*LIVE A NATURAL LIFE SUPERNATURALLY*
_Ishi maisha ya asili kwa namna isiyo ya asili_
*ʍաӀ Թɾօօ*
*0762879363*
Shalom Aleichem!
Karibu katika kujifunza kweli ya neno la Mungu, ili nguvu iliyo katika neno hai la Mungu ibadilishe maisha yetu kwa Jina la Yesu Kristo aliye Mwokozi na Bwana.
*🌈 MALENGO YA SOMO*
*❶ Kuwawezesha watu wa Mungu (waamini) waishi maisha ya kiwango kama watu wa rohoni.*
🧬 Tumechoka kuwa na wanaoshindwa kila eneo la maisha, elimu, biashara, huduma etc
🧬 Waamini ambao bado wana vifungo vya kipepo
🧬 Waamini ambao wanakaliwa na maradhi/magonjwa na kuishi kwa mfumo wa kitabibu badala ya kuishi kwa imani yao
🧬 Waamini ambao wana-Compromize wokovu wa Yesu wenye gharama kubwa, kwa sababu ya ugumu wa maisha. (Wapo ambao walijitahidi kulinda enzi zao kwa muda, mambo yalipokuwa magumu zaidi wakakubali kufanya mambo ambayo walijua kabisa hapa naachana na Mungu, ila compromize ililetwa na ugumu wa maisha..
🧬 Tumechoka kuwa waamini wanaorushwa na upepo wa kila elimu, mpaka wanajikuta wamejiingiza kwa manabii tapeli na feki, wakaharibikiwa ndoa zao, wakaharibikiwa maisha yao ya kiroho.
🧬 Tumechoka kuwa na wakristo tegemezi, waliofikia viwango vya kuwalipa watu pesa wawaombee, akitaka kulala anafoadi meseji kwa mtume wa mitandaoni kwanza, ndipo aamini anaweza lala salama, kila anachoota ni mpaka afoadi kwa social media kuomba msaada, utoto huu mpaka lini??
*❷ Hizi zama za mwisho, waamini wasio na ujuzi, waliolishwa dini, hawaishi wala kuenenda kwa Roho (Galatia 5:25), hawatakuwa na impact yoyote. Hivyo kwa masomo haya ya sasa, nipo kumwandalia BWANA watenda kazi (1Korintho 12:6, Math 9:37).*
_mwlproo_
*🌈 KWA NINI MAISHA YA ASILI UYAISHI KWA NAMNA ISIYO YA ASILI*
Zaburi 115:16, Yohana 15:19, Filip 3:20, Ebrania 6:5
🧨Maandiko hayo juu yanatuundia *equation* muhimu sana. Mbingu ni mbingu za Bwana bali nchi, amewapa wanadamu, tena anasema ninyi si ulimwengu, kisha anasema wenyeji wetu (our citizenship) uko mbinguni, kisha anasema katika Ebrania 6 kuwa mtu anaweza kuishi katika dunia hii, lakini akaonja nguvu za zamani zijazo (eternity is cousin to supernaturality)... Na sisi waamini tumeitwa kuanza kuyaonja hayo yote tukiwa bado kwa hii planet earth 🌍. Hivyo maisha haya tuyaishiyo sasa duniani ingawa yako natural, but we are supposed to live supernaturally, kama tunataka kufikia kwenye standard ya kutembea na Mungu.
🧨 Mwanadamu, yuko na Mwili, Nafsi, na Roho (Mwili uliwekwa na Mungu for Naturals (bound to nature), Nafsi ni driving force (eneo la reflection), lakini roho za wanadamu ni za kiroho, sio za asili ya dunia asili ya roho zetu ni rohoni i.e., mbinguni (Enoch 15:8-9), So to say, our spirits are bound to Supernaturality (Supernaturals/Spirituality)... Hakuna namna mwanadamu mwenye roho ndani yake atafikia kiwango cha maisha ya kiroho cha kutembea na Mungu kama hataishi na kuenenda kama mtu wa rohoni (1Korintho 2:14-15, Galatia 5:25).
