*VITA VYA ROHONI*
_(SPIRITUAL WARFARE)_
🔫⚔💣🗡🛡
By Mwl Proo
0762879363
©2011
Kwamba tumeokoka, haina maana tutakuwa mafundi wa kila aina ya ujuzi wa kiroho (Tunahitaji kufundishwa). Yako mambo ya kiroho ambayo ni ujuzi (Profession) maalum, haya utayajua tuu kama Roho Mtakatifu ameamua kukufundisha mwenyewe au kwa kufundishwa na watumishi ambao Mungu amewapaka mafuta kwa ujuzi huo. Mungu hatamfundisha kila mtu maarifa yote, maana sio wote wame-tune on kwenye frequencies za kufundishwa ujuzi (profession) fulani wa kiroho. Vita vya kiroho ni ujuzi maalum (Profession).
*Mambo ya Ujuzi (Experience)*
Mifano ya kibiblia kuhusu kweli hii, ni jinsi ambavyo watumishi wa Mungu walivyoweza kupata experience kwa kuona na kufunzwa na watumishi ambao wao walipata direct toka kwa Mungu. Mfano; Musa alifundishwa na Mungu (Zb. 103:7) moja kwa moja (direct revelation). Lakini Yoshua hakuwa na wakati na Mungu kama Musa, lakini alitumiwa kwa ishara kubwa kama ile ya kusimamisha jua (Yosh.10:12). Amini ni zaidi ya asilimia 70 ya ujuzi wa kutembea na Mungu kwa kiasi cha miujiza, Yoshua aliupata kwa Musa. Jaribu kukumbuka habari ya Elisha na Eliya. Eliya alijifunza direct toka kwa Mungu, lakini asilimia zaidi ya 70 ya impact kwenye maisha ya Elisha (Ishara, maajabu na miujiza) ilikuwa ni Experience impartation toka kwa Eliya. Elisha naye ilimpasa kumfundisha Gehazi experience ya kimungu, lakini katika kumwandaa, mtumishi wake Gehazi alikosea, na hivyo Elisha alikufa na ujuzi wake na upako wake bila ku-impart kwa yeyote. Baada ya hapo hatusomi tena nabii yeyote kutumiwa kwa mfano wa Eliya na Elisha. Hata wakati wa Yohana mbatizaji, pamoja na kazi kubwa ya Yohana mbatizaji, hakuna historia ya muujiza wowote aliotenda, hii bila shaka ni kwa kuwa, hapakuwepo mahali pa kupata Experience, wala hakufunuliwa direct (Lakini labda pia wito wake haukuhitaji miujiza)..
*KWA NINI TUJIFUNZE VITA VYA KIROHO.*
Vita vya kiroho ni ujuzi maalumu (Profession) na anayeweza kuvipiga lazima awe AMEHITIMU KUPIGANA (Wimbo ulio bora 3:7-8).
Pia tunasoma katika (2Falme 13:19), habari za Yehoashi mfalme, alichoma mshale mara tatu tuu, wakati Elisha alimtazamia achome mara tano au sita ili ashinde kabisa kabisa. Watu wa Mungu wengi wana mshinda shetani kidogo tuu, hadi inadhaniwa kuwa shetani ana nguvu sana. Kwa hiyo pata fundisho hili maalum (SPECIAL COURSE) ili uwe mshindi daima.
*MISINGI YA SOMO*
💫Katika vita vya kiroho, twaweza shinda bila shaka (HESABU.13:30)
💫Shetani adui mkuu ni kiumbe tu (He's just a creature. Ezek. 28:2, 6, 8, 15, 19)
💫Aliye ndani yetu ni mkuu kuliko adui yeyote aliyepata kuweko (1 Yoh. 4:4).
💫Jeshi la shetani halilingani na Jeshi la Mungu. Yoshua alikutana na malaika aliyejitambulisha kama Amiri wa jeshi la Bwana (Yosh. 5:14)
Malaika asingetaja majeshi hewa (kuna majeshi), na Mungu wetu asingejifunua kama BWANA wa majeshi, kama hana majeshi.
