*UHUSIANO WA NENO NA UNYOFU WA MOYO*
*Na Mwl Proo*
*0762879363*
Hallelujah To Jehovah, Bwana awabariki nyote!
Ili kulipokea Neno, ambalo linafananishwa na mbegu (Luka 8:11), lazima udongo (moyo), uwe unaofaa (Mnyofu)
Luka 8 : 15
*_Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia._*
Mtu asipokuwa na unyofu ndani ya moyo, hatalipenda neno, wala hatalifurahia. tusome maandiko yafuatayo;
Yeremia 6 : 10 *_Niseme na nani na kushuhudia, wapate kusikia? Tazama, sikio lao halikutahiriwa, wala hawawezi kusikiliza; tazama, neno la Bwana limekuwa matukano kwao; hawalifurahii._*
Mika 2 : 7
*_Je! Maneno yangu hayamfai yeye aendaye kwa unyofu?_*
UKO UHUSIANO WA MOJA KWA MOJA, KATI YA UNYOFU WA MOYO NA NENO LA MUNGU, IWE KULISOMA BINAFSI KWA NJIA YA MAANDIKO, KULISIKIA LIKIFAFANUSHWA NA WENGINE KWA MAFUNDISHO, NA KULIPA NAFASI KWA KUTAFAKARI, ILI LIKUSAIDIE. MOYO WA MWANADAMU UNA SIRI KUU MNO (Yer 17:9-10), MUNGU ANAUTAKA MOYO, NA NENO LAKE LINAUHITAJI MOYO WAKO (Mithali 23:26). WAKATI AKILI ZA KAWAIDA ZIPO KICHWANI, MTU WA ROHONI AKILI ZINAKUWA MOYONI (Kutoka 35:35, Mithali 10:8), NA MAMBO MENGINE PIA, YANADAI NAFASI MOYONI. NDIO MAANA KUNA MAONYO YA KUTOURUHUSU MOYO WAKO KUAMBATANA NA MACHO YAKO KWA KILA KITU MACHO YANAONA (Ayubu 31:6). NA KWA KUWA MOYO WA MTU UNAWEZA KUJIKITA KATIKA KUANGALIA WAPI UMEWEKEZA SANA, WAPI UNA HAZINA (Math 6:21), KWA SABABU HIYO, BIBLIA INASEMA, MALI IZIDIPO, MSIIANGALIE SANA MOYONI (Zaburi 62:10). KWA NINI MSIIANGALIE MOYONI, IKIFIKA MOYONI MWAKO, ITAITWAA NAFASI YA MUNGU. KWA HIYO UKIFANIKIWA KUMILIKI MAJUMBA (MANSIONS), UKAONGEZA IDADI YA MAGARI NA VIWANJA NA BIASHARA KUBWA NA KAMPUNI, VITU HIVYO VITAZAME KWA MACHO TUU 👁👁, KISHA SEMA MOYONI MWAKO, ASANTE MUNGU KWA HAYA YOTE, NINAJUA NI WEWE UMENIPA. UTAFANYA KOSA KUBWA KAMA UTAULEKEZA MOYO WAKO.
Kwa mtu uliyeokoka, unaagizwa kuulinda moyo wako, kuliko vitu vingine (Mithali 4:23). Kwa nini hasa, moyo wako Mungu anautaka uwe kwake Yeye na Neno lake lipate nafasi, tena Mungu mwenye wivu hatapendezwa kuona moyo wako upo kwenye mambo mengine mbali na yeye. Mtume Paulo aliongea kitu kizuri sana, kwamba umtumikie Mungu, pasipo moyo wako kuvutwa na mambo mengine (1Korintho 7:35).
Kukitoke hitilafu moyoni, lazima uwezo wako wa kukaa na Neno, kulipenda, kulifurahia, kuliishi, neno kuwa hai ndani mwako kutaathiriwa.
Yakobo 2 : 4
*_je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu?_*
👆🏽👆🏽Kama kunavyotokea hitilafu za umeme (electric shock), ndivyo moyo usiolindwa unaweza kupata hitalafu, na matokeo yake ni kulinyima nafasi Neno la Mungu.
Mafarisayo walikuwa na hitilafu ya mioyo, hawakuweza kulipolea Neno la Yesu, Jesus told them, you have got no room in your hearts for my word (John 8:37). Hawakuwa na nafasi mioyoni shida kubwa ilikuwa ile hitilafu. Mfalme wa Israel (Ahabu) katika 1Falme 22:1-40, tunamsoma hakuwa na unyofu wa moyo, na hivyo hakuwa radhi kulipokea Neno la Bwana. Alikuwa anajua Neno la Bwana, analo Mikaya Bin'Imla, lakini hakutaka kupokea, alikuwa radhi awasikie manabii waongo sio Neno la Bwana.
NYAKATI TULIZONAZO, WATU WAMEKUWA NA ROHO NZITO, HAWALIFURAHII NENO, HATA MASOMO NINAYOANDIKA, WATU WANALAUMU NI MAREFU, WENGI HAWASOMI KWA KIGEZO CHA UREFU, LAKINI NI WATU HAO HAO WANAKOMAA NA GAZETI LA UDAKU 📰🗞MWANZO MWISHO. WATU WENGI WANAHITILAFU MIOYONI, AMBAZO ZINAZUIA KULIFANYA NENO LIWE ZURI (Ebra 6:5).
