Wednesday, May 13, 2020

LINKS

*J͟͟E͟͟! U͟͟N͟͟A͟͟H͟͟I͟͟T͟͟A͟͟J͟͟I͟͟ K͟͟U͟͟Y͟͟A͟͟P͟͟A͟͟T͟͟A͟͟ M͟͟A͟͟S͟͟O͟͟M͟͟O͟͟ Y͟͟A  N͟E͟N͟O͟ L͟A͟ M͟U͟N͟G͟U͟ (TEXTS&VIDEOS) K͟U͟T͟O͟K͟A͟ K͟A͟T͟I͟K͟A͟ K͟U͟R͟A͟S͟A͟ N͟A͟ A͟K͟A͟U͟N͟T͟I͟ Z͟O͟T͟E͟ Z͟A͟ A͟L͟L͟ T͟R͟U͟T͟H͟?*

*Hapa chini kuna links (U͟R͟L͟) za kukuwezesha kuyafikia kwa wepesi zaidi*

1. Njia nyepesi  kuzifikia  videos za masomo zilizopo YouTube kwa Online Tv iitwayo *Mwl Proo Tv*. Fuata link hapa chini

https://youtu.be/HeiwpJMX1KM

2. Njia ya pili, nyepesi pia, ni kupitia ukurasa wa ALL TRUTH uliopo Facebook.Fuata link hapa chini

https://www.facebook.com/1753714571520311/posts/2463886217169806/

3. Njia nyingine  ya kuyafikia masomo karibu 200 yaliyoandikwa tangu 2015, ni kwa njia ya blogspot. Fuata link hapa chini

http://alltruthjohn1613.blogspot.co.ke/2016/?m=1

4. Masomo pia yako _pinned_ kwenye kundi letu la All Truth Telegram

https://t.me/joinchat/FExBMF0jT5jDzPgE

5. Njia nyingine nzuri ya kuyapata masomo ni kwa njia ya android app ya playstore iitwayo *Mwl Proo*. Fuata link hii hapa kuipakua

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.mwl.proo

6. Kwa wale walioradhi kujiunga na makundi ya WhatsApp ya ALL TRUTH ambapo masomo haya hutumwa basi wafuate links hizi hapa chini.

https://chat.whatsapp.com/EDh7ypvFUt7JcBNPhmbA7V

AU

https://chat.whatsapp.com/HOJCzEl3oVQI6sniaoMibQ

AU

https://chat.whatsapp.com/K9BuTV7lnpu1VKdO6VL5Ir

FOR ENGLISH SPEAKERS  (NON-TANZANIANS), FOLLOW THIS LINK (+255 ARE NOT ALLOWED HERE)

https://chat.whatsapp.com/HzNspp0Pd6g5cMIA8p3Dd0

Bonyeza https://wa.me/255762879363 kuchati na Mwl Proo moja kwa moja kwa whatsapp

Bwana Yesu Kristo akubariki sana!!!

Kwa mawasiliano zaidi
+255762879363

UOVU WA WAAMORI

*MAANA HAUJATIMIA UOVU WA WAAMORI BADO*

_Ufafanuzi mfupi na Mwl Proo_
0762879363

Bwana Yesu Kristo apewe sifa! Naamini BWANA Mungu anaendelea kukutunza na kukuhifadhi (Zaburi 91:14). Tauni hii _covid-19_ itapita nawe utahifadhiwa na wema wa Mungu, iko neema ya kukunusurisha na kila janga litakalozuka katika nyakati hizi, pokea hiyo neema kwa Jina kuu la Yesu Kristo ✋๐Ÿพ

Niliwekewa moyoni mwangu kuandika ufafanuzi wa mstari huu hapa chini, Mwanzo 15:16, wakati Mungu akizungumza na Abramu (badae Ibrahim) juu ya uzao wake.

_*"Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado."*_
(Mwanzo 15:16)

*_"But in the fourth generation they shall come hither again: for the iniquity of the Amorites is not yet full."_*
(Genesis 15: 16)

⚖ Katika somo langu la _Kikombe changu kinafurika_ nilitoa moja ya tafsiri za kinabii kuhusu kikombe ☕ nikikihusianisha na ghadhabu/hukumu.. ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ (Yeremia 25:15, Ufunuo 14:10, 16:19). Kabla Mungu hajaachilia hukumu yake lazima kuwe na kiwango fulani cha uovu kimeenda beyond His tolerance (before He execute His divine judgement, iniquity/wickedness should reach a certain degree beyond tolerance and beyond His dispensational time)... Inaweza kuonekana kana kama haijakaa sawa kwa namna tunavyomfahamu Mungu alivyo wa rehema na msamaha. Mungu hataadhibu bila kuleta maonyo kwa ustahimilivu mkuu. Ni kama kunakuwa na kikombe kimehifadhi uovu ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ☕ watu wakitubu, zinafutwa na Mungu hawahesabii tena huo uovu/dhambi (Zaburi 32:1, Isaya 43:25), lakini kama watu hawatatubu wakaendelea tu kutenda maovu juu ya maovu, kikombe kinaweza kujaa, kikombe cha uovu kikijaa, hukumu ndicho kitu pekee kitakachofuata, maana pamoja na Mungu kujaa rehema na msamaha (Daniel 9:9) hawezi kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia (Kutoka 34:7) labda kuwe na michakato hapo kati iliyohusisha toba, au neema kwa njia ya Yesu watu wakiikubali. Kuna wanaofundisha neema to the extreme bila kujua kuwa neema iko na terms and conditions za kwake, mtu akiipungukia neema kuna namna atakuwa _dealt out_ na hasira ya Mungu na wasiolewa watashangaa. Neema ya Mungu haijambadilisha Mungu (Malaki 3:6), God's  attributes  zimebaki vilevile, He's always willing to save the sinners, lakini nani asiyejua kuwa mtu akifanya uovu, anamfuta katika kitabu chake alichokiandika? (Kutoka 32:32-33), na *UKWEKI HUU UWAFIKIE WAHUBIRI WANAOHUBIRI NEEMA YA MUNGU BILA KUZINGATIA MIPAKA YA MAANDIKO, KUWA KUNA SIKU HUYU MUNGU WA NEEMA YOTE ATAWATUPA KATIKA ZIWA LA MOTO BILLIONS OF HUMAN RACE INTO THE LAKE OF FIRE, IKIWA NI ETERNAL PUNISHMENT*. Neema imewabadilisha wanadamu, neema imewawezesha na imewafundisha wanadamu kuwa kama Mungu (Tito 2:11-13) ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ nayo yatufundisha kuukataa ubaya (hii ni side B ya neema ambayo wengine wamekuwa wakiiacha). Mfano kama kuna mchungaji ambaye kaipokea neema, anaijua, anaihubiri, ila anaendelea kuziishi dhambi (in the full knowledge), anazini na washirika, anafanya kila ubaya, pamoja na kuwa kwenye kipindi cha neema, wema wa Munyu utakuwa unamvuta atubu, lakini kuna muda wa Mungu kuvumilia (2Petro 3:9 ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Huvumilia kwetu, He's patient with us), kunakuwa na muda aliouweka katika mamlaka yake mwenyewe huo ni kama matazamio, kuona kama utatubu kwa kule kuvutwa na wema wake au la (Ufunuo 2:21, Rumi 2:1-4, 11:22-24). Hivyo moyo wa toba (Rumi 2:5) utapelekea dhambi/uovu kufutwa, kuendelea na uovu/dhambi kunaweza pelekea kikombe kujaa. Kikombe kikijaa hakuwi na kingine zaidi ya hukumu... Unasikia Mungu anasema kuwa dhambi za Sodoma na Gomora zimefika mpaka juu mbinguni, akiwa ana-infer kwa issue ya kikombe kujaa ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ☕ _mwlproo_

⚖ Wakati Mungu anaongea na Ibrahim, ambaye alikaa kati ya mataifa ya Kanaani (Canaanite nations), uovu tayari ulikuwepo mwingi mno (Mwanzo 13:13, 18). Lakini Mungu aliona bado kikombe cha ghadhabu yake hakijaa, akatoa muda zaidi (dispensation). Anasema hivi *_Maana haujatimia uovu wa Waamori_*  kwenye KJV iko hivi *_For the iniquity of the Amorites is not yet full_*, kama watu watatubu kikombe kinakuwa _emptied_, lakini wakiendelea muda ukifika kitajaa, na hukumu itakuja. Mungu anamwambia Ibrahim kuwa uzao wako nitawapa hii nchi, wakazi wa Kanaani, mataifa yote yale (Maana Kanaani mtoto wa Ham alizaa makabila yote ya kule Canaan ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Mwanzo 10:15ff). Sasa walikuwa wanakaa kule kwa halali kabisa, na walipewa nchi ile kwa halali kabisa... Nimesikia mjadala katika kundi huko Facebook wakisema Mungu wa WaKristo ni KATILI, anaua mataifa mengine bila sababu ili awaweke wazayuni (wayahudi). Sasa Je! Mungu ni mkatili? God is just (Righteous Judge).... Tusome maandiko hapa chini

_*"Si kwa haki yako, wala kwa unyofu wa moyo wako, hivi uingiavyo kuimiliki nchi yao; lakini ni kwa uovu wa mataifa haya Bwana, Mungu wako, awafukuza nje mbele yako; tena apate kuliweka imara hilo neno Bwana alilowaapia baba zako Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo."*_
(Kumbukumbu la Sheria 9:5)

Mungu hakuja kuyaangamiza yale mataifa for fun, alifanya accurate calculations, kuwa kwa muda wa miaka ambayo uzao wa Ibrahim utakuwa Misri, basi kikombe cha haya mataifa kitakuwa kimejaa tayari kwa hukumu, na akikusudia alitumie taifa dhaifu la Israel kuyapiga mataifa ambayo hayakuwa na human races za kawaida.

⚖ Iko hivi, Mungu anasena haujatimia bado uovu wa Waamori, uovu gani, kwa nini Waamori?  Waamori imetajwa kuwakilisha mataifa yote ya Kanaani kwa kuwa lilikuwa kabila kubwa, lenye nguvu zaidi, lililojieneza magharibu yote ya Mesapotamia. Mataifa yote haya yalifanya machukizo, Mungu aliamua ku-buytime kungoja kikombe kijae (utimie uovu wa waamori)... Wale majitu (Nephilims ambapo wana wa Anaq majitu yalitokea kwa Wanafeli, Gibborim (Nimrod naye alikuwa ni jitu kutoka kwa jamii hii), kuna mfalme aitwaye Ogu wa Bashani alitokea kwa Warefai (Rephaim). Nchi ya Kanaani ilijaa majitu (Giants), and God always wished to wipe away hii jamii ya watu. Alifanya jambo la kwanza kuwaondoa kupitia Noah's flood (gharika), mafanikio hayakuwa ya 100%, maana kwenye safina shetani alikuwa amekwisha penyeza uzao wa kijitu kupitia wakweze Nuhu, na hivyo  katika hawa watoto wa Nuhu  yaani Ham na Yafeti wote walikuja kuzaa majitu kwa mujibu wa Historia, kasoro Shemu tu (babu wa Yesu)... Ukweli huu unatupia nje dhana zote kuhusu *Double Incursions* kwamba wale Wanefili tunaowaona katika Hesabu 13, ni uvamizi mwingine wa majitu katika dunia... Wale wote ni products za kizazi cha Nuhu fuatilia vizuri vizazi katika *Mwanzo 10*, ... Haya majitu (giants) hawajawahi kuwa wema wala kuwa na tabia za maadili, kila unapotaja Majitu una *Moral Depravity* kila ubaya ulibuniwa na hii jamii ya watu. Na vyanzo vinaonesha miongoni mwa mambo yalimfanya Mungu aandae mpango wa kuitoesha kabisa hii jamii (it was His dream that one day giant-races are all extirpated)... Miongoni mwa mambo yalichochea sana urafiki wa Mungu na Daudi, ni pamoja na Daudi kwa kutumia watu wake wenye nguvu kushambulia masalia ya majitu.

⚖ Kuhusu kizazi cha nne, ambapo tafsiri nyingi za kingereza zimesema *In the fourth generation*, kuna dhana kazaa hapo kati... Kwanza neno la kiEbrania kwenye kizazi  limetumika *dowr/dor* katika kiYunani wameweka neno *genea* ikiwa inafanana kabisa na maana ya kiRumi ya neno *Soeculum/Seculum* lenye maana ya Century hivyo ikitujuza kuwa kizazi kimoja kiko denoted na miaka 100 (kuna mjadala mpana kwamba hilo neno huashiria miaka 30/40, that discussion is purposely excluded in this topic ili niwe focused na jambo moja...). Hivyo kuna uwezekano wa kwanza kuwa vizazi vinne ni vya Ibrahim, ambapo vyanzo vingi vimekubaliana kuwa ni kuanzia kwa Lawi, Kohath, Amram, hadi Musa/Haruni.. (alternatively tukianzia kwa Yuda kizazi cha nne ni Kaleb)... Hili limehusianishwa na miaka 400 aliyoisema Mungu hapo nyuma kidogo yaani (Mwanzo 15:13)

Lakini pia inaweza kuwa vizazi vinne vya waamori (more probable) kwa sababu ya mfuatano wa hoja katika sentensi,  kama tusomavyo hapa Mwanzo 15:16

_*"Lakini nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini naliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini."*_
(Amosi 2:9)

*MUNGU WA HAKI, ALISUBIRI KIKOMBE KIJAE, AKA-ANNIHILATE JAMII YA WAOVU, NA ARDHI YAO AKAWAPA TAIFA LA ISRAEL AKIWAONYA MBELE KUWA WASHIKE SHERIA ZAKE, ISIJE NCHI YA KANAANI IKAWATAPIKA KAMA ILIVYOTAPIKA MAJITU. AMBAO UOVU WAO ULIJAZA KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU. WALE WAPELELEZI KUMI WALIOLETA TAARIFA MBAYA, HAWAKUDANGANYA, NI KWAMBA TU HAWAKUMPENDEZA MUNGU KWA KUWA NA WOGA, ILA WALIONA MAJITU KWELI, KWAMBA WALIONA NCHI ILE IKILA WATU, NI TABIA ZA MAJITU KULA WATU WA KAWAIDA, TABIA HIYO WALIIFANYA ZAMA ZA YAREDI MPAKA NUHU, NA KIPINDI HIKI TENA WALIIRUDIA HIYO TABIA, NA MUNGU AKAWAWEKA AKIBA KAMA VYOMBO VYA GHADHABU, AKASUBIRI UOVU WA WAAMORI UTIMIE, AKASHUSHA HUKUMU*

Mungu akubariki msomaji wangu unapoendelea kufuatilia masomo haya kuongeza maarifa ya Neno la Mungu ndani yako..

