Friday, August 3, 2018

ROHO YA MAZOEA

*🐠WAKRISTO WENGI KUNGIA MOTONI, KWA SABABU  YA ROHO YA MAZOEA🐠*                 

🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥

*_Hii ni baada ya kufika mbinguni, na kushuhudia ukumbi wanaoingia watakatifu, na kukuta ni wachache, wakati viti ni vingi, tena viko wazi. Wengi watataka kuingia lakini hawataweza.... (Mathayo 22:14, 7:13-14)._*

🔥🔥 Nakumbuka katika sehemu ya pili ya ushuhuda huu, niliandika kwamba; nilipoona idadi ya wanaoingia ni ndogo kuliko wingi wa watu wanaojiita wameokoka (yaani watu 7 kati ya 5,000), nilinilia na kuhoji kuwa mbona wachache hivi?😥. Pia nilipogundua kuwa wengi wa waliokufa tukidhani wameingia, kumbe hawakukidhi viwango vya kuingia, pia nilihoji wameenda wapi?🙇🏾‍♀.

🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥

Katika awamu hii, Mungu alitaka kunijibu wako wapi niliowatafuta. Ukweli ni kwamba katika mambo yote, jambo ambalo nilipiga magoti na kuomba lisitokee ni habari kwenda kuzimu 😢😢. Niliomba sana nisipelekwe huko, kulingana na moyo wangu kuogopa, baada ya kusikia kunavyotisha. Lakini wajua atakalo Bwana yeye atatenda kwa utukufu wake (Zaburi 115:3).

Ilikuwa zamu nyingine tena! Hakukuwa na mazingira ya mawasiliano kati yangu na mbinguni. Siku hiyo kulikuwa na kukumbushwa kwingi, kuwa mbona nimenyamaza sifanyi kitu kuhusu nilichoona? Mbona siwaambii watu juu ya maono haya?. Ni kweli nilikuwa kimya tangu nianze kuona, ni watu wa karibu tu na walioamini ndio nilijaribu kuwajulisha. Na nikajiambia kuwa nitafute pesa, niende redioni nikalipie kipindi kisha nishuhudie. Kumbe kwa kuwaza hayo, nilikuwa nachelewesha kusudi la Mungu. Kwa hiyo mazingira ya kupelekwa kuzimu, hayakuwa na maandalizi, na ninajua Bwana alijua sitakuwa tayari kwenda. Hivyo nilijikuta tu tayari nipo sehemu ya ajabu!. Haina uhai kabisa, ni rangi kama jangwa na hakuna nuru ya jua. Kiuhalisia panatisha tu japo sikuona chochote kwa hatua ya kwanza, niliona tu ukiwa umejaa pale na niko peke yangu!. Nilishaogopa mbona niko hapa? Ghafla ndio nikashangaa kuona nakusikia vilio vya ajabu kugeuka naona ni moto umetapakaa hata sikuona mwisho wake!. Tayari nikajua, niko sehemu nisiyoipenda kuliko zote, na sitaki kuendelea kutazama wala kujua. Ila ole wangu!, Nilichukua mikono yangu nikauficha uso wangu na macho nikafumba🙈. Sitaki kuona haya! Sitaki kuona haya!🤦🏽‍♀ ndicho kilikuwa kilio changu. Ndipo nikasikia sauti ikitoka juu tena, na mimi niko bondeni pakutisha. Sauti ilikuwa ya kutisha na kali, si kama siku zingine. Iliniambia kwa lugha ya kiroho ambayo sijawahi kuisikia duniani wala popote. Ajabu ni kwamba, nilikuwa naielewa vizuri ile sauti ilichomanisha!. Iliniambia, *_"Nimekuleta hapa uone watu wangu wanaishia huku, na wewe nimekutuma kwao ungali umenyamaza!"_*. Nilikuwa sina tena uwezo wa kuzuia macho, ila naona sasa moto umewashikilia watu, ndani kuna vilio vyakutisha! visivyovumilika!. Na sauti za watu wengi zilikuwa za Wakristo, kwani walikuwa  wakilia kwa lugha za kikristo. Wengine walimtaja Bwana, yaani unaweza kujua kuwa hawa wanaolia wengi walimjua Yesu, na wengi waliishi katika vipawa na karama zake (walitambulika hivyo)!. Sikuvumilia sana sauti ile iliponikemea, nilikuwa tayari moyo wangu umeyeyuka kwa toba, nikitamani nitolewe pale haraka na nijikute duniani, ili naanze kazi mara moja!.