🧨 Unalazimika kuishi kwa jinsi isiyo ya asili maisha haya ya asili kwa sababu, vitu halisi vyote viko rohoni, huku nje (in the physical) ni vivuli tu, ukishugulika na vivuli mwishoni utajikuta umechoka na haukufanya kitu chochote cha maana. Mambo yote yanaanzia rohoni, ili kufanya chochote cha kuathiri huku mwilini (affecting changes in the physical) sharti hayo mabadiliko uyasababishe rohoni, then huku nje yatatokea tu hata kama utakuwa umelala fofofo. Unataka kuifuta ajali iliyoko mbele, ifute rohoni haitatokea mwilini. Unataka kufuta kifo alichoandikiwa mtu na adui, kifute rohoni, hatakufa huku nje. Unataka kumbadilisha mume mlevi 🍻🍺? kwa maombi, mbadilishe rohoni, huku nje ataacha, ndivyo ilivyo kwa mambo yote, ukiweza kuli-adjust jambo rohoni, litatokea huku nje likiwa na hizo adjustments, maana dunia inazunguka huku nje (rotation/revolution) huku iki-comfrim na ku-comform mambo ambayo yalikwisha tokea rohoni. Yesu Kristo kama Mwanakondoo wa Mungu 🐑, alikwisha chinjwa kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu, kwa ajili ya dhambi zetu, lakini huku nje kulikuwa kunasubiri majira (Galatia 4:4), muda ulipofika likatukia jambo ambalo lilikwisha fanyika rohoni milenia nyingi za tangu zamani tangu milele.
_mwlproo_
*🌈 NI KWA NAMNA GANI MTU ANAWEZA KUYAISHI MAISHA UA ASILI KWA NAMNA ISIYO YA ASILI*
*🧨 Ubatizo wa Roho Mtakatifu, na kuutunza moto usizime (Baptism of the Holy Spirit, and keeping the fire unquenched)*
🕊🕊🕊🕊🔥🔥🔥🔥
Joel 2:28, 1Thes 5:19, Walawi 6:13, Yohana 14:17
💥 Holy Spirit should be very alive inside you... Mimi mwalimu wa Jiografia kitaaluma, nafundisha kuhusu *Volcanoes* zinaweza kuwa katika hali tatu za kimsingi 1. Active state (Alive/Hai), 2. Dormant state (Sleeping/Inakuwa katika usingizi) na 3. Extinct state katika kufa, Volcano yenye hali ya 1 iko hai, inalipuka muda wowote tu, hiyo ya 2 imelala hailipuki, ila imewahi lipuka muda si mrefu, na hiyo ya tatu imekufa, ina historia ya kulipuka, ila haitazamiwi kulipuka tena. Mwamini anayeweza kuyaishi maisha ya asili kwa jinsi isiyo ya asili, ```SHARTI AWE NA ROHO WA KRISTO NDANI YAKE AMBAYE NI ACTIVE & ALIVE```
*🧨 Orientation to the spiritual realms (spirituality)*
Kutambulishwa/kujuzwa mambo ya rohoni (Getting exposed to spirituals)
🧬 Mtu anaweza kuwa-oriented rohoni na
👉🏾 Ufalme wa nuru (Kingdom of light/Holy Spirit)
👉🏾 Ufalme wa giza (Kingdom of darkness )
#Shetani
#Falme na Mamlaka
#Pepo wabaya (Demons)
*SWALI*
Who introduced/oriented you to spirituals????????
🧬 Roho Mtakatifu yuko *commissioned* kututambulisha *_orienting us_* rohoni, kufanya tuyajue ya rohoni, tujulikane rohoni na kutufanye tu-operate rohoni. Usishangae rohoni tuko na badge au IDs ambazo viumbe vya kiroho vinatuona navyo na kusalimu amri. Waulize wana wa Skewa (Mdo 19), walipokemea pepo wabaya, wale pepo walisema *YESU TUNAMJUA, NA PAULO TUNAMFAHAMU*, NINYI NI AKINA NANI? WE DON'T SEE YOUR IDs KABISA, YOU KNOW THE STORY BILA SHAKA.
Yohana 16:13, 1Kor 2:10-13, Isaya 48:6.
🔥 Mtu akiishabatizwa kwa Roho Mtakatifu, na kujifunza utendaji wake, ghafla anaanza kuona mambo ya rohoni, anaona mambo yake, ya wengine, ya nchi na kadhalika Atayaona ya kiMungu hata ya Shetani atayaona, maana amekuwa oriented to spirituality mahali ambako Mungu (the spirit-God) yuko, na mahali ambako shetani (the spirit-devil) yuko, usisahau hili, Ibilisi naye ni roho, hivyo usijistress sana na vitu vya nje when dealing with him, ukawa bize kumwagia chumvi ya upako kwenye nyumba yako kumkinga shetani, wakati yeye kama roho ameyatawala maisha yako kwa dhambi (tabia ambazo yeye ni baba kwazo), unamfukuza shetani kwenye biashara kwa stika ya upako wa nabii, ila yeye amejaa moyoni mwako.
🧬 Lakini mtu anaweza kuwa spiritual-oriented kwa kutambulishwa rohoni/kiroho na roho zingine
*🌈 TOFAUTI YA MTU ALIYETAMBULISHWA ROHONI NA ROHO WA MUNGU AU ROHO ZINGINE ZA KIGENI*
🧨 Kwa aliyetambulishwa na Roho wa Mungu, darasa litaanza baada ya Ubatizo wa Roho Mtakatifu (In some few & rare cases, mtu anaweza kutambulishwa rohoni akiwa bado hajabatizwa kwa Roho, then ubatizo ukija, unakuja kumweka sawa. Unajua hata Sauli aliyeitwa Paulo alikuwa oriented to spirituals akiwa hajabatizwa na Roho bado. Kitendo cha yeye kumsikia Yesu, katika ile nuru ambayo rafikize hawakusikia (Mdo 9:1-20) ni tendo la orientation to spirituality. Ubatizo katika roho ulikuja baadae kumweka sawa katika mambo ya kiroho. Lakini masikio yale yaliyofunguliwa rohoni pale njiani kuelekea Dameski 👂🏽👂🏽 angeweza kuendelea kusikia vitu vya rohoni iwe vya Mungu au vya Shetani, maana tayari yuko spiritually-oriented to spirituals.
*NB*
```Mtu anaweza kuwa alikuwa nabii wa kweli wa Mungu, kisha akaharibu njia zake, akakataliwa na BWANA, na bado vipawa vya kiroho vikaendelea kufanya kazi, sio kwa sababu ya his/her uprightness kwa Mungu, No! alikwisha kuwa spiritually-oriented to spirituals na hivyo macho yale-yale, masikio yale-yale, ngozi ile-ile, ufahamu ule-ule bado unaweza ku-sense na kuopereti kule rohoni. Na wengine wakiharibu systems zinaBlock, anatambulishwa upya rohoni na nguvu za kinyume na Mungu ili kupoteza na kukengeusha wengi```
🧨 Kama ni Roho Mtakatifu amekutambulisha (orient) rohoni, Woga+Kushanga na hali ya Sintofahamu (state of uncertainty) itakuwa ni ya muda mfupi sana (will be temporary)... ATAKUSAIDIA NA KUKUKOMAZA
*NA ISHARA/KIASHIRIA KIKUBWA CHA KUONESHA ALIYEKUTAMBULISHA ROHONI NI ROHO MTAKATIFU, NI UHURU (LIBERTY/AUTONOMOUS FREEDOM) MAANA PALIPO NA ROHO WA BWANA PANA UHURU (2KOR 3:17), NA MWANA AKIWAWEKA HURU MTAKUWA HURU KWELI-KWELI (YOHANA 8:36, 32).*
🧨 Kiashiria kibubwa kwamba kuna roho za kigeni *strange spirits* zimeku-orient rohoni, ni Woga, Wasiwasi, Utisho, Kukosa amani, Sintofahamu *endless dilemma and confusion* yaani kuchanganyikiwa kunakuwa permanent. Labda kama umejitoa kwa moyo kuwa wakala au machawi etc haya hayataonekana maana utakuwa umevikwa roho ya ibilisi, itakayokufanya yote uone ya kawaida tu, hata ukiambiwa utafune nyama za watu.