Pokea ufahamu wa Neno la Mungu (Katalambano ✋๐Ÿพ)

Mwl Proo
*0762879363*
alltruth5ministries@gmail.com

Monday, May 11, 2020

ZAMU YA NNE ⏰

*NAMNA MASAA (ZAMU) YALIVYOHESABIWA KIBIBLIA*
~_*MwlProo*_~

Shalom...! Nimeandika posti hii fupi, kujibu swali lililoulizwa na mwanakundi mwenzetu kuhusu *Zamu ya  nne*

Tangu Adamu babaye Sethi mpaka karne zaidi ya 14 baada ya Yesu, hakukuwa na kifaa chochote "kitunza muda" kwa namna ya saa (watch/clock). ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ ๐Ÿงญ⏱⏰ . Kila mahali duniani watu walikuwa na namna tofauti za kuhesabu masaa. Mpaka mwaka 1656 ambapo m-Dutch (a polymath&horologist) mmoja mwerevu sana na fundi saa (inventor) aitwaye  Christiaan Huygens alipogundua saa... Na kuanzia hapo mpaka miaka ya 1930's saa ziitwazo *_Pendulum clock & Spiral-hairspring_* ziliendelea kutumika.

*ZAMA ZA BIBLIA*
Biblia imeandikwa kwa miaka karibu 1,500, Yaliyoandikwa Agano la Kale (iwe muda au mambo mengine lazima yamulikwe kwa jicho la kiEbrania) na yaliyoandikwa Agano Jipya lazima yamulikwe kwa jicho la kiYunani (lugha iliyotumika kuandika Agano jipya) na kiRumi yaani dola iliyokuwa inatawala wakati huo. Mifumo miwili iliyotumika kuhesabu saa katika Biblia ni mifumo ya Kirumi na Kiyahudi. Warumi waligawanya masaa ya usiku katika Zamu Nne (4), Hivyo masaa 12 yalikuwa na mgawanyo wa makesha manne (Four Watches of Night), Kuna jambo ambalo nitaliondoa katika posti hii kufupisha maelezo, lakini kwa ufupi Warumi waliweza kuwa na tofauti ya muda wa kuanza kesha la kwanza kutegemea na majira ya mwaka au vipindi vinne (i.e., Spring Equinox  kesha la kwanza lilianza saa moja jioni, Summer Solstice kesha la kwanza lilianza saa mbili usiku, Autumnal equinox kesha la kwanza lilianza saa kumi na mbili jioni, na Winter Solstice kesha la kwanza lilianza saa kumi na moja jioni. Makesha au Zamu nne ni hizi, yaani Vigilia Prima (ZAMU YA I) kuanzia 1700hrs (saa kumi na moja jioni) mpaka 2000hrs (saa mbili usiku). Kisha kuna Vigilia Secunda (ZAMU YA II) Kuanzia 2000hrs (saa mbili usiku) mpaka 2300hrs (Saa tano usiku) kisha kuna Vigilia tertia (ZAMU YA III) kuanzia saa 2300hrs mpaka 0200hrs (saa nane usiku). Na kisha kuna zamu ya nne iitwayo Vigilia quarta kuanzia 0200hrs mpaka 0500hrs (saa kumi na moja alfajiri).. Huu ni mfano wa zamu nne kwa majira ya (Winter Solstice) saa la kwanza la zamu likibadilika masaa yote yatakuwa tofauti.
Wayahudi walikuwa na zamu tatu tu (Kesha la kwanza/Zamu ya kwanza ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Omb 2:19, kesha/zamu ya kati/middle watch ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Amu 7:19, na kesha/zamu la asubuhi ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Kut 14:24, 1Sam 11:11, walianza saa 6pm mpaka 10pm (ZAMU YA I), kisha 10pm mpaka 2am (ZAMU YA II), na mwisho ni kuanzia saa 2am mpaka 6am (ZAMU YA TATU). Mfumo wa Wayahudi uliingiliwa na mfumo wa dola tawala hivyo nao mgawanyo ukaongeza zamu moja ya nne, na masaa yakawa hivi ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ1st (6pm – 9pm); ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ2nd (9pm – 12am); ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ3rd (12am – 3am); ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ4th (3am – 6am). Zamu hizi ziko sawasawa za zamu nne za kiRumi zilizoanzia saa 1800hrs kwa msimu wa *Autumnal equinox*. Na huu ndio mfumo unaowasilishwa katika Mathayo 14:25

NB:-
_mwlproo_
Ikumbukwe wanapotaja zamu ya nne, halitajwi saa moja. specific bali ni saa yoyote tangu saa 3.00am mpaka 6.00am (iwapo tutatumia zamu za kiYahudi zilizorekebishwa wakiwa chini ya utawala wa kirumi). Katika mgawanyo wa zamu za mchana utakuta katika Biblia kumetajwa sana yapata saa tatu, yapata saa sita, yapata saa tisa....Walikuwa wana-estimate tu muda ndani ya zamu (Ingawa warumi walikuwa na kifaa _era Sundial_ ambacho kiliweza kuonesha muda kwa kivuli kupita juu ya alama zao walizozichora juu ya mwamba uliochongwa vizuri). Na hapa ndipo tunaweza jibu swali la Je! Yesu alisulibiwa saa tatu asubuhi (Marko 15:25) au saa sita mchana (Yohana 19:14)? Fahamu kwamba  si rahisi ku kukuta muda mfano saa mbili na nusu, au saa nane kasoro-robo maana mfumo haukuruhusu. Na kama mpo zamu ya pili mwishoni (let say saa tano asubuhi), uko huru kuuita huo muda ni saa tatu (according to Mark), na muda huohuo unakaribia zamu ya tatu inayoanza saa sita, hivyo Yohana hakukosea pia kuita ni saa sita (mmoja ka-refer zamu ya pili mwishoni na mwingine zamu ya tatu mwanzoni)..


Naamini kwa sehemu umepata mwanga.. Maelezo ya ziada kuhusu hizi tofauti na mengine mengi, yapo kwa kina katika somo langu Mimi Mwl Proo, liitwalo *Kutofautiana kwa taarifa kwa injili zinazofanana yaani Different reporting in Synoptic Gospels*

Sunday, May 3, 2020

KONDOO-MUME, BEBERU, NA SIKU 2,300

*๐Ÿ…š๐Ÿ…ž๐Ÿ…๐Ÿ…“๐Ÿ…ž๐Ÿ…ž ๐Ÿ…œ๐Ÿ…ค๐Ÿ…œ๐Ÿ…”, ๐Ÿ…‘๐Ÿ…”๐Ÿ…‘๐Ÿ…”๐Ÿ…ก๐Ÿ…ค, ๐Ÿ…๐Ÿ… ๐Ÿ…ข๐Ÿ…˜๐Ÿ…š๐Ÿ…ค ❷,❸⓿⓿*
*_The Ram, The He-Goat, And  The 2,300 Days_*

*DANIEL 8:1-27*

*สีกำ€ ินษพึ…ึ…*
*0762879363*

Shalom Aleichem!!
Nawakaribisha katika mwendelezo wa masomo ya awali, yanayotuandaa katika masomo ya matukio ya siku za mwisho, siku chache zijazo. Mungu ameweka moyoni mwangu kuanza na ufafanuzi wa moja ya vitabu vya ufunuo wa siku za mwisho (Apocalyptic Books For Eschatological Events).

Daniel aliona maono haya mwaka wa tatu wa kutawala kwake Belshaza, akiwa Shushani (Susa) miaka mitatu baada ya maono ya wanyama wanne. Hii desturi ya Mungu kuja kusema kuhusu jambo mara ya pili na ya tatu (Ayubu 33:14-16), ili kutia mkazo wa utimilifu wa unabii au ujumbe wake ambao unakaribia utimilifu wake, na akiurudia anaweza kuuleta kwa lugha pana ya kueleweka (with intricacy).

*1️⃣ DONDOO ZA DANIEL 8*
*❶. KONDOO-MUME/ THE RAM*
๐Ÿ Daniel aliona kondoo-mume mwenye pembe mbili, lakini pembe moja ndefu zaidi. Kisha anasema, *"Akisukuma upande wa magharibi, na kaskazini, na kusini"*

*❷. BEBERU/ HE-GOAT*
๐Ÿ Daniel alipokuwa akifikiri kuhusu yule kondoo-mume akatokea beberu toka magharibi mwenye pembe mbili pia.
๐Ÿ๐Ÿ Huyu beberu akamwonea hasira kali yule kondoo, akamshambulia. Badala ya huyu beberu zikazuka pembe nne...

๐Ÿ Kutoka katika moja ya zile pembe nne ikazuka pembe ndogo, ambayo badae ilikuwa sana.

๐Ÿ Pembe hii ndogo imetajwa kwa sifa nyingi ambazo nitazijadili sehemu inayofuata kuhusu tafsiri. Lakini miongoni mwa mambo yalifanya na pembe hii ndogo ni kuondoa au kukomesha sadaka ya kutekezwa, patakatifu kukanyagwa na kuangushwa

*❸. SIKU 2,300 (2,300 EVENINGS & MORNINGS)*
๐Ÿ“† Swali linaulizwa mastari wa 14 kwamba hayo matukio yatachukua muda gani, yaani tangu kukomeshwa kwa dhabihu (daily sacrifice) mpaka kutakaswa kwa patakatifu (Cleansing of the sanctuary), jibu likatolewa kuwa jioni na asubuhi 2,300 (complete 24h-hours day). Mstari wa 17 (v17) Daniel anajuzwa kuwa maono hayo ni ya wakati wa mwisho,. Ndugu msomaji najaribu kurahisisha uelewa wa hiki kitu hivyo kuna mambo sijayaweka kwa summary nitayaweka  na kuyawekea tafsiri yake moja kwa moja.
_mwlproo_

*2️⃣ TAFSIRI/INTERPRETATION*
๐Ÿคด๐Ÿพ Kuanzia mstari wa 16 Daniel anasema alisikia sauti ya mwanadamu ikimwagiza malaika Gabriel amfahamishe maana ya yale aliyoyaona. Mstari wa 20 inatolewa tafsiri.

*❶. KONDOO MUME (RAM)*
๐Ÿคด๐Ÿพ Kondoo mume mwenye pembe mbili aliwakilisha utawala wa Umedi-Uajemi (Pembe mbili ziliwakilisha wafalme wawili, two horns ๐Ÿ‘‰๐Ÿพ kings of Media/Persia). Pembe ya pili (Persia/Ajemi) ilikuwa kubwa kuliko ya kwanza (Umedi) na ndivyo ilivyokuwa. Ikumbukwe Daniel mtumishi wa Mungu alikwishajua kwamba Babeli inaenda kuanguka. Na yeye ni waziri katika serikali hiyo hiyo inayoenda kuanguka, maana alioneshwa mambo haya mapema sana katika utawala wa Belshaza. Belshazzar hakuingia madarakani mara baada ya Nebukadreza, ilipita miaka mingi sana hapo kati Babeli ikiwa chini ya Evil-Merodaki, bado haijajulikana sana sababu za Daniel kutoandika matukio ya wakati huo wote. Jambo jingine hapo ni kwamba watumishi wa Mungu manabii, kama hawatajihusisha na siasa kwa ushabiki na mihemko ya kibinadamu, wanatoa nafasi nzuri kwa Mungu kuwajuza kila kinachoenda kutokea. Daniel aliendelea kufanya kazi za mfalme kwa utii na kicho, huku akijua six years to come hakuna kitu  kitabaki mikononi mwa Babeli

๐Ÿคด๐Ÿพ Mstari wa 4 anasema alimwoma Kondoo akisukuma pande kadhaa za dunia... Ni muhimu kufahamu kufahamu maeneo ambayo nabii ameyataja tu kusini au kaskazini..Mfano magharibi ilitaja maeneo ya kiutalawa (Mesapotamia, Syria, Minor Asia), kisha kaskazini yaani Colchis, Armenia, Iberia, Caspian Sea, na kisha kusini yaani Judea, Egypt, Ethiopia, Libya, na India pia (wakati wa Dario), Mashariki haijatajwa maana Uajemi yenyewe ndiyo mashariki (Isaya 46:11)
_mwlproo_

*❷. BEBERU (HE-GOAT)*
๐Ÿคด๐Ÿพ Daniel alimwona Beberu ๐Ÿ tokea magharibi akiwakilisha mfalme wa Uyunani (King of Grecia), anatajwa kuwa pembe kubwa (mfalme wake wa Kwanza) tafsiri chache zikimtaja King Philip (Grecian King), na vyanzo kadhaa vimemjadili Caranus mfalme wa Macedonia, lakini kwa yanatojwa hapo yako dhahiri wakati wa utimilifu wake kuwa aliyetajwa hapo ni Alexander the Great (Iskanda Mkuu), mstari wa tano umetaja kitu cha ajabu (v5) yaani huyu Beberu anaeza akaenda bila kugusa nchi, ikiwa inazungumzia *swiftness* sifa ya Alexander katika conquests zake zote za kivita. Na utaona Beberu ana sifa zilezile za Chui/Leopard tuliyejifunza somo lililotangulia (Daniel 7:6). Haya yanathibitishwa na simulizi ya namna Alexander alivyovamia Medo-Persia mwaka 331BC na kumshinda Darius Codomanus.
_mwlproo_

*❸. PEMBE NNE/ THE FOUR HORNS*
๐Ÿคด๐Ÿพ Pembe nne zilizozuka zinawakilisha falme nne, kama tu yule Chui (Uyunani) tuliyemwona kuwa na vichwa vinne katika somo letu lililopita (jitahidi ulipate, liko mtandaoni) vichwa vinne viliwakilisha watawala-warithi (successors of Diadochi kingdoms), ambapo popular interpretation inatuambia ni Cassender, Lysimachus, Ptolemy   na Seleucus. (Haya siyajadili kwa kina hapa maana yako kwa masomo yaliyotangulia).