NI WATU WACHACHE SANA NYAKATI HIZI ZA UTANDAWAZI, AMBAO WANA RATIBA MAALUM ZA KUSOMA NENO, WALE AMBAO WANAJIFUNGIA CHUMBANI KUSOMA NENO HATA MASAA MAWILI MATATU, AMBAO SAA NNE USIKU INAMKUTA MEZANI 📖KAFUNGUA BIBLIA ANASOMA NA KUTAFAKARI AJABU YA NENO LA MUNGU. KWA MUDA WAKO SOMA ZABURI 119:1-176, MISTARI HII 176 INAONESHA UNYOFU WA MOYO, UNAVYOLIFURAHIA NENO LA MUNGU, ILE SHERIA AMBAYO WASIO WANYOFU WANAONA NI TANZI, HUYU MNYOFU ANAITAMANI KULIKA SEGA LA ASALI, NENO LA MUNGU LIMEKUWA WIMBO WAKE, NA ANALISIFIA SANA.....!!
ZAMA HIZI AMBAZO MTU AKISHTUKA USIKU, USINGIZI UKAKATA HAWAZI KUOMBA WALA KUSOMA NENO LA MUNGU, BALI ANAIWAHI SIMU📱, AKIWAZA KUNA MAGRUPU YA WHATSAPP HAKUPITIA MESEJI. NA WATU WAMEJIKWAA KWA TEKNOLOJIA, WHATSAPP NA MITANDAO MINGINE YA KIJAMII, IIMEWANAJISI WATU NA KUWALETEA HITILAFU MIOYONI, AS A RESULT, MTU HAWEZI KUHISI KIU YA NENO. WATU WALIOJERUHIWA KWENYE MAHUSIANO, AMBAPO UGONJWA NI MKUBWA ZAIDI NYAKATI HIZI KULIKO WAKATI WOWOTE, HAWAWEZI KULIFURAHIA NENO LA MUNGU, MAANA ILIPASWA MOYO UWE MNYOFU. NI VIJANA WACHACHE WANAOMWANDAMA BWANA, ASEME NAO DIRECT AU KUPITIA NENO, MAANA MIOYO YA VIJANA IMEJAA MAMBO AMBAYO DUUUH 😰 (Mwanzo 8:21). MIMI NAJUA UMUHIMU WA KUWA MNYOFU NOYONI, MAANA HATA KUKITOKEA SHIDA TU NDOGO IKANIVURUGA MOYONI, NA MSITISHA HATA KUANDAA HAYA MASOMO, NA KWA SABABU HIYO, NAJITUNZA MOYO WANGU SANA. NISIINGIZE NENO LISILOFAA, SITAKI KUWA NA MOYO MBOVU (Ebr 3:12). MOYO UKIJAZWA MANENO MACHAFU, UKAJAZWA MAWAZO MACHAFU, UKAJAZWA PICHA ZA UCHI, NA SINEMA ZA NGONO, UKAJERUHIKA KWA MAHUSIANO YASIYO SAHIHI, UNAKUWA MBOVU. NDIO MAANA WEWE MTU WA MUNGU NI MUHIMU DAIMA ULINDE UNAYOYAINGIZA NAFSINI/MOYONI MWAKO.
UKILOSOMA NENO UKIWA NA UNYOFU WA MOYO, UTAMHISI ROHO WA YESU, KWA WAZI AKIKUFAFANUSHIA HAYO UYASOMAYO, NA KUZIFUNUA AJABU ZILIZOSITIRIKA NDANI YA NENO. MARA KADHAA NIMEKUWA NASOMA NENO KATIKA MAANDIKO, MPAKA NACHEKA MWENYEWE, NAPIGAPIGA MGUU CHINI KWA FURAHA, NALIJADILI PEKE YANGU NJIANI, NA NINAJIFURAHISHA KWA BWANA, KWA NJIA YA NENO LAKE. SASA KAMA NITARUHUSU HITALAFU YA MOYO, HUO UTAMU SITAUHISI TENA, MAANA NENO LAMFAA MNYOFU WA MOYO.
*TIBA/REMEDY*
Kama unajigundua kwa wazi, kiu yako ya Neno, imuepunguka, tafuta kujua ulianguka wapi, nu mambo gani uliyaruhusu maishani mwako, yakaiba nafasi ile uliyoipa Neno la Mungu. Ukiona upo kwenye mahusiano yoyote yanakunyima uhuru kwa Mungu na kwenye Neno lake ni wazi kwamba hayo mahusiano hayako authorised, mlifanya tu kitu ambacho sicho. Mahusiano sahihi kwa mfano ya uchumba, hayatakunyang'anya uhuru mbele za Mungu, lakini ukiona uneanzisha mahusiano, halafu unaona haya na uzito kumwendea Mungu, ujue wazi ulibugi stepu. Mungu anakutaka, anauhitaji moyo wako. Roho Mtakatifu naye, anakutamani, kiasi cha kuona wivu (Yakobo 4:5). ONDOA VIKWAZO VYOTE, HATA IKIKUGHARIMU KUMWAMBIA HUYO SIJUI MWANAMKE WAKO, KWAMBA SASA BASI!!!✋🏾, DO IT, ILI MUNGU AWE MUNGU MOYONI MWAKO, UKIMTAKASA KRISTO MOYONI MWAKO (1Pet 13:14,15).
Mungu awabariki nyote
Mwl Proo
0762879363
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment