHABIKI UTAWAONDOLEA KUYAJUA MAKUSUDIO YA MILELE YA MUNGU JUU YA WATAWALA WANAOPASWA KUWEPO. TUNAPOLEKEA KWENYE UCHAGUZI WATU WA ROHONI WANAPASWA KUOMBA MAANA, SHETANI ANAWEZA KUWEKA MTU WAKE (BWANA MGUMU) ILI AWEZE KU-TORTURE KANISA NA WATU WENGINE KWA MKONO MZITO, MKIKAA KISHABIKI HAMWEZI GUNDUA HILO, NA MTAACHA KUOMBA MKIHISI KILA ANAYEPITA AMEWEKWA NA MUNGU.

(Danieli 10 )
------------
*20 Ndipo akasema, Je! Unajua sababu hata nikakujia? Na sasa nitarudi ili nipigane na mkuu wa Uajemi; nami nitakapotoka huku, tazama, mkuu wa Uyunani atakuja.*
*21 Lakini nitakuambia yaliyoandikwa katika maandiko ya kweli; wala hapana anisaidiaye juu ya hao ila huyo Mikaeli, mkuu wenu.*

☄ Falme na Mamlaka za giza, zinaamua eneo husika la chini ya Dunia, liweje kiroho, kiuchumi, kisiasa, kidini n.k... Zilifunika eneo kwa giza la umaskini, hata kama hilo eneo litapokea misaada toka Benki ya Dunia, litabaki na umaskini wake mpaka watu wa nuru waliondoe lile giza kwanza. Kuna maeneo yana machafuko ya kisiasa miaka nenda rudi, zitatajwa sababu nyingi na wanaharakati ila sababu moja watakayoiacha ndioya kweli, kwamba falme na mamlaka za eneo hilo zimeachilia spirit of political instability... UN itapoteza resources zake mpaka siku ya unyakuo, shida iko rohoni... Mambo yanayoendelea EUROPE kwa sasa ni kazi za falme na mamlaka, nimeona picha za makanisa yanauzwa (Church Buildings For Sale) 💒⛪🏛

☄ Watu wenye vifungo vigumu zaidi ni wale ambao wako *initiated* kwenye hizi falme na mamlaka. Bila shaka umewahi sikia wanawake/mabinti kadhaa wakisema nilienda kuzimu 👩🏾👩🏾‍🦰👱🏾‍♀ nikafanywa kuwa malkia 👸🏾👸🏾... Sasa swali linaweza kuwa malkia wanakuwa wangapi huko kuzimu? Hawa watu hata kama walikutana na mkuu aliyejitaja kama Lusifa, kiukweli wanakuwa wapo tu kwenye moja ya falme na mamlaka (Kingdoms and Principalities), vifungo vya ambaye yuko initiated kwenye ngazi hii ya pili toka kwa shetani, inaweza kuhitaji nguvu kubwa zaidi katika kumfungua kuliko ambaye yuko possessed na mapepo. Mtu akiwa initiated kwa falme na mamlaka anakuwa ni wakala wa hizo nguvu ni tofauti na mtu aliyepagawa pepo kwa kawaida.

☄ Falme na Mamlaka kwa kuwa ni ngazi ya juu sana, inatawala eneo kubwa la uso wa nchi. Chini yao kuna wakuu wa giza hili (au wakuu wa anga). Rejea chati iliyo katika somo langu la *VITA VYA ROHONI* hizi ngazi za chini zinawezeshwa na kupokea maagizo toka nguvu ya juu zaidi... Vyote vinatimiza makusudi ya moyo wa Shetani... Waamini ambao wana maarifa kamili ya ulimwengu wa roho ndio jamii pekee ya wanadamu yenye uwezo wa kushughulikia hizi ngome zote.  Kuna wakati nilisikia Mwl Christopher Mwakasege akisema, *"Kuna maeneo ukienda usianze kusema nakemea mapepo yote  yahame hapa, kwamba kuna sehemu yapo kihalali kabisa"*, hiki kitu ni cha ufahamu wa juu ambacho wasiozingatia maarifa hawawezi kuelewa.

KUNA MAENEO MNAWEZA MKAENDA KIHUDUMA, MKAONA MAMBO MAGUMU TU, MNASHAMBULIWA NINYI NA VITU VYENU. KUMBE MKUU WA ANGA WA ENEO HILO AMEFANYA VITA NANYI HAMSTUKI (MATHAYO 12:29), USIDHANI KWAMBA HIZI FALME NA MAMLAKA HAZINA NGUVU KABISA. MUNGU YUKO SYSTEMATIC, ALIWAUMBA NA NGUVU NA UWEZO, NA WALIPOASI HAKUWANYANG'ANYA NGUVU WALA ULE UWEZO (i.e, THE FALLEN ANGELS POSSESS GOD'S POWER BUT THEY USE IT FOR EVIL PURPOSES, AND THUS MAKES POWER OF LIGHT TO BE POWERS OF DARKNESS). MKISHAMBULIWA KIROHO MNAWEZA KUDHURIKA KIROHO, MKADHURIKA MIILI YENU, AU PHYSICAL ASSETS, MAGARI, VYOMBO VYA MUZIKI, MAJENGO, HATA MIFUGO INAWEZA KUPATA SHIDA IKIWA NI KIASHIRIA KUWA MKUU WA ANGA AMEFANYA VITA NANYI NA KUNA MAHALI AMEWASHINDA. KAMA MTAFANYA VITA VYA ROHONI NA KUMSHINDA KABISA MKUU WA GIZA NA MAJESHI YA PEPO, BASI ANAWEZA KUTUMIA HUMAN-AGENCIES KUJA KULETA HATA VURUGU ZA KAWAIDA TU AMBAZO SIO ZA KUKEMEWA BALI KUSHUGHULIKIWA KWA HATUA STAHIKI BAADA YA KUOMBA. HAPA WAZOEVU WA MAMBO YA KIROHO WATASAIDIA ZAIDI, MAANA  MNAWEZA TUPIWA ROHO YA CONFUSION, MKAANZA KUSHINDANA KWENYE MAMBO YA KIJINGA TU, MKAKATU MMEBADILISHIWA FOCUS NA TARGET (mwl proo).

*❹ YESU KRISTO AMEKITI KUUMENI MWA KITI CHA UKUU MBINGUNI, PAMOJA NA WOTE WALIOMWAMINI*

Ufunuo 5:9-10
1Kor 15:24-28
Kolosai 2:10, 15, 1:16
Efeso 1:21, 2:6
Somo hili limekupa kutambua kuwa kuna falme na mamlaka za giza rohoni.... Kuba Ufalme, mamlaka, nguvu, usultani. kuna majina yenye nguvu, kuna vitu vya enzi.... LAKINI YUPO YESU KRISTO ALIYEINULIWA JUU YA KILA NGUVU, KILA JINA, KILA UFALME, KILA USULTANI.... ALIPOKETISHWA YEYE AMEKETI NA KILA MWAMINI KWA JINSI YA ROHO

☄ Mtu anapomwamini Yesu kabisa kabisa na kuokolewa, ananyofolewa kule kwenye ufalme wa giza (Kolosai 1:13), wanakofungiwa wasioamini wote. Tukio la Yeye kuketishwa mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha ukuu pamoja na Kristo linafanyika mara moja. Mtu akiamini na uchanga wake huo, anakuwa ameketishwa juu sana....(Far above ) kuliko hizo falme kuliko mamlaka za giza, kuliko wakuu wa giza, kuliko majeshi ya pepo...

Mwaka 2004, nilihudhuria ibada moja ya saa ya maajabu kwa Askofu Kakobe... Aliita mbele watu ambao kwa mara ya kwanza wanataka kumwamini Yesu awe Mwokozi na Bwana... Kisha baada ya hapo, akafanya maombezi ambayo pepo wachafu walidhihirika kwa wengi... Alipata ufunuo kwamba pepo hao wanapswa kutolewa na waamini wapya waliokata shauri muda huo huo...Na kila mwomgofu mpya alitoa pepo siku yake ya kwanza, hata hawakuwa wamejua namna nzuri ya kuomba. Nakumbuka pepo mmoja alikuwa akinguruma kama simba 🦁 akijisema kuwa yeye ni pepo-simba, hawezi kutolewa na mwongofu mpya,akamwambia Kakobe "mimi unitoe wewe mwenyewe, na si hawa".... Lakini ili kuthibitisha neno la kweli katika ufunuo, akaitwa mwamini wa siku hiyo, ambaye bado hajajua hata mambo ya ufalme huu, lakini ameamua kumwamini Yesu, na jina la Yesu likafanya kazi yake sawa-sawa.

*☄ NIWEKE SAWA JAMBO MOJA HAPO. KUKETISHWA NA KRISTO JUU SANA KULIKO FALME NA MAMLAKA, KULIKO USULTANI NA NGUVU NA MAJINA YOTE YATAJWAYO, NI TOFAUTI NA KU-OPERATE AU KUTENDA KAZI KWA MAMLAKA NA MADARAKA MAKAMILIFU YA KRISTO. MTU ANAWEZA KETISHWA NA KRISTO NA AKABABAISHWA VIPEPO VIDOGO TU. MTU AKISHAAMINI, LAZIMA AKAE KATIKA UTAKASO (1THES 4:7), LAZIMA AUKULIE HUO WOKOVU (1PETRO 2:2) KWA MAZIWA YASIYOGHOSHIWA, LAZIMA APATE NENO LA KWELI NA MAARIFA YA ROHONI ILI KUMFANYA IMARA AWEZE KU-OPARATE KAMA *MFALME NA KUHANI* MWENYE KUTAWALA PAMOJA NA KRISTO.

Tukutane katika somo lijalo

*Mwl Proo*
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

Saturday, July 20, 2019

SUPERNATURAL LIFE

*LIVE A NATURAL LIFE SUPERNATURALLY*
_Ishi maisha ya asili kwa namna isiyo ya asili_

*ʍաӀ Թɾօօ*
*0762879363*

Shalom Aleichem!
Karibu katika kujifunza kweli ya neno la Mungu, ili nguvu iliyo katika neno hai la Mungu ibadilishe maisha yetu kwa Jina la Yesu Kristo aliye Mwokozi na Bwana.

*🌈 MALENGO YA SOMO*

*❶ Kuwawezesha watu wa Mungu (waamini) waishi maisha ya kiwango kama watu wa rohoni.*

🧬 Tumechoka kuwa na wanaoshindwa kila eneo la maisha, elimu, biashara, huduma etc
🧬 Waamini ambao bado wana vifungo vya kipepo
🧬 Waamini ambao wanakaliwa na maradhi/magonjwa na kuishi kwa mfumo wa kitabibu badala ya kuishi kwa imani yao
🧬 Waamini ambao wana-Compromize wokovu wa Yesu wenye gharama kubwa, kwa sababu ya ugumu wa maisha. (Wapo ambao walijitahidi kulinda enzi zao kwa muda, mambo yalipokuwa magumu zaidi wakakubali kufanya mambo ambayo walijua kabisa hapa naachana na Mungu, ila compromize ililetwa na ugumu wa maisha..
🧬 Tumechoka kuwa waamini wanaorushwa na upepo wa kila elimu, mpaka wanajikuta wamejiingiza kwa manabii tapeli na feki, wakaharibikiwa ndoa zao, wakaharibikiwa maisha yao ya kiroho.

🧬 Tumechoka kuwa na wakristo tegemezi, waliofikia viwango vya kuwalipa watu pesa wawaombee, akitaka kulala anafoadi meseji kwa mtume wa mitandaoni kwanza, ndipo aamini anaweza lala salama, kila anachoota ni mpaka afoadi kwa social media kuomba msaada, utoto huu mpaka lini??