*❹. PEMBE NDOGO/LITTLE HORN*
๐Ÿคด๐Ÿพ Daniel anaitaja pembe ndogo ambayo badae ilikuwa kubwa sana kuelekea kusini. Ni nani huyu pembe ndogo? Pembe ndogo ametajwa na sifa ambazo sifa kadha wa kadha zinaweza kumwakiliha mfalme aliyetokea kwa Seleucus ambaye ni Antiocus Epiphanes kwa popular interpretation imekubaliwa lakini bado ziko sifa na matendo ambayo yanamwondoa Antiochus na kumweka hapo mpinga kristo.
๐ŸŒ Alternative ya kwanza ya kuzilinganisha pembe nne zilizozuka kama watawala wanne walimrithi Iskanda Mkuu, inaonekana Antiochus Epiphanes anafit kuwa mlengwa wa unabii. Lakini yako mambo kadhaa yanayotuambia si yeye. Mfano ufalme wa Mungu ulipaswa kuwa established mara baada ya pembe ndogo hapa duniani, ambapo mwaka 164 BC alipokuwa Epiphanes hayakufanyika hayo. Pembe ndogo ya Daniel 7 na Daniel 8 inaonekana kutaja kitu kimoja (Identical). Antiochus hakutimiza nabii zote za pembe ndogo, ikiwemo kupaangusha patakatifu (casting down of the sanctuary), na kuna swala jingine kuhusu warithi wanne wa Iskanda, inasadikika uwepo wa washindani karibu na nane na tawala tatu (hili tuliacha kuepusha mjadala mrefu)..Ukiachana na sababu hizi... Pembe ndogo inatajwa kuwa na uso mkali (fierce countenance), afahamuye mafumbo (understanding dark sentences), kuwaangamiza walio hodari na watakatifu. Pia pembe ndogo atashindana na aliye Mkuu wa wakuu (Jesus is the Prince of princes), then huyu pembe atavunjika bila kazi ya mikono (rejea somo letu la Ndoto ya Nebukadreza kuhusu Jiwe lililoponda miguu). Hizi sifa ambazo zimewekwa hapa zinamwondoa tena Epiphanea Antiochus katika nafasi... Alternative ya pili ni kwamba pembe nne zinapaswa kuwekwa parallel na tawala kuu nne za dunia sawa na sanamu ya Nebukadreza, pia maono ya Daniel kuhusu wanyama wa nne. Na hivyo kwa alternative hii pembe mdogo (mpinga kristo) atatokea baada ya utawala wa nne (miguu ya chuma) au mnyama wa kutisha. Ila hili sio hitimisho, tuendelee mbele kidogo.
_mwlproo_

*❺. SIKU 2,300 (2,300 EVENINGS & MORNINGS)*
๐Ÿ“† Miongoni mwa mambo yamefanya unabii wa Daniel 8 kuwa mgumu ni pamoja na hii *cipher* ya siku 2,300. Nikiri wazi kuwa hapa ndipo mahali ambapo waandishi wengi wameparuka na kutoandikia chochote (No comments).

Naomba niliweke tena andiko hili Daniel 8:13-14

(Danieli 8 )
------------
*13 Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi?*
*14 Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.*

HUU MUDA WA KUONDOLEWA KWA SADAKA YA KUTEKETEZWA NA YALE MACHUKIZO MENGINE YA PATAKATIFU MPAKA WAKATI WA KUTAKASWA KWA PATAKATIFU, IMEBAKI MJADALA MREFU, LAKINI LEO NITAWEKA NURU KIDOGO ITAKAYOKUPA KUJIFUNZA KWA JICHO JINGINE SWALA HILI.
_mwlproo_

*❻. UCHAMBUZI WA KINA KUHUSU SIKU 2,300*
๐Ÿ“† Moja ya tatizo kubwa la kithiolojia katika uchambuzi wa maandiko ni pale ambapo ufafanuzi unajiegemeza kwenye dhana au shule ya mawazo ya kidhehebu na imani ya kikanisa. Tatizo hili liko mpaka sasa kila panapotokea ufafanuzi wa maandiko hasa kwa haya ya matukio ya siku za mwisho.

๐Ÿ“†  Katika kujifunza jambo hili  nilitamani kujua commentators wakuu katika historia waliojitia kuzungumzia swala hili  ambapo mafafanuzi ya wengine wote yamejiegemeza kwa moja ya watu hao. Hatuwezi kumwacha mtu aitwaye Dr C.I Scofield (msomi mkubwa wa kimaandiko wa kiProtestant) na ndugu William Miller (mchungaji wa kiBaptist) ambaye mafundisho yake na mafafanuzi yake ya mafunuo ndiyo yanaweka msingi mkubwa wa mafundisho ya Seventh Day Adventist baada ya kufanyiwa refinement kidogo na ndugu Hiram Edson na Bi Ellen G. White hasa baada ya baadhi ya mabashiri yake kukosea (predictions proved fault).

๐Ÿ“† Tatizo la kimahesabu la kwanza kutoka kwa hawa watu wawili (Scofield) na (Miller) ni kwamba, kanuni ipi itumike kuhesabu siku 2,300? Je! hesabu hiyo ianzie lini? Ikumbukwe kila kinachofundishwa na Protestant Churches kwa asilimia kubwa ni cementations za Scofield juu ya mafundisho ambayo naye aliyafanyia tu refinement toka kwa Catholic preacher (Jesuit Scholar) aitwaye Francisco Ribera (1537-1591)... Ambapo Scofield alichukua mawazo yake akaboresha machache kwa kuongeza wazo la *Pre-Second Coming Rapture*  na mawazo hayo yalikuja kuingizwa rasmi kwenye *British Albury Park Conferences (1826-30)* nayasema haya ili ujue muda waProtestant na waPentekoste wanafundisha kanisa kuondolewa kabla ya mpinga kristo ni mawazo ya karne ya 16 (ya Catholic Jesuit scholar) na kufanyiwa maboresho karne ya 19 ).. Ikumbukwe pia ni wazo hili ndilo ambalo lilifanya juma moja la sabini katika  majuma 70 liwekwe wakati wa mpinga kristo likiwa limetangwa na yale majuma 69  na gepu hapo kati lijulikanalo kama *Dispensation of the Christian Church*.
Na upande wa pili wa mafafanuzi ya siku 2,300 ni yale yaliyotoka kwa William Miller (Baptist Priest)... Ambapo mafafanuzi ya mafunuo ya Daniel yanavyoelezwa na SDA church asilimia kubwa ni yale yaliyowekwa kwanza na Miller.

*❼.  MAWAZO YA SCOFIELD JUU YA SIKU 2,300 NA PEMBE NDOGO*

๐Ÿ“†๐Ÿคด๐Ÿพ Mawazo makuu ya Scofield ni kwamba pembe ndogo ni Epiphanes Antiochus IV na siku 2,300 zote zinatimia katika kipindi chake. Kanuni ya kinabii ya *Day-Year Theory* ile ya kila siku moja ni mwaka mmoja, haikutumiwa na Scofield katika swala la siku 2,300 ingawa naye ameitumia kanuni hiyo kwenye majuma 70 ya Daniel 9, ambapo nimefafanua katika somo langu la Majuma Sabini. Ni kweli kwa mujibu wa historia na vitabu vya apocryphal (apocryphal writings) vimethibitisha mambo yaliyofanywa na Epiphany kwa sehemu yanatoshea kile kinaelezwa kuhusu pembe ndogo. Aliwaudhi Wayahudi, alilinajisi hekalu kiasi cha kuchinja nguruwe patakatifu... Makabayo 1:20-50 (Inaeleza juu ya kukomeshwa kwa dhabihu). Hivyo hesabu iko hivi December 6, 167BC (Desecration of the temple ) ndipo mahali Scofield alibenchmark mwanzo wa siku 2,300 na kuishia March 27, 160BC wakati ambapo Komando Nicanor aliuawa, maana hata baada ya Antiochus kufa hakukuwa na shwari mpaka alipouawa Nicanor. Kuanzia 167 mpaka 160 kuna siku 2,300  kwa kutumia lunar year (360) according to Scofield

yaani 360+360+360+360+360+360 +110=2,270
maanake kuna miaka 6 na siku 110
Ili zitimia siku siku 2,300 waliongeza siku 30 kufidia siku wa kalenda (Adjustment of 7 year calendar) haya mambo ya kufix tarehe za kalenda yako katika masomo yangu mengine. Hivyo kwa mujibu wa Scofield siku 2,300 ni siku 2,300 wala sio fumbo la miaka.

*❽. MAWAZO YA MILLER KUHUSU SIKU 2,300 NA PEMBE NDOGO*

๐Ÿ“†๐Ÿคด๐Ÿพ William Miller, katika hesabu zake ali-maintain matumizi ya kinabii ya Hesabu 14:34 & Ezekiel 4:6 yaani *Day-Year Theory*  hivyo siku 2,300 zinakuwa miaka 2,300. Na hivyo kuweka madai kuwa huu ndio unabii mrefu kuliko zote katika Biblia kuhusu wakati wa mwisho. Lini zihesabiwe siku hizi. Miller alifafanua kuwa unabii wa Daniel 8 unapaswa kuanza parallel na majuma 70 ya Daniel 9, hivyo mwaka ule ule 457BC wa Barua ya Artashasta Longimanus ndio umetumika pia kuhesabu miaka hii pia.

HESABU YA MILLER:
2,300-490= 1,810, Kisha miaka 1,810 inajumlishwa kwa 34 (34AD mwaka wa masihi mkuu kukatiliwa mbali). Hivyo 1,810+34=1844
Na ndipo akaset dhana za Kurudi kwa Kristo mara ya pili kwa mwaka huo (kusafisha patakatifu)... Wazo ambao badae akina Hiram Edson na Ellen White walilibadilisha kwa maana halikutimia, ndipo ikaingizwa concept ya *Hukumu ya upelelezi/investigative judgement* mambo ambayo yatajadiliwa katika masomo yetu yanayofuata. Ufafanuzi mwingi wa kuhusu pembe ndogo na mpinga kristo ambaye alichomekwa Papa wa kikatoliki, hayatajumuishwa katika somo hili.

*❾. ๐Ÿ…—๐Ÿ…˜๐Ÿ…ฃ๐Ÿ…˜๐Ÿ…œ๐Ÿ…˜๐Ÿ…ข๐Ÿ…—๐Ÿ…ž*
Commentaries za Biblia zilizopo zimelalia kwenye moja ya dhana either za Scofield au Miller kwa sehemu kubwa. Lakini kuna kitu kinaonekana katika sifa za pembe ndogo, zilimzungumzia Antiochus IV (Epiphanes), kama picha ya mpinga kristo atakayekuja, na ndio maana kuna sifa Antiochus hana na kuna nabii hajazitimiza. Nimependa wazo la moja ya commentary iitwayo John Gill's Exposition ambapo hesabu za miaka 6 na siku 110 (2,300 days) wamesema ni lugha ya kinabii kumaanisha miaka mingi itakayoishia kwenye milenia ya sita (sixth millennium or thereabout) kwamba pembe ndogo itazuka na kutimiliza yote yaliyo katika unabii. Antiochus ni uvuli wa mpinga kristo kwa agano la kale, lakini anatazamiwa mpinga kristo atakayeyatimiza hayo yote, maana unabii uliotiwa muhuri unajulikana sana muda wa utimilifu wake.

Sura zilizobaki katika Daniel yaani 10&11&12 zitajadiliwa katika masomo ya kitabu cha ufunuo kuhusu matukio ya siku za mwisho.

Ubarikiwe na Bwana, naamini umepata mwanga wa kuanza kujifunza kitabu cha Daniel kwa mtazamo mwingine.

*Mwl Proo*
0762879363
alltruth5ministries@gmail.com

Wednesday, April 22, 2020

WANYAMA WANNE (DANIEL 7)

*๐Ÿ…ฆ๐Ÿ…๐Ÿ…๐Ÿ…จ๐Ÿ…๐Ÿ…œ๐Ÿ… ๐Ÿ…ฆ๐Ÿ…๐Ÿ…๐Ÿ…๐Ÿ…”*
*Four Beasts In Daniel 7*

*สีกำ€ ินษพึ…ึ…*
+255762879363

*1⃣ UTANGULIZI*
Neema, amani, uzima  baraka, na ushindi toka Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ziwafunike. Namwomba Mungu kwamba awatunze, awahifadhi, na kuwanusuru na tauni za nyakati hizi za mwisho. Amini Mungu kuwa mtalindwa salama, kwa Jina la Yesu.
Nakukaribisha kujifunza kweli ya neno la Mungu, muhimu kwa majira yetu.
Daniel na Ufunuo wa Yohana ni vitabu vimeongea mambo yote muhimu kwa nyakati za mwisho, hizi tuko nazo.. Ni muhimu kuelewa, na usiache kufuatilia mfululizo wa masomo haya. Nashauri kama hujasoma masomo yaliyotangulia ya Daniel 2&9 basi hakikisha unayapata hayo pia.

☄ Danieli anasimulia kwa kuandika ndoto na maono aliyoyaona mwanzoni mwa kutawala kwa Belshazzar mfalme wa Babeli. Maono haya  yaliyorekodiwa katika sura ya saba aliyaona kati ya mwaka 556BC--553BC. Mpangilio wa sura katika kitabu hiki haukufuata muda, ndio maana sura ya 6 unaona Dario ni mtawala, lakini sura ya saba anatajwa Belshaza aliyekufa sura ya 5

☄ Mafunuo waliyoyaona Daniel na Yohana mtume yana accuracy ya 100% bila kuhitaji estimation. Maandiko yao yanakubaliana 100% yenyewe kwa yenyewe huku yakikubaliana na maandiko mengine ya Biblia nzima yaliyogusia habari sawa.

☄ Usifanye kosa la kutafsiri andiko la unabii pahala pamoja kwa kuwa unaona linafaa hapo, huku linakataa kufaa pengine. Ni lazima maandiko hasa ya unabii yakubaliane kote, we don't just pick a verse and fix it where we want because it sounds good to us kuweko hapo, hapana!!!!.

*NB:*
*KWA NINI MAFUMBO YA NAMBA, VITU, WANYAMA N.K VITUMIKE KUSEMA UJUMBE WA KINABII (WHY SYMBOLISMS IN PROPHETIC WRITINGS?) SABABU YA KWANZA NI KULIFANYA JAMBO LIELEWEKE ZAIDI (FAMILIARITY), KAMA ATATAJWA MNYAMA BASI ATATAJWA AMBAYE JAMII YA HADHIRA INAMWELEWA NA KUMFAHAMU SANA,NA MNYAMA HUSIKA ATAWAKILISHA TABIA ZA UFALME HUSIKA NA MFALME HUSIKA YESU ALIPOSEMA KAMWAMBIENI YULE MBWEHA LEO NA KESHO NATENDA MIUJIZA NA SIKU YA TATU NITATHIBITIKA, HAKUWA ANATUDUNDISHA KUTUKANA VIONGOZI, BALI ALIJUA UFALME ULE UNAONGOZWA NA ROHO YA MBWEHA KIROHO, BASI ZIKITAFUTWA TABIA ZA MBWEHA ZITAONEKANA ZOTE KWA MTAWALA HUSIKA.  NA PIA KUFANYA WATU WAUTAFUTE UKWELI, MFANO AKITAJWA NYOKA KUMWAKILISHA SHETANI, HUO NI UKWELI/SIRI INAYOJULIKANA NA BIBLIA YENYEWE THROUGH THE ENTIRE SCRIPTURAL TEXT. PIA MAFUMBO HUTUMIKA KUFICHA MAANA ILI KUMLINDA MWANDISHI NA MAANDIKO YENYEWE. MFANO YOHANA MTUME ALIONA JAMBO KUHUSU RUMI KUANGUKA AKAITAJA KATIKA UFUNUO KAMA BABEL (MYSTERY BABYLON) (SHIKA HII KICHWANI KUWA KINABII KUNA BABELI YA KISIASA/POLITICAL BABYLON ๐Ÿ‘‰๐ŸผINAYOJUMUISHA SYRIA+LEBANON+IRAQ) NA BABELI YA KIDINI/RELIGIOUS BABYLON (RUMI/ROME). HIVYO KAMA YOHANA MTUME ANGEITAJA RUMI KWA UWAZI HIVYO, KITABU CHAKE KINGEHESABIWA KAMA DOCUMENT YA KISIASA KINYUME NA DOLA INAYOTAWALA, HUENDA ANGENYONGWA ALIPOTOKA PATIMO, NA WAKATI KAMA ULE DIOCLETIAN ALIPOTANGAZA VITABU VITUKU (SACRED BOOKS) VYOTE VITIWE MOTO, UFUNUO KINGEKUWA CHA KWANZA. HIVYO MUNGU ALIMTAJIA BABEL KWA FUMBO, KUMLINDA MWANDISHI NA MAANDIKO YENYEWE.*

*2⃣ NDOTO NA MAONO YA DANIEL KUHUSU WANYAMA WANNE*

☄ Daniel aliota na kuona ndoto na maono. Katika sura ya saba anajaribu kutuambia haikua zote kwa mara moja, mstari wa 2, wa 7, na wa 13. Na hivyo tunaweza pata mgawanyo wa sehemu tatu za maono yake, sehemu ya kwanza anaona wanyama watatu, sehemu ya pili anamwona mnyama wa nne, na sehemu ya tatu anaona mmoja aliye na mfano wa mwanadamu akija na mawingu ya mbingu.
_mwlproo_

☄ Daniel anaoneshwa kitu kilekile tulichojifunza  katika somo lililopita la Daniel sura ya 2. Nebukadreza alioneshwa tawala nne za dunia kwa kielelezo cha sanamu ya mtu na utawala wa mwisho wa Masihi Mkuu Yesu aliyeonekana kama jiwe lililochongwa mlimani likivunja utawala wa kibinadamu, na Danieli sasa anaoneshwa kitu kilekile, wanyama wanne wakionesha tawala za dunia mpaka wakati wa mpinga kristo na utawala wa mwisho wa Yesu Kristo duniani, kisha katika mbingu na nchi mpya.

☄ Daniel anatueleza kuhusu pepo nne za mbinguni kuvuma, na kisha kutoka katika bahari kubwa wanatoka wanyama (moja ya vyanzo vya kithiolojia vimejadili pepo nne za dunia kama _agitations of political sea_ iko hivi wanyama wanaotajwa ni wafalme/tawala kwa mujibu wa Daniel 7:17, tawala hizi zote zilipatikana kwa njia za mapinduzi ya kisiasa na uvamizi wa kivita, utawala wowote una grounds za kisiasa au za kidini ndivyo historia inavyoonesha, na hiyo ndio sababu ya wanyama katika Daniel na Ufunuo kutoka either katika bahari au katika nchi, bahari inataja mataifa, jamaa, kabila za watu na lugha (Ufunuo 17:15 pia ona Ufunuo 13:1, Luka 21:25, Yer 46:7,8). Na hivi ndivyo itakavyokuwa kwa mpinga kristo na nabii wa uongo, wakati mpinga kristo (mnyama wa I, Ufunuo 13:1) atatoka katika bahari (political sea), nabii wa uongo (mnyama wa II, Ufunuo 13:11) atatoka katika nchi (religious grounds).
_mwlproo_

*❶  SIMBA/LION* ๐Ÿฆ
☄ Mnyama wa kwanza kumwona alikuwa simba, huyu ni kama kile kichwa cha dhahabu katika sanamu ya Nebukadreza. Na Simba huyu mwenye mabawa ya tai, aliwakilisha utawala wa Babeli. Nebukadreza na Babeli mara kadhaa ililinganishwa na simba katika maandiko ya unabii yakitaja nguvu yake na ari yake, na hali yake ya kivita (Yer 4:7)...utawala ulioanza kutawala  dunia mwaka 606 BC mpaka 539BC, kinabii tawala hizi zina-exist maana zitakuja kuinuka tena (nitalifafanua hili mbele kidogo)

*❷  DUBU/BEAR* ๐Ÿป
☄ Dubu (the all-devouring animal) aliwakilisha Waajemi (Persians).. Tabia za Dubu maisha ya milimani, ukatili, ni sifa ya utawala wa kiajemi (Isaya 13:17, 18)... Watawala wawili wakiAjemi kama Cambyses, na Ochus walikuwa wakatili sana wakisadifu sifa za dubu 100%, unaweza ukaona namna mtu akikiuka sheria za kiajemi (Daniel 6:24) sio tu yeye atashughulikiwa, bali wanabeba na wake zako, na watoto wote mnanywea kikombe cha ghadhabu ya kiajemi. Ametajwa kuwa na meno ambayo kwayo anaweza akayashughulikia mataifa (subjugate many nations) na ana mbavu tatu mdomoni, zikiwa zinawakilisha mataifa matatu aliyoyafanyia ukatili wakati wa kuingia kwake katika kushika hatamu yaani  Egypt, Lydia, na Babeli

*❸ CHUI/LEOPARD*
Chui ni mdogo kuliko simba, ila mwenye kasi zaidi (Swiftness) Habakuki 1:8, pia ana ukali (cruelty) Isaya 11:6... Huyu chui alimwakilisha mtawala wa Uyunani Iskanda Mkuu (Alexander the Great) na utawala wake... alikuwa na mabawa manne huyu chui, pia alikuwa na vichwa vinne ๐Ÿฏ๐Ÿฏ๐Ÿฏ๐Ÿฏ ... Vichwa vinne (Daniel 8:8, 22) tunaita Kingdoms of Diadochi (successors)... Himaya ya Iskanda mkuu iligawanyika maeneo manne ya utawala baada ya kifo chake, chini ya majemadari wake wanne ndivyo hivyo vichwa vinne. Himaya nne ni hizi (Macedon+Greece) zikisimamiwa na Cassender, pia (Thrace na Bithynia) zikiwa chini ya Lysimachus, na kisha Egyptikiwa chini ya Ptolemy, na kisha Syria chini ya Seleucus. Alexander Mkuu wa Macedon alikuwa na sifa chui katika mapambano kama chui awapo katika mawindo, na ndiye alimshambulia Dario mwajemi, na aliyatia mataifa haya katika kitanzi chake kwa miaka 12, yaani Europe, Asia, Illyricum, Adriatic, Ganges. Rejea somo langu liitwalo *Falme na Mamlaka* Alexander hakupata utawala huu kwa nguvu zake bali Mungu wa nyakati aliruhusu, maana haingewezekana jeshi lake la askari 3,000 kushinda yale majeshi yenye malaki ya askari.  Mwanahistoria Josephus (katika kitabu chake cha Antiquities) anasema Alexander aliwahi msimulia kuhani wa Yerusalemu kuwa akiwa kwake aliwahiona maono Mungu akimruhusu kwenda Asia na hayo maeneo mengine kuwa atashinda.

*❹ MNYAMA WA NNE*
Wakati ndoto ya Nebukadreza ilionesha utawala wa Rumi kama miguu ya chuma, Maono ya Daniel yalikosa mnyama halisi wa kumfananishia na utawala wa Rumi. Hivyo akasema aliona mnyama mwenye kutisha, mwenye nguvu, ana meno ya chuma (teeth of iron) ikifanana kidogo na material ya miguu ya sanamu ya Nebukadreza. Kisha mnyama huyu alionekana kuwa na pembe kumi, na kisha pembe ndogo itakayoinuka na kujing'oa pembe tatu katika hizo. Mnyama huyu wa nne yuko tofauti kabisa na wale watatu. Na hivyo fuatana nami sehemu ya tatu, ambayo nitachambua kwa kina kuhusu mnyama wa nne anayewakilisha utawala wa nne

*3⃣ UFALME WA NNE NA PEMBE KUMI*
☄ Ndoto ya Nebukadreza na maono ya Daniel vinakubaliana kuwa utawala wa tano utakuwa ni wa Mwana wa Mungu kuja kuuvunja utawala wa kibinadamu. Nebukadreza hakuona mwendelezo kamili wa utawala wa nne kuwa mwishoni kuna mpinga kristo. Daniel katika nafasi yake kama nabii akaona kitu cha ziada kikubwa. Wakati Nebukadreza aliona jiwe (Yesu) litakuja wakati wa utawala wa dola kumi (10 toes), Daniel anamwona mnyama wa nne akiwa na pembe kumi, zikiwalilosja watawala 10 (Daniel 7:24) horns=powers.. ambayo kwa hatua ya kwanza twaweza yatambua kama Roman Kingdom with Germanic & Slavonic tribes (wakati wa Reformation), ikumbukwe kuwa Empire ya magharibi mwa Rumi iliendelea mpaka 731AD, na ya mashariki mpaka 1453AD,

☄ Vidole kumi vinawakilisha falme kumi (Daniel 2:41, Ufunuo 13:1, 17:12). Daniel na Yohana Mtume katika Ufunuo, wanakubaliana pia kuwa utawala wa mpinga kristo utaingia katika wakati wa utawala wa hizo dola kumi. Lazima kutakuwa na mataifa makubwa 10 (makubwa kinabii kisha kisiasa, kiuchumi, kinguvu  etc) ambazo zitaHand over nguvu zao kwa mpinga kristo. Unapoendelea kujifunza maswala haya ya kinabii kuna kila sababu ya kuyafahamu baadhi ya mataifa yanayoambatana na unabii wa siku za mwisho. Mataifa hayo ni Iraq, Syria, Lebanon, Iran, Ethiopia, Egypt, Greece, Turkey, Israel, Russia (Haijalishi taifa litaonekana dhaifu sasa, muda wa unabii kutimia unapokuja kila kitu kitajiweka kwa nafasi. Kuna mataifa yanaweza kuwa na vurugu sasa na nguvu kubwa ila hayako katika unabii wa maandiko, na huenda muda huo ukifika yakawa yamepoteza nguvu na umashuhuri wake kabisa. Lakini pia hifadhi akilini mwako mataifa haya saba au serikali saba zinazowakilisha vichwa saba vya joka au vya yule mnyama (Ufunuo 12:3, 13:1) the seven world empires (7 heads) yaani Egyptian , Assyrian, Roman, Mid-Persia, Greece, Babylon, Anglo-America.
_mwlproo_

*❶  PEMBE NDOGO/LITTLE HORN*
☄ Daniel na Ufunuo wa Yohana vinawezwa kuangaliwa kwa pamoja kwa maswala haya, maana vimetaja kila kitu sawa, swala pembe kumi, vichwa saba. Linakuwa dhahiri sana kuhusu utawala wa mpinga kristo duniani na serikali za dunia zitakazomuunga mkono. Pembe ndogo inaonekana wazi katika maandiko kuwa ni mpinga kristo, ambayo imetajwa katika Daniel na katika Ufunuo kuwa muda wa operation yake ni miaka mitatu na nusu  (1260 days) (soma Ufunuo 12:6, 13:1, 17:11, 1214, 16, 13, 14, 16, 2Thes 2:3). Pembe ndogo inaonekana kuziondoa pembe tatu katika 10, na hivyo kufanya serikali saba za mataifa pamoja na ya nane ambayo ni hiyo pembe ndogo (Ufunuo 17:11), lakini ikumbukwe katika Daniel mnyama wa nne aliondoa wale watatu wa mwanzo ila uhai wao (verse 12) ulihifadhiwa.  Pembe ndogo inatajwa kuwa na kinywa, inatajwa kuwa na macho ya mwanadamu ikiwa inaashiria intelligence (Ezekiel 1:18, Mwanzo 3:5), na atakuja akiwa na mfano wa Kristo (Caricature of Christ). Pembe ndogo ataitawala dunia kwa hekima kubwa ya kidunia na kufanya civilization kubwa kuwahi kutokea katika historia ya mwanadamu na ataileta dunia yote chini ya utawala wake (verse 23). Ndicho kipindi ambacho utawala utajiweka kinyume na Mungu sana (Atheism, Antitheisism, and Autotheisism). Pembe ndogo atanena makufuru kinyume na Mungu kama alivyoona Daniel na kama alivyoona Yohana katika Ufunuo. Mungu ndiye mwenye kubadili nyakati (Daniel 2:21) lakini mpinga kristo atajionesha kuwa yeye ndiye afanyaye hayo naye ataazimu kubadili majira na nyakati.

*❷  VITA NA WATAKATIFU*

*☄ Daniel anasema pembe ndogo (mpinga kristo ) atafanya vita na watakatifu na kuwashinda (verse 21). Hili limathibitishwa tena katika Ufunuo 11:7, 13:7). Jambo hili kama linaweza fananishwa na adha ya kanisa katika kipindi cha mpinga kristo. Mtazamo wa unyakuo wa kanisa  kabla ya kuinuka kwa mnyama (pre-tribulation) unaweka madai kuwa hawa watakatifu ni waisrael na kwa sehemu nyingine ni wakristo waliachwa katika unyakuo. Lakini bado pia yako maandiko mengi yanayoonesha uwepo kanisa katika kipindi cha utendaji wa mnyama (mpinga kristo), yanayozaa mtazamo uitwao mid-tribulation rapture. Haya yote hayatajadiliwa kwenye somo hili kwa kuwa yatachambuliwa kwa kina sana, kwa masomo yajayo siku za usoni. Somo hili lilikuwa linaleta ufahamu tu juu ya wanyama katika Daniel 7.

*❸ UJIO WA KRISTO*
_Christ's advent during the persecution of saints_

☄ Daniel anatuambia wazi kwamba wakati pembe ndogo ikitesa watakatifu (Daniel 7:22, 26-27) ndipo hukumu itawekwa kukomesha utawala wa pembe ndogo, jambo hili linataja kuja kwa Kristo kuuvunja utawala wa mnyama na kuusimamisha utawala wake milele (Ufunuo 16:13-16), Daniel hajatenganisha utawala wa Yesu wa miaka elfu 1 duniani (Ufunuo 20) na ule katika mbingu mpya na nchi mpya (Ufunuo 21). Swala kufunuliwa kitabu na hukumu ambalo Daniel aliliona kama Yohana, litajadiliwa katika masomo yajayo siku uchache za usoni, nikipata neema na muda kuandika.

Ndugu msomaji. Usisite kupekua zaidi katika vyanzo. kwa chochote unachohitaji kujifunza zaidi... Mimi nimekuwekea tu njia. Bila kusahau kumwomba Roho wa Kweli akusaidie.

Mwl Prosper Kadewele
0762879363
alltruth5mimistries@gmail.com

Wednesday, April 15, 2020

SANAMU YA NEBUKADREZA

*๐Ÿ…ข๐Ÿ…๐Ÿ…๐Ÿ…๐Ÿ…œ๐Ÿ…ค ๐Ÿ…จ๐Ÿ… ๐Ÿ…๐Ÿ…”๐Ÿ…‘๐Ÿ…ค๐Ÿ…š๐Ÿ…๐Ÿ…“๐Ÿ…ก๐Ÿ…”๐Ÿ…ฉ๐Ÿ…*

_*Nebuchadnezzar's Statue*_
*สีกำ€ ินษพึ…ึ…*
*+255762879363*

Shalom Aleichem!!
Nambariki Bwana, aliye Kristo (Yesu) kwa neema amenipa kukuandikia ndugu mpendwa, namwamini Mungu kwa bandiko hili, litakuwa msaada na nuru gizani. Zaidi sana litakupa msingi wa kujifunza matukio ya siku za mwisho (end-time events).

*_❶. KUHUSU UNABII NA UTIMILIFU WAKE_*

๐Ÿ”ญ Unabii wa kiMungu haufungwi na chochote. Mungu anaujua mwisho tangu mwanzo (Isaya 42:9, 46:10) na hivyo akisema, hata ikipita miaka elfu 4,000 lazima kila kitu kije kitukie kwa namna ile ambayo alisema... (ona Maombolezo 2:17b)

*" The LORD hath done that which he had devised; he hath fulfilled his word that he had commanded in the days of old....."*
(Lamentations 2: 17b SUV)

๐Ÿ”ญ Muda wa kutimizwa kwa unabii ukifika, kila kitu kitajisogeza chenyewe kwenye nafasi ya kuruhusu unabii utimie. Hata kama inadhaniwa kuwa ni ngumu sana kulingana na mazingira, muda wa unabii ukifika unakuja na njia ya kuufanya utimie. Haikuingia kichwani mwa Belshaza, wala Nebukadreza baba yake, wala Nebopolasa babu yake kwamba kufumba na kufumbua Babeli (mji) ungevamiwa kwa usiku mmoja tu bila vita kubwa wala nini. Muda wa unabii ulipofika Koreshi wa Uajemi usiku mmoja wa tarehe 2 mwezi Oktoba mwaka 539 aliuvamia na kuipindua Babeli. Hakukuwa na mazingira wezeshi kwa jeshi la kiajemi, ila majira ya unabii yalikuja na namna, kulikuwa na mto mkubwa Euphrates (Frati) ambao walioufanyia *diversion*  (badilishia uelekeo) ⚡ wakapata njia ya kuingia.

๐Ÿ”ญ Isaya alitoa unabii mwaka 742BCE kwamba kuna wakati mfalme Koreshi ataamuru Hekalu lijengwe, na mji wa Yerusalemu pia... Haya aliyaongea kinabii yakatokea kama alivyosema miaka 200 badae, kama nilivyoeleza katika somo lililopita kuhusu majuma 70 ya Daniel.

*_❷. SANAMU ALIYOIONA NEBUKADREZA_*

*(Danieli 2 )*
------------
*32 Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba;*

*33 miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo.*

Nebukadreza hakuoneshwa ndoto hii kwa sababu ya hali yake nzuri ya kiroho wala mahusiano yake na Bwana, bali madhabahu ya nafasi aliyokuwa nayo. Katika ule mzunguko wa mataifa yenye nguvu (superpower nations) wakati huo (606BCE mpaka 539BCE) Babeli ndiyo ilishika hatamu. Hivyo Mungu akamwonesha huyu mtu yajayo kwa sababu ya madhabahu ya nafasi aliyokuwa nayo. Na alimsahaulisha ili kumtengenezea njia ya ukuu Daniel mtumishi wake. Unaweza kutembelea familia fulani, mji, nchi fulani, kama kiroho kiko safi, ni rahisi sana kuoneshwa issues za familia, mji, au nchi hiyo.

Nebukadreza alioneshwa sanamu (statue made of different metals/minerals).. Sanamu ilikuwa ni ya mwanadamu, ikionesha utawala wa kibinadamu duniani tangu wakati huo mpaka mwisho wa zamani zijazo. Katika mstari wa 32&33 tunasoma

1⃣ Kichwa (Head) ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Dhahabu (Gold)
2⃣ Kifua/Mikono ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Fedha (Silver)
3⃣ Tumbo/Viuno ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Shaba (Copper/Brass)
4⃣ Miguu ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Chuma (Iron)
5⃣ Nyayo ๐Ÿ‘ฃ ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ ½ Iron (chuma) na ½ Clay (Udongo)

*❸. TAFSIRI YA KILA KIUNGO CHA MWILI KATIKA SANAMU*
Sanamu ilionesha tawala za kibinadamu juu ya uso wa nchi kuanzia wakati wa ndoto hiyo hiyo 599BC mpaka mwisho wa nyakati zote.

*๐Ÿ‘พ KICHWA CHA DHAHABU*
Kichwa cha dhahabu kiliwakilisha utawala/ufalme wa Babeli uliodumu kwa miaka 66 na kidogo (i.e., 606BC mpaka 539BC)

*๐Ÿ‘พ KIFUA NA MIKONO YA FEDHA*
Kifua na mikono ya fedha iliwakilisha utawala ambao ulikuja baada ya Babeli, ambao ni Medo-Ajemi (Medes&Persia) chini ya Persian King Cyrus (Koreshi) mwaka 539BC walimpindua Belshaza mwanae Nebukadreza na kushika hatamu, utawala uliodumu ukitawala dunia kwa miaka 208 (i.e., 539BC mpaka 331BC)

*๐Ÿ‘พ TUMBO NA VIUNO VYA SHABA*
Hii iliwakilisha utawala uliofuata yaani Uyunani (Greece), kama alivyotabiri malaika Gabriel (Daniel 10:20) kwamba nikiondoka huku mkuu wa Uyunani atakuja... Miaka 200 tangu Malaika aseme hivyo, Iskanda Mkuu (Alexander the Great) alivamia na kuushinda utawala wa Medo-Ajemi mwaka 331BC, na utawala huu ulidumu miaka 163 yaani kuanzia (331BC mpaka 168BC).. Utawala wa Alexander Mkuu ulijikita maeneo ya Egypt, Asia, Anatolia, Macedonia.. na huyu alikufa kwa kuwekewa sumu mwaka 323BC (watu wake waliotawala na maeneo yake manne makubwa ni Cassender, Lysimachus, Seleucus, Ptolemy )

*๐Ÿ‘พ MIGUU YA CHUMA*
Miguu ya chuma iliwakilisha utawala uliofuata ukaitweza nguvu Uyunani, nao ni utawala wa Rumi (Roman Empire) mwaka 168BC. Huu ni utawala uliokaa muda mrefu zaidi kwa zaidi ya karne tano i.e., 168BC Mpkaa 476 AD

NB:
*Kila utawala uliowakilisha na aina fulani ya madini (metals/minerals) uliwakilisha sifa husika za huo utawala kwa wenye ujuzi wa maswala ya rocks au extraction of metals wanajua vyema kuwa hizi shaba, dhahabu, chuma, etc zina sifa tofauti....sifa za kila utawala zilikuwa sawa na sifa za madini yaliyofananishwa  nao.

*๐Ÿ‘พ NYAYO ZA CHUMA NA UDONGO*
Rumi ilivunjika, mtawala mmoja wa kijerumani (Germanic leader) alimshinda mtawala Romulus the Roman Emperor... Lakini hapo nyuma mwaka 395AD Roman Empire iligawanyika mara mbili magharibi na mashariki, tawala ya magharibi ilianguka, ya mashariki kama Constantinople/Byzantine mpaka 1453AD

*๐Ÿ‘พ CHUMA NA UDONGO*
Ndoto hii ilionesha nyayo na vidole vya miguu vikiwa na mchanganyiko wa chuma na udongo, ambapo hizi materials mbili haziwezi-shikamana, ikizungumza kuwa baada ya utawala wa miguu ya chuma Yaani Rumi, hakutakuja tena kuwa utawala mmoja superpower wa kutawala dunia, kwamba hata hizo tawala ndogo zikijaribu kuungana hazitafanikiwa, maana kuufanya udongo uungane na chuma ni ngumu... Huku pia sifa za udongo na chuma zikiashiria tawala zingine zitakuwa dhaifu na zingine zenye nguvu.