NB:-
*MOTO ULE ULIKUWA NA UWEZO WA KUMRUSHA-RUSHA MTU KAMA MPIRA 🏀 🏉 ⛹️, UNAMPELEKA MPAKA CHINI SANA NA KUMWIBUA TENA JUU, INATISHA SANA*

🔥 Lakini kati ya wengi walio kule, ni kwa sababu ya *roho ya mazoea*. Walizoelea Ukristo wao, wakaishi bila badiliko hadi mauti ikawakuta. Kweli usifanye mchezo kuzimu hata kwa matembezi hapafai, ni sehemu ya kutisha! Ni makao ya mauti, mwenye uhai huwezi vumilia. Acha kuuchezea wokovu wako, utaangamia siku usiyodhani. Nilipotoka hapo, nilirudi nikiwa nimepata majibu kuwa kweli tusijifariji na jina la Ukristo. Tukumbuke ilivyoandikwa, *_"Si wote waniitao Bwana! Bwana!, watakaoingia katika ufalme wangu"_* (Mathayo 7:21).

Namshukuru sana Bwana Yesu, hakuniingiza ndani huko ninakosikia wengine huingia, naamini alisikia maombi yangu nilipoomba. Pia atakuwa anaujua moyo wangu ulivyo, kwani hakika mimi ni mwanamke wa machozi😭😭. Mara nyingi nalilia kanisa, hata ninapoona vitu tu vya kawaida vyaniumiza sana.
Nilirudishwa tena duniani nikiwa na picha hii ya kutisha! Nilipata shida sana kutwa nzima, mimi nateswa na zile picha za haya maono. Niliingiwa huruma sana juu ya wakristo wenzangu, hata tunapokuwa pamoja nawatazama kwa huruma nikisema, _"Bwana msaidie huyu asiende kule nilikoona"_. Na ilikuwa, nikisikia Mkristo kafa au mtu kafa, mimi nikienda msibani nahangaika, nitafuatilia kwa ukaribu kwa familia ya marehemu hata kama sina ukaribu nao. Na nitamani kujua hatua za mwisho za huyo mtu alipoondoka duniani, Je! aliondokaje?. Nikiambiwa aliumwa na akafa, maelezo yakaonyesha hakupata toba ya kweli, naanza kulia kwa uchungu, hata hao ndugu wa marehemu watanishangaa (kwa sababu si mhusika wa karibu, lakini siri ya moyo ni nzito najua tayari kaenda kwenye sehemu ile). Na ilipotokea nimeenda msibani, nikafuatilia habari, nikaambiwa mazingira ya kifo cha huyo mtu kilikuwa cha usafi na utakatifu, nilikuwa nashukuru nakupata amani. Nilikuwa natembea duniani lakini mawazo yangu nitofauti, na ninaweza lia peke yangu hata njiani. Nikiona binti kavaa vibaya  👙👗👖, naogopa kuwa akifa hivi alivyo ataenda kule 😥.  .Nilikuwa nikijitahidi kumsimamisha kila mtu, nikimwambia habari za Yesu, ili atubu asiende kule kuzimu. Nilikuwa nahubiri kwenye daladala, masokoni n.k nilikuwa na mzigo mzito! Nikimhurumia kila mtu hata mme wangu! Nikawa nashangaa watu wana amani tu, wanatembea, wanaangalia TV, Wanafurahi. Mimi nikaona kuwa hawajui hatari iliyoko mbele yao. Bwana wasaidie! 😪🙌🏾.

Nikafika mahala mzigo huu ukawa mzito kwangu😭😭. Nikapiga magoti nikalia kwa sauti kuu ndani yangu, "Bwana nihurumie, maisha haya nimagumu kwangu. Nisaidie niishi duniani kama wengine maana nateseka, sina amani muda wote ninapowaona wanadamu, hasa wenye dhambi!. Naumia, nitaishi mpaka lini nikiteseka! 😣 Mbona wenzangu wanaishi kawaida! Hawajali!. Mimi nawahubiria wengine wananicheka, na kunidhihaki!. Hali hii ilinichochochea sana kuhubiri mitaan nk. Ila badae Mungu alianza kunipunguzia mzigo kidogo; japo mpaka sasa sipendi kusikia mwizi kachomwa moto; mtu kauawa ovyo, au mkristo kafa kifo cha ghafla. Naumia, nakumbuka makali ya moto ule na sehemu ile mbaya yakutisha!! Kweli sitaki mwanadamu aende kule😭 usikubali kushindwa, jitahidi, nakulilia mtu wa Mungu 😭😭😭. Nakuombolezea usiende kule, Kristo hataki tupotee. Badili mwenendo wako, acha dhambi, mizaha, mazoea, nk. Maanisha katika wokovu wako.

Asanteni 🙏🏾, wenu Mchungaji Mariamartha C. Kailembo.
Mjumbe wa uamsho. Amka amka ewe ulalaye... (Efeso 5:14, Yona 1:6)

Mhariri: Mwl Proo