*USISUBIRI MAZINGIRA WEZESHI*
Mwl Proo
0762879363
HALELUYA!!!!
Wengi wetu kuna mambo fulani, ambayo tunatamani kuyafanya, na tunajua kuwa hali zetu zitakuwa nzuri zaidi, tukiyafanya hayo, lakini tunasubiria mazingira wezeshi (supportive environment), ili kuanza kuyafanya. Hapo nashuhudiwa na Mungu, kuwa wapo wengi mno. Tusome andiko la msingi.....
Mhubiri 11 : 4 *_Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna._*
👆🏼👆🏼👆🏼👆🏼NI MUHIMU KUKUMBUKA, TUNAENENDA KWA IMANI, SIO KWA KUONA (2KOR 5:7). MUNGU KAMWE HAKUFANYA JAMBO LOLOTE KWA KUTEGEMEA SUPPORT YA MAZINGIRA RAFIKI (FAVORABLE ENVIRONMENT), ILI ATENDE KAZI YAKE. HAKUSUBIRI MAZINGIRA MAZURI, ILI AUMBE, KUKIWA NA GIZA, UKIWA, AKAANZA KUFANYA ANAYOKUSUDIA (MWANZO 1:2-3). HAKUSUBIRI TUTUBU, TUJITAKASE ILI ATUOKOE, BALI TUKIWA BADO WENYE DHAMBI KRISTO ALIKUFA ATUOKOE (RUMI 5:6,8). NDIO MAANA, ANDIKO LETU LINASEMA, MWENYE KUANGALIA UPEPO, HATAPANDA! NAYE ATAZAMAYE MAWINGU, HATAVUNA!.
Ndugu yangu, kuna watu humu, wamejipa-udhuru (exemptions), kutofanya majukumu ya kiroho kadhaa, wakiamini mazingira hayaruhusu. Kuna watu wanatamani kufanya huduma, lakini wanasubiri mazingira wezeshi, kuna watu wanataka kufanya maombi na kufunga, lakini wanasema unajua kaI zangu hizi, zinanikinga, nitafunga na kuomba likizo (iko moja kwa mwaka), kuna watu wanasukumwa kutoa kwa ajili ya kazi ya Mungu, nao wameji-exempt, wakisubiri mazingira wezeshi. Hiyo ni kwa mambo ya kiroho na mambo mengine pia, kwa kuendelea kusubiria mazingira wezeshi, wengi wanaacha muhula walioandikiwa upite;
Yeremia 46 : 17 *_Wakalia huko, Farao, mfalme wa Misri, ni kishindo tu; muhula alioandikiwa ameuacha upite._*
👆🏼👆🏼MUHULA ALIOANDIKIWA AMEUACHA UPITE. VITU VIMEFUNGWA KWENYE MUDA (MAJIRA NA NYAKATI-KAIROS/CHRONOS). BILA SHAKA UNAKUMBUKA YALE MAPEPO NDANI YA MGERASI, YALIMHOJI YESU, VIPI UMEKUA KUTUTESA KABLA YA MUHULA WETU?. YAANI YANAJUA KUNA MUDA UNAFIKA, TUTATESWA MILELE, ILA MBONA MUDA TUNAHISI BADO!!👹👹👹👉🏾⏰. UNAPOSHINDWA KUFANYA MAMBO ANBAYO ROHONI MWAKO, UNAJUA KWA HAYO UTAKUWA NA HALI NZURI ZAIDI, LAKINI UNASUBIRI MAZINGIRA WEZESHI, UNAUACHA MUHULA UPITE KWA HASARA.
*MAMBO YA KUZINGATIA*
♻ *USIOGOPE MWANZO MDOGO*
Sio lazima, mambo yaanze yakiwa level ya juu tayari, unaweza anza kwa kiwango kidogo, itaongezeka, cha msingi anza!
Ayubu 8 : 7
*_Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana._*
Unaamka kuomba, hauhisi hata kauwepo kidogo. Usisitishe anza na huo ukame hivyo hivyo, nguvu itakuja tuu, hata kama utaona nusu saa ya kwanza ni kama haizai matunda, just press on!
♻ *USIYAOGOPE MAUMIVU MADOGO YA MUDA MFUPI, YANAYOTOKANA NA MAZINGIRA YASIYO WEZESHI*
Wewe ni mfanyakazi, ukiangalia number of tasks kutwa nzima, kazi zinazohitaji energy kubwa,unaamua kupitisha maamuzi, kuwa sitafunga, hadi likizo. Sasa kuisubiria likizo (mazingira wezeshi) unapoteza sana ndugu yangu. Yavumilie hayo maumivu madogo kwa muda, utagundua kuna nguvu itakuwezesha, anza kwa nguvu uliyonayo
Waamuzi 6 : 14 *_Bwana akamtazama, akasema, Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma?._*
👆🏼👆🏼KAMA GIDEON ANGEENDELEA, KUSUBIRIA MAZINGIRA MAZURI, HAKUNGEFANYIKA KITU, LAKINI ALIPOINUKA NA KUANZA KUTENDA, NDIPO AKAJIGUNDUA NI MTU HODARI HASWA! KWA HIYO NENO LA BWANA KWAKO UNAYE-POSTPONE MAMBO YA KIROHO, KWA KUHISI LABDA SHIDA NI MAZINGIRA, LA HASHA. NILIPOTIA MOYO WANGU UFAHAMU WIKI ILIYOPITA, KUWA NAPASWA KUFUNGA, NIKAANZA NA LEO NI SIKU YA NANE MFULULIZO NIPO KATIKA KUFUNGA, SIPO LIKIZO, NI MTUMISHI WA SERIKALI, NAENDELEA NA MAJUKUMU YANGU YOTE KAMA KAWAIDA TOKA ASUBUHI MPAKA JIONI. LAKINI NINGESUBIRI MAZINGIRA RAFIKI, NINGESUBIRI WAKATI MWINGINE, MAANA UNAWEZA KUTA MAJUKUMU MENGINE UNAPASWA KUYAFANYA, UKIWA UMECHOKA SANA MWILI. ILA UNAPOENDELEA, NDIPO UNAGUNDUA KUNA NGUVU KUBWA YA KUKUWEZESHA KWA UWEZO WOTE (KOL 1:11).
♻ *MUDA WA SASA NI BORA ZAIDI, KULIKO ULE UNAOSUBIRI*
Wewe ni kijana, nguvu ulizo nazo leo za mwili, hutakuwa nazo ukifika miaka 45 na kuendelea. Mungu anajua umuhimu wa muda wa ujana, na akatoa ushauri kwamba kama unataka kuitwaa nira yake Mungu, ufanye katika ujana maana unazo nguvu (Maombolezo 3:27, 1Yohana 2:14). Shetani naye anajua siri nyingi sana za kimungu,anajitahidi kuwapotezea muda vijana, kwa mambo mengine. Wale wanaosubiri wastaafu 👴🏾👵🏿, ili waanze rasmi kujitoa kwa BWANA, wanakuja kugundua kuwa muhula walioandikiwa, waliuacha upite. Mzee wa miaka 60, akikazana kuamka kusoma Biblia saa nane usiku, usingizi unamshinda kabisa kabisa, akikazana kufunga muda huo,anaishia kupata ULCERS (vidonda vya tumbo) tuu. Kumbe kulikuwa na wakati, alipaswa kuyabana yote, hata kama mazingira hayakuruhusu kabisa.
♻ *KWA SISI WATU WA IMANI, SIO LAZIMA VIGEZO VYOTE VIZINGATIWE, ILI MAMBO YATENDEKE, BALI KWETU NENO LA MUNGU NDIO HATMA YETU*
Waswahili wanasema dalili ya mvua ni mawingu 🌧☁🌦🌨. Na kuna msemo mashuhuri unaosema, vigezo n masharti kuzingatiwa (terms&conditions applied). Sasa hiyo sio lazima iwe kwetu, Sisi tunao mfumo wetu, ambao tuki-adopt huu wa dunia, ni kumwekea Mungu mpaka (Zab 78:41). Kwa hiyo hata hiyo ya kusema, dalili ya mvua ni mawingu, sio lazima iwe applied kwetu, maana Mungu alinyesha mvua ingawa kulikuwa na kawingu☁ kadogo kama mkono wa mtu✋🏾 (1Falme 18:44-45). Kwetu alichosema kwenye Neno lake, ndicho kilicho halisi, kuliko tunachoona huku nje. Akisema Nimeamuru kunguru wakulishe 🕊🕊🕊 (1Falme 17:4ff), haihitaji *Reasoning*, kwamba sasa itakuwaje?🤔
♻ *SHETANI ATALETA VIKWAZO FEKI, ILI USIANZE LILE UNALOKUSUDIA*
❌Atakuinuliwa watu wa kukukatisha tamaa, ukiwa katika mchakato. Kumbuka walichokifanya Sanbalati na Tobia. Muda Nehemia na wengine wanatia juhudi kujenga ukuta wa mji, wao wanawapumbaza eti, haka kaukuta hata akipanda mbweha🐱 katadondoka haka.
Nehemiah 4 : 3
*_Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe._*
>Unaweza ukawa unawaza kufungua biashara, mtu akakuwahi, sikuizi fremu ni shida kupata...huyu anakuwa ni Tobia mjumbe wa Shetani kwenye kusudio lako.
>Unaweza kupanga maombi na kufunga, kanainuka kaugonjwa hukaelewi elewi 💊💉. Ukiona hivyo kuwa mjanja, kupanda nao kwa kuukemea kabla ya kuwahi madawa, maana unakuwa ni ugonjwa feki tu, sio halisi.
♻ *KATIKATI YA HALI MBAYA, KWAKO WEWE KUTAJAA NEEMA*
Usiogope kuanza chochote, eti kwa sababu watu wanalalamikia inflation (mfumuko wa bei), au kodi za TRA zimekuwa nyingi. Kumbuka Biblia inasema, Mungu ametujalia sisi neema iliyozidi. Katikati ya hizo kodi nyingi, bila hata kukwepa au kuiibia serikali, Wewe utazidishiwa neema ya kupata faida tu. Kumbuka wakati wa njaa ile wakati wa Isaka, akakimbilia na mkewe huko Gerari, kwa Abimeleki. Ardhi na utaratibu wa kilimo haukuruhusu, lakini yeye alipopanda mbegu, alipata kipimo kimoja kwa mia (Mwanzo 26:12) yaani kama alipaswa kupata magunia 10 yazidishe (10x100)= 10,000. Na Mungu yuleyule aliyefanya mazidisho yale habadiliki, hajabadilika (Mal 3:6, Ebr 13:8, Yak 1:17), anaweza kutenda kwako leo.
*_MUNGU AKUBARIKI ULIYESOMA, USISITISHE CHOCHOTE CHENYE MANUFAA YA KIROHO, KIUCHUMI AU KIJAMII, KWA KUYAONA MAZINGIRA HAYARUHUSU, HAYAKUPI SUPPORT, WEWE ANZA, UTAUONA MKONO WA MUNGU UKIKUSHIKA NA KUKUWEZESHA._*
Mwl Proo
0762879363( All Truth Whatsapp Group)
alltruth5ministries@gmail.com