*๐Ÿ‘พ VIDOLE KUMI*
Kuvunjika kwa dola ya Rumi, kulizaa dola kumi za Ulaya... ambazo ni vidole kumi miguuni mwa sanamu
๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Saxon (Uingereza)
๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Franks (Ufaransa)
๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Alaman (Ujerumani)
๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Visigoths (Hispania)
๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Suevovs (Ureno)
๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Lombardi (Italia)
๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Burgundi (Uswis)
๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Herulous (Huu ulipotea/Vanished)
๐Ÿ‘‰๐ŸผVandals (Vanished away too)
๐Ÿ‘‰๐Ÿผ Ostrogoths (Ulivanish pia)

*❹. JIWE LILICHONGWA MLIMANI*

Historia inaonesha watawala wakubwa wa Ulaya waliojaribu kutaka kuunganisha hizi falme, bila mafanikio. Udongo na chuma haviwezi kuungana. Lakini Daniel anamweleza  Nebukadreza kitu ambacho kitatokea mwisho wa siku, kwamba aliona jiwe lilichongwa mlimani, bila kazi za mikono, hilo jiwe linawakilisha utawala mmoja wa Mungu, utakaosimamishwa hata milele. Jiwe na kazi zake, na sifa zake zinamwakilisha Yesu Kristo. Maandiko mengi ya unabii yanaonesha Yesu atakuja kuusimamisha ufalme juu ya falme zote za dunia (kwanza katika dunia ya sasa ๐Ÿ‘‰๐Ÿผ millenial kingdom, kisha wa milele yote baada ya hapo).. Kuna mataifa 10 yenye nguvu yatampa mkono wa shirika mpinga kristo, na mpinga kristo kwa kutumia nguvu ya tawala hizo atataka kutekeleza mpango mmoja juu ya Israel ambapo Bwana Mkubwa Yesu Kristo ataingilia kati, na kuyashinda yote (Harmagedoni), hiyo itampa nafasi ya kusimamisha utawala wake kwa namna ile alioneshwa Nebukadreza. Siri za hayo mataifa na mambo yaliyosalia hapa, yako katika somo lijalo.

MUNGU AKUBARIKI UNAPOENDELEA KUFUATILIA

Mwl Proo
0762879363
alltruth5ministries@gmail.com

Saturday, March 28, 2020

CORONA (English)

*I SUMMON THOSE WITH GRACE TO PRAY, LET'S PRAY!*

My name is Minister Prosper, Before I slept last night, I was meditating on a video clip showing dead bodies in Italy 'are just dumped' like rubbish (mass burial), and I asked God what is this!?. I wanted to know what really happens. At midnight I saw in the spirit a dark gang of unknown folks (evil spirits from hell) conspiring to bring "corona virus disease". Suddenly I saw an abyss,  it was deep (Rev 9:1ff, Isaiah  5:14), As I was looking at the mouth of the pit, a very big serpent came up out of the abyss (Isaiah 27:1ff), the serpent's height reached the sky (Dan 4:20). I couldn't see its head which was about 24,000 feet high. I got an idea to call my friend who's a prayer warrior so that we can intervene through prayers. The serpent was able to destruct lives of people of the city in minutes. I was shocked because this prayer warrior changed his mind and went to attend lecture session instead of offering prayers.

*Interpretation*
*The destroyer (satan) Nahum 2:1, has come to destroy (John 10:10), what's happening now in the world about COVID-19 is devil's work (I leave away the idea of God punishing the wickedness of the world), because of what  I saw. The prayer warrior I saw represents those who are able to pray  but have just ignored it, and are busy with other things. The presence of Christ's church in the world should bring relief to all humanity including the wicked. The life of these people who are dying just like fowls is entrusted to the church. We can do something and save lives. The life of people who travelled with Paul (Acts 27:9-28) was entrusted to Paul the apostle read verse 24 and see. Don't be hasty to say God is punishing  the globe because of iniquity. He is not delighted in the death of sinners (Ezekiel 18:32)*

*WE CAN STOP THE DEVIL FROM KILLING PEOPLE. THE BELIEVERS USE PSALMS 91 FOR THEIR OWN PROTECTION, THAT IS NOT ENOUGH, EVEN UNBELIEVERS CAN BE RESCUED THROUGH YOUR PRAYERS. LET'S JOIN TOGETHER AND PRAY, LET'S STAND TO INTERVENE THE SITUATION, GOD WILL SAVE THESE PEOPLE WHO ARE DYING. BY HIS GRACE THEY WILL BE SAVED ONE DAY, THEY CANNOT RECEIVE SALVATION AFTER DEATH*
+255762879363 (WhatsApp)

CORONA

*WENYE NEEMA YA KUOMBA KWA JUHUDI, TUOMBE*

*_Usiku kabla sijalala mimi Mwl Proo niliitafakari video ambayo wameonesha miili ya watu huko Italy  ikimwagwa kama takataka kwenye jaa la takataka.. Nikasema Mungu hii ni nini lakini!?, nilitamani kujua nini kinaendelea. At midnight nikaona mpango ukisukwa kuhusu corona virus disease (naamini ule mpango ulisukwa kuzimu)... Ghafla nikaona kuna shimo linaloonekana kwa wazi kuwa ni refu sana (Ufu 9:1ff, Isaya 5:14),  muda nalitazama nilitarajia kitu kitoke, na kweli lilitoka joka 🐍🐉 (Isaya 27:1ff), urefu wake unafika hata mbinguni (Dan 4:20), ni mkubwa na mrefu, pale niliposimama sikuweza kuona juu kichwa chake chafika mpaka wapi maana alienda juu kiasi cha kufika hata futi 24,000 kwenda juu. Nikapata wazo nimfuate mwanamaombi mmoja ambaye  najua yeye yuko tayari kwa maombi kila wakati hasa ya dharura, ili tushughulikie hilo swala kwa maombi, maana nilivyomwona yule joka anaweza kuudhuru hata mji mzima in minutes. Nikafika kwa huyu mwanamombi najisikia vizuri kwamba tunaenda kuomba, tukiwa njiani nikaona ghafla amebadili uelekeo akawa anaingia kwenye jengo kama  "lecture theatre" na akaniambia ana vipindi huko, nikawa shocked maana naona hatari ni kubwa na hajaonesha kujali sana._*

*Tafsiri fupi*
*Shetani mharibifu (Nahumu 2:1) amejiinua anaua wenzetu sana, kinachoendelea duniani ni kazi ya shetani, (sipingani na wanaosema ni Mungu anaadhibu uovu huo ni mtazamo wao), ila nasema kwa nilichoona mimi kazi hii ya uaribifu ni ya shetani na mpango huu haujaandaliwa mbinguni bali ni kambi ya uharibifu (ya shetani), yule mwanamaombi amewakilisha wote wenye uwezo wa kuomba lakini wamepuuza na kuwa bize na mambo yao. Uwepo wa kanisa duniani unapaswa ulete relief/ahueni kwa wanadamu wote hata waovu. Dhamana ya uhai wa hawa wanandamu wanaokufa kama kuku wamekumbwa na castle disease iko kwetu kanisa.. Tunaweza fanya wakanusurika na uharibifu wa shetani, (Matendo 27:9-28 soma mstari wa 24l)..Abiria wote waliosafari na Paulo, uhai wao uliwekwa mikononi mwa Paulo Mtume. Uhai wa wanadamu wote unatutegemea sisi, usikimbilie kusema Mungu anawaadhibu, Mungu hapendi kufa kwa hao watu (Ezekiel 18:32), we can stop the devil, kuwa acha hawa watu.. Wewe unayetumia Zaburi 91 kujitamkia usalama wewe peke yako haitoshi hiyo, hata ambao Biblia hawaisomi, unaweza wanasuru na huu uharibifu, swala la kukokoka watavutwa na Bwana mwenyewe huko mbele kwa mapenzi Yake, lakini kumzuia shetani na kuwakingia kifua hawa wanadamu wenye roho, nafsi, na mwili hilo kila mwokovu analiweza.*

Tuesday, March 24, 2020

MAJUMA SABINI

*๐Ÿ…œ๐Ÿ…๐Ÿ…™๐Ÿ…ค๐Ÿ…œ๐Ÿ… ๐Ÿ…ข๐Ÿ…๐Ÿ…‘๐Ÿ…˜๐Ÿ…๐Ÿ…˜*
_*SEVENTY WEEKS OF DANIEL*_
*สีกำ€ ินษพึ…ึ…*
_+255762879363_
~70|70|70|70|70|70|70|70|70~

Ndugu msomaji na mpendwa wangu katika Yesu aliye Kristo na Bwana, nakukaribisha katika bandiko hili, litakalokupa mwanga wa siri za Mungu zilizofunuliwa kwa neno lake lililoandikwa. Hiki ni kizazi sahihi cha kuelewa mafumbo yote ya Mungu (1Kor 2:10ff), hakuna jambo ambalo limeandikwa katika vitabu 66 vya maandiko ya Biblia ambalo hatupaswi kulielewa, kama kuna siri hatupaswi kuzijua (Kumb 29:29) basi hazijaandikwa kwenye Biblia.

*❶. KANUNI YA KUHESABU SIKU NA MIAKA*

๐Ÿ“‰ ```KUNA MASWALA MENGI KUHUSU NYAKATI ZA KIBIBLIA (BIBLICAL CHRONOLOGY) BADO HAYAJAELEWEKA KWA WATU WENGI, MFANO NI WACHACHE WANAJUA KUWA ISRAEL HAIKUWA UTUMWANI MIAKA 400. ILE SIKU WANATOKA MISRI (EXODUS) ILI UFIKIE MIAKA 400 INABIDI URUDI MPAKA SIKU MWENYEZI MUNGU ANAZUNGUMZA NA IBRAHIMU JUU YA JAMBO HILO (MWANZO 15:13), NA ILI ITIMIE MIAKA 430 ILE YA KUTOKA 12:40 INABIDI URUDI NYUMA MPAKA WAKATI IBRAHIMU ANAITWA (KUTOKA 12:1ff). HILI NDIVYO LILIVYO NA PAULO AMELISEMA ILA KWA KIFICHO KIDOGO (GALATIA 3:17)```

๐Ÿ“… Katika somo langu la _Ukweli kuhusu Krismasi_ nilifanya utangulizi mrefu kidogo juu ya majira/muda na yanavyohesabiwa. Kwa somo hili nitaenda upande ambao sikuugusa mwanzo

๐Ÿ“… Kuna Kalenda nyingi duniani, lakini kwa msingi wa mafundisho haya naweza kukutajia walau nne hizi ambazo zinahusiana na mambo tunayojifunza. Kalenda ya Henoko (yenye siku 364 kwa mwaka), Kalenda ya Julia (yenye  siku 365.25), Kalenda ya Gregory (yenye siku 365 kasoro mwaka mrefu wa nne), na Kalenda ya Kiyahudi (yenye siku 360). Kuhesabu siku za mwezi ni kitu kilichotegemea mwezi, nyota, jua, na uhusiano wake na nafasi ya dunia ๐ŸŒ๐ŸŒŸ⭐๐ŸŒ›๐ŸŒ—๐ŸŒ’☀ .  Yako mambo yanayojadiliwa kuwa yaliifanya dunia isiwe katika nafasi yake ya asili ambayo sitayajadili hapa maana sio kusudio la somo. Lakini jua kwamba idadi ya siku katika kila Kalenda hutofautiana, ninayo maelezo mengi hapo mimi binafsi, kwa kuwa ni mwalimu wa Earth Sciences (Geography).

๐Ÿ“… Katika maswala ya unabii wa Biblia, tunalazimika kutumia Kalenda ya Kiyahudi (ambayo naweza kuiita ya kinabii) maana hesabu za wazi zilizotajwa kwenye Biblia zinaBalance kwa Kalenda yao tu. Kalenda yetu ya siku 365 inafanya tofauti ya mwezi mzima kila ndani ya miaka 6, ikilinganishwa na lunar calendar. Mfano mgawanyo wa miaka saba ya Ufunuo 11:3 & 13:5 (siku 1260 kwa miezi 42) zinaleta hesabu kamili kama tu tutatumia mwaka mmoja wenye siku 360 (i.e., 42x30=1260, na kinyume chake 1260÷30=42). Itakapobidi kutumia hizo zingine zitatumiwa pia ili kutoleta hesabu nyingi kuliko fundisho la msingi.

*❷. SIKU MOJA NI MWAKA MMOJA KINABII*

๐Ÿ“… Kuna muda, na kuna wakati (Kairos&Chronos), maswala ya nyakati Israel kama taifa na matukio yao ni   pahala pa kurejelea _point of reference_. Taifa la Israel ni taifa la kinabii, na hivyo Mungu alianza kuwazoesha mapema sana wayajue mafumbo ya kinabii hata katika maisha yao ya kawaida. Mfano alitaka wapate ujuzi wa kinabii kuwa siku 1 ni mwaka 1, angalia Hesabu 14:34

*",....... yaani, siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka, ........."*

Na katika zama za manabii jambo hili likawa dhahiri zaidi kwao.. Hebu tazama hapa Ezekiel 4:6

*"Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu wako wa kuume, nawe utauchukua uovu wa nyumba ya Yuda; siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagizia."*

HIVYO KWA HATUA YA KWANZA NAOMBA TUONDOKE NA TAFSIRI HII YA KINABII, MAANA TUNAENDA KUSHUGHULIKA NA UNABII WENYE NAMBA (CIPHERS).

*❸. MAJUMA 70 YANAANZA LINI, YANAISHA LINI?*
_mwlproo_
Daniel aliposoma vitabu akakutana na unabii wa Yeremia (Yer 25:11) kuwa utumwani wataitumikia Babeli miaka 70, na wakati huo walikuwa wamekwishakaa miaka 68. Aliingia kwenye maombi ili kuona ahadi ya Bwana kuwajilia tena inatimia. Ndipo Gabriel anakuja na issue muhimu sana... Daniel 9

Mstari wa 24.... anasema _"Muda wa majuma 70 umeamriwa juu ya watu wako..."_

⌚ Malaika Gabriel, alikuwa akimjuza Daniel kuwa swala la ninyi kutoka huku after 2 years liko guaranteed, ila sasa kuna muda wa majuma 70 ulio mbele yao, kuhusu watu wake (Israel) na kuhusu (Jerusalem)... Huo muda umeamriwa na baraza ya Mungu, ndio umebeba kila kitu kuhusu taifa la Israel kuanzia hapo utakapoanza kuhesabiwa mpaka mwisho wake, ndipo itakuwa mwisho wa vipindi kwa taifa hilo la Israel....Usisahau juu ya watu wako, na juu ya mji wako (Jerusalem).

*HESABU 1*
Neno la Kiebrania _Shabuwa_ ni majuma (specifically likitaja miaka/years)

Majuma 70 (70 Weeks)
Ni sawa na miaka 490, Kwa namna gani? Kila siku moja ni mwaka mmoja. Hivyo
Juma 1= Siku 7
Majuma 70= Siku 490
Then, Siku 490=Miaka 490

Majuma haya 70 (miaka 490) kama siku 173,880 (kwa lunar calendar) Malaika aliyagawa mafungu matatu, ambapo mimi nitaweka vipindi vinne kuufikia mwisho wa juma la sabini (seventieth week). Yaani Majuma 7 (miaka 49), kisha majuma 62 (miaka 434) kuna gepu hapo kati ambalo linaitwa _Majira ya Mataifa_ ambacho pia ni kipindi cha kanisa (Church Age), kisha kuna juma la sabini (miaka 7) ya mwisho ili kutimiza majuma 70 juu ya watu wa Daniel (Israel).  Sasa majuma 7+ majuma 62 tunapata majuma 69 ambayo ni sawa na miaka 483

⌚ Tunahesabu kuanzia lini?
_mwlproo_

Mstari 25
*"Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba;*

⌚ Kuna jambo ambalo ni huru kwa lumbano (open to debate) kuhusu tamko lilitoka lini haswa, kuna makadirio fulani tangu mwaka 460 BC mpaka mwaka 445 BC, Watawala hawa wa Umedi&Uajemi (Medes& Persia) walitawala zama hizo. Koresh/Cyrus [538-529]BC, na Dario [wa I, 521-485]BC, na Artaxerxes (Artashasta) [wa kwanza, 464-423] mfalme wa Ajemi, yuko Artashasta wa II, ambaye hana la kumhusu kwa case hii. Sababu hasa ya tofauti hizo ni kwa kuwa kuna matamko (decrees) kadhaa katika Ezra na Nehemia tangu kwa Koreshi (Cyrus), Dario mpaka Artashasta (Artaxerxe) yanayotoa order ya kujengwa kwa hekalu hiyo kuanzia Ezra 1-6, utakutana nayo. Lakini katika sura ya 7 agizo lilikuwa likisema Yerusalem ujengwe, hii ndio inaweza kuhusishwa moja kwa moja na tamko la Gabriel katika Daniel 9:25. Documents kadhaa zimetumia amri ya Artashasta (Ezra 7:21-26) kuwa ni mwaka 457BC, kwa kuwa alitoa tamko lake mwaka wa saba wa kutawala kwake ambapo alianza kutawala  464BC. Wako wengine wametumia decree ingine, ya kile kilicho kwenye Nehemia kwamba mwaka wa 20 wa kutawala kwake............ (inayokadiriwa kuwa 445/444 BC).. Tofauti hapo ni kwamba, Mwaka 457BC iliwekwa amri Yerusalem ujengwe, ila ujenzi haukuanza instantly, na wakati huu sasa kwenye Nehemia 1&2 unaona Nehemia anapewa tena orders baada ya yeye kuweka request kwa mfalme, akiwa ni mnyweshaji huko ikulu. So mwaka 445BC ni mwaka wa kuanza kwa ujenzi na sio kuwekwa amri ya kujengwa kwa Yerusalem. Jambo hili liko  open to debate,  kwa kutumia lunar year 360 days  mwaka huu 445BC unaangukia "close to" wakati wa masihi kukatiliwa mbali (Crucifixion) yaani 483 ukitoa 445 utapata miaka 38 ya baada ya Kristo, ambao hiyo miaka karibu nane inayozidi hapo inaelezwa kwamba kama itahesabiwa zile siku 173,880 kwa kwenda mbele kwa siku za Lunar Calendar hilo gepu linatoweka.. Mimi sijasimama kwa hayo makadirio, badala yake napendekeza kuhesabu majuma 70 kuanzia ilipitolewa amri na Artashasta Longimanus mwaka 458BC mwishoni au 457BC mwanzoni.Na tukianza kuhesabu haya majuma tangu siku Mfalme Artashasta (Artaxerxe) alipotoa agizo/amri ya kuutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu, Majuma 69 yatakamilika karibu sana na kipindi cha kutokea kwa masihi aliye mkuu (Kristo). Wale wanaoanza kuhesabu toka 457 inabalance kama watatumia kalenda ya Julian Caesar. Lakini waandishi wa awali wa Seventh-Day Adventist kama bwana Smith, Larkin, na waandishi wa miaka ya 90 kama bwana Shea, wameanzia 457 BC na kuyamaliza majuma yote 70 (490) inayokuja kuangukia kama mwaka 34 AD, kwa kuwa unabii wa Daniel 8:13-14  yaani 2300 yrs, wameufanya uumeze muda wote wa majuma 70 bila gepu.  Wahubiri kama William Branham na wengine (walioshika msimamo wa kutumia 360 calendar) walihesabu kuanzia mwaka 445 BC mpaka kukatiliwa mbali kwa masihi aliye Mkuu inaleta jumla ya miaka 475 badala ya 483 yani majuma 69, na inagharimu kutumia Kalenda ya mwezi (360) ili hesabu ije kamili (msomaji upo huru kujifunza zaidi kuhusu hilo, nimekupa mwanga tu (soma tena Ezra 7:21-26)..
Jambo moja linalothibitishwa na historia ni kwamba ujenzi ulitumia miaka 49 kamili, yaani majuma saba kama alivyosema malaika Gabriel. Pia miaka hii miaka 483  inaishia muda ambao Yesu alisulibiwa (mijadala ya lini haswa alisulibiwa mwaka 29AD, 30AD, 33 AD au 34AD) haitatosha kwa mjadala huu. Ila Malaika Gabriel was accurate, hizi distortions zimetokea njiani kwa binadamu kujivuruga katika maswla ya tarehe.

*❹. MAMBO YANAYOTIMIZWA KATIKA MAJUMA 69 (MIAKA 483)*
_mwlproo_

1. Kukomesha makosa,
2. Kuishiliza dhambi,
3. Kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu,
4. Kuleta haki ya milele,
5. Kutia muhuri maono na unabii,
6. Kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu."
(Danieli 9:25 )

"Na baada ya yale majuma sitini na mawili (483 years), masihi atakatiliwa mbali (Kusulubiwa kwa Kristo, possibly from  30-33 AD), naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu (Commander Titus of Rome) atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu (70 AD); na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa."
(Danieli 9:26 )

HIVYO, KUFIKIA MWAKA 70 AD, YOTE YALIYONENWA KUHUSU MAJUMA 69 YANAKUWA YAMETIMIA YOTE, YALITIMIA YOTE BILA KUPUNGUA. HIVYO TUMEBAKIWA NA JUMA MOJA TU, JUMA LA SABINI (7 YEARS) ILI KUIMALIZA MIAKA 490 ILIYOAMRIWA JUU YA WANA WA ISRAEL.

*❺. MAJIRA YA MATAIFA*
⌚ Watu wote waliojaribu kufanya makadirio ya kuja kwa Yesu walijikuta katika kukosea kwa sababu kuna kipindi cha majira ya mataifa au pia twaweza ita kipindi cha kanisa ambacho ni _unknown_ na hivyo kufanya ujio wa Yesu kwa ajili ya kanisa uwe haujulikani, MPAKA SASA KUNA MIAKA 1986 IMEPITA TANGU HIKI KIPINDI KIANZE. Unabii wa Daniel ni mwepesi kueleweka maana kuna numericals (ciphers) zinazorahisisha kazi, lakini unabii wa Yesu kuhusu mwisho wa zama za majira ya mataifa (utimilifu wa nataifa) hayana hesabu badala yake yana dalili/ishara tu.. waliotumia unabii wa Daniel 8 (2300yrs), na kutaka kuamini kwamba 1884 kuna tukio kubwa lazima litokee, au kosa kama lilifonywa na Branham katika mahesabu na kutaka kuamini mwaka 1977 kitu fulani kitokee, yalikuwa ni majaribio ya kutafuta kuDeal na _the unknown/concealed_ yaani *The Times Of the Gentiles*

Hebu tusome......

_*"Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia."*_
(Luka 21:24)

⌚Yako mafafanuzi mengi yaliyohusisha mstari huu na UN, WWII, tukio la 1948, na lile la 1967... Ukweli uliofichika ni kwamba, Malaika Gabriel kwa kuwa alikuwa akiongea na Danny haswa juu ya watu wake, na juu ya mji wake mtakaitifu..Utaona ghafla mastari wa 27 anazungumza habari ya Mpinga Kristo (Ufunuo 11&13), ambapo kuna kipindi kilirukwa intentionally, na ndicho kinatenganisha Majuma 69 na Juma la 70 (miaka 7 ya mwisho). Hayo yanayotajwa katika verse 27 ni yale yatakayofanywa na Antichrist katika miaka saba ya juma la 70. Juma la 70 litaanza mara majira ya mataifa au (utumilifu wa mataifa) yatakapitimia... Wakati wowote ambao kanisa la Kristo litakuwa  duniani kabla ya Mungu kuanza kushughulika na taifa la Israel kwa upya, kipindi hicho chote kinatajwa kama *Majira ya Mataifa*. Najua tayari tumeingia kwenye mjadala mwingine wa Unyakuo (Pre-Tribulation, Mid-Tribulation, na Post-Tribulation).. Well, hatutaingia huko sasa, lakini katika mfululizo huu wa sasa hatutaepuka mjadala huo kwa masomo yanayofuata siku za usoni.
Hivyo kusema ni kwamba, miaka saba ya kipindi chote cha mpinga Kristo, ndilo juma la sabini litakalotimiza miaka 490 iliyoamriwa juu ya Israel.   Kilele cha miaka hiyo ni pamoja na Harmagedoni (Somo hili la vita vya Armageddon lipo tayari mtandaoni, nililiandika miaka mitatu iliyopita)...

*Mwl Proo*
+255762879363

alltruth5ministries@gmail.com

Sunday, February 23, 2020

GIFTS VS CHARACTER (KARAMA NA TABIA)

*๐Ÿ…–๐Ÿ…˜๐Ÿ…•๐Ÿ…ฃ๐Ÿ…ข  vs  ๐Ÿ…’๐Ÿ…—๐Ÿ…๐Ÿ…ก๐Ÿ…๐Ÿ…’๐Ÿ…ฃ๐Ÿ…”๐Ÿ…ก*
_*KARAMA NA TABIA*_
*Mwl Proo*
~0762879363~
~0718922662~

Mbarikiwe kwa Jina la  BWANA aliye Mwokozi na Kristo. Wale ambao akili zao kwa kutumiwa zimezoezwa kupambanua mema na mabaya nawakaribisha kula chakula kigumu, ili tujengwe zaidi na kupokea hatua nyingine kiroho.

๐Ÿ’Ž Neno karama ambalo kwa somo hili nitatumia kama Gift, ni pana kimaana  ambalo limetumika kote katika Agano la Kale (O.T) na katika Agano Jipya (N.T). Biblia ya kiEbrania (Tanakh) imetumia maneno kama _Shachad, Mattan, Nathan, Minchah_ ikitaja neno Gift, ikiwa inatofautisha kidogo kati ya kipawa, kipaji, na karama... lakini tafsiri za kingereza maneno yote hayo yalitaja tu *Gift*..... Agano Jipya ambalo liliandikwa kwa lugha ya Kiyunani (Greek) limetumia maneno mawili kutaja Gift, yaani Dorea (karama ya asili ๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Gift of nature au kipaji na wakati mwingine hata huduma.... Pia imetumia neno _Charisma_ ikitaja karama ya Roho (karama au kipawa kinachohitaji uwezesho wa kiMungu kukitumia ๐Ÿ‘‰๐Ÿพ divine enablement)  kimetajwa zaidi kama Charisma.

๐Ÿ’Ž Kuna karama za Mungu, kuna karama ya Kristo, kuna karama za Roho Mtakatifu
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Za Mungu (mfano; Rumi 11:29, Mhubiri 5:19, 1Petro 4:10

๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Za Kristo (Ephesians 4:7)

๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Za Roho (1Korintho 12:7ff)
Kuna wakati fulani ambapo  maneno haya vipawa, vipaji, na huduma hutumiwa tofauti... Lakini kwa kuwa vitu hivi watu hupokewa (Dorea), kwa ujumla wake (1Kor 4:7) huitwa "Gifts", pamoja na kuwa na huduma (services/offices) za Bwana, lakini kwa somo letu la leo, tutavijumuisha vyote kwa neno moja tu *Gift* (1Kor 12:28ff) katika andiko hili unaona namna fulani Paulo Mtume amechanganya huduma za Bwana na karama za Roho, zote kama Gifts tu....

Warumi/Romans 11:29

*"For the gifts and calling of God are without repentance"*
Andiko hili linasema kwa maana karama za Mungu hazina majuto wa mwito wake.. Katika Biblia za Kiswahili cha kisasa pameandikwa..... _Karama za Mungu hazifutiki_ Mimi nimepekua tafsiri nyingi na commentaries kadhaa, kilichoandikwa hapa Warumi 11:29  ni kwamba *The gifts of God are not to be withdrawn... cannot be revoked, when given, not even to be regretted* Mungu akikupa Gift...haifutiki, haiondolewi, hainyang'anywi

๐Ÿ’Ž Mungu akiishatoa gift hana desturi ya kuiondoa.
Mungu alimwumba kerubi mmoja ambaye sasa anaitwa "Mshtaki" yaani shetani, ibilisi, mwovu, akiwa amemwekea *Gifts* yaani vipawa vizuri mno

EZEKIEL 28 (Sitajadili hapa kwamba hizi sifa ni za shetani au mfalme wa Tiro na Sidon, maana nimefafanua hayo katika masomo yangu matatu tofauti)

shetani ambaye aliumbwa kwa daraja la kerubi (sio malaika) aliumbwa na gifts hizi hapa

๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Karama ya hekima (Gift of wisdom) mstari 3-4, 11
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Karama ya uzuri (Gift of beauty) mstari 11-13
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Karama ya maongozi (Gift of administration ) mstari wa 14 (ulikuwa kerubi afunikaye...a cherub that covereth...kiEbrania pameandikwa _Sakak_ ikiwa inataja eneo la kiutawala lenye mipaka... (see also Isaiah 14:16)
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Karama ya Muziki  (Gift of Music).. mstari wa 13 (see also 14:16ff)
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Karama ya ushawishi (Gift of influence/convincing) (mstari wa 9)..

*☝๐Ÿพ☝๐Ÿพ☝๐Ÿพ☝๐Ÿพ Hiyo mistari ni ya Ezekiel 28*

๐Ÿ’Ž Tabia "character"  ya shetani ilibadilika (Eze 28:17). Mungu hamkunyang'anya shetani zile *Gifts*, alimwumba kama kerubi akampa nguvu, hakunyang'anya nguvu zake kwa kule kuasi, alimwumba akampa dunia awe a cherub in charge wa ๐ŸŒŽ.... Hakunyang'anywa hiyo kwa ile *Rebellion* aliyoiwaza juu ya Mungu
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Yesu anasemaje? anamwita shetani *The Prince of  this earth* yaani mkuu wa ulimwengu huu (Yohana 12:31, 14:30, 16:11)...... Paulo mtume anamwita shetani ni _mungu wa dunia hii_ (2Kor 4:4)

๐Ÿ’Ž Malaika waasi (malaika za shetani ๐Ÿ‘‰๐Ÿพ hawa sio mapepo wachafu/majini) hawakunyang'anywa *GIFT* kwa kukubali kumtii kerubi mwasi "shetani".
La sivyo yule prince wa uajemi (medes&persia)..asingekuwa na namna ya kuweka resistance kieneo hata kumchelewesha malaika Gabriel siku 21 kampiga pini asivuke (Daniel 10), so to say nguvu za shetani ni za Mungu, ila baada ya kuasi anazitumia kwa uovu (power of darkness)

*HITIMISHO LA UTANGULIZI*
*_Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya Gifts/Karama na Tabia/Character_*

*❷. Juxtaposition of Gifts & Character*
(Kuzilinganisha karama na tabia)
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Karama haimvuti Mungu, ila tabia (Mdo 13:22)
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Mungu hawi surprized na gifts lakini tabia hufanya hivyo (Ayub 1:6-9)
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Shetani hashambulii karama ya mtu bali tabia (he doesn't fight against the gift but character )
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Anointing/upako wa kugusa maisha ya watu haupo kwenye gift bali kwenye tabia
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Lazima ujue kuwa tabia _good character_ inaweza haribiwa (can be corrupted) 1Kor 15:33

❸.  SEXUAL SINS (DHAMBI ZA KIZINAA/KINGONO)
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Nimetumia lugha hiyo hapo juu ili kujumuisha sex of all types (tendo la ngono na matendo yote ya kingono ๐Ÿ‘‰๐Ÿพ sexual activities and sexual plays)..Watu wanaweza fanya zinaa hata mawasiliano (sexchats).. Ndio maana lile andiko la mazungumzo mabaya huharibu tabia........limeandikwa _evil communication _ kiYunani *Homilia au Kakos Homilia* hapo ndani mpaka Sex imehusishwa na zile njia ovu za kikahaba za mawasiliano (evil communication ways) MITHALI 6:12-13..Zinaa kama kosa kuu (Ayub 31:9-10)..... ni miongoni mwa vitu vikubwa vinavyoCorrupt (haribu) TABIA (character) kwa haraka sana... Mimi ni mwalimu wa sekondari kwa miaka mingi tu sasa...Wanafunzi waliokwisha jihusisha na ngono...reaction kwenye tabia huwa ya mara moja tu... anaweza ghafla tu kuona walimu wote mko sawa naye..
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Sex (Ngono) ni silaha ya mwisho ya shetani ambayo imempa mafanikio makubwa mno...

Kwa kutumia silaha hii, shetani amefanikiwa kutengeneza makundi mawili ya watumishi katika kanisa
I. ๐Ÿšซ Watumishi wakubwa wa Mungu waliopoa.. Kuna watu ambao walipakwa mafuta kwa huduma kubwa na karama nyingi za Roho, wakawa moto sana katika mwili wa Kristo... Baada ya maanguko ya zinaa.....wakapoa...wamefyata mkia...hata kama GIFTS zinafanya kazi..ila wamejikunyata na kujificha...wanamkwepa Bwana, wanakwepa huduma...wametulia chini ya miretemu ๐ŸŒณ๐ŸŒณ๐ŸŒณ๐ŸŒณ

II. ๐Ÿšซ Watumishi wakubwa wasanii... Kwa kutumia silaha ya zinaa/ngono... shetani amefanikiwa kutengeneza watumishi wakubwa tu katika mwili wa Kristo, ila ni wasanii... wameshindwa kabisa kuacha zinaa...ila kwa kuwa karama  zinafanya kazi...zinavutia...zinawafanya wa-earn their living... basi wameona waendelee tu huduma (USANII)... unaweza kuwanasa hawa watu hata kwa sermons zao tu... full of compromizes.... naiweka tu hivyo, Roho atakujuza mwenyewe hapa kwa kina

NB:-
*MTU YEYOTE TU ANAWEZA ANGUKA KWENYE ZINAA AKITENGENEZA/RUHUSU MAZINGIRA, WATAFUTE WAINJILISTI AMBAO WALIKUWA FIRE ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ THEN WAKAANGUKA KWENYE ZINAA, USIDHANI ILIKUWA KAZI KUBWA SANAAAAA, ILIKUWA TU KAMA KUMSUKUMA MLEVI CHAKARI AANGUKE CHINI, HII INATOKEA UKIRUHUSU TU MAZINGIRA*

๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Mtu akishaanguka, Yesu atasimama pembeni akuangalie, unaifanya iwe tabia au unajutia kwa toba nzito ukiangalia kuwa huanguki tena (Yeremia 13:23)... Na kuna muda wa matazamio kuangaliwa kama utafanya toba (Ufunuo 2:21), Yesu akiona huna mpango wa kugeuka anaweza kukuacha ( hakikisha unasoma somo langu _Mwl Proo_  liitwalo "kukuondolewa kinara")

๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Matendo ya ibada yanaweza kuzoeleka, huku mhusika akiwa na _corrupted character_
๐ŸŒช Mtu hapaswi kukosa kushiriki maombi, kufunga, huduma zote zinazokamilisha ibada. Lakimi hizi zote sio kipimo cha good character,mtu anaweza kuzoea hata kufunga na kuomba (fasting & prayer  ) akiwa bado ana matabia ya kizinzi-zinzi tu

๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Mtu akiangalia sana kipawa na kujipa ujasiri kwacho, atapotea, atakufa..... Biblia inasema kipawa (gift) ni kito cha thamani ๐Ÿ’Ž kwake aliye nacho (Mithali 17:8)..... *BUT I bet you.... KARAMA ZITAPELEKA WATU WENGI JEHANAMU*

๐ŸŒ€ Mkumbuke Samsoni (Amuzi 16:1-3)..Alipewa gifts.... ila mauzinzi yake na mauasherati yake yalibaki kama yalivyo kwenye CHARACTER... Samson aliishi kukiwa tayari na Torati ya Musa, pamoja na kushukiwa na Roho ya Bwana mara kwa mara, hakuonaga tabu kulala kwa kahaba all night long akisherati.. Hivi ina maana gani Samson kukwepa divai ๐Ÿท๐Ÿ‡ lakini anasherati ovyo.. ALIKUFA
๐ŸŒ€ Nimepewa ushuhuda wa mwinjilist fulani, aliyekuwa anaaminika kwa kutoa pepo wachafu ndani ya watu... Tena watu wakipagawa pepo...yeye ndiye alikuwa anaachiwa hiyo kazi washirika wengine wakirudi makwao.. Alifikia kiasi cha kutoa pepo akiwa amekaa zake juu ya meza akinywa soda na mapepo yakawa yanapiga kelele na kutoka kwa watu.. Lakini tabia zake za uasherati hazikujulikana...mpaka binti ambaye alikuwa akisherati naye sana kanisani kwenda kujisema kwa mchungaji... na mwinjilist hakuweza kukana, ila akamwomba mchungaji asitangaze...Sasa kumbe hata ule uzinzi wake haukuzuia gifts zake kufanya kazi... Uwe makini sana...Usikae unaamini-amini watu (Mika 7:5, Mathayo 10:17)

๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Kazi nzuri na matokeo mazuri ya gifts hayamthibitishi mtumishi, bali Yesu anathibitisha neno lake tu (Marko 16;20)

*❹.  KUMNYANG'ANYA YESU MAISHA YAKO*
๐Ÿ’Ž Watu wengi wanatamka vitu bila kuvizingatia sana.. Ukweli ni kwamba mtu akiokoka anakuwa amempa Yssu maisha yake...
๐Ÿ’Ž Lakini watu humnyang'anya tena Yesu maisha yao (Galatia 2:20, Kolosai 3:3, Galatia 5:13)
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Maisha ya mtu yakiwa mikononi mwa Yesu, anakuwa huru, anakuwa salama
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Pepo wabaya (wachafu) hawawezi kumtesa ambaye ameshibana na Yesu

๐ŸŒช Anaweza tu kusumbuliwa na pepo katika hali ya uchanga kiroho
๐ŸŒช Kama mtu alikwisha tembea katika ujuzi wa ile kweli na akaenjoi ule uhuru (ukasikia tena amekuwa demon-possessed, anakuwa alifanikiwa kumnyang'anya Yesu maisha yake... YESU AKISHIKILIA MAISHA YAKO, AKAONA UNA BIDII YA KUMNYANG'ANYA ILI UYAISHI MWENYEWE UTAKAVYO, ANAKUACHIA MAISHA YAKO (LUKA 13:34-35).... kwamba hakuna cha kututenga na upendo wa Mungu (Waroma 8:35ff) haina maana wewe huwezi kujitoa kwenye wema wa Mungu (Waroma 11:22) au kwamba huwezi ipungukia neema (Ebr 12:15ff)...

*KUNA MAKUNDI MATATU (3) YESU ANAYAONA, NA ANA NENO JUU YAO*
_mwlproo_

๐ŸŒ€ 1. Waliompa Yesu maisha yao, ila kuna muda wanahisi kuchoka, kuna majira kunakuwa na kaukimya fulani, mpaka unasema hivi mbona wengine wanaendelea tu na uhuru wa kuyatumia maisha yao... wanajaribiwa kama nao kidogo waonje dunia.. Nimepigiwa simu na binti fulani... nikamhoji unaendeleaje kiroho? Haujaanguka? akasema sijaanguka... Ila kuna muda nahisi yani kama na mimi nifanye tu........ haya yalikuwa majibu yake...She's despairing....anakata tamaa na anachoka...amesubiri ndoa...kwa kujitunza haoni dalili....Nikamtia nguvu kuwa bakia umesimama hivyo hivyo..

๐ŸŒ€ 2. Kundi la pili ambalo tuko nalo kanisani, ni watu ambao currently kule rohoni wanayavuta, na kukwapua maisha yao mikononi mwa Yesu

*Neno la Yesu kwao*
_Usininyang'anye maisha yako, huwezi peke yako bila mimi, mambo yanayokuvutia nje yangu, yamejaa uchungu kama pakanga (wormwood/artemisia absinthium)_ ๐Ÿคฎ

๐ŸŒ€ 3. Wako ambao walifanikiwa kumnyang'anya Yesu maisha yao.
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Hawa wanakuja kanisani, maana hawana pa kwenda jumapili (it's liturgical), amekulia mazingira ambayo Jumapili wanaenda kanisani.
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Hana haja ya kumtafuta Mungu...maana nafsini yake yajua sana kuwa hatamwona
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Analazimika kuzitumainia njia za asili katika kutatua matatizo yake yote.

*Neno la Yesu Kwao*
Yesu ambaye sifa yake kubwa ni UPOLE, wala hakemei (Mathayo 21:5, Yakobo 1:5)....Yupo tayari kuyapokea upya  maisha yako...Wema wa Mungu unakuvuta upate kutubu (Warumi 2:4)

Mwl Proo
alltruth5ministries@gmail.com
+255762879363