*KIASHIRIA KIKUU CHA KWAMBA ROHO ZA KIGENI NDIZO ZIMEKUPA ORIENTATION KATIKA ROHO, HUTAKUWA HURU!*
``` Bila shaka mmekwisha wahi ona mtu sio mwamini (hajaokoka), lakini anaona vitu vya rohoni, na akisema vinatokea kweli. Bila shaka mmekwisha wahi ona kuna watu hawajisumbui hata na maombi na kukaa katika utakaso, ila wanaona katika roho, na wamejawa na vitu vya kiroho. Huenda ni dhaifu mno kiroho na mazoezi ya kiroho, wala havipigi vita vizuri vile vya imani, lakini mkikutana kwa sala yeye ndiye anatoa unabii wa kweli. LAKINI MKIMCHUNGUZA HUYU MTU KWA MAISHA YAKE, HAYUKO HURU, ANAWATABIRIA VITU VYA KWELI KWA FELLOWSHIP LAKINI MKIANGALIA MAISHA YAKE HAYANA MUNGU, ANAHITAJI KUSAIDIWA SANA KWA NJIA YA BWANA. HUYU MTU AMETAMBULISHWA ROHONI NA ROHO ZA KIGENI.```
_*🔥 Kama unaona upo kwa hali hii, taarifa utakazokuwa unazipata rohoni ni za kweli, lakini wewe mtoa taarifa hauna uhuru utokoa kwa Mwana wa Mungu*_
⚔ LORD'S WINNOWING FORK WILL BE SENT (PEPETO LA BWANA LITATUMWA, UKIFUNGUA MOYO WAKO, MUNGU ATAKUSAIDIA, TAFUTA MSAADA KWA WATUMISHI WA MUNGU).
⚔ SOME PEOPLE ARE TO BE DISCONNECTED FROM THESE STRANGE SPIRITS, YOU CANNOT PERFORM WELL WITH GUESTS INSIDE YOU.
⚔ HIZI ROHO ZITAFANYA UJIONE UPO NA MUNGU, THEN BAADA YA MUDA ZINAKUPANDIKIZIA VIFUNGO VIBAYA SANA, ILI USIJE UKA-EXCEL KWA LOLOTE, MAANA MWIVI HAJI ILA...........(Yohana 10:10).
_mwlproo_
*🌈 FAIDA ZA KUWA SPIRITUAL-CONSCIOUS PERSON (SUPERNATURAL LIVING)*
🧨 Roho yako itafufuliwa (rectified, rejuvenated)
Isaya 57:15, roho za wanadamu hazifi (mathayo 10:28 imezingatiwa, kuwa kuua mwili na roho ni maana tofauti), lakini roho zinawezwa kupigwa usingizi wa milele, zisiwe *SENSITIVE TO SPIRITUALS*
Hivyo, mtu akiwa oriented to spirituals na Roho wa Kweli, ataweza kuishi maximized life to full capacity...Hatukuitwa kuishi maisha kikawaida tu.. Mtu wa rohoni kwa kuwa anamfuata Yesu aliye *master of the nature* anaweza pindua chochote cha asili hata yale ambayo yako inherent au genetically-transferred toka kwa vizazi vya kwenu au systems za serikali. Mfano huenda kwenu wote wanajifungua operations na unaambiwa hiyo iko hivyo mpaka kwa shangazi zako, hiyo issue sio mara zote inakuwa ni uchawi but it has to do with nature tu, kwamba genetically, cervical paths za uzao wenu ziko namna hiyo... mtu wa rohoni anao uwezo kubadili lolote ambalo ni la nature akitaka na akiwa spiritual-oriented.
HAPA KUNA SHUHUDA NYINGI MNO ZA NAMNA WATU AMBAO SPIRITUALLY WAKO SENSITIVE, wameweza kuvuka maeneo mengi ambapo nature imesema NO! mimi hapa mwandishi ni shuhuda wa kwanza kwa hili.
🧨 Utakuwa chombo kinachofaa kutumiwa na Bwana kwa kazi yoyote mahali popote (You'll be fit for Kingdom's ministry)
🧨 Bwana atakuamini. Ni mambo mawili tofauti kumwamini Mungu na kuaminiwa na Mungu. Ukiisha kumwamini Mungu, panda viwango ufikie pa kuaminiwa na Mungu, ili kwamba Mungu akijua mahali wewe upo basi anaamini mambo hayataharibika... atajisemea moyoni, *_" Proo yuko pale"_* kwa namna ile-ile ya kujigamba kwa shetani, umemwona huyo Ayubu? 🤓... Sasa mtu hayuko spiritual-oriented anakuwa hajasimika mizizi yake mbali sana, dakika yoyote kufumba na kufumbua mara ashaanguka kwenye zinaa, yupo juu-juu tu kama mbegu zilizoanguka kwenye mwamba.. Mungu akusaidie unapoanza kuchukua hatua mpya ya kiroho, kwa Jina Kuu la Kristo Yesu... Amen, nimeomba kwa ajili yako...
Mྂwྂlྂ Pྂrྂoྂoྂ
*+255762879363*
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment