*KUITULIZA MIOYO MBELE ZA BWANA*
_(Undivided Attention Before The LORD)_
*M͟͟w͟͟l͟͟ P͟͟r͟͟o͟͟o͟͟*
_0762879363_
Salamu nyingi kwa Jina la Bwana na Mwokozi Yesu. Ndugu msomaji imempendeza Mungu kwa majira haya ya siku za mwisho kukuandikia haya. *_Kwa kuwa Bwana hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira;_*
(1 Nyakati 28:9 ). Mapema sana mwaka jana (2018), nikiwa natoka kanisani kwenye maombi ya jioni, moyoni mwangu kukawa na namna fulani ya kusemeshwa, kuwa watu wengi huwa hawaombi. Nikaanza kuwanza huwa hawaombi kwa namna gani?. Hapo ndipo Mungu akanikumbusha andiko la msingi nilikuwa nalijua tayari kitambo ila sio kwa ufunuo huu.
*_"Katika hili tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, nasi tutaituliza mioyo yetu mbele zake,"_*
(1 Yohana 3:19 SUV)
*This is how we know that we belong to the truth and how we set our hearts at rest in his presence (Our hearts will be still in His presence)* 1 John 3:19 NIV
Mjadala huu haukuisha ndani yangu mpaka nikapata somo. Na nikaelewa kuwa tuna Wakristo wengi nyakati hizi za mwisho, hawaombi wala hawaabudu maana mioyo yao haijatulizwa mbele za BWANA (set hearts at rest in His presence/undivided attention when worshipping/praying). Mwanadamu sio roho peke yake, bali ni roho, nafsi na mwili. Mtu anaweza kuomba kwa akili zilizomo ndani ya nafsi au akaomba kwa mwili (kinywa 👄👅) kwa sababu the spirit-man aliunganishwa na mwili wa nje ili kumwezesha mtu kuomba hasa wakati wa kunena kwa lugha zingine, lakini haya yanaweza yakaendelea wakati moyo (nafsi) haiko kwa ushirika na maombi au maabudu hayo.
Ni muhimu kukumbuka Mungu anautaka moyo/nafsi (mawazo na fikra zake), anasema katika Mithali 23:26, *'Mwanangu nipe moyo wako'*. Jambo la ajabu sana mtu anaweza akaomba saa moja au zaidi akiwa hajautuliza moyo wake mbele za Mungu (divided attention), hii inapelekea watu kutofika vilindini, wanachodhani wamepokea kwa Bwana ni *0.0001%* ya kilichokusudiwa na Mungu. Ugonjwa huu unaweza kumkuta mkristo yeyote (clergy/layman). Siku najifunza jambo hili nikagundua mtu anaweza kuanza maombi lakini mawazo ya moyo wake yamerudi ofisini anapanga mikakati ya kazi mwanzo wa maombi mpaka mwisho, mwanamke anaweza kuanza maombi lakini akili na mawazo ya moyo wake yapo saluni, anashiriki kikao na mjadala wa saluni mwanzo mpaka mwisho kwa mawazo ya moyo tu, mtu ni dereva anaomba au anaabudu huku akipanga apite njia ipi atumie spidi ipi. akwepe vipi traffic polices, hivyo mtaona mdomoni anafuliza kuomba (spontaneously) kumbe hayuko hata. Kuna watumishi wachache kwa sababu ya ratiba nyingi za kuhudumu kwa kuhubiri na kufundisha basi wamefanikiwa kidogo, muda anaomba akilini mwake anahubiri/anapanga points za kufundisha/anafanya huduma kwa fikra za nafsini. Hata wao hawajafanikiwa kuituliza mioyo mbele za Mungu. Kuomba kwa roho na kuomba kwa akili vyote vinapaswa kuwa sambamba ingawa ratios ndizo zitakuwa tofauti, kuomba kwa roho kuwe na nafasi kubwa zaidi ya 90% ya maombi yote.