Majeshi ya Mungu kiidadi ni mengi kuliko ya shetani (soma 2 falm. 6:16)
Pia kithiolojia, 1/3 (theluthi moja) ya malaika walishawishiwa na kuasi pamoja na shetani (Ufun 12:4).
Hatujui idadi kamili, lakini tukiitumia hesabu ya kinabii ya majeshi ya Mungu ya bilioni ishirini (20,000,000,000 ya magari ya vita/chariots) soma (Zab. 68:17). Huenda hii isiwe takwimu kamili, lakini tujifunze. Kama theluthi waliasi,
(ni 6.5 billion) ya malaika, kwa hiyo bado kuna theluthi mbili ilibaki (13.3 billion). Okey tuachane na mahesabu maana sio kusudio langu la hizo hypothetical information.
*_UHALISIA WA VITA VYA KIROHO._*
Vita tunavyosoma katika Agano la kale, vilikuwa vya kimwili (Physical Fighting) ingawa in some cases, vita vilipigwa katika ulimwengu wa roho na kuleta matokeo (impact) katika ulimwengu wa mwili (physical world).
Yoshua 6:1-20, Amuz. 5:20, 25-26
Kutoka. 17:8-16, 2 Nyak. 20:15-24.
Vita ya kiroho ipo kwa mtu binafsi (individual level) hadi level ya bara zima (continental wise).
*The personal experience of spiritual warfare*
Mifano hii ni halisi, lakini kimaandishi haiwezi kuandikwa yote.
💫Siku wanafunzi wenzangu waliponisikia nikitoa sauti kama ya kilio fulani nikiwa nimelala. Nami nakumbuka kulikuwa na vita kali sana siku hiyo, kiasi cha kuona nilipekekwa sehemu nyingine.(Yaani niliondolewa kabisa mahali nilipokuwepo), Wakati huo nikiwa kidato cha kwanza (Pugu secondary school) na ni mchanga tu kiroho (Mwenye juhudi kubwa kiroho).
💫Siku moja nilipanda kitandani, nikaona baridi imeniangukia miguuni,inapanda kuja juu, ghafla, niliona ceiling board inayotenganisha Cubicals katika bweni, ikitikisika kama kitambaa, na dudu moja la ajabu, kubwa, lenye mikia mingi kama pweza 🐙👹, lilitokomea katika ceiling board hiyo.
💫Siku moja nikiwa macho, nyakati za usiku hakukuwa na umeme eneo lote, wala taa. (Kumbuka nguvu za giza, zinafanya kazi sana, kukiwa na giza). Nikiwa natembea niliona mkanda wa kufunga suruali unatetemeka na kuzunguka kwa nguvu. Nikaushika kwa mkono, ghafla ndani ya suruali nilihisi joto na baridi kwa pamoja, kisha nikahisi vita kali rohoni.
💫Siku niliposikia sauti ikiniambia, Kuna vita kubwa sana katika ulimwengu wa roho nilikuwa nimelala, nami nilihisi sauti ya vita.
💫Siku nilipohisi uwepo mwingi kama wa Mungu, but haukuwa halisi, kumbuka shetani anazo copies (nakala) za vitu vya kimungu, ila sio halisi. Lakini baadae nilishtuka kuwa ule uwepo haukuwa wa kimungu, ila ni UVAMIZI wa kiroho. Ingawa nilikuwa ibadani, Mungu alikwisha nifundisha kuwa uwepo wake unakuja kwa wewe kujiandaa, kuukaribisha na kuuhitaji sio kwa ghafla bila kuutaka.
💫Siku nilipoomba masaa zaidi ya manne usiku, kuanzia saa 5 usiku hadi saa tisa, nikiwa pekeangu, kwenye chumba chenye giza. Nilipomaliza na kulala, usingizi mzito ulinigubika kwa sababu ya shughuli za jana yake mchana. Niliposikia sauti kwa ghafla, ikinishtua kwa kusema, "Adui anakuja", vita ilikuwa kali siku hiyo, lakini Roho Mtakatifu alinipa kushinda. Hata baada ya kuamshwa na Roho Mtakatifu, sikuweza kuamka sababu ya uchovu mwingi, haikupita hata dakika moja, nguvu za adui zilinivamia, nilibanwa viungo vyote vya mwili, sikuweza kufurukuta. Kwa njia ya maandishi haitoshi kueleza yote na jinsi nilivyoshinda, HAYO NITAYAELEZA NIKIWA NAHUDUMU LIVE, NIMELIST TU KUJIKUMBUSHA.
NB:-
Ndugu msomaji, hiyo ya juu ni mifano michache ili nikupe picha ya uhalisia wa vita ya rohoni.
Unaweza kuwa macho au umelala, itakujia tuu. Ni muhimu kuwa na Roho Mtakatifu kama Antenna ya ku-sense mashambulizi ya kiroho.
B. GROUP-WISE WARFARE. (Vita kwa kundi)
Vita ya kiroho inaweza kuwajia mkiwa kundi la watu either katika huduma au jambo lolote mnalofanya.
Tuliwahi kuwa katika mkesha, na wote tulishambuliwa; hatukufanya vita vya kiroho kwa ujuzi, na hivyo wote tulishambuliwa mwingine alikamatwa na kichomi, mwingine kwikwi isiyoisha, mwingine tumbo kujaa gesi, mwingine kichwa kuuma, kila mtu alishambuliwa kivyake, tukajikuta maombi hayaeleweki.
Paulo na wenzake walizuiwa na shetani waziwazi (1Thes. 2:18)
MFAHAMU ADUI
Ukipambana bila kumjua adui yako vizuri, unaweza kupigwa vibaya. Ni muhimu umjue adui yetu, nguvu zake, silaha zake na mbinu zake za kivita.
Shetani (Lucifer) ndiye adui mkuu.
Alikuwa malaika mwenye daraja la kwanza kwa cheo. Ezek. 28:14-16 Isay.
14:12-14
Anatajwa kama Mungu wa dunia hii (2 Kor 4:4)
Dunia yote hukaa kwake ( 1 John. 5:19)
Anatajwa kuwa ni mwenye nguvu (Math. 2:29)
Anatajwa kuwa ni mwenye nguvu (Math. 12:29)
Anatajwa kama mkuu wa ulimwengu Yoh. 12:31, 16:11, 14:30.
Anao ufalme wake Mark. 3:22-27
*AUTHORITATIVE STRUCTURE OF SATAN'S KINGDOM*
(Pata kielezo cha chati kilichochorwa vizuri)
*MAELEZO YA CHATI*
Shetani kwa kujua kuwa ameasi kinyume chake yeye aliyemwumba, na upinzani atakaoupata, amejidhatiti kwa kuweka utawala na majeshi. Kumbuka katika ufalme watawala na majeshi ni kitu muhimu sana.
Ngazi zilizo chini, zinapokea nguvu kwa ngazi za juu.
Zinatoa report ya utendaji kwa ngazi ya juu.
Ngazi inayolemewa inaomba msaada sehemu nyingine.
FALME NA MAMLAKA
Hii ni ngazi ya kwanza ya cheo baada ya Lucifer. Inahusika na kuzuia au kupinga yanayotoka juu kwenda kwa watu wa Mungu. (Dan. 10:12-13)
Hapa utasoma habari ya wafalme wa Uajemi, falme na mamlaka hutumia jina ambalo juu yake wanatawala. Mfano tukiwa Dodoma au Tanga, usikemee wakuu wa uajemi, Wamedi na Waajemi (Medes and Persians) ni mashariki ya kati, hupaswi kutaja wakati wa kukemea, wewe utataja wakuu wa anga ya Dodoma au Tanga!
Na inapotokea yanayotoka chini kwa watakatifu kwenda juu, yakipenya ngazi zote, hapa lazima kutakuwa na kazi ya ziada ili wao nao waachie.
Kuna mambo ambayo watakatifu waliopo duniani, waliyataka toka juu, kiti cha enzi cha Mungu kikaachiliwa mahitaji na majibu, yakakwama hapa. Wao hawanufaiki kwa chochote wanapoyashikilia, ila walioomba kama hawataendelea kuomba, wataendelea kushikilia. Lakini kama jambo limepelekwa kwa force kubwa, wanapisha, wala hawazuii kabisa.
Falme na mamlaka zinaamua eneo husika liweje kiimani, kiuchumi au kisiasa.
Dini zote ambazo muasisi wake si YEHOVA BWANA, AU YESU KRISTO, ni kazi ya falme na mamlaka. Dini kama Buddhism, Hinduism, Taoism and all others, including traditional religion, zote hizi ni kazi za falme na mamlaka kutimiza uhitaji wa shetani (Lucifer) Kuabudiwa
WAKUU WA GIZA/ANGA
Efeso. 6:12, 2:2
Hii ni nafasi ya tatu toka kwa shetani, inapokea maelekezo toka kwa falme na mamlaka.
Katika eneo husika wanalo tawala wanajenga ngome (2 kor.10:4)
Wanatumia majeshi ya pepo kuachilia maasi/maovu/dhambi za namna yeyote mahali wanapokusudia.
Mfano
Albino killings in Tanzania
Prostitution business in Las Vegas (U.S.A )
Abortion in United Kingdom.
Kuzuia maombi ya watakatifu (No break through)
Kupinga mambo yote ya huduma ya kiroho
Kwa kufanya mioyo ya watu kuwa migumu.
Kuifanya anga kuwa nzito (no anointing)
MAJESHI YA PEPO WABAYA
Hii ni ngazi ya nne kwa cheo, imegawanyika makundi mawili.
Majini (Lawi. 17:7) hapa kwa mara ya kwanza katika biblia, tunasoma neno hili Majini (Water/marine spirits kwa kiarabu Jinn(kilichofichika/unseen)).
Pepo wachafu (Evil spirits/ Demons) (Kumb. 32:17) Hapa tunasoma kwa habari ya mapepo kwa mara ya kwanza.
Majini (Water spirits) na mapepo,yanaelezwa kuwa na tofauti kadha wa kadha na utendaji kazi wao. Lakini ukweli hawa ni roho walewale tu wamoja.
Pepo wakiwa wengi kwa mfumo wa majeshi, Wakifikia 6,000 huitwa Legion
Mambo yote yaliyo kinyume na amani, furaha, raha, baraka, utulivu, afya njema, upendo, masaidiano, maendeleo, na kila lililo jema; yanasababishwa na pepo wachafu na majini.
Pia mapepo yanabadilisha matumizi ya asili (Luk . 8:27) - kuishi makaburini Rumi. 1:26-28
Yanafanya kazi kwa bidii, yakijua wakati wao sio mwingi Math. 8:29, Ufun. 12:12
BAADHI YA MAJINI/PEPO NA KAZI ZAO.
JINI HUSNA HUNAN AU JINI CHAFANYA KUU POPOBAWA (INCUBUS/SUCCUBUS)
INCUBI-Shambulio la kiroho la tendo la ndoa bila hiari katika ndoto kwa wanawake.
SUCCUBUS- Sawa na hilo hapo juu ila hapa, ni jini la kike kuvamia
wanaume kwa ngono.
JINI KILOLINDI NA JINI WARIDI JEKUNDU (Kazi yake ni kuamsha hamu ya ushoga)
SUBIANI- (Kazi yake ni kubadili tabia za watu).
SUBISUBI- Jini wa vitisho
JINI SHEIKH- Jini mtawala
JINI SAHABINI ALWAH-JINI WA KUTOA MIMBA (ABORTION)
JINI MARUHANI- Jini linalozuia vitu kuingia au kutoka (No entry, no exit)
JINI MAKATA- Mtenda kazi wa siku 13 anayeishi kwenye milima kazi yake ni kuua na kutawanya.
JINI KASKASHI- KUSHOTO MWENYE KULETA MAUMIVU, HUZUNI NA Kadhalika.
JINI MEEKA- Jini anayewavuta watu kupenda muziki wa kidunia kama Bongo fleva.
JINI LUMYATA- Jini anayewanasa watu wa dini kwa ngono na kuwaleta kwa shetani.
JINI NYOKA ZEHEL- Pepo wa ushirikina wa aina zote.
Kuna umuhimu wa kutaja jina la jini husika, kama umegundua ni yupi anayefanya kazi, kama unajua jina.
Kama hujui jina usikisie, taja kazi ya pepo iliyojidhirisha.
Mfano:- roho ya mauti au ajali nakuamuru toweka; au nasambaratisha pepo la ushirikina.
Kuna majini yanayo-operate sehemu Fulani, na sehemu nyingine hayatendi kazi, ila wanadamu wenyewe wana-transfer zile kazi.
Mfano:- Malkia wa baharini anatenda kazi sana kwenye Coastal regions. Au Roho ya Yezebel (Ufunuo. 17:1-5-kahaba mkuu) ufunuo: 2:20-22 Isaya. 3:1-3
Jina Yezebel unasoma kwenye biblia kama mke wa Ahabu mfalme wa Israel, lakini alikuwa na sifa ya uchawi na uzinzi (2 Flame. 9:22), Na ni roho kamili katika ulimwengu wa roho.
Kuna mambo yanayohamasisha uasherati ( fashion&style) yanasababishwa na roho hii (tembelea
http://www.albatrus.org/english/church-order/women-matters/jezebel_in_our_society.htm
🗡Dalili za utendaji kazi wa roho hii mahali Fulani
Kushamiri kwa ibada za sanamu.
🗡Kujengwa kwa madhabahu ya shetani ndani ya kanisa.
🗡Kuenea kwa dhuluma na kupotea kwa haki za watu, (ufisadi).
🗡Kuuawa kwa wenye haki au wanaotetea haki.
Kuchochea uasi ndani/mbele ya watu.
🗡Kuenea kwa uasherati, uzinzi, ushoga na aina zote za uzinzi kwa kutumia viungo ambavyo havikuumbwa kwa makusudi hayo.
🗡Kutoa vitisho kwa watumishi wa Mungu, wanaosimamia kweli.
🗡Kushamili kwa mambo ya ushirikina na unajimu.
🗡Usingizi wakati wa ibada, kusoma neno. Huu ni mfano tu.
*WACHAWI, WAGANGA NA AINA ZOTE ZA USHIRIKINA*
Kwa mara ya kwanza tunasoma kuhusu wachawi na waganga kwenye (kut. 7:11)
Hii ni ngazi ya mwisho katika utendaji wa shetani.
Ngazi inaofanya kazi moja kwa moja kwa wanadamu kwa kutumia na pepo/majini.
Upigaji ramli, kuloga, kuagua, kutuma majini, kuwafunga watu ni kazi zao kubwa.
*_WALIMU, MITUME NA MANABII WA UONGO NA IMANI POTOFU._*
Hii nayo ni ofisi ya shetani, inayolenga kuwanasa wanaomtafuta Mungu wa kweli.
Watumishi hawa wa uongo, wanatumiwa na pepo kuingiza fundisho ambalo ni kinyume na kweli, ili waamini washambuliwe kiurahisi.
Imani potofu nayo inapotosha watu kuabudu kitu kingine kwa kudhani wanamwabudu Mungu wa kweli, inaiga mifumo ya ibada za kweli. (HILI NI SOMO JINGINE, HAKIKISHA UNAPATA SOMO LANGU LA *ROHO ZIDANGANYAZO*)
*SIFA ZA ANAYEWEZA KUVIPIGA VITA VYA KIROHO.*
Kama tulivyoona katika utangulizi, vita vya kiroho ni ujuzi maalum (Profession) hivyo kuna watu wenye sifa za kupigana vita hivi.
Lazima awe anamwamini YESU KRISTO, yaani AMEOKOKA.
Lazima awe amejazwa roho mtakatifu.
Lazima awe amefundishwa vita ya kiroho.
Lazima awe anamfahamu adui.
Lazima awe amevaa silaha.
Mwl Proo
*ASKARI WA KIROHO SAWA NA Efeso 6:10-18*
(Hakikisha unaona kielelezo hiki cha mchoro wa picha)
*SILAHA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.* 🔫💣⚔🛡🗡
Neno linasema, Bwana amefanya silaha za kufisha (Zb. 7:13), neno amefanya katika mstari huu maana yake, ametengeneza.
Silaha za mwili za ulimwengu huu hazina kazi katika ulimwengu wa roho (mwimba tenzi- mteteeni Yesu) Aliimba, Nguvu zenu za mwili hazitatufaa.
Mungu wetu ni wa vita (kut. 15:3) lazima awe na silaha.
Tunaagizwa kuvaa silaha. Efes. 6:11, Rumi. 13:12, Nah. 2:1
Kuna silaha makundi mawili
🔴DEFENSIVE WEAPONS.(Silaa za kujilinda)
🔴OFFENSIVE WEAPONS. (Silaha za kushambulia)
Nchi kama ya TANZANIA ina defensive forces (JKT na JWTZ), Vikosi hivi vyote ni vya kujilinda, hatuna ARMIES Kwa ajili ya mashambulizi. Mataifa kama U.S.A, GERMANY, RUSSIA na CHINA yana OFFENSIVE ARMIES.
Ni muhimu kukumbuka, lugha ya neno (BIBLIA) ndio lugha ya roho (au inayotambulika sana rohoni) so much pronounced!
Usiige misemo ya wana wa dunia kwenye vita ya kiroho.
Mfano: Ushindwe na ulegee kama usemi haupo kwenye maandiko, na umebuniwa tu na watu wa mwilini, unakua ni mzaha kwenye ulimwengu wa roho.
NB:
Ni muhimu kufahamu ulimwengu wa roho, umejaa uhalisia wa vitu vyote, sauti zina maana zaidi (1 kor. 14:10), hata ukiongea upuuzi, unasikika sana katika ulimwengu wa roho. Nguvu (forces) zinazofanya kazi ni nyingi kuliko za duniani/tunazo soma kwenye Physics /Geography. Kuna forces ambazo zinaweza kuumba kitu unachotaja hata kama hakijawahi kuwepo. Unaweza ukasogeza kitu popote kwa mwendo (speed) wowote. You can zoom in, zoom out kwa ukubwa ( size) yoyote.
*SILAHA KUNDI NO. 1*
Tunazo silaha ambazo zina nguvu katika Mungu ( 2 kor. 10:4)
*JINA LA YESU*
Mdo. 4:12,2:21, Math. 12:21 Jina la Yesu lina mwali ya moto🔥, linatajwa,
kama YAHU (Zab. 68:4, 89:8 Wimbo. 8:6)
Mith. 18:10
Kwenye jina la Yes kuna
🗡Mamlaka ya Mungu
🗡Uweza wa Mungu
🗡Kidole cha Mungu.
*DAMU YA YESU.*
Ebr 12:24, Math 26:28 (Damu ya Agano) Damu ya Yesu ni silaha kubwa kwenye ulimwengu wa roho, na hasa kwenye kuwafungua waliofungwa. Ushuhuda binafsi, siku moja nikiwa katika vita vya kiroho, kila nilipotaja damu la Yesu, nilisikia sauti kama ya risasi imefyatuliwa.🔫
*MSALABA WA KRISTO YESU*
(I Kor 1:18) Hii pia ni silaha kubwa kwenye mambo ya ukombozi, toka katika nguvu za giza.
NENO LA MUNGU
Ebr. 4:12, Efes. 6:17, Yer. 23:29, 5:14 Zab. 147:15, 18.
SIFA KWA MUNGU (PRAISE)
2 Chron. 20:16-20 Zab. 22:3, 149:6 sifa ina fananishwa na silaha ya vita.
Katika lugha ya asili ya Biblia (Kiebrania) sifa ina tafsiriwa kama Halal ambayo ni muunganiko wa aina nne za sifa yaani. Shaback- Shouting (Zab 63:3), Tehilla kuimba tenzi na zaburi (Zb 40:3) Towdah- Dhabihu ya kushukuru (Zb 100:4) na ya mwisho ni zomar- kuimba kwa
kutumia vyombo vya muziki (zab. 33:2) sifa yenye mambo hayo manne ni silaha kubwa.
*WEAPONS IN THE STORE (GOD'S ARSENAL)*
Neno linasema, Bwana amefungua akiba yake silaha (ARSENAL), (Yer 50:25). Kumbe kwenye ulimwengu wa roho kuna storeroom ya silaha za kila aina, hizi hapa chini ni silaha unazoweza kuzitumia kwa kadili ya uhitaji wako.
💣Upepo wa mashariki [Kut 10:13, Zab 78:26, 18:15, Yona 4:8, Hos. 13:15 Hab. 1:9, Isa. 50:2, Isa. 11:15
💣Mishale, ngao, upinde na mikuki ya moto na umeme, zek. 10:4-5 Yer. 51:11, 50:29, Hab. 3:911, Zab. 35:2-3, 7:13 2Falme. 13:17, Yer. 45:3-4, Zab. 18:14, 9:14
💣Magari ya vita/moto yer. 47:3, Zab. 68:17, 2 Falm. 6:17, 2:11.
💣Radi na mvua ya mawe Zab. 18:13, mawe ya teo (SLINGSTONE) Zek. 9:15
💣Kuna misumari, Zek. 10:4
💣Chungu cha maji yenye nguvu, Hab. 3:15
💣Kuna minyororo, Nahum. 3:10
💣Kuchafua usemi (Lugha), Zab. 55:9, Gen. 11:7-9.
💣Kuna mapanga ya umeme kumb 32:41, Isa. 27:1
💣Kuna majembe, miundu na mikuki Yoel. 3:10, Yer. 50:36, Zab 7:12, Yer.47-6
💣Matuo ya Bwana (forces of the Lord) Yoel. 2:11.
💣Kuna moto (Yoe. 2:3, Ebr 12:29, Kumb. 4:24)
💣Kuna mawe ya barafu (Yoshua. 10:11)
💣Kuwapiga adui kwa
usingizi wa milele (Yer. 51:39)
*JINSI YA KUVIPIGA VITA VYA ROHONI.*
Neno linasema, Bwana ananifundisha mikono yangu kupigana vita (2 Sam 22:40) ni muhimu kujua vita vya kiroho ipo kwa ajili yetu, ikikupata usimuulize Mungu, kwa nini! Wala usihoji wako wapi malaika wanaonilinda. Utajifunza mbele kidogo ni wakati upi malaika wanatumika katika vita.
Tukiwa na maarifa ya jinsi ya kuvipiga vita, hatutafanya kosa la sisi kukusanyika wengi kwa ajili ya adui mmoja. Mfano:- kukitokea na mkabaji mmoja, hawezi kuvamia kundi la watu 3, wala hana silaha yoyote ya kutisha).
Hesabu za kibiblia(Lawi. 26:8).. 5 of us will chase 100 enemies 100 of us will chase 10,000 enemies.
Pia katika, Yosh. 23:10 na Isa. 30:17, the Bible says, .at a threat of one, thousand will flee, at a threat of five, all will flee.
Kwa hiyo ni muhimu kufahamu strategies and schemes, kwani shetani (Adui mkuu) anajua mbinu za kivita. 2Kor. 2:11 (schemes), Efes. 6:11.
Pia ni muhimu kufahamu structure ya vita vya mwilini, ambayo Mungu alimfundisha Daudi ndio muundo wa kupigana katika roho.
Mfano: kuweka waviziao (setting an ambush) 2 Nyak. 20:22, Amu. 20:29.
Lazima awepo anayeongoza. (AMU. 7:17), msifanye bila mpangilio (randomly). Jaribu kupata picha, mnakemea pepo mchafu mwingine anamuuliza jina lako nani, mwingine anasema, funga kinywa mtoke, kila mtu anaamuru cha kwake.
Lazima muanze na kujiweka sawa, kwa kujitakasa (huenda yupo ambaye si safi, anaweza kuleta usumbufu) Yoel. 3:9.
Kuvaa silaha. (Yote haya yafanyike kwa mfumo wa confessional Prayers) kama kiongozi anavyo-direct.
Sehemu yaku-set ambush, mnaweza kunongona.
Lakini mkianza vita lazima ifanyike kwa sauti kuu (kelele) Yosh. 6:20, Luk. 23:23, Hesab. 10:5-9.
Ni muhimu kushambulia ngome, zilizojengwa na wakuu wa giza/anga (Yer. 48:41)
Ni muhimu kushambulia vituko (Yer. 51:32), katika ulimwengu wa roho kuna madaraja kama haya ya mwilini, yanawasaidia mapepo au majeshi
mengine ya adui kuvuka toka upande mmoja kwenda upande mwingine, na kuna miundo mbinu mingi inaharibika wakati wa vita.
Maombi ya vita vya kiroho hayafanywi kwa utulivu, mnapokuwa kundi la askari wa Yesu, manavipiga vita lazima kuwe na MSHINDO (Yer. 50:22, Yoe. 2:5, Nah. 2:4).
Angusha kuta zote zote zilizosimamishwa na wakuu wa giza Yer. 51:44
Hatupaswi kupotosha safu zetu. Asiwepo anayechoka upesi, na kukatisha maombi kabla ya vita kuisha. Wote mpigeni adui sawa. (Yoel. 2:7-8)
Kumbuka kuzuia vyanzo vya msaada.
wa adui. Tunasoma katika 2 Falme. 3:25 Jinsi wana wa Israel walivyoziba chemchem za maji kwa mawe, ili adui wasipate maji ya kunywa wawapo jangwani. Pia kama mnakemea pepo, mkiona hirizi au nyezo yoyote msiiache, choma moto.
Ni muhimu kuingia rohoni ili uweze kujua kama adui amekimbia au amejificha.
Mark. 9:26
Ni muhimu kulinda njia, yasije majeshi meingine ya mbali, ili kufupisha muda wa vita. (Nahum 2:1)
*MANENO MASHUHURI YA KIBIBLIA YA KUTUMIA WAKATI WA VITA.*
Yer. 1:1:10, 51:43, Isa. 6:11, Kut: 15:5, Efes. 6:16, Luk. 10:19, Isam. 2:10, Yer. 51:20, 2Kor. 10:4-5
Ninaangusha, nainashambulia, nainasambaratisha, ninangoa, ninaharibu, ninavunja, ninabomoa, ninafunga matita matita, ninapatiliza, ninateka nyara, ninayeyusha naangamiza, ninanyamazisha, ninaponda, ninakanyaga, ninadisconnect, ninafunga, ninatowesha, nasaza maganjo, nafanya ukiwa, ninavua enzi nafunikiza, na mengine mengi utakayoyapata kwenye neno la Mungu.
*SOME WARFARE SITES IN THE SCRIPTURES..
Yer. 6:4-5 ( Kabla ya kuanza)
Yer. 46:3-4 (Kabla ya kuanza)
Yer. 46:5 (Baada ya vita)
Yer. 47:1-7 (Kabla ya vita)
Yer. 48:1-4 (Kabla ya vita)
Yer. 48:15-25-44 (Baada ya vita)
Yer. 50:21-32 (Kabla ya vita)
Yer. 50:34-46 (Baada ya vita )
Yer. 51:11-13 (Kabla ya vita)
Yer. 51:20-23 (Kabla ya vita)
Yer. 51:30-32, 37-56 (Baada ya vita )
Mwl Proo
(Prosper Kadewele)
©2011
alltruth5ministries@gmail.com
Visit website