*❷ Hizi zama za mwisho, waamini wasio na ujuzi, waliolishwa dini, hawaishi wala kuenenda kwa Roho (Galatia 5:25), hawatakuwa na impact yoyote. Hivyo kwa masomo haya ya sasa, nipo kumwandalia BWANA watenda kazi (1Korintho 12:6, Math 9:37).*
_mwlproo_

*🌈 KWA NINI MAISHA YA ASILI UYAISHI KWA NAMNA ISIYO YA ASILI*
Zaburi 115:16, Yohana 15:19, Filip 3:20,  Ebrania 6:5

🧨Maandiko hayo juu yanatuundia *equation* muhimu sana. Mbingu ni mbingu za Bwana bali nchi, amewapa wanadamu, tena anasema ninyi si ulimwengu, kisha anasema wenyeji wetu (our citizenship) uko mbinguni, kisha anasema katika Ebrania 6 kuwa mtu anaweza kuishi katika dunia hii, lakini akaonja nguvu za zamani zijazo (eternity is cousin to supernaturality)... Na sisi waamini tumeitwa kuanza kuyaonja hayo yote tukiwa bado kwa hii planet earth 🌍. Hivyo maisha haya tuyaishiyo sasa duniani ingawa yako natural, but we are supposed to live supernaturally, kama tunataka kufikia kwenye standard ya kutembea na Mungu.

🧨 Mwanadamu, yuko na Mwili, Nafsi, na Roho (Mwili uliwekwa na Mungu for Naturals (bound to nature), Nafsi ni driving force (eneo la reflection), lakini roho za wanadamu ni za kiroho, sio za asili ya dunia asili ya roho zetu ni rohoni i.e., mbinguni (Enoch 15:8-9), So to say, our spirits are bound to Supernaturality (Supernaturals/Spirituality)... Hakuna namna mwanadamu  mwenye roho ndani yake atafikia kiwango cha maisha ya kiroho cha kutembea na Mungu kama hataishi na kuenenda kama mtu wa rohoni (1Korintho 2:14-15, Galatia 5:25).

🧨 Unalazimika kuishi kwa jinsi isiyo ya asili maisha haya ya asili kwa sababu, vitu halisi vyote viko rohoni, huku nje (in the physical) ni vivuli tu, ukishugulika na vivuli mwishoni utajikuta umechoka na haukufanya kitu chochote cha maana. Mambo yote yanaanzia rohoni, ili kufanya chochote cha kuathiri huku mwilini (affecting changes in the physical) sharti hayo mabadiliko uyasababishe rohoni, then huku nje yatatokea tu hata kama utakuwa umelala fofofo. Unataka kuifuta ajali iliyoko mbele, ifute rohoni haitatokea mwilini. Unataka kufuta kifo alichoandikiwa mtu na adui, kifute rohoni, hatakufa huku nje. Unataka kumbadilisha mume mlevi 🍻🍺? kwa maombi, mbadilishe rohoni, huku nje ataacha, ndivyo ilivyo kwa mambo yote, ukiweza kuli-adjust jambo rohoni, litatokea huku nje likiwa na hizo adjustments, maana dunia inazunguka huku nje (rotation/revolution) huku iki-comfrim na ku-comform mambo ambayo yalikwisha tokea rohoni. Yesu Kristo kama Mwanakondoo wa Mungu 🐑, alikwisha chinjwa kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu, kwa ajili ya dhambi zetu, lakini huku nje kulikuwa kunasubiri majira (Galatia 4:4), muda ulipofika likatukia jambo ambalo lilikwisha fanyika rohoni milenia nyingi za tangu zamani tangu milele.
_mwlproo_

*🌈 NI KWA NAMNA GANI MTU ANAWEZA KUYAISHI MAISHA UA ASILI KWA NAMNA ISIYO YA ASILI*

*🧨 Ubatizo wa Roho Mtakatifu, na kuutunza moto usizime (Baptism of the Holy Spirit, and keeping the fire unquenched)*
🕊🕊🕊🕊🔥🔥🔥🔥
Joel 2:28, 1Thes 5:19, Walawi 6:13, Yohana 14:17

💥 Holy Spirit should be very alive inside you... Mimi mwalimu wa Jiografia kitaaluma, nafundisha kuhusu *Volcanoes* zinaweza kuwa katika hali tatu za kimsingi 1. Active state (Alive/Hai),  2. Dormant state (Sleeping/Inakuwa katika usingizi) na 3. Extinct state katika kufa, Volcano yenye hali ya 1 iko hai, inalipuka muda wowote tu, hiyo ya 2 imelala hailipuki, ila imewahi lipuka muda si mrefu, na hiyo ya tatu imekufa, ina historia ya kulipuka, ila haitazamiwi kulipuka tena. Mwamini anayeweza kuyaishi maisha ya asili kwa jinsi isiyo ya asili, ```SHARTI AWE NA ROHO WA KRISTO NDANI YAKE AMBAYE NI ACTIVE & ALIVE```

*🧨 Orientation to the spiritual realms (spirituality)*
Kutambulishwa/kujuzwa mambo ya rohoni (Getting exposed to spirituals)

🧬 Mtu anaweza kuwa-oriented rohoni na
👉🏾 Ufalme wa nuru (Kingdom of light/Holy Spirit)

👉🏾 Ufalme wa giza (Kingdom of darkness )
#Shetani
#Falme na Mamlaka
#Pepo wabaya (Demons)

*SWALI*

Who introduced/oriented you to spirituals????????

🧬 Roho Mtakatifu yuko *commissioned* kututambulisha *_orienting us_* rohoni, kufanya tuyajue ya rohoni, tujulikane rohoni na kutufanye tu-operate rohoni. Usishangae rohoni tuko na badge au IDs ambazo viumbe vya kiroho vinatuona navyo na kusalimu amri. Waulize wana wa Skewa (Mdo 19), walipokemea pepo wabaya, wale pepo walisema *YESU TUNAMJUA, NA PAULO TUNAMFAHAMU*, NINYI NI AKINA NANI? WE DON'T SEE YOUR IDs KABISA, YOU KNOW THE STORY BILA SHAKA.
Yohana 16:13, 1Kor 2:10-13, Isaya 48:6.

🔥 Mtu akiishabatizwa kwa Roho Mtakatifu, na kujifunza utendaji wake, ghafla anaanza kuona mambo ya rohoni, anaona mambo yake, ya wengine, ya nchi na kadhalika Atayaona ya kiMungu hata ya Shetani atayaona, maana amekuwa oriented to spirituality mahali ambako Mungu (the spirit-God) yuko, na mahali ambako shetani (the spirit-devil) yuko, usisahau hili, Ibilisi naye ni roho, hivyo usijistress sana na vitu vya nje when dealing with him, ukawa bize kumwagia chumvi ya upako kwenye nyumba yako kumkinga shetani, wakati yeye kama roho ameyatawala maisha yako kwa dhambi (tabia ambazo yeye ni baba kwazo), unamfukuza shetani kwenye biashara kwa stika ya upako wa nabii, ila yeye amejaa moyoni mwako.

🧬 Lakini mtu anaweza kuwa spiritual-oriented kwa kutambulishwa rohoni/kiroho na roho zingine

*🌈 TOFAUTI YA MTU ALIYETAMBULISHWA ROHONI NA ROHO WA MUNGU AU ROHO ZINGINE ZA KIGENI*

🧨 Kwa aliyetambulishwa na Roho wa Mungu, darasa litaanza baada ya Ubatizo wa Roho Mtakatifu (In some few & rare cases, mtu anaweza kutambulishwa rohoni akiwa bado hajabatizwa kwa Roho, then ubatizo ukija, unakuja kumweka sawa. Unajua hata Sauli aliyeitwa Paulo alikuwa oriented to spirituals akiwa hajabatizwa na Roho bado. Kitendo cha yeye kumsikia Yesu, katika ile nuru ambayo rafikize hawakusikia (Mdo 9:1-20) ni tendo la orientation to spirituality. Ubatizo katika roho ulikuja baadae kumweka sawa katika mambo ya kiroho. Lakini masikio yale yaliyofunguliwa rohoni pale njiani kuelekea Dameski 👂🏽👂🏽 angeweza kuendelea kusikia vitu vya rohoni iwe vya Mungu au vya Shetani, maana tayari yuko spiritually-oriented to spirituals.

*NB*
```Mtu anaweza kuwa alikuwa nabii wa kweli wa Mungu, kisha akaharibu njia zake, akakataliwa na BWANA, na bado vipawa vya kiroho vikaendelea kufanya kazi, sio kwa sababu ya his/her uprightness kwa Mungu, No! alikwisha kuwa spiritually-oriented to spirituals na hivyo macho yale-yale, masikio  yale-yale, ngozi ile-ile, ufahamu ule-ule bado unaweza ku-sense na kuopereti kule rohoni. Na wengine wakiharibu systems zinaBlock, anatambulishwa upya rohoni na nguvu za kinyume na Mungu ili kupoteza na kukengeusha wengi```

🧨 Kama ni Roho Mtakatifu amekutambulisha (orient) rohoni, Woga+Kushanga na hali ya Sintofahamu (state of uncertainty) itakuwa ni ya muda mfupi sana (will be temporary)... ATAKUSAIDIA NA KUKUKOMAZA

*NA ISHARA/KIASHIRIA KIKUBWA CHA KUONESHA ALIYEKUTAMBULISHA ROHONI NI ROHO MTAKATIFU, NI UHURU (LIBERTY/AUTONOMOUS FREEDOM) MAANA PALIPO NA ROHO WA BWANA PANA UHURU (2KOR 3:17), NA MWANA AKIWAWEKA HURU MTAKUWA HURU KWELI-KWELI (YOHANA 8:36, 32).*

🧨 Kiashiria kibubwa kwamba kuna roho za kigeni *strange spirits* zimeku-orient rohoni, ni Woga, Wasiwasi, Utisho, Kukosa amani, Sintofahamu *endless dilemma and confusion* yaani kuchanganyikiwa kunakuwa permanent. Labda kama umejitoa kwa moyo kuwa wakala au machawi etc haya hayataonekana maana utakuwa umevikwa roho ya ibilisi, itakayokufanya yote uone ya kawaida tu, hata ukiambiwa utafune nyama za watu.

*KIASHIRIA KIKUU CHA KWAMBA ROHO ZA KIGENI NDIZO ZIMEKUPA ORIENTATION KATIKA ROHO, HUTAKUWA HURU!*

``` Bila shaka mmekwisha wahi ona mtu sio mwamini (hajaokoka), lakini anaona vitu vya rohoni, na akisema vinatokea kweli. Bila shaka mmekwisha wahi ona kuna watu hawajisumbui hata na maombi na kukaa katika utakaso, ila wanaona katika roho, na wamejawa na vitu vya kiroho. Huenda ni dhaifu mno kiroho na mazoezi ya kiroho, wala havipigi vita vizuri vile vya imani, lakini mkikutana kwa sala yeye ndiye anatoa unabii wa kweli. LAKINI MKIMCHUNGUZA HUYU MTU KWA MAISHA YAKE, HAYUKO HURU, ANAWATABIRIA VITU VYA KWELI KWA FELLOWSHIP LAKINI MKIANGALIA MAISHA YAKE HAYANA MUNGU, ANAHITAJI KUSAIDIWA SANA KWA NJIA YA BWANA. HUYU MTU AMETAMBULISHWA ROHONI NA ROHO ZA KIGENI.```

_*🔥 Kama unaona upo kwa hali hii, taarifa utakazokuwa unazipata rohoni ni za kweli, lakini wewe mtoa taarifa hauna uhuru utokoa kwa Mwana wa Mungu*_

⚔ LORD'S WINNOWING FORK WILL BE SENT (PEPETO LA BWANA LITATUMWA, UKIFUNGUA MOYO WAKO, MUNGU ATAKUSAIDIA, TAFUTA MSAADA KWA WATUMISHI WA MUNGU).

⚔ SOME PEOPLE ARE TO BE DISCONNECTED FROM THESE STRANGE SPIRITS, YOU CANNOT PERFORM WELL WITH GUESTS INSIDE YOU.

⚔ HIZI ROHO ZITAFANYA UJIONE UPO NA MUNGU, THEN BAADA YA MUDA ZINAKUPANDIKIZIA VIFUNGO VIBAYA SANA, ILI USIJE UKA-EXCEL KWA LOLOTE, MAANA MWIVI HAJI ILA...........(Yohana 10:10).
_mwlproo_

*🌈 FAIDA ZA KUWA SPIRITUAL-CONSCIOUS PERSON (SUPERNATURAL LIVING)*
🧨 Roho yako itafufuliwa (rectified, rejuvenated)
Isaya 57:15, roho za wanadamu hazifi (mathayo 10:28 imezingatiwa, kuwa kuua mwili na roho ni maana tofauti), lakini roho zinawezwa kupigwa usingizi wa milele, zisiwe *SENSITIVE TO SPIRITUALS* 
Hivyo, mtu akiwa oriented to spirituals na Roho wa Kweli, ataweza kuishi maximized life to full capacity...Hatukuitwa kuishi maisha kikawaida tu.. Mtu wa rohoni kwa kuwa anamfuata Yesu aliye *master of  the nature* anaweza pindua chochote cha asili hata yale ambayo yako inherent au genetically-transferred toka kwa vizazi vya kwenu au systems za serikali. Mfano huenda kwenu wote wanajifungua operations na unaambiwa hiyo iko hivyo mpaka kwa shangazi zako, hiyo issue sio mara zote inakuwa ni uchawi but it has to do with nature tu, kwamba genetically, cervical paths za uzao wenu ziko namna hiyo... mtu wa rohoni anao uwezo kubadili lolote ambalo ni la nature akitaka na akiwa spiritual-oriented.

HAPA KUNA SHUHUDA NYINGI MNO ZA NAMNA WATU AMBAO SPIRITUALLY WAKO SENSITIVE, wameweza kuvuka maeneo mengi ambapo nature imesema NO! mimi hapa mwandishi ni shuhuda wa kwanza kwa hili.

🧨 Utakuwa chombo kinachofaa kutumiwa na Bwana kwa kazi yoyote mahali popote (You'll be fit for Kingdom's ministry)

🧨 Bwana atakuamini. Ni mambo mawili tofauti kumwamini Mungu na kuaminiwa na Mungu. Ukiisha kumwamini Mungu, panda viwango ufikie pa kuaminiwa na Mungu, ili kwamba Mungu akijua mahali wewe upo basi anaamini mambo hayataharibika... atajisemea moyoni, *_" Proo yuko pale"_* kwa namna ile-ile ya kujigamba kwa shetani, umemwona huyo Ayubu? 🤓... Sasa mtu hayuko spiritual-oriented anakuwa hajasimika mizizi yake mbali sana, dakika yoyote kufumba na kufumbua mara ashaanguka kwenye zinaa, yupo juu-juu tu kama mbegu zilizoanguka kwenye mwamba.. Mungu akusaidie unapoanza kuchukua hatua mpya ya kiroho, kwa Jina Kuu la Kristo Yesu... Amen,  nimeomba kwa ajili yako...

Mྂwྂlྂ Pྂrྂoྂoྂ
*+255762879363*

alltruth5ministries@gmail.com