✍🏾Si vibaya kuomba kwa kutembea-tembea, haswa ukigundua kuna dalili ya kuwindwa na usingizi nawe una targets zako za kutumia saa kadhaa kwa kuomba. Lakini asilimia kubwa ya wanaoomba kwa njia hii pekee ukabiliwa na ugonjwa sugu wa kuomba kwa mwili (👅👄) au kwa lugha za roho lakini mawazo ya nafsi yakiwa kwingine, yaani anakuwa na *divided attention*, anaomba anatembea akiwa amefungua macho ili kukwepa kujigongeza mahali (kumbuka hakuna andiko linaloelekeza ufunike macho muda unaomba, ila ni katika kutafuta moyo usihame, sasa hakuna maana ya kufnika macho kama moyo haupo), huku muda huo itampasa aone mambo mageni, ataona yanayoendelea nje na kutwaa usikivu/umakini (attention ya kiroho), atake asitake ataanza kujadili mambo kwa moyo wake huku kinywa kikiendelea kuomba, lakini mawazo ya moyo, ambayo ndio uhitaji mkubwa wa Mungu, yatahamishwa katika mambo mengine, anaweza kuanza kujadili juu mahudhurio hafifu kanisani, mapambo ambayo hayako sawa kanisani n.k n.k. Ndugu msomaji, Mungu atusaidie sana kwa sababu hii case iko serious, ndio maana watu wanatoka mbele za Mungu baada ya kuabudu au kuomba wakiwa hawana kitu kipya, hawana ufunuo mpya, wako tu na vitu vya kawaida maana hawakufika vilindini. Wengi wanaofundisha kwenye nyumba za ibada au hata mitandaoni, wanayoyafundisha mengi ni Basic Christian Doctrines, sio mambo yaliyotokana na ufunuo mkubwa baada ya kutuliza moyo kwa Bwana. Ni wachache sana wanaCapture hiyo frequency na kutoka na ufunuo mkubwa wa kiMungu, hata akifundisha common topics kama za maombi, utakatifu, uaminifu, siku za mwisho, utoaji, imani n.k haitakuwa kama basic doctrine bali itabeba ufunuo mkubwa wa kiMungu wa kuwavusha watu kulingana majira waliyo nayo. Nyakati hizi si ajabu mtu karespond meseji ya WhatsApp 👩🏽💻 📱📲👨🏽💻 akiwa hajanyamaza kuomba mdomoni 👄👅. Si ajabu mtu akaendelea kuhudumu madhabhuni akiwa ame-Go Live na anataka comments za fans zote azichungulie........ Masumbufu ya maisha yamejaza mambo mengi kwenye mioyo na kuifanya mioyo kutoweza kuwa attentive au kutulia katika uwepo wa Mungu. (Nitayaongea hayo kwa kina katika somo lijalo liitwalo *"MAPITO YA ZAMANI"*). Kuna watu wanatumika kwa karama za ufunuo, wanaweza kutuliza mioyo kwa sehemu kidogo sana kwa sababu ya nature ya hizi karama, hivyo anayaona mambo ya rohoni kwa haraka sana, ila kukosekana kwa *undivided attention* wanayoyaona hawayaelewi kwa wakati ili kusaidia, sababu kubwa ni hii ya kutoweza kuituliza mioyo mbele zake, na kukosa ufahamu wa kutosha (roho ya ufahamu ina-operate kwa kiwango cha chini sana), yote ni matokeo ya kutoituliza mioyo mbele za BWANA ambaye ni Mungu wa maarifa.
(Isaya 42 )
------------
*19 Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? Au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani? Naam, kipofu kama mtumishi wa Bwana?*
*20 Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake ya wazi, lakini hasikii.*
👆🏽👆🏽👆🏽
Nilikuwa mahali fulani muda wa maombezi mhubiri akaoneshwa mwezi 🌘 kwa macho ya kiroho.... alitumia muda mwingi sana kuelewa kuwa Roho Mtakatifu anamwelekeza ahudumia wadada wenye disorders za Menstrual Periods, kumbuka lugha za roho huja zikiwa *encoded* mara nyingi zaidi, ili kung'amua kwa wepesi alama iliyotumika ina maana gani ni mpaka kuwe na undivided attention na ufahamu wa rohoni wa kutosha.
Mungu hayuko mbali, wala uwepo haujaadimika kama watu wanavyofikiri, ila watu wanakosa mguso kwa kukosa ujuzi wa kuutuliza moyo mbele za Bwana. Ni watu wachache sana wamejizoeza kukamata connection kwa kutuliza mioyo (full attention). Muda unaimba nyimbo za kuabudu kanisani, muda unaomba ukijizoeza kuwa *nia isiyogawanyika/undivided attention* you're likely to get connected na kufanya maombi na maabudu yako kuwa valid.
Usimsogelee Mungu kwa ibada na maombi ukiwa na haraka zako, utapata shida kushindana na mawazo ya moyo na ule utulivu wa kutuliza moyo kwa Mungu (Mhuburi 8:3a). Neno linasema usifanye haraka kuondoka mbele ya mfalme (Yesu ni mfalme wetu, don't be hasty, don't be in a hurry to leave His presence, but set yourself at rest in His presence). Kuna siku tulikuwa mahali tukifanya ibada ya nyumbani, wakasema jamani tufanye haraka haraka ili tuiwahi *tamthilia* fulani kwenye Televisheni, niliwaambia bora hata tusifanye ibada hiyo...... Mungu anautaka moyo, uliotulizwa mbele zake, ila kama unawaza kuiharakisha ibada ili uwahi vipindi vya Tv, kuwahi mchuano wa mpira timu yako pendwa sana inacheza, utampunja Mungu sana kwa kumweka kwenye foleni ya mambo ya kuyatekeleza.... Mungu anapaswa kuwa Mungu tu, na mioyoni mwetu kumtakasa Kristo (setting Him apart), kumpa special attention muda umeamua kusogea mbele zake.
*HATUA ZA MUHIMU KUCHUKUA ILI KUJIZOEZA KUTULIZA MOYO KWA BWANA*
1. Ni kufanya maombi mfululizo kumwomba BWANA kwa habari ya neno hili, kwamba Mungu nisaidie na unifundishe.
2. Anza kufanya mazoezi, ukiwa kwenye maombi kila unapogundua mawazo yanahamia kwingine unayarudisha na kuConcentrate kwenye maombi yako tu.... usiruhusu dakika nzima ya kuomba moyo unajadili kikao chake. Unaweza kuwa kuna jambo limekukamata moyo, mfano una tishio la kufukuzwa kazi, au nasomo, au kufukuzwa kwenye nyumba uliyopanga, mambo haya yakajirudisha kwenye maombi au muda wa maabudu, badala ya kushiriki vikao vya usuluhishi na mijadala kwa fikra/mawazo ya moyo, unaweza kuamua kujifunza kutupa chini kila fikra ijiinuayo, ili kupata utulivu usioingiliwa kabisa *uninterrupted mind for worship*, magumu yapo tu, ila amua kumpa attention Yeye aliye mkubwa kuliko hali mbaya zote na matatizo yote..... Ukifanikiwa hapo, ni rahisi sana kila unapotoka kwenye maombi au ibada za namna nyingine ukawa na majibu ya mambo yako mengi mno. Anza sasa kufanya hili zoezi ingia kwenye maombi ya saa nzima ukijitahidi kuibakiza attention yote kwenye kuomba tu...
3. Badilisha styles za maombi na ibada zisizo-support utulivu wa mawazo ya moyo... Kama ukigundua maombi mengi unayofanya ya jumla-jumla kanisani hayakupi kuutuliza moyo, basi hakikisha pamoja na hayo, uwe na ratiba zako binafsi za mahali pasipo na watu (solitary place), na ujizoeze kuomba au kumwabudu Mungu kwa moyo wote bila kugawanyika kimawazo (HILI LINAWEZEKANA). Kuna makanisa mengine hayatoi muda wa watu kuconcentrate mbele za BWANA, dakika za watu kuimimina mioyo kwa Mungu ni kidogo sana (1Sam 1:15), muda wote wa ibada ni matukio-tukio tu, wengi wanaondoka hawaja-enjoi ule utamu wa kumsogelea Mungu, vitu vinakimbizwa kimbizwa tu, mara Ooooh Praise Team imbeni kwa ufupi sana leo tuna mambo mengi mno, na ukute ni swala la mnada tu kanisani, lina-rob nafasi ya watu kumsogelea Mungu na kujipatia nafasi kwenye vilindi vya moyo wa Mungu.
Mimi ili kupata utulivu ninaoutaka kuna muda natafuta mazingira mazuri zaidi... Niko chuoni kwa sasa, hakuna mahali pa kuomba kwa kutulia sana kiasi cha moyo kutulizwa mbele za Mungu, nikisema niombee hostel dakika yoyote Room-mate atabisha hodi na kunitoa kwenye concentration yangu..... Sijayaruhusu mazingira yaniibie nafasi yangu, na hivyo nilitafuta cha kufanya, nikagundua kwenye viwanja vya michezo, usiku kuna kuwa na mazingira mazuri, yasiyoingiliwa na chochote, hakuna anayepita wala chochote kile cha kuweza kuniondoa mawazo...Hivyo nilipopata waza hilo basi najitahidi saa nane usiku niwe kwenye viwanja vya michezo, naomba kwa sauti ninayoitaka, muda wa kutosha, utulivu mkubwa wa kimwili na kiroho and so my heart remains still before God.
HILI NDILO NENO LA BWANA KWAKO.
Mwl Proo
0762879363
alltruth5ministries@gmail.com